Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,568
Dar es Salaam. Kesi ya wabunge wa viti maalumu waliofukuzwa uanachama katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na wenzake 18 dhidi ya chama chao hicho cha zamani imeanza kuunguruma mahakamani, baada ya kukwama mara tatu.

Mdee ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake wamefungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama.

Kesi hiyo iliyofunguliwa Mahakama Kuu Masjala Kuu, imeanza kusikilizwa leo Ijumaa Oktoba 7, 2022 na Jaji Cyprian Mkeha, ambapo mawakili wa Chadema wameanza kuwahoji walalamikaji hao kuhusiana na malalamiko yao.

Hatua ya kuwahoji baadhi ya walalamikaji inatokana na maombi ya mawakili wa Chadema wanaoongozwa na Peter Kibatala ambao waliomba siku ya kuanza usikilizwaji wa kesi hiyo wapewe nafasi ya kuwahoji walalamikaji wanane kati yao, akiwemo Mdee na wenzake saba.

Mbali na Mdee wengine walioitwa ni Nusrati Hanje, Ester Matiko, Ester Bulaya, Jesca Kishoa, Grace Tendega, Hawa Mwaifunga na Cecila Pareso.

Wa kwanza kuwekwa kikaangoni leo Ijumaa ni Tendega, aliyekuwa katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake wa chama hicho (Bawacha), ambaye amehojiwa na Wakili Kibatala anayeongoza jopo la mawakili wa Chadema.

Katika mahojiano hayo, Kibatala anamuuliza kuhusiana na madai au malalamiko yake kama alivyoyaweka katika kiapo chake, pamoja na mambo mengine akidai kufukuzwa uanachama bila kufuata utaratibu kwa kutokupewa haki ya kusikilizwa.

Hata hivyo, wakati Wakili Kibatala akimhoji Tendega kuhusiana na madai yake hayo, katika majibu mengine amekuwa akidai hajui huku mengine akikiri kuwa hajawasilisha mahakamani ushahidi hususani vilelezo kuthibitisha madai yake hayo.

Lakini pia amehojiwa kuhusiana na taratibu za ushughulikiaji matatizo ya wanachama wanaotuhumiwa ukiukwaji wa taratibu kanuni na katiba ya chama.

Pamoja na mambo mengine, wanalalamikia kuitwa kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu kwa njia ya WhatAsapp lakini alipopewa Katiba ya Chadema inatambua matumuzi ya tehema kama moja ya njia za mawasiliano.

Pia, amekiri hakuwahi kuandija barua kuwataka Katibu Mkuu, John Mnyika na mwenyekiti, Freeman Mbowe wasishiri kikao cha Baraza Kuu walikokata rufaa kupinga uamuzi wa kamati kuu kwa madai walioa kauli za kuwahujumu hata kabla ya vikao.

Kutokana na mahojiano hayo, shauri hilo limeahirishwa kwa saa moja kwa ajili ya maandalizi ya mahakama kuangalia vilelezo vya ‘flash disketi’ mbili kusikilizwa kauli walizozizungumza Mnyika na Mbowe ambazo wanazilalamikia.

Chanzo: Mwananchi

====

Mwenendo wa Shauri la HALIMA MDEE vs CHADEMA
Leo Ijumaa October 7,2022.


Jaji anaingia Mahakamani muda huu Saa 9:30 asubuhi...

Watu wote hapa Mahakamani wanasimama....

Kesi namba 36/2022
Halima James Mdee na wenzake/s CHADEMA inasomwa Leo Ijumaa October
7, 2022 hapa
Mahakama kuu
Mbele ya Jaji
Cyprian Mkeha..

Mh Jaji:
karibuni...

Anasimama Wakili wa Serikali...
Mh Jaji naitwa
Ayubu SANGA nipo wenzangu
Leonia Maneno
Stanley Kalokola
Wote tunamwakilisha washtakiwa watatu

Mh Jaji Naitwa
Kipilinga Panya nipo pamoja mawakili wasomi..
Aliko Mwamanenge
Emanuel Ukashu
Edson Kilatu
Matinde Wankashu
Kwa pamoja tuwawakilisha waleta Maombi Halima James Mdee na wenzake kumi nane..

Anasimama Peter Kibatala...
Ikupendeze Mh jaji
Naitwa
Peter Kibatala nipo wenzangu..
Hekima Mwasipu
Dickson Matata
Faraji Mangula
Deogratias Mahinyila
Selemani Matauka
Pamoja tunamwakilisha mjibu Maombi wa kwanza...

Badae pia tutaungana na Wakili Jeremiah Mtobesya

Wakili Serikali:
Mh jaji shauri ili limekuja Kwa ajili waleta maombi kuja kuhojiwa na mawakili wa wajibu maombi tupo tayari kuendelea.

Wakili Panya:
Mh jaji na sisi pia tupo tayari kuendelea na Waleta maombi Grece Tendaga na Hawa Mwaifunga wapo tayari kuhojiwa na mawakili wa wajibu maombi.

Mleta maombi namba mbili anaitwa Grece Tendaga anapanda kizimbani.

Jaji:
Majina yako

Shahidi:
Grece Tendaga

Jaji: umri wako

Shahidi: 57

Jaji: dini yako

Shahidi: mkristu

Jaji: utakula kiapo

Shahidi anaapa:

Wakili Kibatala: Majina yako ni Grece Tendaga

Shahidi: Ndio

Kibatala: Unakumbuka tarehe 18.7 2022
Ulikuwa wapi?

Shahidi: Mh jaji naomba unilinde nitakayosema hapa mimi nilikuwa kiongozi Katibu mkuu wa Baraza wa wanawake naomba mengine ya Siri nitakayosema unilinde!

Jaji: Ndugu mleta maombi hutakiwa kusema Chochote ambacho ambacho hujaulizwa na Wakili Kibatala.

Kibatala: Narudia tena tarehe 18.7.2022 ulikuwa wapi!??

Shahidi: Nilikuwa dodoma

Kibatala: Chukua hii fomu soma kumbuka upo chini ya kiapo!

Shahidi: Mh jaji naomba niseme..

Jaji: Huna la kusema soma ulichoelekezwa..

Shahidi anasoma
Nilikuwa Dar Nakula kiao kwenye moja ya ofisi.

Kibatala: Unakumbuka tarehe 29.7.2022 niliwapa nini hapa mahakamani..

Shahidi: Sikumbuki...Embu nipe nione..

[Shahidi anasoma]..Mheshimiwa jaji nimeona, ni nyaraka..

Wakili Panya anasimama: Mh naomba Wakili Msomi Kibatala anamuliza maswali yako nje..

Jaji: Nadhani mtafafanua badae.l

Kibatala: Mh jaji nayetajikiwa kujibu ni mteja ndio sheria inasema hivyo!

Kibatala; Unakumbuka tarehe 7.11.2020 wewe na wenzako mlihudhuria kikao Cha Kamati kuu!..

Shahidi: Nakumbuka

Kibatala: Na mnakumbuka wewe na Halima Mdee mlilikiri mbele kiapo Cha nyongeza kuudhuria kikao hicho?

Shahidi: Nakumbuka

Kibatala: Mnakumbuka wewe na wenzako baada kula kiapo CHADEMA walipinga!

Shahidi: Nakumbuka

Kibatala: Unakumbuka mlialikwa Kamati kuu November 25.11.2020?

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Unakumbuka yote uliandika hapa kwenye fomu hii unayakumbuka?

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Katika kiapo chako Aya ya 7 unakumbuka ulimtaja Mtu anaitwa John Komba?

Shahidi: Nakumbuka Kuna aya nilimtaja kijana wa Bavicha Aitwa Jonh Komba ila sikumbuki vizurii

Kibatala; kwenye Aya 7 ya kiapo hicho Jonh Komba unakumbuka maelezo John Komba!

Wakili Panya anaingilia: Mh jaji Shahidi kasema hakumbuki Wakili anamlazimisha!

Kibatala: unakumbuka kiapo chako ulisema Kuna flashi uliyoileta iliyotengenezwa na John Mnyika mahakamani kama ushaidi ulikuwepo wakati unayengenezwa!

Shahidi: sikuwepo

Wakili Panya anasimama: Mh jaji Wakili Msomi Kibatala
Anamuliza maswali IT mteja wangu ambaye sio mtaalu wa maswala ya IT

Jaji: Wakili Panya Sasa unataka haya maswali nani ajibu? Wakati shahidi yupo chini ya kiapo? Kuna mtu mwingine wa kujibu?

Wakili Panya: Mh jaji yupo

Jaji: Wapi?

Wakili Panya: Kimya

[Mahakama kicheko🤣🤣🤣🤣🤣]

Kibatala: Kwenye hiyo flashi uliyoileta kama kielelezo Kuna sauti ya John Mnyika aliwambia vijana waandamane?

Shahidi: ziponflash nyingi ila siwezi kukumbuka..

Kibatala: Wakati Mnyika anawapa wito kuudhuria kikao kamati kuu Cha November 27, kwenye hiyo Kuna huo wito..?

Shahidi: haupo

Kibatala: Nakusogelea Nakuonyesha kiapo chako.. tarehe ngapi Mnyika aliwapa wito kuudhuria kikao kamati kuu

Shahidi: November 25,2020

[Wakili Kibatala ananongenezana Wakili Mataka!]

Mh jaji: Kwa Nini upande wa waleta maombi mna wasiwasi sana na maswali..? Jibuni tu.

[Mawakili wote Kicheko...]

Kibatala: Ni sahihi kuwa Barua ya wito wewe na wenzako ililetwa kwenu Kwa njia WhatsApp?

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Hiyo Barua ya wito ya Kikao November 25 sio?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Kwenye kiapo chako ulitaja namba ya simu?

Shahidi: Sikutaja

Kibatala: Msingi wa Kesi hii ni kuwa wewe ulipata barua ya wito kuudhuria kikao kamati kuu Kwa njia zisizo HALALI za WhatsApp?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Nakuonyesha KATIBA ya CHADEMA..

Kibatala: Msomee Jaji sura ya tano ibara sita..

Shahidi inasoma: Katiba ya CHADEMA inatambua matumizi ya TEHAMA..

Kibatala: Nakuonyesha sehemu ya Katiba 6:3 ya Katiba inatambua matumizi yote ikiwemo Barua pepe kama njia ya mawasiliano!

Shahidi: Natambua lakini Kuna changamato..

Kibatala: Ulitunza kumbukumbu za mawasiliano ya simu yako juu nyaraka hiyo? Soma Katiba kuhusu kutunza kumbukumbu..

[Shahidi anasoma..Kisha anaendelea]...Mheshimiwa jaji, Wakili Msomi anapotaka kunipeleka siko maana ananiuliza mamba ya simu mwaka 2020 kumbuka Simu zinapotea

Kibatala: Hiyo simu ulimkabidhi mh jaji?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Tuhuma ulizoleta kuhusu Barua zilikiuka msingi wa katiba ya Chama?

Shahidi: Kweli

Kibatala: Soma katiba ibara ya 7.7.16 ili mahakama iridhike

Kibatala: Kwenye kiapo chako Aya 16 inasema kuwa Barua ya kamati kuu ya CHADEMA inasema kulikuwa na madai mapya ilileta madai mapya tofauti na yake ya awali ya kuwafukuza nyie uanachama?

Shahidi: Naomba nisome Sehemu ya Pili

Kibatala: Katika Barua hii Aya 16 mnasome ipo kinyume ndio hii?

Shahidi: Ndio hii

Kibatala: Ni sahihi kuwa Barua hiyo iliyofukuza nyie ilikiuka ibara ya Katiba 7.7.1 Q

Shahidi: ndio

Kibatala: Katika Barua yenu mmasema kuwa Kuna tuhuma mpya nyie kufukuzwa ni zipi?
Kwa mujibu ya Barua 30.11.2020...somee mh jaji!

Shahidi: Barua hii ilitutaka kufika mbele ya kamati kuu ili kujibu tuhuma za mimi kuapishwa kuwa mbunge wakati ukijua kinyume katiba ya Chama. Na hii ya November 30 Niya kutaarifiwa kuvuliwa uanachama. Na Barua ya November 25 ilikuwa ni wito wa kufika kwenye kikao kamati kuu bahari beach ili kujibu tuhuma kushiriki tuhuma kula njama kujiapisha...

Kibatala: Barua ya November 25 ilikutuhumu kosa Gani!?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Na Barua November 30 ilitekeleza ibara ya Katiba 7.7.16

Shahidi: Ndio lakini kuna mambo yalikiukwa kufikia hatua hiyo

Kibatala: Katika kipapo chako Aya 12 umasema Haki yako ilikiukwa?

Shahidi: Embu nione.. Ndio

Kibatala: Umasema ilipata wito kuudhuria kikao kamati kuu November 25, 2020 Kwa njia WhatsApp na ulikuwa dodoma?

Shahidi: ndio

Kibatala: Kuna kielelezo chochote ulitoa Kwa jaji kuwa ulikuwa Dodoma?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Uliandika barau yoyote kuhusu kutohudhuria kikao iwe Kwa Katibu mkuu wa chama au Mkt Mbowe?

Shahidi: Sikuandika

Kibatala: Ni sahihi kuwa wajumbe wa kamati kuu wametajwa na kwenye katiba ya Chama!

Shahidi: ni sahihi

Kibatala: Ulikuwa unafahamu kuwa Haki Haki wewe kuwambia mkt na katibu wajitoe?

Shahidi: Mimi najua unataka kwenda wapi

[Mahakama kicheko🤣🤣🤣🤣🤣]

Kibatala: Ni kweli kwenye Barua ya November 25 ilikutaka ufike Makao makuu ya CHADEMA Kwa ajili kupewa maelezo zaidi?

Shahidi: Naomba nione

Shahidi anasoma... Kweli!

Kibatala: Kwenye hiyo Barua Kuna sehemu inasema kuwa kikao Cha Kamati kuu kitafanyika Makao makuu ya CHADEMA?

Shahidi: Kwenye barua haipo ila kwenye Simu IPO..

Kibatala: Ni sahihi kuwa Barua November 26 ilikutaka kufika baada ya wewe kujibu ile Barua ya November 25 ni kweli sio kweli?

Shahidi: Ni kweli Barua November 26 2020

Kibatala: Ambacho kielelezo namba ngapa?

Shahidi: Namba 4

Kibatala: Soma Barua ya November 26

Shahidi: Napenda kukuarifu kuwa kufuatia ombi la kuhusu usalama wako nakuarifu ufike kwenye kikao kamati kuu Bahari beach November 27.

Kibatala: Wewe Barua ya Mnyika ya November 26 uliipata tarehe ngapi?

Shahidi: Niliipata tarehe 27 November 2020 saa Saba mchana.

Kibatala: Ni wapi mh jaji atangalia ili ajue kuwa wewe ulipata Barua November 27

Shahidi: Hakuna sehemu sikuambatanisha kama kielelezo

Kibatala: Ulijibu lini?

Shahidi: Nilikiwa najiandaa kujibu napata taarifa kuwa nimefukuzwa uanachama

Kibatala: Kwa ruhusu mahakama naomba nikuonyeshe rufaa yenu wewe na wenzako kuwa Barua ya November 26 ilikufikia November 27 saa Saba mchana

Shahidi: Haipo

Kibatala: Kuhusu kiapo chako ni Kuna sehemu unasema kuwa maneno Freeman Mbowe Kuna maneno aliyatoa

Shahidi: Ndio

Kibatala: Kwa mujibu kielelezo namba 8 kuhusu flash Kuna maneno aliyatoa Freeman Mbowe yapo humu?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Unakumbuka 9.8.2022 nyie wote Kwa pamoja mlikula kiapo Cha kujibu kiapo hati kinzani Cha CHADEMA?

Shahidi: Sikumbuki

Kibatala: Umeelewe swali!

Shahidi: Naomba nione?...Shahidi anasoma..

Shahidi: Tulikula kiapo

Wakili Kilatu: Mh jaji tunaomba kielelezo chochote kabla ya kwenda Kwa shahidi tukione

Jaji: Wakili ina maana nyie hamuwasiliani hapo na Wakili Panya kama nyaraka ya uongo shahidi atasema!

Kibatala: Nyie wote 19 mlikula kiapo je unafahamu hii soma hapa ..

Shahidi anasoma.. rufaa na kukuri kuitambua

Kibatala: Hiyo ndio nyaraka uliyosema kuitambua kwenye kikao Cha Baraza kuu Mei 11, 2022?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Shahidi majibu ya CHADEMA ya rufaa yenu mliyaona?

Shahidi: Sijayaona

Kibatala: Moja ya tuhuma zenu kuwa Baraza kuu la CHADEMA lilifanya maamuzi bila kuwasikiliza?

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Unakumbuka awali nilikuonyesha nyaraka ya rufaa yenu?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Unakumbuka pia ulisoma?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Ni sahihi kuwa katika rufaa yenu mliyopeleka Baraza kuu hoja zilikuwa zipo 9?

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Sasa unaposema ukusikilizwa ni ipi?

Shahidi: Kwenye kikao cha baraza kuu lao Kilichofanyika wajumbe wa Baraza hawakutohoji tulipewa karatasi ya rufaa tukaulizwa hii basi hatukurudi tena

Jaji: Msijali mtarudi tena usihofu

[Mahakama kicheko🤣🤣🤣]

Kibatala: Kwa mujibu wa katiba ya Chama ni ibara ya ngapi inasema wajumbe wa Baraza watawahoji? Na wewe ulikuwa kiongozi wa chama?

Shahidi: Hakuna.. Unajua wewe ni Wakili mwanasheria mkuu wa chama ndio maana

[Mahakama kicheko🤣🤣🤣🤣]

Kibatala: Mh tupate break kidogo tujadiliane wenzangu

Jaji: Muda gani?

Wakili Panya: Baada saa moja

Jaji: Tutarudi saa 7:15 chana

Mahakama imerejea...

Kesi namba 36/2022 Halima Mdee na wenzake 18 dhidi ya CHADEMA

Wakili Serikali:
Ikupendeze Mh jaji tuko vile kama awali..tuko tayari kuendelea

Wakili Panya: Mh jaji nasi pia tuko vile vile.. nasi tuko tayari kuendelea

Wakili Kibatala: Mh jaji Kwa upande wetu ameongezeka Wakili Msomi Jeremiah Mtobesya

Mh jaji: Wakili Kibatala

Kibatala: Wakati shauri linahairishwa tulipata muda kupitia vielelezo Kwa ruhusu yako tunaomba flash iwekwe kwenye TV

Jaji: Mh Panya natumaini huna pingamizi na ombi la mh Kibatala

Wakili Panya: Sina tatizo ila naomba shahidi apatiwe kiti akae kizimbani

Jaji: Hakuna tatizo

Sasa TV imewashwa mahakamani..Flashi imewekwa.

Kwenye TV natokea KM Mh John Mnyika anakitoa wito Kwa Halima Mdee na wenzake kufika Makao makuu ya CHADEMA November 27, 2022 Kwa ajili taratibu nyingine..

Kielelezo kilicholetwa kinaongea sekunde 3 kinazima.

Jaji: Mtaalumu wangu wa TEHAMA ananimbia nimpe muda mfupi walau dk 5 ili aweke mitambo yake sawa

Sasa TV imewashwa mahakamani.. Flashi imewekwa. Fundi mitambo kaja na waya mrefu kama mnara wa babel..Anaseti mitambo Haya mitambo imekaa sawa...

KM Mnyika anaanza : Jambo hili linahusishwa mfumo mzima wa NCHI Kuna mashaka.. Swali la kujiuliza lini Katibu mkuu wa chama alisaini fomu na 8D? Pia Kuna mwanachama wetu Nusrat Hanje alitolewa gerezani usiku ili akale kiapo bungeni.. Spika Ndugai anasema alipokea majina ya wabunge viti maalumu kutoka tume ya uchaguzi November 20,2020 wakati Hanje yupo gerezani. Ndugu wanachama nataka niwatoe hofu hakuna majina yoyote yaliyopelekwa bungeni..

Kuna waliopishwa wengine ni viongozi wakuu na wajumbe wa kamati kuu wanajua chama hakijateua majina.


Jaji; imefika mwisho ni sawa?

Kibatala: Ndio Mh Jaji

Kibatala: Shahidi hii flashi ndio tulizungumzia Toka asubuhi?

Shahidi: Ndio, lakini Mh Jaji tulichukua kipande hicho Cha Kwa vile tuliona kina athari Kwetu na Kwa jamii

Kibatala: Unakubaliana kuwa CHADEMA kina wanawachama NCHI nzima?

Shahidi: Ndio

Kibatala: Unafahamu kuwa nyie kula kiapo ilileta taharuki Kwa wanachama?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Kwenye flashi Umesikia Mh Mnyika akisema atapokea maoni ya watu?

Shahidi: Nimesikia.
TV imewashwa tena kipande cha KM aliongea kuwalika wadau watoe maoni juu hatua za kuchukua

Kibatala: Kwenye hiyo video flash Kuna mtu mwingine kaongelewa Aidani?

Shahidi: Ni kweli

Kibatala: Unafahamu Aidani?

Shahidi: Sifahamu

Kwa chini huku waliofukuzwa uanachama wanaongea Kwa sauti...

Jaji: Naomba wazungumzaji mmekuwa wengi wazungumzaji humu ndani ni Wakili Kibatala na Shahidi tu..

Shahidi: mh jaji naomba unilinde maana Wakili anaongea mambo mengi...

Jaji: mm naandika hapa kuwa na amani..

Kibatala: Kwani walipeleka maoni yalipokelewa?

Shahidi: sijui

Kibatala: Kwani uamuzi ulikuwa unafanywa na watu au kamati kuu?

Shahidi: Kamati kuu

Kibatala: Maoni ya watu yalidhuru nini?

Shahidi: Huyu alitoa kauli ni Katibu mkuu wa chama Kwa nini asitumie wajumbe wa kamati kuu?

Kibatala: Unafahamu mjumbe yoyote wa kamati kuu?

Shahidi: Simfahamu

Kibatala: Unafahamu COVID-19 iliyoko kwenye kiapo chako?

Wakili Panya: Mh jaji sijui hayo maneno yanatoka wapi? Wakili anamlisha maneno shahidi.

Jaji: Kwa vile ana kiapo hapo Wacha atusomee...

Shahidi anasoma...

Jaji: Mh Kibatala kwa usiache ikatumika mwishoni

Kibatala: sawa mh Jaji

Kibatala: Tunaomba tuwekee flash hotuba ya Mh Mbowe

Hotuba ya Mh Mbowe inawekwa.... Hotuba ya Mh Mbowe ni fupi

Nukuu: Chama chetu hakijawahi kuteua majina ya wabunge viti maalumu.

Shahidi: Kwenye kielelezo chako Kuna maneno ujaweka? ndio maana nimeweka.....

Kibatala: Unakumbuka unachofanya?

Shahidi: Nasoma kiapo ukurasa wa 3 na 4...

Kibatala: Unawafahamu wadhamini wa CHADEMA?

Shahidi: Ndio ila Lazima wawe wadhamini walioapa

Kibatala: nani ambaye unajua ambaye sio mdhamini ambaye hajala kiapo?

Shahidi: wote

Jaji: Naomba shaidi utoe sauti naona muda uvyoeenda sauti yako inakata

Kibatala: Nani alikwambia hawa wadhamini CHADEMA hawajala kiapo au ulienda Kwa msajili tuambie tu sisi mawakili tutajuaa!

Shahidi: Hiyo ni akili yangu nimejua

Mahakama kicheko🤣🤣🤣

Kibatala: kwenye kiapo chako Kuna sehemu umeonyesha akina Shaban Othumani, Ramadan Nyangoro, Mozek Ramadan Wenzake uliwahi kula kiapo kinzani kukupinga?

Shahidi: Sikuelewi

Wakili Panya: Mh Jaji narudia tena Wakili Kibatala anamlisha maneno shahidi..

Jaji: Hapana shahidi anasema arudiee swali napenda namna shahidi anasema hajaelewa swali ili kutoa nafasi

Wakili Panya: Naomba Wakili Kibatala amsadiee shahidi maana shahidi anatafuta kusoma..

Kibatala: Mm nauliza swali kutokana kiapo chao

Kibatala: Kwa mujibu KATIBA ya CHADEMA 7.7.11 wajumbe wote Kamati kuu ni wajumbe pia Baraza kuu?

Shahidi: Ndio kabisa

Kibatala: Mh ndio hayo tu

Jaji: Kwa kuangalia muda mnaweza kuendelea muda huu?

Wakili Panya: Nina maswali kadhaa ngoja tushauriane wenzangu

Wakili Panya: Tumeteta hapa na wenzangu tumekubaliana tufanye October 13,2022

Jaji: nahirisha shauri hili hadi October 13, 2022
saa 3 kamili Asubuhi Kwa ajili kuendelea shahidi huyu.

Asanten tukutane October 13

KATIBA YA CHADEMA
 

Attachments

  • KATIBA CHADEMA 2016.pdf
    21.2 MB · Views: 12
Hii nia ya Kibatala na wenzake kuwagonga maswali hawa jamaa inaweza kuwaacha hoi mwisho wa siku wajione wameshindwa wenyewe kesi mapema.

Naamini hata haya maswali wanayoulizwa sasa, most likely wangeulizwa kwenye "cross examination", sasa kama ukifika wakati wa "cross examination" wakaulizwa maswali mengine mapya, basi jamaa zangu watafika siku ya mwisho wakiwa wamechoka sana.
 
Ukurasa wa mbele wa Gazeti la Raia Mwema la Jumamosi Oktoba 8, 2022, habari kubwa ni ya wabunge Halima Mdee na wenzake kuhusu sakata la kesi yao ya ubunge.
5ba2d0b5-7753-45c2-9193-b6c247f68cc4.jpg
 
Je hii kesi haiwezi ikaoneshwa moja kwa moja kutoka mahakamani? Je kuna watu waliruhusiwa kufuatilia mahakamani!
Hata mimi imenishangaza kidogo juu ya CHADEMA nao walivyoichukulia hii kesi iendeshwe kimya kimya!

Hata hapa JF ni kama inakuja kinyemela vile, tofauti kabisa na hali iliyozoeleka kwa jambo kama hili.

Sijui, pengine ni katika mipang iliyokubaliwa kwenye mazungumzo ya "maridhiano", maanake naona mabadiliko makubwa sana jinsi CHADEMA inavyofanya mambo yake siku hizi.
 
Baada ya hawa wanafuatia Ndugai na Mahera
Mkuu 'Erythro', hata wewe hukuwa na taarifa wa uwepo wa kesi hii mahakamani leo? Maana imekuwa kama kawaida yetu kukutegemea kwa mambo kama haya yanapotokea.
Ama kuna onyo mlilopewa kichama; maanake hali imekuwa tofauti sana siku hizi.

Silaumu, naeleza tu ninayoyaona binafsi.
 
Dar es Salaam. Kesi ya wabunge wa viti maalumu waliofukuzwa uanachama katika Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Halima Mdee na wenzake 18 dhidi ya chama chao hicho cha zamani imeanza kuunguruma mahakamani, baada ya kukwama mara tatu.

Mdee ambaye alikuwa mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chadema (Bawacha) na wenzake wamefungua shauri hilo Mahakama Kuu Masjala Kuu, wakipinga kufukuzwa uanachama.

Kesi hiyo iliyofunguliwa Mahakama Kuu Masjala Kuu, imeanza kusikilizwa leo Ijumaa Oktoba 7, 2022 na Jaji Cyprian Mkeha, ambapo mawakili wa Chadema wameanza kuwahoji walalamikaji hao kuhusiana na malalamiko yao.

Hatua ya kuwahoji baadhi ya walalamikaji inatokana na maombi ya mawakili wa Chadema wanaoongozwa na Peter Kibatala ambao waliomba siku ya kuanza usikilizwaji wa kesi hiyo wapewe nafasi ya kuwahoji walalamikaji wanane kati yao, akiwemo Mdee na wenzake saba.

Mbali na Mdee wengine walioitwa ni Nusrati Hanje, Ester Matiko, Ester Bulaya, Jesca Kishoa, Grace Tendega, Hawa Mwaifunga na Cecila Pareso.

Wa kwanza kuwekwa kikaangoni leo Ijumaa ni Tendega, aliyekuwa katibu Mkuu wa Baraza la Wanawake wa chama hicho (Bawacha), ambaye amehojiwa na Wakili Kibatala anayeongoza jopo la mawakili wa Chadema.

Katika mahojiano hayo, Kibatala anamuuliza kuhusiana na madai au malalamiko yake kama alivyoyaweka katika kiapo chake, pamoja na mambo mengine akidai kufukuzwa uanachama bila kufuata utaratibu kwa kutokupewa haki ya kusikilizwa.

Hata hivyo, wakati Wakili Kibatala akimhoji Tendega kuhusiana na madai yake hayo, katika majibu mengine amekuwa akidai hajui huku mengine akikiri kuwa hajawasilisha mahakamani ushahidi hususani vilelezo kuthibitisha madai yake hayo.

Lakini pia amehojiwa kuhusiana na taratibu za ushughulikiaji matatizo ya wanachama wanaotuhumiwa ukiukwaji wa taratibu kanuni na katiba ya chama.

Pamoja na mambo mengine, wanalalamikia kuitwa kuhudhuria kikao cha Kamati Kuu kwa njia ya WhatAsapp lakini alipopewa Katiba ya Chadema inatambua matumuzi ya tehema kama moja ya njia za mawasiliano.

Pia, amekiri hakuwahi kuandija barua kuwataka Katibu Mkuu, John Mnyika na mwenyekiti, Freeman Mbowe wasishiri kikao cha Baraza Kuu walikokata rufaa kupinga uamuzi wa kamati kuu kwa madai walioa kauli za kuwahujumu hata kabla ya vikao.

Kutokana na mahojiano hayo, shauri hilo limeahirishwa kwa saa moja kwa ajili ya maandalizi ya mahakama kuangalia vilelezo vya ‘flash disketi’ mbili kusikilizwa kauli walizozizungumza Mnyika na Mbowe ambazo wanazilalamikia.

Chanzo: Mwananchi
Suuh
 
Je hii kesi haiwezi ikaoneshwa moja kwa moja kutoka mahakamani? Je kuna watu waliruhusiwa kufuatilia mahakamani!
Ingewezekana wakodi jamaa wa Citizen TV Kenya, waje wawape uhondo wote, manake Tv zote Tz naona wanaogopa siasa siku hizi, wasije fungiwa........ kazi iendelee
 
Back
Top Bottom