Yaliyojificha juu ya historia ya hifadhi ya taifa Arusha na maajabu ya vivutio vyake (episode 2)

Funa the Great

Senior Member
Aug 1, 2022
160
271
EPISODE 2

Hifadhi hii ina vivutio vingi vyenye upekee wake vyenye kukufanya ubaki na kumbukumbu zisizofutika.

ZIWA MOMELLA

Ndani ya hifadhi ya taifa Arusha kuna mgawanyiko wa maziwa makuu mawili. Hakuna mito inayopeleka maji kwenye maziwa hayo bali huingiza maji kutoka chini ya ardhi.

1. Ziwa Momella dogo.

Hupata maji kutoka chini ya ardhi na maji yake yana chumvi. Pembezoni mwa ziwa kuna eneo lenye maji yasiyo chumvi ambapo ni makazi ya viboko. Hukadiriwa kuwa na urefu wa kina cha mita 4 hadi 10.2. Hupatikana jamii mbalimbali za ndege ikiwemo Grebe, Pochard, Common Sandpiper, sacred & Hadad ibis.
IMG_20231122_023757_131.jpg

2. Ziwa Momella Kubwa

Hupata maji yake kutoka ardhini na maji yake ni ya chumvi ni ziwa lilitokana na mlipuko wa volcano. Hukadiriwa kuwa na urefu wa kina chenye mita 31m. Hupatikana ndege jamii ya Flamingo wanaohama kutoka hifadhi ya taifa Arusha hadi Ziwa Manyara na kinyume chake. Ni ziwa lenye kiwango kikubwa cha madini ya Fluoride ulimwenguni.
IMG_20231122_023903_777.jpg

MTI WA FIG (FIG TREE)

Huu ni mti wenye uwazi mkubwa katikati ambapo magari, binadamu na wanyama wanaweza katiza katikati yake. Hakuna aliyehusika kutengeneza uwazi huu bali ni mizizi ya mti huo ndiyo uota kwa staili iyo.

Mnamo tarehe 09/11/2011 mfalme Charles wa III na malkia wake walipata nafasi ya kufika hapa.
IMG_20231126_180912.png

CRETA YA NGURDOTO

Hii ni creta iliyotokana na mlipuko wa volcano ni creta kubwa ambapo ndani yake kuna jamii ya nyani aina ya mbege wanapatikana. Katika historia inasemekana ndani yake kulikuwa na vifaru ambao baadaye waliuwawa na majangiri.
IMG_20231126_180843.png

SERENGETI NDOGO

Hili ni eneo ambalo lina mchanganyiko wa wanyama mbalimbali ambao hukusanyika na kukaa pamoja. Imeitwa Serengeti ndogo kutokana na mwonekano wake kuwa kama hifadhi ya Serengeti (Ina eneo kubwa la wazi).
IMG_20231126_180810.png

UWANJA WA MBOGO

Hili ni eneo ambalo kuna jamii ya Nyati peke yake hakuna wanyama wengine. Nyati hawa ni wapole unaweza tembea kando yao kwa miguu na ukawapiga picha kwa ukaribu.
images (3)_1701023294506.jpeg

MAPOROMOKO YA MAJI TULULUSIA

Haya ni maporomoko ya maji marefu ambayo humwaga maji yake kwa kishindo. Miaka ya nyuma wamasai walikuwa wakitumia eneo ilo kwa ajili ya mawindo walikuwa wakikaa juu ya maporomoko na kuvizia wanyama waliokuwa wanaenda kunywa maji.
IMG_20230909_002529.jpg

Mnamo tarehe 9/11/2011 mfalme Charles wa III na malkia Camilla Cornwall walipata nafasi ya kutembelea eneo hilo.

MAPOROMOKO YA MAJI MAIO

Haya ni maporomoko ambayo pembezoni yake kuna mandhari tulivu kwa ajili ya kupata lunch kwa wageni. Kitaalamu huitwa PICNIC LUNCH (Chakula ambacho watu huandaa kula ndani ya eneo lenye kivutio).
IMG_20231126_180929.png

MLIMA MERU

Huu ni mlima wa pili kwa urefu baada ya Kilimanjaro ni mlima ambao utauona kwa uzuri sana ukiwa ndani ya hifadhi ya taifa Arusha.
IMG_20231126_180826.png

KWA HUDUMA ZA SAFARI ZA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII CHEKI NAMI +255622174613

SAFARI ZA MAKUNDI, MARAFIKI, FAMILIA, COUPLES, SHULE/VYUO, KIOFISI N.K

KARIBU UJUMUIKE NASI KWENYE SAFARI YA KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA MIKUMI NA MAPOROMOKO YA MAJI CHOMA KUANZIA TAREHE 16-17 DECEMBER 2023 KWA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NAMI KUPITIA?+255622174613

Pia soma:Yaliyojificha juu ya historia ya hifadhi ya Taifa Arusha na maajabu ya vivutio vyake
 
EPISODE 2

Hifadhi hii ina vivutio vingi vyenye upekee wake vyenye kukufanya ubaki na kumbukumbu zisizofutika.

ZIWA MOMELLA

Ndani ya hifadhi ya taifa Arusha kuna mgawanyiko wa maziwa makuu mawili. Hakuna mito inayopeleka maji kwenye maziwa hayo bali huingiza maji kutoka chini ya ardhi.

1. Ziwa Momella dogo.

Hupata maji kutoka chini ya ardhi na maji yake yana chumvi. Pembezoni mwa ziwa kuna eneo lenye maji yasiyo chumvi ambapo ni makazi ya viboko. Hukadiriwa kuwa na urefu wa kina cha mita 4 hadi 10.2. Hupatikana jamii mbalimbali za ndege ikiwemo Grebe, Pochard, Common Sandpiper, sacred & Hadad ibis.
View attachment 2826159

2. Ziwa Momella Kubwa

Hupata maji yake kutoka ardhini na maji yake ni ya chumvi ni ziwa lilitokana na mlipuko wa volcano. Hukadiriwa kuwa na urefu wa kina chenye mita 31m. Hupatikana ndege jamii ya Flamingo wanaohama kutoka hifadhi ya taifa Arusha hadi Ziwa Manyara na kinyume chake. Ni ziwa lenye kiwango kikubwa cha madini ya Fluoride ulimwenguni.
View attachment 2826160

MTI WA FIG (FIG TREE)

Huu ni mti wenye uwazi mkubwa katikati ambapo magari, binadamu na wanyama wanaweza katiza katikati yake. Hakuna aliyehusika kutengeneza uwazi huu bali ni mizizi ya mti huo ndiyo uota kwa staili iyo.

Mnamo tarehe 09/11/2011 mfalme Charles wa III na malkia wake walipata nafasi ya kufika hapa.
View attachment 2826161

CRETA YA NGURDOTO

Hii ni creta iliyotokana na mlipuko wa volcano ni creta kubwa ambapo ndani yake kuna jamii ya nyani aina ya mbege wanapatikana. Katika historia inasemekana ndani yake kulikuwa na vifaru ambao baadaye waliuwawa na majangiri.
View attachment 2826162

SERENGETI NDOGO

Hili ni eneo ambalo lina mchanganyiko wa wanyama mbalimbali ambao hukusanyika na kukaa pamoja. Imeitwa Serengeti ndogo kutokana na mwonekano wake kuwa kama hifadhi ya Serengeti (Ina eneo kubwa la wazi).
View attachment 2826163

UWANJA WA MBOGO

Hili ni eneo ambalo kuna jamii ya Nyati peke yake hakuna wanyama wengine. Nyati hawa ni wapole unaweza tembea kando yao kwa miguu na ukawapiga picha kwa ukaribu.
View attachment 2826164

MAPOROMOKO YA MAJI TULULUSIA

Haya ni maporomoko ya maji marefu ambayo humwaga maji yake kwa kishindo. Miaka ya nyuma wamasai walikuwa wakitumia eneo ilo kwa ajili ya mawindo walikuwa wakikaa juu ya maporomoko na kuvizia wanyama waliokuwa wanaenda kunywa maji.
View attachment 2826165

Mnamo tarehe 9/11/2011 mfalme Charles wa III na malkia Camilla Cornwall walipata nafasi ya kutembelea eneo hilo.

MAPOROMOKO YA MAJI MAIO

Haya ni maporomoko ambayo pembezoni yake kuna mandhari tulivu kwa ajili ya kupata lunch kwa wageni. Kitaalamu huitwa PICNIC LUNCH (Chakula ambacho watu huandaa kula ndani ya eneo lenye kivutio).
View attachment 2826172
MLIMA MERU

Huu ni mlima wa pili kwa urefu baada ya Kilimanjaro ni mlima ambao utauona kwa uzuri sana ukiwa ndani ya hifadhi ya taifa Arusha.
View attachment 2826167

KWA HUDUMA ZA SAFARI ZA KUTEMBELEA VIVUTIO VYA UTALII CHEKI NAMI +255622174613

SAFARI ZA MAKUNDI, MARAFIKI, FAMILIA, COUPLES, SHULE/VYUO, KIOFISI N.K

KARIBU UJUMUIKE NASI KWENYE SAFARI YA KUTEMBELEA HIFADHI YA TAIFA MIKUMI NA MAPOROMOKO YA MAJI CHOMA KUANZIA TAREHE 16-17 DECEMBER 2023 KWA TAARIFA ZAIDI WASILIANA NAMI KUPITIA?+255622174613

Pia soma:Yaliyojificha juu ya historia ya hifadhi ya Taifa Arusha na maajabu ya vivutio vyake
Very nice.
Episode ya kwanza iko wapi?
 
Makadirio ya safari kwa siku ni shs ngapi kwa familia ya watu wanne??
Gharama hutegemeana na mambo yafuatayo

Hapo kutakuwa na gharama ya kiingilio kwa watoto na watu wazima, watoto chini ya Miaka 5 hawalipii ni bure, miaka 5-16 wanalipia. (Sijajua watoto wana umri gani?)

Gharama ya usafiri, itategemea mnakodi au mnalo private., kutakuwa na malipo ya gari getini (parking fee). (Sijajua mna Usafiri binafsi au lah?)

Gharama za kufanya utalii wa kutembea kwa miguu (walking safari)
Gharama za Mwongoza watalii.

Nikishafahamu ivyo nitakupa Gharama Whatsapp +255622174613
 
Niwe mkweli niliwahi kutembelea hii hifadhi wanyama ni wachache Sana sana Yani.....
Unahitaji wanyama wengi kwani unakwenda kununua useme utakosa machaguo mengi, isitoshe mleta mada kaongelea sana mazingira nasio wanyama.Aisee wabongo tunakurupuka!.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom