Yaliyojiri: Mkutano wa Maalim Seif katika Viwanja vya Gombani, Chake Pemba- Oktoba 19, 2014

Updates: Jussa, kuna wakubwq wa ccm wamesikaka wakisema cuf 2015 tayari wameshachukua nchi, pia wako waliopiga kura ya ya Ndio na sasa wamejuta jusa amewataka kabla ya uchaguzi wajiokeze hadharani kuunga mkono mamlaka ya zanzibsr na waeleze dhahiri namna wanavyojuta kupiga kura ya ndio

uzi umeanzisha wewe, weka updates kwenye uzi mama
 
Mheshimiwa Asaa Othmani Hamad mwakilishi wa wete(CUF) wamesema kapiga kura wakati hakushiriki bungeni.Maalim anazidi kushusha nondo
 
Mkutano umeisha hayo ni baadhi ya mambo yaliyojiri leo kwenye mkutano wa CUF.
Mungu ibariki CUF
Mungu ibariki Chadema
Mungu ibariki NCCR mageuzi
Na wafuasi wote wa UKAWA.
Pamoja na Wananchi wote wa Zanzibar na Tanganyika wenye kutambua ukweli kuhusu nchi zetu hizi.
 
Jua ni kali sana nataweka picha sasaivi inachewewa kuload hapa ni nyomi tu mkuu barabara zimefunga kote

Vipi mzee unaijua Pemba kijiografia ama kisiasa tu?
Gomban Kongwe imepitiwa na Barabara moja kwenda na Kurud na sio two way ni one way tu ambayo inaanzia mkoan mpaka Mpaka Makangale kule Vumawimbi.
So ukitoa habari wacha ushabiki uende vizuri!
Wapemba wenyewe tumo pia humu
 
jpg.gif
20141019_164317a1.jpg (1.23 MB)
 

Attachments

  • 20141019_164317a1.jpg
    20141019_164317a1.jpg
    396.9 KB · Views: 1,828
Gombani, 19.10.2014

Tunawashukuruni nyote muliojitokeza kuja kutusikiliza na kutuunga mkono katika harakati zetu za kuirejesha Zanzibar katika nafasi yake inayostahili katika muungano pamoja na kuipinga rasimu yenye lengo la kuibana zaidiZanzibar na mamlaka yake.

Tulichokieleza leo ni ukweli wa namna rasimu inavyotishia uwepo wa mamlaka ya Zanzibar na kuenda kinyume na maoni ya wazanzibari walio wengi waliochoshwa na mfumo mbovu unaopendekezwa.

Ni udanganyifu mkubwa kwa wananchi kuwaeleza kwamba rasimu iliopendekezwa imewapatia wazanzibari madai yao yote walioyataka. Ukweli ni kwamba kilichopendekezwa ni unyang'anyi wa wazi kwa Mamlaka ya Zanzibar kwa kutumia ghilba na hila na ni lazima kwa wananchi kuamka na kuikataa CCM kwa kushindwa kusikiliza vilio vyao hasa katika suala nyeti la Mamlaka yetu na nafasi yetu katika Muungano.

Rasimu iliopendekezwa imekiuka hata misingi mikuu ya Mkataba wa Muungano ambayo kwa uwazi na kwa nguvu za kisheria inatambua Mamlaka ya Zanzibar. Kutolewa kwa mafuta na gesi asilia katika masuala ya muungano ni uhadaifu kwa vile kilichowekwa kwa sasa ambacho hakikuwemo katika Mkataba wa Muungano ni suala la ardhi.

Utawezaje kuwa na uwezo wa kunufaika na Mafuta na gesi asilia ikiwa ardhi ulionayo imepokonywa na kutiwa katika kapu la muungano hasa ukizingatia udogo wa ardhi yetu na ongezeko kubwa la watu liliopo? Lazima wananchi tuikatae rasimu hii yenye lengo la kuibana zaidi Zanzibar na kutupora mamlaka yetu ya kujiongoza na kujikita katika maendeleo ya nchi na wananchi wetu.

Si kweli kwamba kuna msururu wa makampuni yaliotayari kuchimba mafuta kwa vile mafuta na gesi asilia yametolewa katika muungano. Zanzibar hatuwezi kuruhusu uchimbwaji wa mafuta bila ya kujua kwanza sheria na sera zipi zitakazotumika kuhakikisha neema hizi zinawanufaisha wananchi wetu na nchi yetu.

Lazima tuwe na chombo chetu wenyewe wazanzibari cha kushugulikia uchimbaji wa mafuta, ambacho kitakuwa na usimamizi mzuri utaohakikisha kila Mzanzibari ananufaika na mafuta na gesi, ikiwemo suala la ajira.

Uchaguzi ujao mwakani uwe ndio funzo kwa wale wote waliosaliti Zanzibar na wananchi wa Zanzibar kwa ushindi mkubwa kwa CUF ambayo itahakikisha Zanzibar na Mamlaka yake inalindwa vyema pamoja na kuiweka Zanzibar katika nafasi yake inayostahili katika muungano wa heshima, haki na usawa.

Tulioyashuhudia Dodoma katika mchakato wa katiba yatuzidishie mshikamano wazanzibari katika kuitetea nchi yetu na hili tutaliwafikisha pamoja kwa ushindi mkubwa wa pamoja wa kuikataa CCM na madalali wake.

Tunawasihi wahusika kutotuleta rasimu walioipendekeza na yenye maslahi nayo kwa vile umoja wetu, wingi wetu na mapenzi yetu kwa Zanzibar yatashinda dhambi za wasaliti wachache wasioitakia mema nchi yetu. Kwa hili Zanzibar imesimama pamoja kupinga njama na hujma juu ya mamlaka yake.

Vyema kwa wananchi kuhakikisha mwaka 2015 tunaing'oa CCM madarakani na tunarejesha heshima ya mamlaka yetu na nafasi yetu katika muungano utakaotupa usawa, haki na heshima. Hili litawezekana kwa ushindi mkubwa wa CUF na kuhakikisha tunashika uendeshaji wa serikali yenye manufaa na maslahi ya wazanzibari.

Ahsanteni.

Haki Sawa Kwa Wote.
 
Gombani, 19.10.2014

Utawezaje kuwa na uwezo wa kunufaika na Mafuta na gesi asilia ikiwa ardhi ulionayo imepokonywa na kutiwa katika kapu la muungano hasa ukizingatia udogo wa ardhi yetu na ongezeko kubwa la watu liliopo?

Wazanzibari mmemsikia Maalim SEIF? mjiandae kuondoka Soko la samaki feri na wazanzibari wote wanaovua samaki bara na kuuza samaki na pweza wajiandae kutimuliwa bara sababu ardhi si suala la muungano.Na wenye mashamba makubwa morogoro, pwani na mikoani wajiandae kukiona cha mtema kuni sababu kilimo na uvuvi si suala la muungano KWA mujibu wa CUF na msemaji wao Maalim SEIF.Wazanzibari hasa wapemba kinawaleta nini bara wakati mnajua hayo mambo si ya muungano?
Halafu Maalim SEIF mnafiki hivi yale mashamba yake kibaha anayamiliki kama nani wakati yeye si mtanzania bara na ardhi haiko kwenye muungano.?

Sera za CUF zitawaumiza wazanzibari.Hiyo ya kuweka ardhi kuwa jambo la muungano hasa ni kuwasaidia wazanzibari zaidi sababu ndio wengi wako bara wakijishuughulisha na kilimo na uvuvi lakini kama hawataki basi poa.Kila mtu abaki na ardhi na samaki wake arudi kwao.
 
Wazanzibari mmemsikia Maalim SEIF? mjiandae kuondoka Soko la samaki feri na wazanzibari wote wanaovua samaki bara na kuuza samaki na pweza wajiandae kutimuliwa bara sababu ardhi si suala la muungano.Na wenye mashamba makubwa morogoro, pwani na mikoani wajiandae kukiona cha mtema kuni sababu kilimo na uvuvi si suala la muungano KWA mujibu wa CUF na msemaji wao Maalim SEIF.Wazanzibari hasa wapemba kinawaleta nini bara wakati mnajua hayo mambo si ya muungano?
Halafu Maalim SEIF mnafiki hivi yale mashamba yake kibaha anayamiliki kama nani wakati yeye si mtanzania bara na ardhi haiko kwenye muungano.?

Sera za CUF zitawaumiza wazanzibari.Hiyo ya kuweka ardhi kuwa jambo la muungano hasa ni kuwasaidia wazanzibari zaidi sababu ndio wengi wako bara wakijishuughulisha na kilimo na uvuvi lakini kama hawataki basi poa.Kila mtu abaki na ardhi na samaki wake arudi kwao.

Usitutishe nyau.....wabara wako wengi zaidi znz wengine wameenda kwa mkumbo wa mwenge .
Wale wamasai wauza shanga nao vp ?
Na jeshi nalo wakurwa waondoke pia
Ardhi ya znz ni ndogo haiwezi kuwa huru kwa kila mtu.kama hili litafanya muwafukuze wapemba basi fanyeni haraka na nyie ondokeni tabu iko wapi
 
Usitutishe nyau.....wabara wako wengi zaidi znz wengine wameenda kwa mkumbo wa mwenge .
Wale wamasai wauza shanga nao vp ?
Na jeshi nalo wakurwa waondoke pia
Ardhi ya znz ni ndogo haiwezi kuwa huru kwa kila mtu.kama hili litafanya muwafukuze wapemba basi fanyeni haraka na nyie ondokeni tabu iko wapi

Seif ni kiongozi mmoja very selfish yeye anadhani kuongea hivo ndio atapata urais nakumbuka aliongea zaidi aya hivi kipindi cha salmin na kipindi cha aman kabla hajapewa tonge ..kawaambukiza hawa wapemba wenzake wamekuwa hawana tena uwezo wa kupambanua mambo kila analosema bwana mkubwa hewala . kuna vitu vingine huyu jamaa yuko sawa ila vingi sana yuko WRONG anasukumwa na masifa tu
 
.....duh CCM wanapigwa kila kona hii ni hatari sana,hivi hawaoni ishara hizi?
 
Hivi Dr. Shein akienda Pemba anaweza kupata hata nusu ya watu aliopata Maalim Seif?!

I can see Watangayika tunaweza kupata nchi yetu kupitia MGONGO wa WAPEMBA.
 
attachment.php


Wapemba Maalim Seif Shariff Hamad ni Nabii na Mtume huko Pemba hata akiwaambia jambo la kijinga wanalikubali hivi ardhi ikiondolewa katika muungano wazanzibar wanaozaliana kama panzi wataenda wapi ?.Wawaulize wenzao waKenya,na Rwanda wanavyolilia ardhi ya Tanzania utadhani fisi kaona mzoga.
 
'' Wapemba wanaweza maana wameshadhihirisha kuwa hawaitaki CCM tangu mwaka 1995 ila sehemu nyingine na mikoa mingine bado wanapigia kura Tshirt, Kofia na pilau''

Khalifa Bin Hemed 2001
 
Back
Top Bottom