Elections 2015 Yaliyojiri Chato: Mkutano wa Mgombea urais kwa tiketi ya CHADEMA/UKAWA, Edward Lowassa

lowasa jamani mkuwa na huruma,kukupenda tunakupenda,kura tunakupa si ungemsamehe magufuli nyumbani kwao na najua siku akienda monduli atahutubia magamba toka mikoa mingine maana morani wa huko hata wabebwe na ndege hawaji mkutanoni
 
Jamani CCM si wamesema watashinda kwa asilimia 69,na wanasema utafiti wa kisayansi unaonesha hivyo kuwa watashinda hawana shaka................Marope Jr amejinasibu kuwa watashinda tu
 
LowassaChato.jpg

kama nyumbani kwao pako hivi ,ni wapi magufuri ataponea? labda la mkono
 
Sisi CCM tutasomba wanaCCM wote wa mikoa ya manyara arusha na moshi kusikiliza JPM Arusha. Baada ya hapo tutakuwa tumesawazisha ama vipi?
 
Niko chato ntaenda kwenye mkutano zikiwa zmebaki dk5 mkutano kuisha sababu na jua jamaa ataongea dk2 tu nakuondoka

Hatuitaji mtu anayeongea kama kameza cd alafu mwisho wa miaka mitano anaogopa hata kupita mitaa aliyopiga kampeni maana hana alichotekeleza. Uliza meli za ziwa victoria ziko wapi.
 
Hapa wote tuna akili, hivi kweli mnamsikia Lowasa akiongea? Kweli kila mtu anaweza patwa na chochote na hujafa umeumbika, kweli Lowasa anaweza kuongea jamani, mimi namkubali sana lakin naona kama jamani hebu tuwe fair kwa nchi yetu labda kama ni wasaidizi tu wataendesha nchi. Hakuna mtu anamweza kufurahia kuona mwenzake anaumwa lakin honestly anahitaji mapumziko. Nimesikiliza akiongea Geita there is nothing unaweza kusikia. Namuombea Mungu ampe afya njema InshaAllah.

Si bora hata huyo Lowass anaongea kidogo…lakini sisi tumedhamiria kuwa hata jiwe(ambalo haliongei) likishindana na CCM sisi tutachagua jiwe..Issue yetu hapa sio kuongea bali ni kulitoa shetani CCM…Bora kukaa kimya badala ya kutukana watu..umeshasahau Magufuli alivyotutukana sisi wa Kigamboni?? "Kama hamna nauli pigeni mbizi"" Na hapo Chato kawatukana watu wa kwake "WANYE BARABARANI WASAMBAZE KINYESI IWE RAMI"
Sasa si bora kukaa kimya ndio busara mkuu!!
 
mkuu nimeangalia link yako mbona hali ni ya hatari sana...
nimeamini kuwa watu wanataka mabadiliko....yaani sikutegemea hali kama ipo hivi...
pia nimemuona magufuli mwishoni kaunga mkono chadema kwa kuonyesha alama ya v kwakutumia vidole...au nimekosea....duhhhh lowassa noma yaani noma sana....ccm kinacho wasaidia wamenunua midia maana vitu kama hivi wana vifuta mkuu


Nyie jamani msipende kudanganywa na maccm, hebu Magufuli aitishe walau mikutano miwili tuu na waambiwe watu hakuta kuwa na wasanii ndio mtauona mziki wake ulivyo mgumu. Mikutano yote ya CCM inaonekana na watu wengi ni kwa vile kuna wasanii basi. Hiyo ndio sababu CCM iko tayari kuwalipa kiwango chochote wasanii ili kuficha aibu.
Hali halisi bila wasanii ni kama hivi
https://www.facebook.com/peter.datti/posts/1667488713467547
 
Anangoja kuapishwa kwa kuwa wote hao wamejiandikisha kupiga kura na watampigia!! Lowasa anatosha!!
 
Kidole kitamponya, maana nape sasa anajiandaa kutumia kidole badala ya mkono
 
MAKAMBA:LOWASA ALIFUKUZWA KAZI,
HAKUJIUZULU!
Katibu mkuu mstaafu wa CCM luteni mst Yussuf Makamba amesema kuwa aliyekua Waziri Mkuu Edward Ngoyai Lowasa alikua ameshafukuzwa kazi kabla ya kujiuzulu.
Makamba ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa kampeni za Urais za CCM katika kiwanja cha Kawawa mjini Kigoma.
Akifafanua suala hilo mzee Makamba amesema kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM katika kikao kilichokaa mjini Dodoma, baada ya kuridhika kuwa Lowasa alihusika na kashfa ya Richmond,iliteua watu watatu kwenda kumuona Rais Kikwete kumueleza kuwa kwa maslahi ya nchi na chama amfute kazi Waziri Mkuu wake Edward Lowasa kwakua kamati ya uongozi imeridhika kuwa alimuita na kashfa ya Richmond na kulifedhehesha taifa.
Watu hao watatu walikua katibu mkuu wa CCM wakati huo mzee Makamba, mzee Samuel Malecela na mama Anna Abdallah.
"Tulipofika kwa Rais Kikwete tulikutana na Lowasa nje akitokea ndani kwa Rais, tukaingia na kumkuta bwana mkubwa. Tukapewa kahawa. Kisha tukamueleza kuwa tumetumwa na kamati ya uongozi ya wabunge wa CCM kuwa Waziri mkuu amehusika na kashfa ya Richmond na kwa heshima ya CCM na taifa amfukuze kazi.
Rais Kikwete akatuuliza,
...hamjakutana nae hapo nje?
Tukajibu...tumekutana nae anatoka...
Akasema...nimekwisha kumwambia kuwa kwa heshima ya taifa na CCM hawezi kuendelea kuwa waziri mkuu tena na kwamba nateua waziri mkuu mwingine...
Makamba alisema kuwa baada ya Rais kumfukuza kazi Lowasa, kesho yake asubuhi Lowasa aliamkia bungeni na alipopewa nafasi ya kujitetea alisema tatizo nu uwaziri mkuu na kwamba amemuandikia barua Rais aachie ngazi.
"Ukweli ni kwamba Rais alishamfukuza kazi Lowasa usiku wa kuamkia siku aliyotangaza kiachia ngazi na kujiuzulu. Lakini tuliamua kumsitiri. Sasa kwakua kaamua kusema, nasi tumekuja kueleza akiba tuliyoweka."

Na Mwandishi wetu,
Kigoma
 
Back
Top Bottom