Yaliyojiri mahakamani Mnyika vs Hawa Nghumbi case

Wakili:je,,matokeo yaliyoko kwenye form namba 21 ambayo ni ya matokeo ya jumla ya kwenye vituo yanayoonyesha ulipata kura 50544 unamashaka nayo?
Hawa:Sina mashaka nayo
Wakili:Kama huna mashaka nayo basi hakuna tatizo kwenye ushindi wa Mh.Mnyika
Hawa:sikulalamikia ushindi bali utaratibu

KWA NINI ASIUSHITAKI UTARATIBU AU TUME YA UCHAGUZI KWA KUWA NDIYO INAYOSIMAMIA UCHAGUZI?
KWA NINI AMSHITAKI MNYIKA KWA DAI HILI?

na mi bado nashangaa!
 
Lua: Siwezi kuchangia bila kukushukuru kwa juhudi zako za kuweka thread yenye maelezo marefu yaliyoko katika staili ya tamthilia........mbali na hayo nimecheka sana huyu Hawa kama alivyosema kiongozi mmoja Watu waitwao hawa ni balaa wana ghasia kweli
 
Nina wasiwasi na uwezo wake wa kufikiri huyu mama, naomba CV yake. There after apelekwe Elimu ya watu wazima akajifunze Lugha,Mapishi, nidhamu na utulivu,watu kama hawa ni JANGA KTK TAIFA. Shame enough
 
Hii ndio tz bana usikia nyingine fake,mbunge anataka kwenda bungeni akaongee kingereza cha kuokoteza kama alivyosema mwenyewe,inatia aibu sana tena sana sio kidogo aiseee.....sasa siku ya siku kwenye mijadala ya maana huyu ataongea nini??
 
Hahahaha kwa kweli inafurahisha , nitaiitumia hiyo conversation kama script nitengeneze a comedy show!
 
Ilianza hivi
1..DAI LA KWANZA KURA 14854 HAZIJULIKANI ZILIKOTOKEA WAKATI WA MAJUMUISHO
Wakili upande wa mlalamikaji;siku ya kutangaza matokeo ulikuwepo?
Hawa:Sikuwepo
Wakili:kwann hukuwepo kwenye kituo cha majumuisho?
Hawa:wakala wangu alikuwepo
Wakili:je ulisaini form ya matokeo
Hawa:Sikusain
Wakil:inatakiwa kama hujasaini ujaze form je ulisain?
Hawa:Wakala wangu hakupewa
Wakili:Aliomba?
Hawa:Hakuomba
Wakili:Je unafaham tofauti ya kura zako ulizopata na za mh Mnyika ni ngapi baada ya matokeo kutangazwa?
Hawa:ndio nafaham
W

Hapo kwenye nyekundu, huyu anayemuuliza Hawa ni wakili wa mlalamikaji au mlalamikiwa? Hii conversation haionyeshi kama ni mahojiano kati ya mlalamikaji (Hawa) na wakili wake. Otherwise huyo wakili anataka kumtosa mteja wake!
 
sasa dada Hawa,apa unamshtaki mnyika au tume ya uchaguzi?ccm bwn!
 
..mimi nadhani aliyeanzisha thread anatutania, sidhani kama ni kweli. Kama ni kweli tatizo ni kubwa kuliko tunavyodhani, anawakilisha wakuu wa wilaya, CCM na viongozi wake na wabunge wa CCM! Halafu kuna watu wanategemea CCM iwaandalie mipango ya maendeleo.....kwa aina hii ya watu
 
mama yangu wewe hivi hawa watu huwa hawapewi ushauri kabla ya kufungua kesi?


Mnyika mbunge mpaka 2015 OVA

Hawa anajua fika alishindwa kihalali lakini kwa kuwa ccm inapende kutumia vibaya kodi ya walala hoi ndiyo iliyofungua kesi.kesi hii ni sawa ya mh Lema nayo haina cha maana nikupoteza pesa na muda wa mahikumu kuamua kesi nyingine.
 
Makamba alimwingiza chaka huyu mama yeye makamba yupo busy kucheza na vijukuu moro na bumbuli
 
mama yangu wewe hivi hawa watu huwa hawapewi ushauri kabla ya kufungua kesi?


Mnyika mbunge mpaka 2015 OVA

Si waliambiwa na Katibu wao Makamba kuwa CCM ifungue kesi majimbo yote waliyoshindwa. Nafikiri strategy ilikuwa ni ku-pre empty kutenguliwa kwa wagombea wao waliopita kwa Chakachua. Sasa unpoambiwa ufungue kesi hata kama haipo haya ndiyo matokeo yake.
 
Matokeo ya kuchanganya mihimili ya dola. Nijuavyo mimi kabla kesi kwenda mahakamani DPP(kama ofisi) anatakiwa kujiridhisha kwamba kuna kesi ya kujibu kwa mujibu wa sheria. Hii ina maana polisi/mshtaki awe amemridhisha DPP(narudia tena kama ofisi) kuwa kuna kesi ya msingi ya kujibu. Sasa ukiangalia kwa majibu aliyotoa Dada/Mama Hawa ni kuwa kuna udhaifu mkubwa(wa makusudi, kutokujua au bahati mbaya) katika ofisi ya DPP katika kutayarisha kesi ziendazo mahakamani. Labda na ndiyo maana tunaona kesi nyinigi za msingi na hasa za ufisadi zinaishia kwenye kutupwa, na mara nyingi kwenye hatua za awali.

Hapa namaana chain(mtiririko) wa madaraka kwenye uongozi wa nchi uko blurred(??) sana.. Rais anateua Jaji mkuu, IGP, Mkuu wa majeshi, Wenyeviti wa tume zote, Ceremonial leaders (e.g. Mkuu wa Mkoa, Wilaya e.t.c) na titles zingine zoote muhimu hata bila kuwa queried(kuulizwa) na bunge!!!!! Unategemea hao wateule watatumikia mamlaka zao au Rais????

Lets be serious the system as it is will never work even for a 10,000 years! Period
 
dah! sasa nimeamini msemo wa politics is too important to be left to politicians. Yaani huyu mama nae angekuwa bungeni eti kama mtunga sheria wetu. Tayari tunae Lusinde, bibi Makinda, maji marefu, Siyoi nae anataka kuingia. Astagafirulahi this must stop now. Ni muhimu sana kuweka mchunjo wa nguvu watu wa design ya hawa watu niliowataja wasivuke kwenye kura za maoni ndani ya vyama. Hili si jambo la ushabiki wa vyama, Chadema vs CCM. Hapana, hii ni kwa ajili ya kuokoa taifa kwa maslahi ya kizazi cha sasa na kijacho. Unaweza kuamini huyu mama alipata kura zaidi ya 50,000, Ubungo?
 
Kimsingi huyu mama hana uwezo wowote, Hata huko Bukombe alikokuwa DC ilikuwa ni matatizo matupu. Ila tatizo ni huyu JK ndiye alilazimisha kupitishwa huyu mama kwa mizengwe sijui ana hisa gani naye. Mimi natokea JIMBO LA UBUNGO eneo la Makoka, niliwahi kusikiliza kampeni za huyu mama siku moja eneo la Makoka Mwisho hakuna chochote cha maana alichoogelea siku ile zaidi ya Mipasho. Washauri wake wote walikuwa wacheza taarabu.

Ifahamike kuwa jimbo makini na watu makini kwa Dar-es-Salaam ni Ubungo na linahitaji mtu makini sana. Kama inafikia wakati mpambe anakwambia fulani kakukashifu kwenye mkuntano wa kampeni hata bila kuangalia ratiba ya Tume kama siku hiyo kulikuwa na kampeni kwa aliyekukashifu hili nalo ni tatizo.

Wala msishangae ya mahakamani mkipata ya Bukombe akiwa DC mtalia.
 
MUCHETZ, Usichanganye mambo, hii kesi ni binafsi iliyofunguliwa na mtu binafsi na si polisi. Kesi binafsi haziendi kwa DPP kuziproof read kama zinafaa au la, ni hela yako tu. Na ndio maana kesi za mtindo huu ni sintofahamu.Mbaya zaidi wakili hawezi kumshauri mteja wake kuwa asifungue kesi, akihofia kukosa mshiko. Ingawa hapa hata wakili anaonekana bogasi pia.
 
Back
Top Bottom