Yaliyojiri kutoka Diamond Jubilee Dar: Mkutano Mkuu wa Chama cha NCCR Mageuzi, Yeremia Kulwa Maganja ateuliwa kuwania Urais Tanzania

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,987

Heshima kwenu Wakuu,

Leo nccrmageuzihq Wanafanya MKutano Mkuu ambao unafanyikia katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Jijini Dar Es Salaam. Mwaka huu NCCR wamejipanga kushiriki Uchaguzi mkuu wa mwezi Oktoba kikamilifu.

Dira na Madhumuni ya NCCR ni Kuwa chama chenye nguvu kinachofuata itikadi ya UTU, kinachoongoza taifa na kanda (ndani ya Afrika) kwa mawazao tokevu ya kimaendeleo ili kurejesha na kuendeleza ustawi wa jamii, haki, na mafanikio ya mwanadamu.

Kauli Mbiu ya NCCR ni Utu, Ambayo Misingi Yake Ni Udugu, Maadili, Usawa, Haki, Imani, Mabadiliko, Uhuru, Wajibu, Asili, Kazi Na Endelezo.

Nitawaletea kile kinachojiri kutoka Ukumbi wa Diamond Jubilee.

Stay Tuned
===


UPDATES:

Tayari Viongozi wakuu na Wanachama mbalimbali wa NCCR Mageuzi wameingia mkutanoni kwa ajili ya tukio la leo. Tazama baadhi ya picha kutoka ukumbini hapa chini:
1596784871442.png

1596784910350.png

Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi - Antony Kalist Komu
Ngungu zangu kazi yangu leo ni ndogo sana kwa sababu kama mnavyojua swala la kutinia nia limeshika kasi kwelikweli katika nchi yetu ukifungua kila chombo cha habari watia nia watia nia.

Sisi tuliokaa kwenye siasa kwa muda kidogo ukikutana na watu wanaokufahamu unaulizwa hujatia nia, kwa hiyo na leo sisi NCCR tunaingia kwenye ukurasa huo kwenye ngazi ya juu kabisa.

Kwa hiyo ndugu yangu Abubakari Juma Abubakari nikukaribishe katika huu mtindo unaoendela sasa na wewe uwe mmoja katika hii historia hivi na niseme jambo moja dogo kabla sijafanya hiyo kazi ambayo ndugu Abubakari amesababisha tuwepo hapa sasa hivi.

Niseme kihistoria chama cha NCCR Mageuzi ndicho chama mama wa mageuzi katika nchi hii 1995 ndio tulikuwa na uchaguzi wa kwanza katika nchii hii na NCCR tulishiriki katika huo uchaguzi na tulifanya vizuri katika uchaguzi huo tuliweka mgombea urais na tulipata asilimia 47 % kura zaidi ya milioni moja na laki nane kwenye ngazi ya urais na ndio tulianya vizuri kuliko vyama vyama vyote vya upinzani.

Mwaka 2000 hatukuweka mgombea na kama mnakumbuka sababu zilizotusababisha hazikuwa sababu za ndani ya chama ila tulisababishiwa na wapinzani wetu.

Mwaka 2005 tuliweka mgombea mnamkumbuka sana marehemu dr. Sengondo Mvungi ndie aliyetuwakilisha na kwa hoja bado tuliendelea kuwa mama wa mageuzi.

Mwaka 2010 tuliweka mgombea ndugu Hashimu Rungwe na mwaka 2015 tulikuwa na mchakato wa katiba mpya na ukifatilia historia katiba mpya ni agenda ya kudumu ya NCCR mageuzi na tuiingia kwenye umoja wa katiba UKAWA na mnajua mafanikio tuliyoyapata.

Mwaka 2020 kama alivyosema Edwaard Simbeye tumeamua kuingia kwa sababu zipo agenda ambazo kama mama wa mageuzi tunataka kuziendeleza na zibaki kama agenda kwenye uchaguzi huu.

Kwenye ubunge kuna watu wameshataka kutia nia kama 230 na kwenye udiwani ni wengi zaidi ya 3000 na kwenye ngazi ya Urais tunaye ndugu Abubakari Juma Abubakari na kwa umri wake sina wasiwasi nae na siamini kama amekuja kujitangaza na kuongeza cv

Naamini ndigu Abubakar anania ana agenda na ana kitu anataka kufanya kwenye uchaguzi huu na sisi tupo pamoja kukuunga mkono kwenye agenda yako hiyo na Mungu akijaalia utakuwa mgombea kupitia NCCR.

Ndugu Abubakari na watanzania wote jambo la uchaguzi ni jambo kubwa sana linaweza kuamua mstakabari wa baadae wa nchi yetu iendelee kuwa na amani au tuingie kwenye mfarakano kwa hiyo nikuombe sana chama chetu tuna katiba tuna kanuni na mambo mengine

Itikadi yetu ni itikadi ya utu misingi yake ni undugu, maadili, usawa, haki, imani , mabadiliko, uhuru, wajibu, asili kazi na endelezo

ACT - Juma Duni Haji Makamu mwenyekiti Zanzibar

Mimi ndugu Mbatia ni mwana siasa mwenzangu kwa zaidi ya miaka 20 na falsafayake ya mama Tanzania, tatizo langu mimi huyu mama Tanzania asigeuke mama wa kambo ikawa watoto wengine wazuri wengine wabaya, Na sisi wengine ndio kinachotusumbua kwamba mama Tanzania wengine anatutenga ila nashukuru mmetualika.

Nimefurahi kwamba mkutano umefana na uwakilishi umeenea mikoa yote na kwamba hiki chama cha asili mageuzi yalianzia hapa na kimeweka wawakilishi maeneo mengi nchi nzima.

Mzee Butiku wakati wanaoongoza nchi hii pamoja na mwali walikuwa wanadai uhuru na walidai uhuru kwa kuwa utawala uliokuwepo ulikuwa unawaonea mababu zetuu mimi nilikuwa nasoma

Uhuru una daraja tatu, wa kwanza ni kuondoa utawala wa kigeni tulikuwa Zanzibar tunatawaliwa na waarabu na huku Tanganyika tulitawaliwa na Wajerumani na waingereza sasa hawapo 1961 na baadae Zanzibar na Tanganyika waliungana na babu zetu waipigana ili sisi tuishi maisha ya heshima, maisha ya uhuru, maisha yenye salama, maisha ya kupendana maisha ya kujua kwamba sisi sote tuna haki hiyo ndio ilikuwa kusudio lao.

Ya pili Uhuru wa kukusanyika tukafanya maamuzi kama tunavyotaka, kukosoa, kutoa maoni kushauri hilo ni la pili na tatu ni kuwa na uwezo wa kauli unasimamiwa na uchaguzi wa demokrasia uchaguzi wa kwenda kwenye sanduku la kura kusema huyu tunamkubali na huyu tunamkataa na atakaechaguliwa anaambiwa wewe tangulia utuongoze na baadaya miaka mitano tunarudi tena kuchagua.

Tunakwenda kuchagua viongozi katika uchaguzi ujao tunachoomba wale waliopo kwenye madaraka watuache tuchague kiongozi tunayemtaka na atakaye shinda aachwe aongoze.

Sasa ndugu zangu umoja utu na mashirikiano kama mnatumbuka tulikuwa na UKAWA tulifanya vizuri kama vyama vya upinzani na tunajua kama kuna chama wanaumia ni chama cha NCCR na machungu mnayopata yana mafanikio. Hakuna kupata kama hujaumia sis ACT tunaamini katika ushirikiano

Na ili tuweze kukishinda chama tawala lazima tushirikiane kwa hiyo katika harakati zenu mkumbuke hilo. tunahitaji mabadiliko na mabadiliko makubwa ni kulinda utu wetu na tunahitaju kuheshimiwa kama watanzania na tunahitaji kuwa huru bila woga ndani ya nchi yetu.

Joseph Roman Selasini kwa niaba ya wabunge wastaafu

Ndugu zangu kwa wale vijana nataka niwakumbushe jambo mlio hapa ndani na mlio nje tarehe 11/06 1991wana mageuzi tulikutana katika ukumbi huu tukiidai serikali mageuzi na baada ya mkutano ule vilizaliwa vyombo viwili cha kwanza NCCR (Baraza la kitaifa la kutafuta marekebisho ya katiba ) kwa hiyo wanaosema agenda ya katiba ni yao wanakosea imeanza siku nyingi iko katika mioyo ya watanzania na wana mageuzi.

Na cha pili kiliitwa KAMAHURU nacho kilikuwa kwa ajili ya kupigania mabadiliko ya katiba upande wa Zanzibar, nimefurahi mkutano huu umefanyika hapa kwa sababu ni kama tunaamsha uhai wa mageuzi na watanzania watambue kuwa wana mageuzi bado tupo na bado tunaendelea.

Upinzani sio uadui na hatuna sababu ya msingi ya kugombana wenyewe kwa wenyewe au hata na chama tawala na kwa kuwa anaegombana au kutumia mabavu ameishiwa hoja na mara nyigi wanyama ndio hufanya hivyo lakini wenye hoja hupambana kwa kupambanisha hoja zao. Na NCCR hatutasita kusema kuwa hoja hii ya ACT ni hoja ya msingi tuibebe na kuiunga mkono pia haisiti kusema hoja hii ya CHADEMA ni hoja ya wananchi iungwe mkono na hivyohivyo hata kusema jambo hili lililofanywa na serikali ni jambo jema liungwe mkono.

Na sababu ni moja tu vyama hivi ni taasisi za watanzania ni taasisi za umma na vyama hivi ndivyo hutoa viongozi na wa nchi na wataalam wake wanatengeneza sera zinazouzwa kwa watanzania ziantengenezewa sheria na zinaongoza nchi ni lazima lile zuri liungwe mkono usipoliunga mkono maana yake hutaki watanzania walipate na NCCR watuko hivyo.

Jambo la pili ni ushirikiano na kwa sababu mimi nimezeekea upinzani, nimesema tulianza miaka ya 91 lakini ukweli tulianza miak ya 88 nakumbuka nikuwa mseminari nimetoka seminari wakanidaka sasa ni miaka 28 tangu tuanze mageuzi. Tunakwenda kwenye uchaguzi mara ya sita na lazima tufanye tathmini mbona mtoto ameshakuwa mkubwa kajitegeme alakini bado tunalialia tu?

Ni vizuri vyama vyote tufanye tatmini tunatoka wapi tunakwenda wapi tufanye nini, kuna mabo ambayo yanatoka kwa wenzetu ambayo sis hatuna mamlaka nayo lakini tuna mambo ambayo tuna madarak a nayo kama hili la ushirikiano , kwa nini hatushirikiani

Hatushirikiani kwa sababu ya mambo kama ubinafsi, uroho wa madaraka, uroho wa mali ... ndio unaotufanya tusishirikiane. Kwa hiyo tusiilaumu serikali kwamba inatugawa ili itutawake vizuri. Mzee Duni wakati Zanzibar ikiwa ina matatizo sana na vifo vile vilivyotokea Zanzibar iiumia sana lakini ikatengenezwa serikali ya umoja wa kitaifa na Maalim akakubali kuwa makamu wa kwanza wa rais wa Zanzibar

Sisi wapinzani huku bara tulipiga kelele kumuita ni CCM B na unyenyekevu na upole wake mwaka 2015 tukaanzisha UKAWA tukaenda kumpigia magoti akasamehe na kusahau na tukatumia ving'ora vyake kujipigia kampeni. Na mwaka fulani kiongozi wa ACT Zitto Kabwe alifukuzwa CHADEMA kwa tuhuma za usaliti na Zittoalianzisha chama na sasa kimekuwa kikubwa na sasa Zitto anaombwa ushirikiano na leo Zitto amesahau .

Na mwanzoni mwa mwaka huu Magufuli alimwalika Mbatia na Lipumba na wengine lakini Mbatia alipotoka ikulu akaambiwa yeye ni CCM B , wale wengine aliokwenda nao sio CCMBna sasa wanatafutwa kwenye ushirikiano na mimi nasema kuna watu katika nchi hii wanaturudisha nyuma kwa maslahi yao binafsi.

Mimi nimesoma hakuna mahali popote kwenye NCCR panapokataza ushirikiano na kwa hii ni kwa sabau msema kweli ni mpenzi wa Mungu Mzee Duni nataka nikutume, Mbowe alipokuwa jimboni kwake alisema hayupo tayari kushirikiana na vyama ambavyo vilishasalimu amri kwa chama tawala (CCM) na chama kimoja wapo alichokitaja ni chama cha NCCR kwa jina. Sasa mwambie sisi tuko tayari kwa ushirikiano na watanzania watusikie na sis hatuko chama tawala na sisi ni waanzilishi wa mageuzi.

Na leo nasema kinachoturudisha nyuma pamoja na tabu tunazopata CCM lakini sisi wenyewe tunarudishana nyuma kwa sababu ya propaganda za kijinga na kitoto. Chama kitafanya hoja ya ushirikiano kama ilivyoelezwa hapo awali lakini tukishindwa kushirikiana hapa juu basi tutahamisha ushirikiano kwa wananchi.

Ukikuta mgombea wa chama chako ni dhaifu na wa CHADEMA ana nguvu na agenda za kuwafaidisha wananchi mpigie kura huyo, ukikuta mgombea wa ACT ana nguvu na wa CHADEMA ni dhaifu mpigie kampeni yule wa ACT maana ndie anayetakiwa na wananchi kwa hiyo kushirikiana na vyama sio dhambi

Na mwisho ni ombo kwa vyama vyote naomba tusiwatupe vijana hata ambao waliohama vyama wakaenda kuanguka kwenyekura za maoni msiwatupe fungueni milango muwachukue muwalee wuwarekebishe kwa kuwa tunachotafuta ni viongozi wa nchi hii.


Mzee Komu
Nchi yetu ni ya vyama vingi na ukiwa na nchi ya vyama vingi maana yake una vyma ambavyo vina tofauti ya kiitikadi, kisera kivipaumbele na hata katika kutekeleza hivyo vipaumbele, Ubaguzi wa vyama sio jambo zuri tukianza kubaguana kwenye vyama tukimaliza tutahamia kwenye dini tukimaliza tutaingia kwenye makabila mpaka kwenye koo zetu, kwa hiyo mtu yoyote anaehubiri ubaguzi huyo tumuogope kuliko kitu chochote.

Katika uchaguzi huu tuiweke nchi yetu mbele na katika dhana hiyo tukahakikishe haturuhusu chama kimoja ama viwili kuhodhi bunge au baraza la madiwani kwa sababu uzoefu umeonesha kuwa uwepo wa chama kimoja unaleta matumizi mabaya ya maamuzi, hivyo tuchague viongozi wa vyama vyote kwa wingi

Leo hoja inaweza kukataliwa kwa kuwa imetoka chama pinzani kwa kuwa hakuna uwiano sawawa watoa maamuzi hivyo ili kuleta maslahi ya taifa basi tuchague viongozi wa vyama mbalimbali ili maamuzi yasiwe kwa maslahi ya chama.

Mzee Joseph Butiku
Nishukuru kwanza kwa heshima ya kunikaribisha na heshima ya kunipa kuzungumza na pia kwa kuitambua taasisi ya Mwl Nyerere, kwa kawaida huwa siji kwenye majukwaa haya na makaratasi leo nimeamua kuadika kusudi niseme mambo ya aina mbili moja ni mambo yanayofanana na uzee, na la pili ni mambo ya misingi kama nilivoyashuhudu=ia katika miaka yangu yote.

Nianze na methali mbili, MSIONE VINAELEA VIMEUNDWA, na MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO taifaletu lina miaka 59 karibu 60 utaratibu wa vyama una miaka 66 tukianzia kwenye TAA mpaka TANU watu wamehangaika wengi tulikuwa hatujazaliwa kina mwalimu na wenzake walihangaika

Leo tumejiwekea utaratibu wa kutafuta viongozi na mkutano huu unatafuta kiongozi wa urais wa kutusiamamia kwa miaka mitano kwa hiyo mnaowatafuta leo sio waasisi ila ni wale wanaokubali kurithishwa yale mema ya waliowatangulia, sasa katika mfumo huu wa siasa na uongozi na utawala kikubwa nini, labda niseme Mbatia kila nikikuona naona ndani yako amani naona umetoshe umenenewa vyema lakini nini kimekuongoza umerithi nini.

Najaribu kuwakumbusha wote taifa hili tumekubaliana kwa muda mrefu kwamba sisi ni watu wenye utu na tupo sawa katika utu huo mnakubali hilo na tuanze kukubaliana na tuache kubishana kwamba sisi si taifa la wanyama ni taifa la watu, watu wenye utu na katika hilo wote tuko sawa hilo tunabishana? nani anadhani kaka na mtu mnyama karibu naye, hakuna si ndio wote mmekaa na watu wenye utu.

Mkiwa watu wenye utu na mko sawa katika utu wenu wote mnastahili haki zilezile, wote mna haki zilezile na msitoke hapa mmesahau na hii ndio nguzo zinazotushikilia kama taifa haki zetu utu wetu usawa wetu, hayo ndio waasisi wametuachia.

Vyama hivi ni vyama vya kuhudumia watu, tunatazamia hamtasahau, serikali ipo kuhudumia watanzania haipo kujihudumia rais akipatikana ni kwa ajili ya kuhudumia watanzania na si kujihudumia

Jeshi la wananchi ni jeshi la Tnanzania jina alitoa Nyerere lipo kwa ajili ya kuhudumia watanzania na kulinda haki kuhudumia watanzania wenye utu wenye usawa si kazi yake kuvuruga haki.

Polisi wanajifunza kuhah=kikisha kwamba haki na heshima zinalindwa si kazi yao kuvuruga haki na utu na hata idaraya usalama wa taifa wanafanya kazi yao na ni kazi nzuri ya kuhakikisha kwamba wanainda haki na utu na si kazi yao kuvuruga.

Tume imeundwa na watot wa kitanzania kwa lengo la kuhakikisha uchaguzi unakwenda kama unavyotakiwa katika katiba na sheria ilivyopanga na ilinde haki na kusiwe na vuipengele vinakiuka haki, mlezi usisahau kazi yako ya ushauri ni chombo cha kitanzania cha kuhakikisaha kwamba utu wao unalindwa.

Utu una sifa zake sifa zake ni mtu ni huru ana heshima kushirikiana na wenzake na kubuni kuyafanyia maamuzi kuyatekeleza na kama ni kubadili basi yabalike kwa mujibu wa sheria.

niwakumbeshe taifa hili lina miaka 59 limeundwa baadhi yetu hatupo limewekewa misingi miwili ni taifa la watu, watu sawa, watu wenye haki sawa linaongozwa na mtu mtu ndani ya chombo kinaitwa rais. ikifika wakati wa uchaguzi watu wanataka cheo wanataka pesa ni nafasi ya kuiba nafasi ya kugeuza vyombo vya watanzania kuwa vyombo vya mtu binafsi kwa hiyo chagueni kwa makini msiweke mtu wa aina hii.

Sasa kuna jambo rushwa, muiepuke isiwepo na naomba isiwepo, watoa rushwa ni watanzania hivyo nawaomba itokomezeni rushwa maana hakuna kitu kinaondoa haki na usawa kama rushwa, Tuwaoombee CCM itoke mle rushwa wala msiwacheke bali muwasaidie.

Kingine Woga, kuogopa ni kusaliti nchi yako wote nyinyi ni maaskari katika kuigania nchi yako muogope Mungu usimwogpe mtu mwenzako na rais mtakaye mchagua hapa halafu mumuogope mimi ningejua nachagua mtu halafu nimeogope nisingechagua , usiogope bali heshimu na namna ya kuheshimu ni kumwambia ukweli.

Tumieni hekima kujenga Taifa lenye watu wenye utu, wenye haki na usawa na kwa sababu unaimarisha uhuru umoja demokrasia na matumizi ya mali yetu kwa uadilifu jengeni chama ambacho hakina tamaa ya mali wala madaraka ya kutawala wengine.

James Mbatia - Mwenyekiti wa NCCR
Amezungukuwa kuwa kutumia ndimi vizuri kwa kusema ukweli na katika uchaguzi huo waangalie wanasema nini maana kauli nzuri ndio zinaweza kuwavusha salama kwenye uchaguzi ujao.

Bora tupate sote kwenye kila kitu tuinuane tusifanye mchezo wa kaa maana mwenzako akifanikiwa ni baraka kwako na yote yalizungumzwa kuhusu muafaka wa katiba na uchumi wa nchi na yote tulioyoambiwa tutayafikisha kwa wananchi .

Wagombea urais wanatakiwa kujua dhamana ya urais na wanatakiwa kujua wanatakiwa kumfanya mama Tanzania asimbague mtoto yoyote maana watu wote wanatakiwa kupata haki sawa. N a tuweze kuwa sauti za wasio na sauti ili waweze kunufaika kwa maslahi mapana ya taifa hili.

=====

UPDATES;
FB_IMG_1596855553430.jpg

Ndugu Yeremia Kulwa Maganja ametangwazwa kuwa mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kipata kura 231 za wajumbe sawa na 89% kati ya kura 258 zilizopigwa.
FB_IMG_1596855567860.jpg

Mgombea Urais wa NCCR-Mageuzi ndugu Yeremia Kulwa Maganja amemteua ndugu Haji Ambari Khamis kuwa mgombea Mwenza.

Pia, chama hicho kimetangaza kuwa hakitasimamisha Mgombea Zanzibar
 
Chama cha Wasaliti. So leo ndio kikao cha kujadili yale majimbo 20 waliyoahidiwa kama zawadi na jamaa yao. Sasa sijui watawatangaza hata kama hawajashinda maana hapo itabidi awapore ushindi wagombea wa CHADEMA , ACT Au CCM, maana hivyo ndio vyama mwaka huuu vinaweza kushinda kura za bunge kihalali. NCCR hawana uwezo wa kupata kura asilimia hata 10% popote pale zaidi ya Vunjo.
 
Back
Top Bottom