Funa the Great
Senior Member
- Aug 1, 2022
- 160
- 271
Hifadhi ya taifa ya mlima Udzungwa inapatikana ndani ya mkoa wa Morogoro, Tanzania. Ni hifadhi ilivyobarikiwa kuwa na mandhari hadhimu yenye kuvutia.
Ni hifadhi ambayo ina upekee wake, ni hifadhi ambayo ina viumbe ambao hupatikana Udzungwa Pekee ulimwenguni kote kitalaamu hufahamika kama Endemic species mfano Mbega wekundu wanaotambulika kwa jina la Iringa Red Colobus.
Ni hifadhi yenye maporoko ya maji yenye kuvutia machoni. Ndani ya hifadhi hiyo kuna maporoko makubwa yenye urefu wa mita 170 yanayofahamika kwa jina la Sanje Waterfalls.
Hukifika Udzungwa hutojutia zaidi utatamani uendelee kusalia hapo maana pamebarikiwa uwepo wa mandhari nzuri yenye kukupatia hewa safi, utaogelea, Kupanda milima na kuona wanyama mbalimbali.
Njooni tutalii pamoja, Utalii ni wetu sote.