Funa the Great
Senior Member
- Aug 1, 2022
- 160
- 271
YALIYOJIFICHA JUU YA HISTORIA YA HIFADHI YA TAIFA ARUSHA NA MAAJABU YA VIVUTIO VYAKE.
EPISODE 1
Hifadhi ya taifa Arusha inapatikana kaskazini mwa Tanzania ndani ya mkoa wa Arusha. Ni hifadhi inayokadiriwa kuwa na kilomita za mraba zisizopungua 500 sq. km. Huchukua takribani dakika 45 kuifikia hifadhi hii kutoka Arusha mjini.
Nakurudisha mnamo mwaka 1876 mwaka ambao haukuwa kwenye mipango ya wewe kuletwa Duniani.
Mnamo mwaka 1876 mpelelezi kutoka taifa la Hungary aliyefahamika kwa jina la Count samuel Teleki alipata nafasi ya kutembelea eneo la Afrika Mashariki hususani nchini Tanzania na Kenya. Alitembelea moja ya eneo linalofahamika kwa jina la Momella. Momella ni miongoni mwa eneo linalopatikana ndani ya hifadhi ya taifa Arusha kwa sasa.
Count Teleki ni mpelelezi wa kwanza kuliona Ziwa Turkana linalopatikana kati ya Ethiopia na Kenya. Pia aliweza kutembelea maeneo mengine ya Tanzania ikiwemo Mlima Kilimanjaro, Pangani na bonde la mto Ruvu. Naam sihitaji nikutoe nje ya mada tuendelee na mada yetu.
Count Teleki hakuwa na mengi ya kusimulia zaidi ya kutoa maoni juu ya kile alichokiona ndani ya eneo ilo, alifanikiwa kuona makundi ya wanyama ikiwemo Viboko na Vifaru.
1907
Familia ya mkulima kutoka Afrika Mashariki aliyefahamika kwa jina la TAPE akiwa na familia yake alitembelea eneo la Ziwa Momella na kuanzisha makazi kwa ajili ya shughuli za kilimo na ufugaji ndani ya eneo ilo. Mnamo mwaka 1960 mashamba hayo yaligeuzwa na kubadilishwa kuwa hifadhi.
1960
Ilianzishwa hifadhi iliyofahamika kwa jina la Ngurdoto Crater. Hifadhi hii ilianzishwa kwa lengo la kuhifadhi maeneo makuu mawili, Crater ya Ngurdoto na Mlima Meru (haya yote ni maeneo yanayopatikana ndani ya hifadhi ya taifa Arusha kwa sasa ikiwa ni miongoni mwa vivutio vya utalii).
1967
Huu ni mwaka ambao hifadhi ya Ngurdoto crater ilibadilishwa jina na kuitwa hifadhi ya taifa Arusha. Ilipewa jina ilo kutokana na jamii ya watu Waarusha waliokuwa wakiishi kwenye eneo ilo. Hadi sasa inaitwa hifadhi ya taifa Arusha. Kuanzia hapo serikali ikaanza kuwekeza nguvu kuweka miundombinu rafiki kwa ajili ya wageni.
UNATAKA KUFAHAMU MAAJABU YA VIVUTIO VINAVYOPATIKANA NDANI YA HIFADHI YA TAIFA ARUSHA? TUKUTANE EPISODE INAYOFUATA.
KWA HUDUMA ZA SAFARI ZA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII CHEKI NAMI +255622174613
SAFARI ZA MARAFIKI, FAMILIA, COUPLES, SHULE/VYUO, KIOFISI N.K
Pia soma: Yaliyojificha juu ya historia ya hifadhi ya taifa Arusha na maajabu ya vivutio vyake (episode 2)