kalulukalunde
JF-Expert Member
- May 27, 2016
- 1,056
- 1,083
MKUTANO wa Nne wa Bunge la 11 umeanza leo mjini Bungeni Dodoma, huku miswada sita ukiwemo wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari ukitarajiwa kuchukua nafasi kubwa.
Pia wabunge mbalimbali wa upinzani ambao mwanzo waligoma kuendelea na vikao vya bunge lililopita kwa madai ya Naibu Spika kutowatendea haki wabunge wa upinzani.
-------------------------------------
MKUTANO wa Nne wa Bunge la 11 unatarajiwa kuanza leo mjini hapa, huku miswada sita ukiwemo wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari ukitarajiwa kuchukua nafasi kubwa.
Katika mkutano huo, wabunge wa kambi ya upinzani ambao walisusia siku kadhaa za mkutano uliopita, wamesema kwamba watahudhuria.
Mbunge wa Vunjo, James Mbatia (NCCR-Mageuzi), alithibitisha jana kwamba wabunge wa upinzani wataingia bungeni.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano ya Bunge kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana, jumla ya maswali 110 yanatarajiwa kuulizwa na wabunge na kujibiwa na Serikali.
Aidha, Waziri Mkuu anatarajiwa kuulizwa maswali 16 ya papo kwa hapo. Taarifa hiyo ilisema miswada sita ya sheria iliyosomwa kwa mara ya kwanza katika Mkutano wa Tatu wa Bunge na baadaye kupelekwa katika kamati husika ili ifanyiwe kazi, itaendelea kushughulikiwa katika hatua zinazofuata ikiwa ni pamoja na kusomwa kwa mara ya pili, kamati ya Bunge zima na kusomwa kwa mara ya tatu.
Miswada hiyo ni pamoja na ule wa Sheria ya Upatikanaji wa Habari ya mwaka 2015, Muswada wa Sheria ya Utathmini na Usajili wa Wathamini wa mwaka 2016, Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serika wa mwaka 2016.
Pia utakuwepo Muswada wa Sheria ya Usimamizi wa Wanataaluma wa Kemia wa mwaka 2016, Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Kilimo wa mwaka 2016 na Muswada wa Sheria ya Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi ya mwaka 2016.
Kufikia jana, mji wa Dodoma ulikuwa umefurika wageni balimbali wakiwemo wabunge na maofisa wa serikali wanaohamia tayari kuanza kuendesha shughuli zao katika makao makuu mapya ya Serikali, mjini hapa.

Mbunge wa Jimbo la Kilolo Venance Mwamoto ameuliza swali bungeni kwanini serikali isifute michezo nchini kutokana mwenendo mbaya wa matokeo?
Tujadiliane kwanini serikali isiifute michezo nchini???
Wadau mnaonaje chango wa mbunge wetu?View attachment 394610