Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe leo Januari 11, 2022. SP Jumanne Malangahe amaliza kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa hadi Januari 13, 2022

Hii kesi wakati mwingine Mashahidi wa Jamhuri, Jaji anashindwa kucheka mbele yao kwa namna wanavyojichanganya anaamua kwenda kucheka chumbani na mkewe. Et, Ugaidi ungefanyika nchi nzima kwa kutumia bastora ya risasi 3,(Redicusly)

Eti Jambazi Sabaya kutaka kuuwawa ni Ugaidi lakini Lissu aliyepigwa marisasi mbele ya viunga vya bunge si Ugaidi (absurd)
Au eti hawana ushahidi wowote wa sauti/video ya hiyo mipango ya ugaidi, na bado wanataka kesi iendeleee
 
Kinachoshangaza, aliyewapa information ya mpango wa ugaidi Afande Urio, sio shahidi kwenye hii kesi na mahakama haina maelezo yake...

Huyu Urio angekuwa mtu muhimu sana mahakamani kwenye hii kesi
... watakwambia hawakuona umuhimu wa kumleta mahakamani kama shahidi; kwanini? sijui!
 
Kibatala: Katika Kikosi chenu wewe ulikuwa Second Command Kama Top leader, Je, Unafahamu timu yenu Kuna Mtu aliwasiliana na Rais Samia Suluhu Hassan?

Shahidi: Hilo sifahamu

Kibatala: Unafahamu alipopata taarifa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mbowe alikuwa anajua atashitakiwa Kwa Ugaidi ndiyo Maana akakimbia nje ya Nchi kukwepa upelelezi?

Shahidi: Hapana... Sifahamu

Kibatala: Kuna kikosi kazi zaidi ya chenu kilikuwa kinafanyia kazi suala hili labda wao walienda kumtaarifu Rais Samia Suluhu Hassan?

Shahidi: Hapana.. Sifahamu

Kibatala: Kesi hii Rais Samia Suluhu Hassan alisema kuna watu wamefungwa katika shauri hili, kwa ufahamu wako kuna watu wamefungwa kwenye shauri hili?

Shahidi: Hilo silijui na siwezi kuliongelea

Kibatala: Kama unajua sema najua au kama hujui sema sijui, Kusema huwezi kuongelea ni ujeuri huo na nitaomba mahakama IKUZIMISHE..

Kwa kweli kesi hii inazidi kuliabisha jeshi la Polisi
 
... that cross-exam ilikuwa balaa kubwa kaka! Anahitaji ulinzi wa jeshi la mbinguni haswa! Maombi maalumu kwa jopo la utetezi; iwe mchana iwe usiku tusiwasahau katika maombi Gabrieli na jeshi lake wakatangulie vita hivi; stadi wa kazi na directives zikitoka moja kwa moja Kiti cha Enzi!
Amina
 
Huyu shahidi kajikanyaga mpaka anatia huruma.
... hata ukicheki tone ya wakili wa serikali wakati wa re-exam ni as if "kawaangusha sana huyu kiazi"! Jana Kibatala alipopata nafasi na kuuliza maswali machache kisha kuomba kesi iahirishwe kwa sababu "ana maswali mengi" kwa huyu shahidi nikajua "shughuli ipo"!
 
Back
Top Bottom