Yaani walimu shule za msingi mmefikia hapa?

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
Tafadhali soma hii taarifa iliyotolewa na Wizara ya Elimu Tanzania, tafakari na chukua hatua!


NB: Kwa wenye kutumia simu taarifa yenyewe ni hii hapa!

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
Anuani ya Simu: “ELIMU”
DAR ES SALAAM.
Simu: 2110146, 2120403, 2122373,
2120412/5/7/8/9
Telex: 42741 Elimu Tz.
Fax: 2113271 Elimu Tz

Unapojibu tafadhali taja:
Kumb. Na.CHA-135/265/01/69
S.L.P. 9121,
DAR ES SALAAM.
Tarehe: 21/05/2012

Makatibu Tawala wa Mikoa
Makatibu Tawala wa Wilaya
Maafisa Elimu wa Mikoa
Maafisa Elimu wa Wilaya
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Kanda
Wakaguzi Wakuu wa Shule wa Wilaya
Wakuu wa Shule za Sekondari
Walimu Wakuu wa Shule za Msingi
TANZANIA BARA.

YAH: MWONGOZO KUHUSU UWEKAJI WA ALAMA NYEKUNDU KWENYE SARE
ZA SHULE KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA MSINGI WENYE MATATIZO YA
KIAFYA

Kumekuwepo na taarifa katika baadhi ya shule za Msingi kuhusu uwekaji wa alama
nyekundu kwenye sare za shule kwa wanafunzi wa shule za Msingi wenye matatizo ya
kiafya wakiwemo wale wenye VVU na UKIMWI. Uwekaji wa alama nyekundu katika
sare za wanafunzi hao ni ukiukwaji wa haki za binadamu pamoja na sheria za nchi.
Uamuzi wa kuwawekea alama wanafunzi hao haukubaliki kimataifa na kitaifa kwani
jamii ina mtazamo hasi juu ya matumizi ya alama hizo. Jambo hili linakuza unyanyapaa
na ubaguzi wa watoto hao na kusababisha wanafunzi hao kushindwa kuhudhuria
masomo ipasavyo.

Mwaka 2008 Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilipitisha sheria ijulikanayo
kama HIV and AIDS (Prevention and Control) Act No. 28 sheria hii inapiga marufuku
unyanyapaa wa aina yoyote kwa watu wenye VVU na UKIMWI.

2
Baraza la Taifa la watu wanaoishi na VVU (NACOPHA) ambacho ni chombo cha kitaifa
chenye jukumu la utetezi wa haki za binadamu kwa watu wanaoishi na virusi vya
UKIMWI kinakemea tabia hiyo ya wanafunzi kuwekewa alama nyekundu mabegani.
Kimsingi uwekaji huu wa alama ni ukiukwaji wa haki za binadamu.
Walimu wakuu wa shule za Msingi pamoja na walimu ni wajibu wenu kuzifuata sheria
za nchi ili mtoto apate haki yake inayostahili ya kupata elimu inayokusudiwa.
Hivyo, wizara inawataka walimu wakuu kusitisha mara moja uwekaji wa alama
nyekundu mabegani kwa wanafunzi wenye VVU na UKIMWI pamoja na wanafunzi
wenye matatizo mbalimbali ya kiafya.

Mwongozo huu unaanza kutumika mara moja.

M.M. Wassena
KAIMU KAMISHNA WA ELIMU
Nakala: Katibu Mkuu, Katiba na Sheria S.L.P. Dar es Salaam
“ Katibu Mkuu (Elimu) TAMISEMI S.L.P. Dodoma
“ Mwenyekiti wa Baraza NACOPHA S.L.P. Dar es Salaam

Chanzo: Wizara ya Elimu. www.moevt.go.tz.
 

Attachments

  • MWONGOZO KUHUSU UWEKAJI WA ALAMA NYEKUNDU KWENYE SARE_ 13_06_2012.pdf
    183.8 KB · Views: 161
Hvi c naskiaga mr dhaifu nae ana ukimwi au ni umbea wa watu tu?
 
Back
Top Bottom