Wizi wakati wa kuweka pesa kwa wakala

Mpigadili Tz

JF-Expert Member
May 4, 2015
1,042
1,821
Habari zenu wakuu,

Mimi ni mfanya biashara katika biashara yangu pia nimeweka mambo ya huduma za kipesa za mitandao (Wakala), sasa jana majira ya saa tisa kuna mtu alikuja akasema:

Jamaa: niwekee Tigo pesa laki 8 na voda niwekee laki moja
Mimi: poa (jamaa akanipa pesa nikazihesabu zikawa sahihi laki 9).
Jamaa: Ah niwekee na 7500 tigo pesa na 3000 voda nifanye kama ya kutolea maana baadae nitazitoa.
Mimi: poa (jamaa akanipa 10500)
Jamaa: Ah sikia basi nipe hizo pesa nimeghairi (mimi nikamkabidhi)
Jamaa: lakini poa we niwekee tu maana kutembea nazo pia naona ovyo (jamaa akanikabidhi tena).

Mimi nikazichukua zile pesa nikazieka katika droo nikamuekea kisha akaondoka dah! Nakuja kuzicheki zipo laki mbili zilizojaa 2000 na 10000 tatu, nikajaribu kuwapigia Voda wamesema jamaa kashazitoa ila nenda polisi alafu nenda TCRA, nikwapigia Tigo wamesema jamaa kashazitoa nikwauliza mtanisaidiaje wamesema hatuna cha kukusaidia.

HIVI WAKUU NINI NAWEZA KUFANYA?
 
Mungu akupe nguvu kwenye wakati huu mgumu kwako,,hope utakua na amani,,,sidhani kama kuna sharia kwenye hili zaidi ya kupoteza muda na hela zaidi
 
Hii mbinu ilishaanikwa hapa JF siku za nyuma, huenda ungepata kupitie ile thread ya yule mdau haya yote yasingekukuta.

Pole sana ndugu.
 
Habari zenu wakuu,

Mimi ni mfanya biashara katika biashara yangu pia nimeweka mambo ya huduma za kipesa za mitandao (Wakala), sasa jana majira ya saa tisa kuna mtu alikuja akasema:

Jamaa: niwekee Tigo pesa laki 8 na voda niwekee laki moja
Mimi: poa (jamaa akanipa pesa nikazihesabu zikawa sahihi laki 9).
Jamaa: Ah niwekee na 7500 tigo pesa na 3000 voda nifanye kama ya kutolea maana baadae nitazitoa.
Mimi: poa (jamaa akanipa 10500)
Jamaa: Ah sikia basi nipe hizo pesa nimeghairi (mimi nikamkabidhi)
Jamaa: lakini poa we niwekee tu maana kutembea nazo pia naona ovyo (jamaa akanikabidhi tena).

Mimi nikazichukua zile pesa nikazieka katika droo nikamuekea kisha akaondoka dah! Nakuja kuzicheki zipo laki mbili zilizojaa 2000 na 10000 tatu, nikajaribu kuwapigia Voda wamesema jamaa kashazitoa ila nenda polisi alafu nenda TCRA, nikwapigia Tigo wamesema jamaa kashazitoa nikwauliza mtanisaidiaje wamesema hatuna cha kukusaidia.

HIVI WAKUU NINI NAWEZA KUFANYA?
Ama kweli wewe boya, usifanye hivyo siku nyingine. Akikwambia nipe nimehairisha, mpe na usizipokee tena kama atakuwa anataka kuwekewa tena. Watoto wa mjini huiita hiyo kanyaboya. Iko tangu longtime.
Kama ndo unaanza biashara kuwa makini na CASH.
Soma kuhusu CASH Management na pia CASH Fraud
 
majina ya kusajilia line si ya kweli utamtafuta ngatuni asha Tanzania nzima hayupo
Nini chakufanya ni rahisi vitambulisho vya Taifa vitakapokamilika nimuhimu kila anayetaka kwenda kufungua na aliyekwisha fungua line ya simu lazima isajiliwe na namba ya kitambulisho cha Taifa.nini maana yake hapo ataka kama mtu akiwa na namba hamsini za simu ila atakuwa na utambulisho mmoja Wa utanzania.na sharia kali itungwe kwa mtandao wowote ambao hautafanya hivyo warawajibika kuwalipa wateja wao haraka sana pesa zao
 
Ama kweli wewe boya, usifanye hivyo siku nyingine. Akikwambia nipe nimehairisha, mpe na usizipokee tena kama atakuwa anataka kuwekewa tena. Watoto wa mjini huiita hiyo kanyaboya. Iko tangu longtime.
Kama ndo unaanza biashara kuwa makini na CASH.
Soma kuhusu CASH Management na pia CASH Fraud
Kila mjanja ana mjanja wake ila nashukuru kwa ushauri
 
pole sana ndugu yngu, kuna muda unaweza fikiria kuroga mtu kwa mambo aya na ukikumbuka jinsi ulivyoanza na mtaji wa laki 1 mpaka umefikia apo ni safari ndefu but kama umeajiliwa unafikiria jinsi ya kuzilipa kwa bosi INATIA HASIRA SANA. tafuta mganga akusaidie.
 
Tatizo lako ulimwamin yule mtu ungezihesabu tena mbona wengi wameshaibiwa kws stail hiyo
 
Hapana nadhani hapa hakuna kumlinda mlaji.mbona watu wakitukana kwenye mitandao kuna kumlinda mlaji na kumjua ni nani anayehusika sasa niulize kitu kimoja wanashindwa nini kumfuatilia aliyechukua pesa
ni kweli aende polisi halafu tcra tumesikia juzi hizi kampuni zimetozwa faini kwa kutoa sm kadi bila kusajili kwa kiwango kikubwa wao wanahusika
 
Back
Top Bottom