Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe leo Januari 11, 2022. SP Jumanne Malangahe amaliza kutoa ushahidi. Kesi yaahirishwa hadi Januari 13, 2022

The Sheriff

JF-Expert Member
Oct 10, 2019
617
1,801
Salaam Wakuu,

Leo tarehe 11/01/2022 kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe inaendelea.

Kufahamu ilipoishia, soma hapa: Yaliyojiri katika kesi ya Freeman Mbowe - Januari 10, 2022. Shahidi namba 8 aendelea kutoa ushahidi. Kesi imeahirishwa hadi kesho 11/01/2022

Ungana nami katika uzi huu ili kujua kila kinachojiri Mahakamani.

UPDATES:

Jaji ameingia Mahakamani Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji naomba Kuwatambulisha;

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Tulimanywa Majige
Ignasi Mwinuka

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikikupendeza naomba Kuwatambulisha Mawakili
Nashon Nkungu
John Mallya
Dickson Matata
Faraji Mangula
Sisty Aloyce
Michael Mwangasa
Gaston Garubindi
Seleman Matauka

Jaji anaita Washtakiwa Wote wanne na wote wanaitika wapo Mahakamani

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri lina endelea Kusikilizwa na Upande wa Mashtaka tupo tayari Kuendelea

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji nasi pia tupo tayari Kuendelea

Jaji anaandika Kidogo wakati Mahakama Ipo Kimya

Wakili Peter Kibatala anasimama na Kuendelea na Maswali kwa shahidi

Kibatala: Shahidi Tulikuwa tunaendelea Kuhusu Kesi yenu Kuwa Mbowe Alimpa Maelezo Urio na Urio Aweze Kutafuta Watu wa Kufanya Ugaidi

Kibatala: Shahidi, Urio bado Yupo Jeshini na Mwanajeshi aliye kwenye Utumishi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: katika Ushahidi Wako Uliwahi Kuongea Lolote hapa Mahakamani Kwamba Urio akiwa Kama Mwanajeshi wa JWTZ Kushiriki katika Vitendo Vizito Vya Ugaidi

Shahidi: Hapana

Kibatala: Ulishawahi kuwasiliana na JWTZ kuhusu Mtumishi wao Urio Kushiriki katika ya Matendo ya Ugaidi

Shahidi: Sijafanya

Kibatala: kwa ufahamu wako Uongozi wa JWTZ unafahamu Mwanajeshi wao Urio alikuwa anafanya Vitendo Vya Kutafuta Watu wa Kufanya Ugaidi

Shahidi: Mimi sifahamu

Kibatala: Je Unakubaliana na Mimi Kuwa Vitendo Vya Ugaidi ni Vitendo Vizito na Vinatikisia Psychology na Utulivu wa Nchi

Shahidi: Ndiyo Kibatala: Je unafahamu Kuwa JWTZ Wana kitengo Cha Ujasusi cha Millitary Intelligence, kazi yao ni Pamoja na Kuchunguza Matendo ya Ugaidi?

Shahidi: Hapana sifahamu

Kibatala: Katika Ushahidi Wako Ulizungumzia lolote kuhusu Kushirikiana na Vyombo Vya Usalama na Kijasusi kama TISS?

Shahidi: Mimi sifahamu lakini Viongozi wangu Watakuwa wamefanya

Kibatala: Sasa Viongozi wako Unawaona hapo Kwenye Kizimba?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Unafahamu Kuwa Moja ya Kazi ya Hizo Taasisi ni Kushughulika na Mambo ya Ugaidi

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Unafahamu Kuwa iwapo taasisi hizo zingeshirikishwa katika ngazi mbalimbali ya vyombo vya usalama na idara ya uhamiaji na wao wangeshirikishwa?

Shahidi: Hilo mimi siyo wajibu wangu Kibatala: umeanza kuleta ujeuri mahakamani Shahidi: Hapana Kibatala: Sasa Jibu, unafahamu au hufahamu

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je Unafahamu Kuwa Mshtakiwa Wa 4 alisafiri Kwenda Nje Mara Kadhaa?

Shahidi: Hapana, Sifahamu

Kibatala: Katika Kikosi chenu wewe ulikuwa Second Command Kama Top leader, Je, Unafahamu timu yenu Kuna Mtu aliwasiliana na Rais Samia Suluhu Hassan?

Shahidi: Hilo sifahamu

Kibatala: Unafahamu alipopata taarifa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Mbowe alikuwa anajua atashitakiwa Kwa Ugaidi ndiyo Maana akakimbia nje ya Nchi kukwepa upelelezi?

Shahidi: Hapana... Sifahamu

Kibatala: Kuna kikosi kazi zaidi ya chenu kilikuwa kinafanyia kazi suala hili labda wao walienda kumtaarifu Rais Samia Suluhu Hassan?

Shahidi: Hapana.. Sifahamu

Kibatala: Kesi hii Rais Samia Suluhu Hassan alisema kuna watu wamefungwa katika shauri hili, kwa ufahamu wako kuna watu wamefungwa kwenye shauri hili?

Shahidi: Hilo silijui na siwezi kuliongelea

Kibatala: Kama unajua sema najua au kama hujui sema sijui, Kusema huwezi kuongelea ni ujeuri huo na nitaomba mahakama IKUZIMISHE..

Shahidi: Hilo silifahamu.

Kibatala: Je unafahamu kuwa Kingai alisema kuwa alimuwekea uangalizi Mbowe hata alipokuwa nje ya Nchi?

Shahidi: Hilo Mimi silifahamu Kibatala: Je Kwa ufahamu wako wewe Freeman Mbowe alikimbia nje ya nchi Ilikuweza kukwepa upelelezi

Shahidi: Hilo silifahamu kwa kweli

Kibatala: Je unafahamu Freeman Mbowe kaenda nchi mbalimbali kutoka August 2020 mpaka Mwaka 2021 July?

Shahidi: silifahamu nchi hizo mimi

Kibatala: Je unafahamu mamlaka chunguzi/ pelelezi za Tanzania ziliwahi kuwasiliana na mamlaka chunguzi za hizo nchi?

Shahidi: Hilo sifahamu

Kibatala: Je unafahamu kuwa mtu ambaye akiwa kwenye uchunguzi na upelelezi wa kesi nzito huwa anazuiwa hata kusafiri?

Shahidi: Hilo linategemea

Kibatala: Linategemea nini?

Shahidi: Hilo sijui kwa kweli

Kibatala: Iambie sasa mahakama ni uchunguzi upi huo uliokuwa unaendelea ambao Uliwafanya usimkamate Freeman Mbowe Wakati wote

Shahidi: Mambo ya Forensic

Kibatala: Mlifanya mawasiliano kwa mara ya kwanza na taasisi za Forensic Mwezi July 2021 baada ya Freeman Mbowe kukamatwa Je wewe unasemaje?

Shahidi: Sina ninachojua....

Kibatala: Kingine kipi?

Shahidi: Mambo ya Intelligence

Kibatala: Intelligence ipi?

Shahidi: Mambo ya Intelligence mengi siwezi kuyazungumzia hapa

Kibatala: Kwa Sheria Ipi inayokuruhusu wewe shahidi usiseme hayo mambo halafu unataka KUMFUNGA mteja wangu?

Shahidi: Ni Mambo ya watu wengine kwenye upelelezi ikiwemo watu wengine waliokamatwa.

Kibatala: Kuna mtu alimakatwa baada ya September 2020?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Sasa nani unayemzungumzia hapa

Shahidi: Hakuna, Ila wengine wanaendelea kufuatiliwa

Kibatala: Kwa hiyo upelelezi wa kesi hii unaendelea?

Shahidi: Hapana, umeisha

Mahakama: Kicheko!

Kibatala: Je, unafahamu kwamba katika Nchi ambazo Viongozi wake ni MADIKTETA, Huwapa viongozi ambao ni wapinzani wao Kesi Ilikuwatisha

Shahidi: Hilo silifahamu

Kibatala: Nchi Kama Sweden, Marekani na Uingereza zinaweza kumkumbatia mtu ambaye ni gaidi wakati ni waganga wa UGAIDI?

Shahidi: Hilo sifahamu

Kibatala: Unafahamu nchi nilizozitaja zinafuatilia kesi hii kwa kutuma wawakilishi wao kuja kufuatilia haki ya Freeman Mbowe?

Shahidi: Hilo Mimi sifahamu

Kibatala: Unafahamu Kitu kinaitwa TRAVEL ADVISORY

Shahidi: Sijawahi kukutana na kitu kama hicho

Kibatala: Askari Mzoefu Wa Miaka 20 hujawahi Kusikia Kitu hicho

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Katika Upelelezi Wenu wote Mpaka Upelelezi Unakamilika, Urio si Ndiyo alikuwa Informant wenu?

Shahidi: Hilo sijaongelea hilo

Kibatala: Kwa hiyo alikuwa ni Whistler blower

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unaifahamu sheria inaitwa Whistler Blower and Protection Act, Juu ya kulinda WATOA Taarifa?

Shahidi: Hapana sifahamu sheria hiyo

Kibatala: Kwahiyo wewe Afisa wa Polisi na kiongozi wa kikosi Kazi hujui sheria ya Whistle Blower and Witness protection Act

Shahidi: Miye sijawahi kuisoma hiyo sheria natumia miongozo yangu tu

Kibatala: Kwa hiyo hufahamu kuwa Whistle Blower anapokuja kutoa taarifa umuandikishi maelezo ya onyo bali kwa taarifa za sheria hiyo?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Na Bado Mnataka tuendelee Na Kesi hii wakati Whistle Blower hajahojiwa kwa Sheria hiyo?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Katika Upelelezi Wenu wote Mpaka Upelelezi Unakamilika, Urio si Ndiyo alikuwa Informant wenu?

Shahidi: Hilo sijaongelea hilo

Kibatala: Kwa hiyo alikuwa ni Whistler blower

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unaifahamu sheria inaitwa Whistler Blower and Protection Act, Juu ya kulinda WATOA Taarifa?

Shahidi: Hapana sifahamu sheria hiyo

Kibatala: Kwa hiyo wewe Afisa wa Polisi na kiongozi wa kikosi Kazi hujui sheria ya Whistle Blower and Witness protection Act

Shahidi: Miye sijawahi kuisoma hiyo sheria natumia miongozo yangu tu

Kibatala: Kwa hiyo hufahamu kuwa Whistle Blower anapokuja kutoa taarifa humuandikishi maelezo ya onyo bali kwa taarifa za sheria hiyo?

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Na Bado Mnataka tuendelee Na Kesi hii wakati Whistle Blower hajahojiwa kwa Sheria hiyo?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ufahamu Wako Freeman Mbowe aliwapa pesa washtakiwa Personally kutoka Kwake?

Shahidi: Ndiyo aliwapa kutoka kwa Urio

Kibatala: Kwa Hiyo zikipitia kwa Urio ni Personally?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Msomi Mzima hujui maana ya Personally?

Shahidi: Nilikuwa sijaelewa

Kibatala: Sasa nitafutie sehemu Iliyoandikwa kwamba Kuna pesa iliyotoka kwa Mbowe kuja Kwa Urio, kisha Urio akawapa wao

Shahidi: Hakuna sehemu hiyo

Kibatala: Kwa hiyo katika Maelezo haya Ling'wenya alikabidhiwa pesa na Urio bila kuambiwa imetoka wapi?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Soma hapa Katika ukurasa wa tatu Mstari wa mwisho baada ya kukutana na Luteni Dennis Urio. Je, alifahamu anaenda Moshi Kufanya nini?

Shahidi anasoma

"Baada ya Kufika tulikutana na Luteni Denis Urio Bar Moja ya Msavu sikumbuki Jina, Baada ya Kukutana luteni Urio alisema Kuwa Kuna kazi ya kwenda kufanya Moshi ambayo ni VIP Protection"

Amemaliza Kusoma ndugu Shahidi..

Kibatala: Hapo Ling'wenya kwenye Maelezo ya Onyo ambayo mnasema amekiri alisema anaenda Moshi Kufanya nini

Shahidi: Kufanya VIP PROTECTION

Kibatala: Sasa katika Statement hiyo nitafutie Mahala ambapo Urio anamwelekeza Ling'wenya Kuwa anaenda Kufanya Kazi ya Ugaidi Moshi

Shahidi: Hakuna sehemu hiyo anayosema kuwa alipewa Kazi ya kwenda Kufanya Kazi ya Ugaidi

Kibatala: Ni wapi ambapo Ling'wenya anakiri Kuwa alipewa pesa na Mbowe Kwenda Kufanya vitendo vya kigaidi

Shahidi: Hakuna sehemu ambayo anasema alipewa pesa na Mbowe kwenda Kufanya Ugaidi

Kibatala: Kuna Mahala Popote katika Statement Ambapo Freeman Mbowe alipiga simu au Kutuma Meseji Kumshawishi Ling'wenya Kwenda Kufanya Kazi ya Ugaidi?

Shahidi: Hakuna Maelezo hayo..

Kibatala: Kwa maelezo yenu Ni kwamba Luteni Denis Urio ndiye aliyeenda Ofisi wa ya DCI Kuleta taarifa na ndiye akawa INFORMANT wenu, je nini kiliwazuia kumpa vifaa kazi mtu huyu kwa ajili ya KUMREKODI Mbowe akitoa maelekezo ya kutenda UGAIDI au KUMDHURU Sabaya?

Shahidi: Mimi kama mpelelezi sina sauti za Mbowe akipanga ugaidi

Kibatala: Je, tuna video yoyote ambayo inaonyesha Mbowe akipanga ugaidi au kutoa maelekezo ya kutenda ugaidi au kumdhuru sabaya

Shahidi: Ndiyo... Hatuna video yoyote

Kibatala: Je Mliwahi Kumwambia Luten Denis Urio kuwa amrekodi Freeman Mbowe hata Kwa simu alitoa Maelekezo ya Kutenda Vitendo Vya Ugaidi au Kumdhuru Sabaya ili zije Mahakamani Kama Ushahidi wenu?

Shahidi: Hatuna Voice Record kutoka Kwa Urio sisi

Kibatala: Je Mli' Infiltrate Mtu Mwingine Aweze Kupata Records za Freeman Mbowe hata Kama Kwa Kutuma Mwanamke aweze Kumrekodi?? Shahidi: Miye siwezi Kufahamu Kibatala: Wewe ulifahamu lini Kuwepo kwa Luteni Denis Urio kama Whistle Blower?

Shahidi: Kwenye Mwezi wa Nane na Wa Tisa Baada ya Kuwa wamekamatwa wakina Ling'wenya

Kibatala: Mpaka Tarehe hiyo Mlikuwa mnafahamu Freeman Mbowe amemuagiza Luteni Denis Urio Kutenda Vitendo Vya Ugaidi, Je alikuwa amefanya Kosa au alikuwa hajafanya kosa?

Shahidi: Alikuwa amefanya kosa

Kibatala: Lakini Mpaka Wakati huo Mlikuwa hamjaona sababu ya Kumkamata

Shahidi: Kimyaaaaaaaaaa

Kibatala: Je, ni sahihi nikisema Mlitumia Luten Denis Urio kuwawekea Mtego Vijana hawa ili Kutengenezea Mbowe Kesi ya Kisiasa?

Shahidi: Si kweli, Wewe siyo Mpelelezi

Kibatala: Mimi na wewe nani ajui Upelelezi Wakati nimekuuliza hapa Kuhusu Mbinu za Kazi

Shahidi: Upelelezi ni Mambo Mengi siyo hayo tuh

Kibatala: Upelelezi gani unaujua wewe zaidi ya Kutesa Vijana wa watu ambao walitumikia Nchi na Jeshi?

Shahidi: Sijatesa Mtu Mimi

Kibatala: nakuuliza hapa chini ya kiapo, Unamjua Tito Magoti au humjui?

Shahidi: Simfahamu Tito Magoti kabisa

Kibatala: Nikimleta hapa mahakamani kama shahidi akisema kuwa ulishiriki kumteka je?

Shahidi: Mie sijawahi kumteka

Kibatala: Na Je unasemaje Juu ya taarifa Kuwa wewe ni miongoni wa watu WASIOJULIKANA na UMESHIRIKI KUTEKA na KUTESA watu?

Shahidi: Hapana Mimi sijawahi kuteka mtu Mimi

Kibatala: Je, Unafahamu Kuwa wewe ni Afisa wa Mahakama?

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: Askari Mzoefu Miaka 20 hujui kuwa PGO inakutambua kama Afisa wa Mahakama

Shahidi: Sijawahi Kujua

Kibatala: Nitafutie Mahala Popote ambapo Ling'wenya anakiri Kukutana katika Kikao cha Kupanga Vitendo Vya Kigaidi

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Nitafutie Mahala Popote katika Statement hiyo ambapo Ling'wenya anakiri kupanga kwenda Kulipua Soko la Kilombero Arusha

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Nitafutie Mahala Popote ambapo Ling'wenya anakiri Kuwa alipanga Kulipua Mkoani Mwanza

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Nitafutie Mahala Popote ambapo Ling'wenya anakiri Kuwa Bastola mliyokamata kuwa ilikuwa inatakiwa Kutumika Vipi Katika Vitendo Vya Ugaidi

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Ni wapi ambapo Ling'wenya amezungumzia katika Statement hiyo aina ya Vilipuzi?

Shahidi: Hakuna Kibatala: Kwa uzoefu wako wewe Kama Afisa wa Polisi, Unaweza Kulipua bila ya Kuwa na Vilipuzi?

Shahidi: Hapana lazima uwe na Vilipuzi

Kibatala: Kuna Mahala Popote katika Statement hiyo ambapo Ling'wenya ameelezea namna walivyo panga Kumdhuru Sabaya

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Unasema Mliwakamata Ling'wenya na Adamoo Pale Rau Madukani

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je, kwa Upelelezi Wenu, Uwepo wao pale Rau Madukani Ling'wenya na Adamoo walikuwa katika matembezi yao au Kwa Kwenda Kutekeleza Mpango wa Ugaidi?

Shahidi: Walikuwa Wanatekeleza Mpango wa Ugaidi

Kibatala: Nitafutie hilo katika Statement Ya Ling'wenya hapo sehemu ambapo anasema walikuwa Rau Madukani Kutekeleza Mipango ya Ugaidi

Shahidi: Hapana hakuna sehemu hiyo

Kibatala: Lengai Ole Sabaya ameshahukumiwa Kifungo Kwa Makosa ya Ujambazi na Kudhulumu watu Mali zao

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ni Nyie nyie Ndiyo mlimshitaki Sabaya Kwa Makosa Ya Ujambazi ambaye Hapa Mnasema alitaka kudhuriwa?

Shahidi: Miye ushawahi kuniona kwa Sabaya?

Kibatala: Si nyie Jeshi la Polisi

Shahidi: Aaah! Sawa hapo sawa, Kama Jeshi la Polisi, Mwanzo Hukuwa specific

Kibatala: Ulishawahi Kuongea na Sabaya ukamwambia Kuna watu wanataka Kumdhuru

Shahidi: Hapana

Kibatala: turudi pale Rau Madukani, Baada ya Kuchukua Bastola Katika Maungo ya Adamoo, na Baadae ukamkabidhi Goodluck

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: na Pale hakuwa na Seizure Certificate ikabidi atoke aende Kwenye Gari Kufuata Karatasi ya Seizure Certificate

Shahidi: Sahihi

Kibatala: na Goodluck akaondola na Ile Bastola Kwenda Kwenye Gari, akarudi tena na Ile Bastola

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Lakini Hukusema Hapa Kwamba Goodluck Alisindikizwa Na Mashahidi Huru Kwenda Kuchukua Seizure Certificate Anita na Esther

Shahidi: Ndiyo sikusema

Shahidi: Lakini tayari nilisha kuwa nimesema Namba na Kila Mtu aliokuwa ameona namba

Kibatala: Sasa uliyasema hapa Mahakamani

Shahidi: Hapana

Kibatala: Na Goodluck ile Bastola Uliyo Mkabidhi aende nayo ilikuwa na zile Risasi tatu?

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Sasa unafahamu Kuwa Zile Risasi Zina Calibre Namba Kwenye kitako

Shahidi: Ni sahihi Zina Calibre Namba

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kama Ulizungumzia hizo tofauti Kuwa Zile Risasi zilikuwa Moja haina namba na Zile Mbili Zina namba tofauti

Shahidi: Hapana Siku Mwambia

Kibatala: na Unafahamu Kuwa kila Silaha ina Origination yake

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: Ling'wenya alikwambia wamepata Wapi hiyo silaha

Shahidi: Haja eleza Katika Maelezo Yake

Kibatala: Katika Upelelezi Wenu Mligundua Adamoo alipata wapi hiyo Bastola

Shahidi: ilikuwa ni unlawful

Kibatala: Sijakuuliza hilo, nimekuuliza, Adamoo alipata wapi hiyo Bastola

Shahidi: Hatujui alipata wapi

Kibatala: na hujasema kuwa alipewa na Freeman Mbowe

Shahidi: Sijasema hivyo

Kibatala: na Hayo madawa ya kulevya aliyokutwa nayo Ling'wenya, mlichunguza amepata wapi

Shahidi: Hatukuchunguza

Kibatala: Je, aliwaambia kuwa madawa hayo ya kulevya yana husiana vipi na njama za ugaidi

Shahidi: Hatukugundua yana husiana vipi

Kibatala: Turudi Dar ea Salaam, Je Mlifika Dar es Salaam Saa ngapi Kutoka Moshi ni Saa 10 kwenda Kwenye Saa 11 au Saa 11 kwenda Saa 12 Shahidi' Ilikuwa Saa 11 kwenda Saa 12

Kibatala: Kwahiyo ni Range ya Lisaa limoja tu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Na Jana ulisema Kumbukumbu Ni Sifa ya Askari Makini

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Wale Vijana wengine Watatu Mliwakamata Kwa Sababu walipita 92 KJ

Shahidi: Hapana

Kibatala: Wewe Si Ndiyo Mpelelezi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Sasa Uliwakamata kwa Sababu ipi au Ndiyo tuseme Jeshi linaonea Wanajeshi Wake waliolitumikia

Shahidi: Hapana Kwa sababu Walikutana kabla kuwa Mwezi July

Kibatala: Kwa hiyo Walikutana wapi

Shahidi: Dar es Salaam

Kibatala: Kwa hiyo Ni Ushahidi Wako Kuwa Ling'wenya alikuwa Dar es Salaam Mwezi July

Shahidi: Hapana Ilikuwa Mwezi wa Nane

Kibatala: Je Unafahamu Kuwa Chadema ilishiriki Uchaguzi Wa Rais, Wabunge Nchi Nzima

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala: Mbowe aligombea Ubunge Kule Hai

Shahidi: Ndiyo nafahamu

Kibatala:
Hivi Dhana ya Mtu Kupanga Kufanya Ugaidi Kudhuru Wananchi na Kwenda tena kwa hao hao Wananchi akiwa anagombea na Chama Chake

Shahidi: Hiyo ni Mtu Mwenyewe Sasa, miye sifanyii Kazi Dhana

Kibatala: Kuna Mahala Popote Wewe na Kikosi Kazi Chako Kuna Mahala Popote Ulizungumzia Kuripoti kwa Kamanda wa Polisi Kilimanjaro na Moshi kuwa Mna kazi ya Kitaifa Mnafanya

Shahidi: Hapa Sijazungumzia

Kibatala: Kuna Mahala Popote Kwenye PGO inasema Kwamba Maelezo Kaandikishie Mahala ambapo Kesi imefunguliwa

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Je, kuna Mwomgozo Wowote unazungumzia hivyo

Shahidi: Hapana

Kibatala: Twende sehemu nyingine, Jana Nilisikia Hapa Unazungumzia Kuhusu Tundu Lissu Kupigwa Risasi, Je Tukio la Tundu Lissu Kupigwa Risasi Kwa Lissu ni ugaidi au siyo Ugaidi?

Shahidi: Siyo ugaidi ni uhalifu wa kawaida
Kibatala: tufanye comperative analysis, Inakuwaje kutaka kumdhuru Mhalifu Lengai Ole Sabaya iwe ugaidi ila kupigwa risasi kwa Tundu Lissu isiwe ugaidi?

Shahidi: Kwa sababu Ilikuwa inaendana na maandamano nchi nzima

Kibatala: Kwani Chadema Wamefanya Marangapi Maandamano

Kibatala: Je, maandamano hayo yalikuwa ni Ugaidi?

Shahidi: mimi Sijui

Kibatala: Kuna Mahala popote umesema Kuwa Mlipofika Dar es Salaam mlimfahamisha DCI?

Shahidi: Sijasema

Kibatala: Kuna Mahali Popote ile Umesema Kwamba Gari ilipo haribika mlimpigia simu DCI?

Shahidi: Kimya

Kibatala: Kuna Mahala ulisema pale Aishi Hotel Kingai alishuka kwenda kumtafuta Moses Lijenje

Shahidi: Ndiyo Nilisema

Kibatala: Kingai alikuwa anamfahamau Moses Lijenje..

Shahidi: Hapana, ilaaaaa....

Kibatala: Hakuna cha ila hapa, ushajibu swali hivyo...

Kibatala: Mheshimiwa Jaji naomba Kielelezo P12

Kibatala: Shahidi Nionyeshe hapa Sehemu ambayo umejeza description za zile Risasi tatu

Shahidi: Si Kujaza, suala la Risasi kwenye Seizure Certificate

Kibatala: unajua Kuwa Seizure Certificate Ndiyo inaonyesha Chain of Custody ya Mali Mnazokamata?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kielelezo Namba P12 imeandikwa Jina na Saini ya anayekabidhiwa

Shahidi: sahihi

Kibatala: Tusomee Mtu anayekabidhiwa

Shahidi: H 4347 Detective Goodluck

Kibatala: hilo ndiyo Jina lake..?

Shahidi: Ndiyo Kwa Mujibu wa Kazi zetu

Kibatala: ulipo jaza wewe Kuna signature au hakuna

Shahidi: hakuna

Kibatala: Ulielezea Mahakama Kwanini Hakuna signature

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mpaka mnaenda Arusha kwa dada yake Moses Lijenje Arusha, Je Mnafahamu Majina yake?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Mlikuwa mnajua Moses Lijenje pale Moshi anakaa Hotel gani?

Shahidi: Hotel Mbalimbali tu

Kibatala: Tutajie Hotel Mbili tu

Shahidi: Hapana sizifahamu!

Kibatala: Nafikiri nimemaliza mheshimiwa jaji

Kibatala sasa anaketi pahali pake, baada ya shughuli ya saa mbili na dakika 20 na shahidi wa jamhuri, SP Jumanne Malangahe

Anasimama Wakili Mwandamizi wa Serikali, Robert Kidando

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba Kupatiwa Vielelezo P11, 12 na 13

Wakili wa Serikali: Shahidi Ulionyeshwa Kuwa Sehemu ya Jina la H4347 kuna Jina na Hakuna Sahihi lakini Kwenye Jina lako Umeweka Sahihi

Shahidi: Kwa sababu Askari Mdogo hatakiwi Kuweka Saini ya Kukoroga anaweka Namba Yake ya kazi tu

John Mallya: OBJECTION Mheshimiwa Jaji hiyo ni fact Mpya ya Ufafanuzi

Jaji: Rudia Swali ambapo halitaleta Majibu Mapya

Wakili wa Serikali: Shahidi Ulionyeshwa Kuwa Sehemu ya Jina la H4347 Kuna Jina na Hakuna Sahihi lakini Kwenye Jina lako Umeweka Sahihi

Dickson Matata: OBJECTION bado ni fact Mpya hiyo

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji sisi tuna Haki hiyo Kwa Mujibu wa Sheria, Siyo Kama tunakatazwa

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji nafikiri wapewa nafasi lakini na sisi tunaomba kurudi upyaaaaa kwenye swali hilo.

Jaji: Sawa ulizeni nitawapa upande wa utetezi nafasi ya kurudi tena...

Wakili wa Serikali: Shahidi Ulionyeshwa Kuwa Sehemu ya Jina la H4347 Kuna Jina na Hakuna Sahihi lakini Kwenye Jina lako Umeweka Sahihi

Shahidi: Kwa sababu Askari Mdogo hatakiwi Kuweka Saini ya Kukoroga anaweka Namba Yake ya kazi tu

Wakili wa Serikali: Kuna Hiki Kielelezo Cha P13 Maelezo ya Onyo ya Mshtakiwa Wa Tatu.. Kwa Mujibu wa statement hii Uliulizwa swali Kama Mohammed Ling'wenya kuhusiana na Mpango Wa Kulipua Vituo Vya Mafuta kuhusu Vilipuzi Ukasema hakukueleza

Shahidi: Ni sahihi

Wakili wa Serikali: Sasa Yeye alikueleza nini

Shahidi: alieleza Nchi Nzima Haku specify Sehemu Moja

Wakili wa Serikali: Uliulizwa hapa Kuhusiana na Denis Urio Kuhusiana na Kuweka Mtego ilikumpa Mshtakiwa wa nne Kesi ya Kisiasa

Shahidi: Si Kweli Shahidi alileta Taarifa Mwenyewe wala hakutumwa na Mtu

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusiana Kuwakamata Wakina Gabriel na Khalid, kuwa Mliwakamata sababu walipita 92 kJ Je, Unasemaje?

Shahidi: Si Kweli tukiwa kamata wakiwa sababu Wali zungumza na Washtakiwa Na wakawa wapo tayari Kujiunga

Wakili Mallya: OBJECTION Neno wapo tayari hakusema Jaji anasoma na Kumbukumbu haionyeshi Kuwa walikuwa wanampango wa Kwenda Kujiunga na akina Ligw'enya.

Wakili wa Serikali: Basi Mheshimiwa Jaji Neno Mpango wa Kujiunga liondoke

Wakili wa Serikali: Tufafanulie Exactly Ni Mwezi upi Khalid na Gabriel Walikutana Mshtakiwa Wa tatu Dar es Salaam

Shahidi: Ni Mwezi wa Saba

Wakili wa Serikali: Ulitoa Taarifa hapa Kwamba ACP Kingai Kuwa hakuwepo Tarehe 09 August 2020 hakuwepo Mbweni, Hebu Tufafanulie hapo

Shahidi: Ni Kwa sababu tulikuwa na Shughuli Ya Kuendelea Kumtafuta Mtuhumiwa Khalfani Bwire

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Pia Kuhusiana na Upekuzi na Ukamataji Pale Rau Madukani Kwamba Baada ya Kukamata Bastola Ulimtuma Goodluck Kwenye Gari na Ukasema Hakuna aliyekwenda na Goodluck Kufuata Seizure Certificate Tufafanulie kwanini Ikitokea hivyo

Shahidi: Baada ya Kukamata Nilisema Namba na wote walisikia, Ndipo Nikamtuma Goodluck na Yeye Mwenyewe ndiye aliyerudi na hiyo silaha

Wakili MALLYA: OBJECTION hayo Ni Majibu Mapya tena Yanajikoroga na Majibu ya awali

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia Kuwa Kama Unajua Kuwa Mshtakiwa Freeman Mbowe alikamatwa Mwanza akiwa Kwenye Mkutano wa Katiba Ukasema ufahamu, Je Nini Unachofahamu Shahidi: Ni nacho fahamu ni kuwa alikamatwa Mwanza Kwa tuhuma Za Ugaidi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia Kama Ulikuwa na Maslahi Binafsi na Washtakiwa

Shahidi: Niliwa kamata kwa Sababu ya tuhuma ambazo zimekuwa reported Polisi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusu na Askari aliyesimamisha Daladala na Kuhusu Taarifa za Yule Dereva, Ukasema Hapakuwa na Umuhimu

Shahidi: Hapa Kuwa na Umuhimu Kwa sababu Tulimkamata Kisheria na Ndiyo Maana Mpaka Sasa Yupo Mahakamani

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu simu Mbili za Mshtakiwa Ukasema hilo hujalitolea Ushahidi

Shahidi: Ni Kwa sababu siyo Mimi niliye Mkamata wala Kufanyia Upekuzi

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kuhusu Mshtakiwa Wa tatu Kufanya VIP protection Ukasema Siyo Kosa, Ulikuwa unamaanisha nini

Shahidi: Kwa sababu siyo Kosa kama Unafanya Kwa nia Njema ila Ni Kosa Unafanya Kama Jinai

Dickson Matata: OBJECTION hapo Mbele Majibu nayapinga sababu Hakusema Mwanzo

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia Katika Kielelezo hicho pia, Kuhusiana Kile Kilicho hamasishwa Kufanya Maandamano Nchi Nzima ni Kosa au Siyo Kosa Ukasema inategemea

Shahidi: Kufanya Maandamano Kwa Kufuata Sheria Siyo Kosa

Wakili wa Serikali: Uliulizwa pia Kuhusu Mkoa gani Umetwajwa Kufanya Maandamano, Ukasema Hakuna Je ni Kitu gani kimesemwa

Shahidi: Kufanya Maandamano Nchi Nzima na Mikoa ipo Ndani ya Nchi

Wakili wa Serikali: katika Statement hiyo Umeulizwa Kuhusiana na suala la Mshtakiwa Wa Tatu Kupewa pesa pale Morogoro Kwa jili ya VIP protection Ukasema Siyo Kosa Sababu inategemea na Malengo

Wakili DICKSON MATATA: OBJECTION swali hilo Siku sema hivyo

Wakili wa Serikali: Sawa narudia

Wakili wa Serikali: katika Statement hiyo Umeulizwa Kuhusiana na suaa la Mshtakiwa Wa Tatu Kupewa pesa pale Morogoro Kwa jili ya VIP protection Ukasema Siyo Kosa

Shahidi: Ni Kwa sababu kama unatuma Kwa nia Njema siyo Kosa Wakili

DICKSON MATATA: Mheshimiwa Jibu la Swali hilo Kwamba nia Njema, Nia njema Haikutajwa

Jaji: Umechelewa Kusimama, Nitakupa nafasi ya Kuhoji tena

Wakili wa Serikali: Nilisikia Unasema Kuwa Watuhumiwa Wataandikwa Kwenye Detention Register Pale tu Watakapo Pokelewa, Unamaanisha Nini

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Kwamba Pale wanapokelewa na Kuwekwa Mahabusu Ndiyo Wanaandikishwa Kwenye Detention Register

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Pia Kuhusiana na Ule Muda wa Ukamataji Ukasema Ilikuwa ni Saa 7 Mchana na Pia Uliandika Kwenye Hati ya Upekuzi.. Na Ukasema Muda huo Ulikuwa Muda Sasa Sana Je Ulikuwa Umaanisha Nini

Shahidi: Nilikuwa namaanisha Haijavuka hiyo Saa Saba

Wakili wa Serikali: Pia Uliulizwa hapa Kwamba Siku ya Tarehe 09 August 2020 Ndiyo Siku Uliwapeleka Kituo cha Polisi Mbweni wewe na Mahita, Ukasema Siyo Kweli, Je Unamanisha Nini

Shahidi: Siyo Kweli Kwamba tuliwapeleka Kituo cha Polisi Mbweni Tarehe 09 August Bali Ilikuwa tarehe 08 August 2020

Wakili wa Serikali: Pia Umeulizwa Kwamba Mlienda Arusha, Ukaulizwa Kama ikiwa Unamfahamu Majina ya Huyo Dada yake Lijenje, Nyumba au Mtaa Ukasema Ufahamu, Hebu tufafanulie

Shahidi: Ni Kwa sababu wao Watuhumiwa ndiyo walikuwa wanatupeleka kila sehemu

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusu Kutomkamata Mshtakiwa Wa Nne Baada ya Wengine watatu Kukamatwa zaidi ya Mwaka Mmoja Ukasema Upelelezi Ulikuwa unaendelea, Je Ni Upelelezi upi

Shahidi: Masuala la Forensics na Upelelezi Mwingine Ulikuwa unaendelea

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Pia Maswali Kuwa katika Bastola hiyo Uliyo kamata ilikuwa ina Maeneo ambayo yangeweza Kutoa Finger Prints Ukasema ni Kweli, lakini haujaleta Mahakamani

Shahidi: Ni kweli Siku leta Ushahidi Wa Finger Prints Kwa sababu Hapakuwa na Mahaka Kwamba Silaha hiyo ilikuwa haina Ubishi kuwa inamilikiwa na Mtuhumiwa

Wakili wa Serikali:
Jana Uliulizwa kuhusu Katazo la Ku unLoad Silaha, Ukasema inategemea, Je Ulikuwa Unamanisha nini

Shahidi: Ni si Silaha ambayo imekuwa eneo la Tukio ndiyo haitakiwi Kuwa Unload lakini Silaha ambayo unataka Ku seize na Umeipata Kwa Mtu Unaruhusiwa Ku unload Kuona Kuna Kitu gani, Ndiyo Nilichomanisha..

Wakili wa Serikali: Uliulizwa hapa Kuhusu Mshtakiwa Wa tatu kuhusu Kwenda Kwa Mlinzi wa Amani ila Ukasema Hukuona sababu ya kwenda na wala Hakuhitaji

Shahidi: Ni Kwa sababu alikuwa tayari Kujaza Maelezo na Hakuona haja ya Kwenda Kwa Mlinzi wa Amani

Wakili wa Serikali: Uliulizwa utendaji wa shughuli Zenu Mmekuwa Mkishirikiana na Mamlaka Mbalimbali, Tufafanulie ni Ushirikiano Gani mnapeana

Shahidi: tunashirikiana na vyombo mbalimbali vya Usalama lakini kwa ngazi za Juu

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji naomba kukomea hapo hatutokuwa na swali lingine

Jaji: Kuna maeneo mawili ambayo mnayarudia upande wa utetezi

Wakili Peter Kibatala: Shahidi Ni kweli wakati unatoa ushahidi wako unaomba kutoa vielelezo hukufafanua kuwa kuna maofisa ambao hawatakiwi kusaini?

Shahidi: Hayo Sikusema

Kibatala: Uliposema maofisa wa chini ulimaanisha nini?

Shahidi:
Kuanzia Staff sergeant kurudi chini

Kibatala: Detective Coplo anatakiwa kusaini?

Shahidi: Hatakiwi kusaini Kibatala: kwa ruhusa ya Mahakama naomba usome Hapa Shahidi "F5914 Detective Coplo Hafidh Mohammed"

Kibatala: Huyo ni Afisa wa chini au siyo?

Shahidi:
Ni Afisa wa chini

Kibatala:
Amesaini au hajasaini?

Shahidi: AMESAINI

Wakili Dickson Matata: Mheshimiwa Jaji naomba P13

Matata: Shahidi, Jana wakati nakufanyia Dodoso Nilikuuliza Mtu Kupewa nauli na pesa ya matumizi Njiani ni Kosa au Siyo Kosa Ukasema Siyo Kosa Leo Wakati Unafanyiwa Re-examination Ukasema Siyo Kosa kama ulipewa kwa nia Njema

Sasa chukua hiyo Statement Nionyeshe Sehemu ambayo Mohammed Ling'wenya amesema alipewa hiyo Pesa ya Nauli na Matumizi ya Njiani Kwa nia Ovu

Shahidi:
Hakuna Aliposema

Wakili Matata: Mheshimiwa Jaji sina Swali Lingine

Jaji aandika Kidogo

Mahakama Ipo Kimya Kidogo

Jaji
Baada ya Maswali hayo Kuulizwa Upande wa Serikali Maswali Lolote?

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Hakuna swali Mheshimiwa Jaji

Jaji: Mmemaliza na shahidi wa 8?

Wakili wa Serikali: Ndiyo Mheshimiwa Jaji

Jaji: Shahidi Tunakuahukuru Kwa Ushahidi Wako

Shahidi anatoka na kuondoka kizimbani

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Huyo ndiye shahidi tuliyekuwa naye leo Hivyo tunaomba hairisho la Kesi hii ili kuja Kuendelea Kesho Kutwa Alhamisi tarehe 13 January 2022 Ambapo tutaleta shahidi mwingine kuja kuendelea na ushahidi

Na Pamoja na kwamba sasa ni saa saba mchana hatukuweza kujua shahidi Huyu angeweza Kumalizia Saa ngapi Hivyo tunaomba hairisho Mpka kesho kutwa kama nilivyo Omba, Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji

Wakili Peter Kibatala:
Hatuna Pingamizi Mheshimiwa Jaji

Jaji: Basi maombi ya hairisho yanakubaliwa mpaka kesho kutwa alhamisi ya tarehe 13 January 2022 Washtakiwa wataendelea kuwa rumande chini ya magereza mpaka siku hiyo Jaji anatoka

Tuendelee na kesi hii hapa keshokutwa tarehe 13
 
Jionee

Huu ndo ushahidi aliotuambia Sirro
Screenshot_20220111-112550.jpg
Screenshot_20220111-112514.jpg
Screenshot_20220111-112333.jpg
Screenshot_20220111-112039.jpg
Screenshot_20220111-111948.jpg
 
Back
Top Bottom