Moja ya kumbukumbu mbaya machimboni nchini Msumbiji. Lakini maisha lazima yaendelee

IBRA wa PILI

JF-Expert Member
Oct 12, 2017
1,448
2,289
Mwaka 2021 nikiwa hapa home tz nilikua na pesa flani ambayo nilipanga niagize bidhaa Ali express nianze kuuza maana Nina uzoefu na kuagiza mizigo huko kutoka China through Ali express bahati mbaya ikaingia Corona ikavuruga mipango yote.

Nilishawai leta thread ya kutaka ushauri wa kununua bidhaa na kuja kuuza tz nafikiri hapa sasa najibu hua naulizwa kwenye Ile thread kama nilifanikiwa Ila Corona ilifanya yake nilishindwa.

Kwani ilikua ukiagiza kitu kina kaa muda mrefu Sana mpaka kuja bongo na mara nyingine visije kabisa so nikaona niache mpaka Mambo yakae Sawa Ila sasa pesa na shida avi msubiri mtu pesa ikaingia kwenye ishu zingne na ikaishia mbali.

Turudi nyuma
Mshikaji wangu mmoja mchizi wangu Sana rafiki wa damu mno mno Sana tume skuli wote kidato mpaka four tume maliza wote bweni moja kitanda kimoja na matukio mengi ya shule tumehusika pamoja wizi ule wa shule mitaani kwa Wana kijiji miogo, mahindi, kuku utoro some day ndio ilikua ivyo miaka 10+ imepita tukiwa secondary.

Kanisaidia vingi pia sivungi kwani kule shule kipesa alikua ananizid bi mkubwa wangu akua na uwezo wa kunipa pesa nyingi skul alinipa walau kwa uwezo mshikaji akunitenga pesa ikiisha basi tuna Ganga wote simtaji Mzee Sana Mzee wangu R.I.P FATHER alitutoka two thousand and four nikiwa mdogo primary.

Kwa class upande wa academic nilimzidi kidogo ukweli na tukiwa kwa paper au exercise za kawaida basi nilikua nikimpa tafu kwa uwezo wangu Ila walikua vipanga wenyewe siwagusi hata robo.

Mwaka 2015 niliingia Mozambique chimbo flani jina kapuni jamaa yangu uyu alikua uko na alienda baada ya ndugu yake kufariki ivyo aliacha aset kule na ishu zingine, so yeye na wa dogo zake wakaenda uko kuendeleza biashara wao waliingia 2011.

yeye ndio aliniunganisha na jamaa mmoja nikafanye kazi ya mpesa na kipindi icho life kitaa limenipiga mno.

Ikawa poa uyo Nika go uko Mozambique kwa usafiri wa pikipiki kwa mara ya Kwanza naingia kule tulipita mto ruvuma mitomoni pale unavuka na mtumbwi then unaendelea na safari unafika getin unakuatana na Askari wa MSUMBIJI na ishu kama izo.

Nimeingia kule nasikia mashine zinapiga kelele Sana kumbe ndio zinasaga mawe kwajili ya kufanya process za kupata dhahabu vijumba vya turubai vipo kwenye milima sehemu zingne baa wadada wapo kihasara mbaya wapo kutafuta lipa pesa upige mzigo akuna mtongozo pesa ndio yenyewe.

Nakumbuka wakati naenda kwa yule bosi nilisikia mlio wa buuuuuuuuu nikaisi zile pigo za kusema msumbji hatari ndio hizi risasi zimeanza nini lakini wenyeji wako Safi tu hawana wasi wasi baadae nilikuja kujua kumbe ni baruti za kulipulia miamba uko migodini ndio walikua wanalipua.

Note
Kule umalaya wa dada wanalipia means kama ufanyi umalaya utajua wewe Ila awajasema wazi wazi iyo ni kila mwezi elf 5 na wanaume elf 10 na ni lazima japo wenyewe wanasema CHANJO ukiwa mgeni utafikiri labda chanjo hii tunayoijua huku tz sio iyo.

Wanaume unalipia ef kumi sababu ya kuchimba madini na mademu wanalipa kwa kuuza uchi Ila haijasemwa wazi so kule mademu wanauza Sana uchi ndio mana machimbo swala la Ngoma ni kawaida na ukija ukiwa mgeni wa wanawake aisee utaishia kufa Ka ngiri kama utumii kinga.

Ndio maana huku mitaani Tanzania wakisikia demu katoka chimbo vijana wanakaa far sababu inajulikana {70%} mademu kule ni kuuza uchi full kulombesha ndio maana huogopeka tofauti na wanaume sioni wakiogopeka.

Mademu wanakuja kule kufanya kazi hizi za bar na migahawani lakini wote mwisho wa siku wanaingia kwenye mkumbo wa kuuza uchi hawa wa bar ndio kuzidi demu akija anaweza akawa na misimamo yake Sana sio wote wengine wanabaki ivyo ivyo au wanakua tu na mtu mmoja basi lakini wengine muda tu anabadilika na kuanza kutumia fursa ya biashara isio filisika na hua wanapiga pesa ki ukweli zile shaha shaha au fasta fasta ndio usiseme una mchukua demu unazunguka nae tu nyuma kwenye maficho anainama unapiga kimoko cha fasta unampa pesa anarudi kuhudumia wateja baani.

Wa migahawani sasa anakuletea msosi geto huko huko unapiga testes (p....u) anachukua chake yani ni shida na full uchafu alafu anarudi kuhudumia mgahawani aise japo hii tabia waliikataza ikigundulika unalimwa faini.

Sababu inayosababisha mpaka kuingia kwenye kuuza miili Kwanza mshahara mdogo na kule wanakaa ki mkataba miezi mitatu mshahara elfu 40 mpaka 50 kila mwezi Kwa lile chimbo nililokuepo Mimi sijui machimbo mengine.

So ni pesa ndogo alafu wanakopa nguo Kali bei juu wanalipaje lazima waingie uko au wapate mtu anae toa pesa Sana ivyo akimaliza mkataba kama Hana madeni anakua na laki na 50 au laki na 20 anarudi vipi na iyo anajiongeza kucheza labda upatu na hii nayo risk mtu anaweza kupokea pesa alafu siku ya pili asubuhi au usiku anatoroka ivyo kimtindo anaweza Rudi na 500k au zaidi lakini mbususu imechakazwa Sana yaani mbaya.

Hii ishu Usipo lipa ukibambwa bakora zake sio za humu sio zile za shule ni kirungu kinapigwa matakoni kwa ukali Sana tena sometimes wanatandika mapajani japo Mimi sijawai kutana na dhoruba iyo zaidi ya kuona Tu.

Well Day 2 nikapelekwa kijiweni baada ya kuelewana na yule bosi ni Ka kibanda tu kapo juu karibu na mlima sababu ya kukajenga hapo pale panashika network ya mtandao flani maarufu Sana kijijini uku tz so kule ule mtandao unakamata sababu ni mpakani mwa tz na Mozambique japo tz ipo mbali Sana lakini network inakamata ili upige simu lazima upande mlima japo kwa sasa aiko ivyo huu mtandao nguvu imeongezeka

Nikaanza pale kazi ya kuuza vocha, vocha ya jero kule buku na ya buku kule ni buku jero ina maana ukinunua za elfu 50 tegemea 50 faida yani nusu kwa nusu kipindi icho watu walikua wengi na muda nimefika Mimi naambiwa watu wamepungua Hali ngumu lakini kwa siku kuuza vocha za lakimbili mpaka 3 kawaida ushakunja faida nyingi Sana.

Bosi wangu alikua mnyachu wa mbeya mtaji wenyewe ulikua wa kuunga Tukaenda ivyo ivyo baadae aka sarenda akaacha Ile biashara Mimi nilikua na pesa yangu nikawa naagiza vocha hii pesa nilikua napata vipi yule jamaa yangu katika zile asset alizo achiwa na uyo ndugu Yao aliefarik akafungua na mgahawa so akaniambia kuhusu chakula, asubuh chai kwake mchana kwake na jioni pale pale mgahawani.

Pale kibandani kwa boss wangu kwa siku nilikua nachukua elf 5 ya kula kabla ajaacha so akasema iyo pesa itakua yangu tunza na mwisho wa mwezi pia nilikua napokea mshahara Ila ndio ivyo bosi aliishia njiani akaacha Ile biashara.

Hii pesa nilikua natuma pia home na maisha yakawa yanaenda na hata jamaa yangu akikwama kidogo alikua anakuja ananiazima kuongezea kwenye mishe zake kama tu upande wake mipango ya pesa aijakaa Sawa au bado kufunga hesabu anaazima jioni ananirudishia.

Nikawa nauza vocha naagiza zinakuja nauza yule jamaa yangu akaamua kutia mzigo milioni kazaa kwenye mpesa na mpesa ikarudi kundini nieleze kitu kule voda ilikua inashika kupitia mitandao ya kule wanasema (roaming) sijui) yani voda ili jina linatoka linakaa jina la mtandao wa kule.

Hiyo mitandao ni mcel na mwingne umenitoka Ila kwa sasa kuna movitel ina nguvu Sana na internet tukiwa kule tunatumia Sana kupitia hii movitel.

Hii voda miamala unafanya lakini huwezi piga au kupigiwa na sio laini za tini ni namba ya kawaida kuna kipindi nilifanya mihamala mpaka ikafika kiwango changu cha mwisho nikasafiri mpaka songea kwenda kuongeza kiwango cha kutuma pesa alafu ukituma elfu 10 ada 1000 inamaana laki ada elfu 10.

Nakumbuka kipindi hicho nipo songea nilipoenda kuongeza kiwango cha laini yangu cha kutuma pesa kuna jamaa akawa ananipigia simu nikiwa songea naendelea kufanya mihamala yani pesa anapokea yeye kule msumbiji anapeleka kwa mshakji alafu mihamala nafanya Mimi ananitumia text ya namba na jina natuma pesa.

Huku songea nilikua na begi la mgongoni ambalo ndani kulikua na pesa miloni 9+ nakumbuka
ki hualisia nilikua bado mdogo nilikua na akili za kitoto toto na nilikua na ona ka ufahari flani ivi kutembea nazo pesa vile nikiishiwa pesa kwenye simu naenda Tu kwa wakala naweka kiasi.

Siku moja nilienda kwa wakala mdada ile nimevua begi nimefungua ndani yule mdada akaona maburungutu ya pesa alinishangaa mbaya nakumbuka Alisema we mtoto je macho yote kwenye pesa alafu anashika begi anachungulia mi nikatoa milioni 3 nikampa aniwekee lakini ananishangaa nilivyo mimi na zile pesa siendani.

Siku chache nikarudi tena Mozambique kuendelea na kibarua changu pale kibandani kama kawaida pale kama ni vishawishi vilikuepo Sana lakini kwa muda huo sikuwai lala na demu yeyote hasa zile habari mbaya za machimbo nilikua na gwaya magonjwa.

Basi nikaendelea na Ile kazi mpaka muda flani nikarudi hom tz nikanunua kitanda, godoro na vitu vingine vya home Ila sikua na mpango wa kwenda tena kule na kipindi hicho nilikua na milioni 1+ nikawaza nipige business Ila bado nilikua sijapata abc sikua na akili za kibiahsara naanzia wapi???

Mbeya nilisikia kule vitu bei poa nikapanda chuma mpaka green city.

Nakumbuka kabla ya kwenda nilipita kwa sangoma anipe dawa ya biashara na alinipa na kusema inabidii nichanganye na maji niogee nikioga leo saa moja kesho sa 2 kesho kutwa sa 3 nikifika nisilaze.

Nilifika gest flani ivi pale mbeya maeneo ya mwanjelwa mitaani uku kinaitwa JOMERA sijui kama ipo mpaka sasa iyo gest sasa kuoga Ile dawa nilioga kwa mbinde sababu ya baridi kama sio dawa nisingeoga ng'o. Nilifanya nipate maji ya moto wahudumu wakanizingua.

Nilikaa mbeya siku tatu nakumbuka siku ya Kwanza asubuhi yake iyo nilijiimia sido mnadani pale mlangoni palikua na kitambaa cheupe kimeandikwa sikumbuki vizuri mwizi tunaua alafu kuna picha ya kuchora rungu na jama ana damu damu kikatuni.

Pale nilichukua t-shirt kazaa na kurudi mpaka gest nikaziweka na kuanza kutembea kushangaa mji.

Usiku mida ya saa tatu niludi nikapotea zunguka fata ramani wapi zunguka Sana Ile gesti siioni mhm nikasimama barabarani kusimamisha boda jina la gest nikasahau boda namwambia naenda romeja gest kumbe ni JOMERA nae romeja ajui nabaki kuduaa boda mmoja nakumbuka alisema romeja au JOMERA hapo alinitoa usingizin nikamwambia JOMERA akanipeleka aliniambia Una bahati hapa mitaa ya Soweto usiku kuna vibaka sana.
Alinikumbusha muda fulani nikiwa hapo Soweto sijui kuna jamaa alikua anapita nikamuomba nimuulize Ile gest ilipo jamaa alinijibu achana na Mimi bwana alafu akatimua mbio.

Baada ya siku tatu Nilirudi hom kutoka Mbeya na siku ya pili asubuhi nilikwenda na nguo zangu mnadani kuuza dooo mnadani paache Tu Pana hitaji uzoefu niliuza lakini bei ya hasara sababu nilikua narusha ivyo mawinga wanavizia so bei ilikua tofaut na nilionunua kule mbeya nikamaliza nikaamia kwenye viatu nachukua bero nakuuza bado mziki ni ule ule pesa airudi hasara dawa ya sangoma Amna kitu uongo.

Ikawa ivyo nikaacha na pesa ikaingia matumizi ya hom pia kipindi icho sikua mtu wa mademu pesa iliisha kwa Mambo muhimu lakini biashara ilinishinda japo nilipata abc nikaanza life la kuunga unga toka niende 2015 mpaka naondoka MSUMBIJI ilikua 2017 kuja tz na mpaka pesa iliponiishia.

Nikaanza life la kuunga unga jamaaa yangu kama kawa tukawa tunakutana ananiachia chenji kidogo yeye alikua anenda Dar kufunga mizigo anapeleka msumbij ikawa ivyo hapa Kati nilipita kwenye msoto Sana ikiwemo kuosha magari na kufanya vibarua vya saidia fundi mradi kupata pesa ya kukimbiza siku.

Baadae jamaa yangu wakati yupo MSUMBIJI akaanza kujishughulisha na biashara ya kununua dhahabu alikua ananipa taarifa na alikua akipata Sana faida sometimes mzigo wa dhahabu wa milioni 20 ambao ni gramu 200 unakuta anakunja faida milion 2 mpaka 2.5 au 3 soko likiwa poa na dhahabu ikiwa na quality nzuri au asilimia nzuri.

Dhahabu bei ilikua laki gram moja
alafu na point moja elfu 10 kwa ambao wamepita machimbo nafikiri wanaelewa hii ishu. Kuna muda soko aliendi vizuri ivyo faida pia inakua ndogo hasa bei ikishuka sokoni pia lazima uwe makini kuna dhahabu feki wanaita (kakumba), kingine lazima uzingatie uchomaji kuna zile dhahabu ambazo wanakamatisha na mercury sio pure maana kuna pure na ambazo sio pure so lazima uchome Moto wa maana sababu sokoni nako wanarudia kuchoma na gas uzito unapungua usipochoma vizuri na unapata hasara tuiache Kwanza hii.

Basi muda ukaenda kuna siku mshikaji baada ya kutoka sokoni Dar kuuza dhahabu alinipitia Tukaenda funga mzigo wa dukani kwake hapa nikamwambia mwana maisha ayasomeki kitaa kama vipi nizame kundini Mozambique tukapige Ile ishu ya mpesa kama kuomba pesa kwako ntaomba mpaka lini?

Jamaa akaniambia vipi bi mkubwa atakubali nikamtell awezi pinga si naenda kutafuta uko, kwann rafiki yangu aliulizia ivi kwa sababu kipindi kile nilipo Rudi tz na baadae kugairi kurudi kule Mozambique, nilimdanganya mshikaji bi mkubwa kasema nibaki Tu hapa hapa ndio maana aliulizia hili swali akasema poa jiweke fresh tusepe nikamwambia Aina noma.

Nikamwambia mother akanipa go ahead na baraka Tele kwa mwanae wa pili nikapambane kwa mara nyingine tena kweli siku ilifika tarehe sikumbuki ni mwezi wa sita mwaka 2021 tulipanda bus ambazo zinaishia boda atukupanda pikipki Ila pikipki tulipanda hapo baada ya kuvuka mto ruvuma na kurejea Mozambique na hapa ndio Ile

Title head line hapo juu inakuja.

Iyo hapo chini ni laini ya Movitel ya nchini msumbiji.

IMG_20230215_005616.jpg



Wakuu Nitarudi chaooooo

NB
Sijawahi kuacha thread njiani Ila ni kesho tena usiku ikiwa kabla ya hapo itakua poa.

Machimbo 1.jpg

Machimbo 2.jpg
 
MUENDELEZO IN ADVANCE...

tulipanda pikipiki baada ya kuvuka mto kutokea ruvuma na sasa tukawa mozambique. Niliskia puuuh, puh puh, gigigigi, puh, puh. Ah, mwanzoni nilidhani ni baruti machimboni ila kumbe wajuba walikuwa wanapambana na majeshi ya serikali .

Tukalala chini huku naona vumbi linatimka jamaangu akaniambia tulia. Aisee nilijamba sana na mavi yaligonga chupi. Kumbuka hapo sikuwahi kugegeda mademu wa kule lakini aisee kuna kamoja wakati tumelala kakanikumbatia kwa nguvu sasa kina chuchu saa 6. Ikabidi palepale nikabandue maana nisijekufa hapa sijabandu wamakonde na wamakua.

Sasa bwana kumbe waasi walikuwa wamevamiwa na majeshi ya serikali. Aisee asikwambie mtu vita ni mbaya. Yani hata kale kadem nilikula tu basi ila vita ni mbaya. Sasa kumbe ilikuwa tarehe 16 march 2021 na kesho yake usiku niko zangu nimelala nashtuka usingizini nakuta kisabufa changu tbc taifa wanapiga nyimbo za maombolezo.

Eh... Nikabadilisha stations zote mara nikasikia sauti ya bi tozo. Khaaa! Ikabidi niingie hapa jf alooooh... Breaking neeews. Jiwe limekata kamba. Pamoja na kwamba siyo mlevi ikabidi nikimbie mbio kutafuta k-vant. Nikashangaa kukuta bar moja watu wanasherekea. Basi ikabidi tu niskilizie kwa hofu nikishangaa muheshimiwa mungu amekataje kamba... Itaendelea...
 
Sasa kwanini mtu kama una nia ya kushea jambo lako usiindike sehemu kwa utulivu kisha ukipost hapa upost mwanzo mwisho kuliko kusumbuana kusoma vitu nusu nusu, kuna haja gani?

Watu wana mishe muda unaopatikana kuingia huku ni mchache so mtu akiingia anatamani asome amalize alichokikuta chote.

Hebu fikiri watu Kumi thread zao waweke pending alafu watoe muendelezo kwa wakati mmoja au lisaa limoja nini kinatokea.

Andika kwenye docs ukitupia hapa kwa ma great thinker tupia kila kitu, huko fb na telegram ndio uwawekee episod
 
Tuendelee 02

Sasa turejee pale juu mwanzo....

Nilipotaka kuagiza mizigo midogo midogo kutoka China kupitia Ali express kwaajili ya business Ila nilishindwa kutokana na Corona na ivyo pesa kufanyia Mambo mengine na ikaisha,
Mambo yakawa msobe msobe mpaka mshikaji wangu alivyofika na nikamueleza kutaka kurejea Mozambique na hatimae kurudi tena Mozambique machimboni.

Baada ya kufika kule kweli palikua toafuti Sana sio kama miaka michache nilivyo paacha pamebadilika sana, kuna watu niliwaacha niliwakuta Wana endeleza gurudumu na wengine wapo awajawai rudi kwao toka waingie huko ndio wamezamia jumla jumla.
Sasa basi zilipita siku kama tatu bado nacheki mazingira na jamaa yangu na baadae jamaa aliniweka dukani sio kwenye mpesa tena kama nilivyozani.
mwanzo pale dukani kuna mtu alikuepo akiuza ila walipishana sababu jamaa alikua mtu wa mbususu Sana mpaka duka likawa linaporomoka ivyo alimuondoa pale.

Na Mimi ndio nikaingia kuanza kuuza lile duka aliongeza mzigo na alichukua na nguo toka dar jezi hizi feki most dar zinauzwa ef 6 mpaka ef 8 kule 30 mpaka 25 zina faida Sana isipokua Tu wale jamaa wa msumbiji kwenye swala la ushuru wasumbufu na ushuru upo juu Acha sometimes wanaita mikutano ya ghafla kila mfanya biashara Una ambiwa Tu pesa inahitajika mwenye mgahawa 25 duka 25 kama Una karasha laki kama unanua Dhahabu laki na 50 iyo ni nje ya ushuru alafu izo pesa zote wanapiga wenyewe kuna ka uonevu flani sema ndio ivyo upo kwenye nchi Yao akuna kupinga.

Kuna kipindi nakumbuka uliitwa mkutano kiongozi yule akatangaza kodi ya kichwa kila mtu alipe pesa nahisi ilikua ef 5 au efu 3 lazima utoe huna ni bakora au unapewa kazi ufanye mahali labda kufyeka au kukwaa kazi ngumu unapewa.
Maisha ndio yapo kama ivyo yapo mengi ya kuandika kuhusu huko sema tutajaza page kibao, basi mi nikaendelea kukaa pale dukani na mshikaji kama kawa akishajaza mzigo wa dhahabu anaingia Dar soko la dhahabu kwenda kuuza uko atafunga na mzigo anarudi tena msumbiji.

Kwenye kitengo cha kununua madini alimuweka mdogo ake ndie aliekua ana nunua wakati huo Mimi nipo dukani kuna siku wakati jamaa yupo tz home kwao uyu mdogo ake aliumwa ghafla kama siku tatu ivi alitibiwa bado Hali aikua nzuri alizidi kuzidiwa ikabidi kufanya process za kumsafirisha kwenda tz kupata matibabu sasa kwenye kununua dhahabu apakua na mtu na nilivyo wasiliana na mshkaji akaniambia nifunge duka Nika stik pale kwenye ununuzi wa madini ikabidi nifanye ivyo na sikua mzoefu nilikua Tu naona sikuwai kaa kununua.

Rasmi nikaanza kile kitengo cha ununuzi wa dhahabu na kuna mtu mmoja nae akawa pale akinisaidia nikitoka namuacha yeye ivyo ivyo ye alikua mzoefu lakini mikoba yote nilipewa Mimi basi nikanunua mzigo Ila nilikua nachanganyikiwa Sana hasa kwenye hupimaji wa dhahabu kingine nikitoka yule jamaa akinunua nikirudi pale sihakiki mi nikuweka sababu nili muamini.

Jamaa yangu alipokuja toka tz tukakaa mezani kupiga hesabu na kupima mzigo aisee palikua na shoti kubwa Tu milioni na point tukarudia Hali Ile Ile Ila jamaa akachukulia poa sababu ndio Kwanza naanza Ile kazi zaidi akaniambia niongeze Tu umakini kila kitu kitakua poa nione business ya kawaida Tu na ndio msingi wenyewe huo pia niwe makini na yule jamaa anae nisaidia anaweza akawa anapiga changa sababu anajua kila kitu nimekabiziwa Mimi kwaiyo kikitokea chochote naonekana Mimi mi nikamulewa mshikaji nikaongeza humakini.

Yeye alichukua mzigo akatimua DSM sokoni kwenda kuuza kule nako nilivyo mpandia hewani phone call akaniambia hili kule sokoni mzigo umeshuka Sana uzito yani nilipokua na nunua sikua nikichoma vizuri zile dhahabu ambazo inabidi uchome au zilizo chomwa lazima urudie sababu mchimbaji Dhahabu anaweza akaipasha Moto Tu ikibadilika rangi Tu kaitoa hapo aijaiva bado ina mercury ambayo ni uchafu kwa muda huo kwaiyo lazima uichome kwa muda mrefu na Moto uwe mkali ili mercury yote iungue ata ukienda sokoni wakichoma itapungua kidogo Sana sio kwaukubwa.

Jamaa akaniambia baada ya kuichoma zimepungua gramu 7 Sawa na shiling laki 7
Hasara iyo mzigo uliobaki akauza faida aliyopata yote kafidia hasara iyo ya laki7 na Ile amabayo ilitokana na Mimi uku pori ivyo alibaki na pesa kidogo Sana na katika iyo biashara akuwai pata loss ya ivyo.

Mi nikapokea na ikabidi sasa nikomae kuongeza umakini akatuma pesa zikaja mi Nika endelea kununua mzigo safari hii nikaongeza umakini kweli Ila kuna muda nikawa najisahau dhahabu wakija kuuza muda mwingine sichomi sasa inakua tatizo pengine huko ajachoma vizuri kababua Tu hapa labda nieleze kidogo mfano labda mtu kaja kuuza dhahabu kupima imeonekana uzito 3.4 == gram 3 na point 4 ambayo Sawa na laki tatu na arobaini sasa kama ajachoma vizuri ukirudia kuchoma alafu uje upime inapungua uzito unakuta labda inabaki gram 3 pekee ina maana zile pont 4 ambayo ni ef 40 ulikua uchafu auja ungua vizuri sasa ukichukua ivyo ikienda sokoni Moto wa gas ikichomwa ikibaki ivyo inakua hasara kama umechukua labda gramu 100 alafu kuna mapungufu kama Ayo hapa Una hesabu shoti unaweza jikuta unabaki na gm 93 au95 Ila kikawaida inabidi angalau zibaki 98 au 99 iyo kawaida sana.

Nikaendelea kununua mzigo mpaka pesa ilipoisha alafu ubaya mwenyewe nilikua si hakiki siku iyo nimempigia simu nikamwambia pesa imeisha akaniambia mzigo upo fresh nikamwambia ndio akasema poa yeye atakuaja nitulie Tu.
Nikarudi nikapiga mahesabu pesa iliyotumwa nikaanza kupima mzigo wa dhahabu na kulinganisha kiasi cha pesa kilicho tumwa nikaona tena shoti bonge la shoti hapa sikuelewa inakuaje au kuna nini??
Yaani mwili ulinitetemeka kama nimepigwa shock ya umeme ahaaa nafidiaje sielewi

Nikavurugwa na hii shoti niliokua naiyona hapa nikapanda hewani nikampigia nikamuelekeza haaa jamaa akuelewa akafoka akapanik mbaya inakuaje akasema kwanza nakuja Leo Leo akakata simu piga apokei nikaona ninalo hapa.
Jioni mida imeenda mshikaji uyu hapa akaingia tayari kashapiga mtungi akaja pale tukapiga story mbili tatu akaingia tena bar kwenda kugida Tungi Ila Tungi zote hizo sio wa kulewa kiasi hicho bado alikua anajitambua mi nimeingia kulala akaja akagonga nikafungua akasema mwanangu njoo tupime Kwanza mzigo nikatoa dhahabu tukaanza grade.

Zile dhahabu pure peke ake na hizi za kukamatisha na mercury peke ake baada ya kumaliza kupima akaniambia tayari Pana shoti tena milioni na ushee mwamba Alimaindi Sana Sana sana aliwaka mbaya iyo mishale ya saa 7 za usiku da kinacho umiza iyo pesa ni Bora ningekua nahonga au kula au kutuma nyumbani lakini aikua ivyo alafu mi sio mtu wa pombe sinywi kabisa sivuti sigara wala bangi na hata mademu sio wa ivyo Kwamba niwe na icho kilevi japo hua napiga piga kidogo lakini kwa wakati huo mpaka hapo sikuwai piga demu hata mmoja.
Hii shoti ilinitoa kwenye reli vibaya jamaa yangu aliwaka mpaka Ile sauti yake ikawa inakoroma Mzee nimeuchuna Tu zaidi nikamwambia bahati mbaya ndugu yangu akuna ubaya labda nimeficha pesa Amna.

Niliisi anaweza akawaza ivyo mi nilimwambia siwezi kukufanyia ivyo na hizi pesa za kuzurumu zitanipeleka wapi lakini kumbuka nyuma tulishawai fanya kazi na wala sikuwai pata shoti yoyote ata 100 iweje iwe leo siwezi fanya ivyo jamaa alijibu we lala bwana mi niache niwaze vyangu hapa usha nivuruga lala mwanangu kesho itabidi nifanye maamuzi Tu magumu da mi nikapanda kwa bedi kulala sikupata usingizi alafu nilikua naumwa mafua mshkaji baadae akaja nae akalala mpaka morning.

Asubuhi aliamka akasepa mahali mi nimeamka nikawasha Moto naota nikatulia pale nikawaza na kuazua inakuaje jamaa kasema anataka kufanya maamuzi magumu nilihisi kabisa anataka kunirudisha tz nikapanga kama atahamua niludi tz sirudi potelea mbali
Nikakumbuka nishawai sikiliza mikasa mingi watu wanazamia mbele uko na nchi jirani kwa madiba south kwaiyo cha msingi akiniambia nisepe naunga boda mbele kwa mbele Niko msumbiji south ni hapo Tu ntasonga mbele kuisaka south Africa sirudi home labda uko mbele nikibaki salama ntarudi.

Nikaona ili ni wazo Bora ukizingatia Mim mtoto wa kiume lazima nijilipue ntaenda mbele zaidi, jamaa alirudi baadae alipofika mshkaji mmoja alimfata alikua ana mdai wakaenda kando kuongea yule mshkaji badae akaja kwangu akaanza niuliza mwanangu vipi ilikuaje hii shoti ikaingia hivi nikamueleza mwanzo mwisho akawaza baadae akasema jamaa yako anataka kukurudisha lakini mi nime msihii akuache Kwanza pengine kwa vile we ni form one ndio maana imetokea ivi nikamwambia ndio ivyo akasema ngoja niongee nae tena.

Baadae mshikaji wangu yule (bosi wangu) alirudi akaniita ndani akasema mwanangu hapa ilibidi kufanya maamuzi magumu lakini utabaki utaendelea na kazi kua makini Sana, pia upande wa pesa sitokuachia pesa zote nitakua namwachia uyu jamaa aliekuja atakua anakupa laki mbili mbili unanunua mzigo pesa ikiisha unampelekea mna pima anakupa tena lakimbili nyingine ndio itakua ivyo Sawa nikamwambia poa Ila ndugu yangu nisamehe Sana sijafanya kusudi akasema sio tataizo Ila tutaanza kufanya kazi kwa mfumo huo nikamjibu poa Ila moyoni nilikua na maumivu Sana Sana acheni Tu Wazee Aya mapito sio mchezo.

Mshikaji akachukua mzigo uliopo na kuja tz Dar sokoni muda wa kuondoka kutoka hapo tuliondoka wote nilimsindikiza alinisistiza Sana kua makini alisepa nikabaki mfumo ukawa huo naenda kwa yule jamaa nachukua laki mbili naanza nunua dhahabu ikiisha napeleka dhahabu ananipa pesa tena yaani nikawa sasa sikai tena na pesa wala dhahabu aya yote baada ya kuingia Tu Ile shoti
Hakika Was sadness ilikua ni huzuni

Nikaanza Ayo maisha yule jamaa aliekua ananipa pesa Napo mpelekea dhahabu akatangaza kwa watu nimetia shoti mpaka kwa wahudumu wa migahawa nikienda kula wale wa dada walikua wananipa hizi story da ikawa aibu Sana kwangu pakawa na maeneno Kwamba hizi pesa zilizoingiza shoti nimeonga demu flani ivi uyu demu ilikuaje uyu demu baada ya kuja chimbo akawa ananifata Sana hasa baada ya kusikia na nunua dhahabu.

Kuna siku alifika geto kwa kuforce akawa anataka kulala na Mimi demu mzuri mzuri Sana lakini nilitia msimamo niligoma demu alifanya vurugu sana eti nim.....mbe kwa lazima ilikua usiku tulizinguana Sana alinishika kidole iki cha Kati mkono wa kushoto alikipinda aisee nilimuwasha Kofi moja Kali Sana akaniacha akaanza kulia nikapanda kitandani ni kalala kalia badae akapanda kitandani akasema we mwanaume wa ajabu Sana mwanamke anakulazimisha kufanya utaki nikamwambia sitaki akapanda yupo uchi akalala kidogo akasema unaniacha na nyege Sawa nikaanza msikia anajipiga vidole kwenye K nasikia chwa chwa chwa alafu anang'ita ahaaa ahaaa haaaa alijipiga mpaka akakojoa akatulia akalala akasema nipe basi ata denda siku mjibu.
Asubuhi alikua wa Kwanza kuamka akasepa uko akatangaza kalala na Mimi na nimempa na pesa ndio ikawa ivyo story zikabamba Kwamba pesa nimehonga uyo demu yani alinichafua Sana mbwa yule.

Ikawa ivyo wakuu nakusanya mzigo napeleka jamaa ananipa ela na nunua napeleka sikua na Uhuru na kazi hata kidogo niliwaza mengi Sana nikakumbuka life la home na wakati huo napitia nyakati ngumu
Stress aziishi kichwani yani nawaza mpaka kichwa kinauma nilikosa Sana furaha Ila nikapiga moyo konde, siku iyo nikachukua simu nikaenda mpigia bi mkubwa ni msalimia mother akaniambia Nina malalamiko nimepewa kuhusu wewe.

Nikamuuliza yapi Ayo akasema rafikio kanipigia simu alikua na namba ya bi mkubwa aKaniambia ndio Ile ishu ya shoti nikamwambia ni kweli lakini mama mi sijafanya kusudi bahat mbaya imenikuta na nilikosa uzoefu ndio ikawa ivyo akasema kua makini basi nikamwambia Sawa.

Sijakaa sawa baada ya mshkaji kurudi toka tz na kuja msumbiji katika kupiga story akaniambia kitu kingine Kwamba kapewa taarifa shoti iliyoingia Ile pesa nimetuma nyumbani dahaaa very stupid Nani Ka kwambia jamaa akuvunga akamtaja uyo ambae hua nampelekea dhahabu na kunipa pesa Kwamba alinisikia naongea na simu nikisema hivi iyo pesa fanyieni cha maana yani Mimi uyo kumbe jamaa alinijengea Ka ubaya kwa mshikaji ili yeye ndio awe ana nunua dhahabu za mshikaji. Ile kusema naongea na jamaa yako akuache usirudi tz ilikua uongo na unafiki mara dufu

Mshikaji akasema lakini Mimi siafiki ilo swala nahisi ana yake sababu namfahamu tabia yake na wewe pia nakufaham cha msingi komaa hua spendi kusikiliza maneno ya watu mpaka nihakikishe mwenyewe du mi nikamwambia poa,
kuna muda nilikaa peke angu nikawaza Sana mtoto wa kiume nilidondosha chozi najikaza yasitoke lakini machozi yalitoka kile kilio cha kiume nyakati ngumu Sana nilipita habari ziko mitaani full.

Yaani ilikua full karaha so Tukaenda na system Ile Ile napewa laki 2 nakusanya mzigo napeleka kwa jamaa wala siku mkunjia baada ya kunichongea na wala sikuonesha utofauti Ila moyoni nilikua nalo na tabasamu husoni lilibaki kawaida Tu maisha yalienda ikafika muda baada ya kazi kwenda vizuri mshikaji akaanza kuniachia tena pesa kama mwanzo na kazi ikawa inakwenda vizuri kabisa.

Zile shoti azikutokea tena na Amani ilirejea kama mwanzo na kazi nikawa nafanya poa kabisa lakini yule jamaa aliekua akinipa zile laki mbili kila nikijaza mzigo akawa anakunja wazi wazi yani kinyongo kwa vile nilishalijua hilo mi nikaishi ivyo na maisha yaka endelea.
Mpaka inafika muda huo ilikua tayari imepita miezi 6 sikuwai gusa mbususu na Yale yaliyonikuta ndio kabisa nilikaa mbali Sana na mbususu japo zipo za kumwaga Tu.

Siku iyo akapita demu nikampanga wakati huo nipo pale geto tukafika muhafaka atafika jioni mida ya saa moja nikakaa kwa kutulia Ile mida alitimba nikambeba mpaka geto la jirani tulikua na mageto mawili pale.
chuma kimeingia ndani nikaweka Mambo vizuri nikaenda kuifanya kazi mbunye
bana bana.
Jogoo akuwika kabla aliwika baada ya kuingia mule ndani demu kavua nguo yupo mtupu jogoo aligoma katakata kuwika jaribu kunishka shka wapi nikajiuliza tatizo nini majibu akuna demu ikabidi avae nikampa 10 akasema kama vipi kesho ntakuja nikamwambia poa sikuelewa shida nini lakin badae peke angu jogoo akawa njema.

Nikasema ngoja kesho atakapokuja tena nione itakuaje siku ya pili yule demu akaondoka sikumuona tena kipindi icho alirud Tz hii kitu iliniuma sijamlamba na kasepa na nilikua nitest mitambo nione kama itazingua tena au wapi.
Sasa Hapa mpaka kwenye bar nikaanza kwenda siku moja moja ikifika usiku nafunga kijiwe naenda lakini sio kunywa pombe maana sinywi pombe zaidi ya soda, maji au energy. Lakini Pia kucheki mbususu angalau siku moja moja siku iyo Nikaona pc flani ipo njema imeenda hewani alafu imebeba mzigo wa maana nikasema Mambo ndio Aya nikampanga akasema nimnunulie bia nikanunua nikampa location afike wapi.

Mida mibovu akatia maguu geto Ila akasema awezi lala nichape asepe kwani ana jamaa yake ambae yeye hua analala huko so atakapo maliza mkataba wa baani pia na uyo jamaa anampa pesa yani unakaa na demu ki mkataba ndio ipo ivyo ukikaa na demu permanent na huku anafanya kazi muda wa mkataba ukiisha anapoondoka kule bar analipwa na wewe unampa pesa kama ni laki tatu basi ndio ivyo unampa kutokana na makubaliano yenu. Lakin analombesha kama kawaida anakusanya mkwanja hii ukiletewa geto ishachanazwa.

Basi Sikulaza damu na jogoo aliwika haraka Sana sijui kutokana na mzigo alionao akavua akapanda kwenye bed hapa na mimi sikulemba nikapanda ametanua mapaja nikachomeka mkuyenge nikaanza kutwanga nilipiga mbunye vya kutosha wazungu wako mbali mpaka nikajishangaa inakuaje na sijafanya muda mrefu mbona sio kawaida na yule demu nae alikua anakata uno alivyoona nachelewa kumwaga akageuka akantegea mbuzi kagoma mtungi na uangalia huu mbunye ipo stable nikachomeka nikatwanga nae anazungusha mtungi punde wazungu mwaaa nikalala pembeni but kinga sikuisahau
demu akaamka akajifuta nikampa 15 nikamwambia kesho itabidi uje kulala akasema mbona kutawaka Moto kama hapa Tu ivi nikamwambia sijafanya kitambo ndio mana imekua ivi akasema tuta angalia.

Aya maisha ya kupiga mbunye ikawa mdogo mdogo siku nikimiss lazima nijichanganye maeneneo kuzisaka Hali ilikua nzuri biashara poa ata mwanga sasa wa nitakapo rudi tz nikaanza uona na vile biashara ilikua inakwenda poa basi ikawa akuna baya kama ni shoti sasa zilikuepo kidogo sio kama zile za mwanzo ambazo sometimes ilikua ni easy kuzifidia japo zikizidi jamaa alikua anawaka na ni ngumu kuepukika ata ukomae vipi japo muda mwingine unafanikiwa.

Muda ulikimbia hatimae ikafika mwaka nipo kule napiga kazi Ila hapa Mambo yakaanza kubadirika Kwanza ikawa dhahabu zime adimika zinakuja lakini ni kwa uchache mzunguko ukawa mdogo mzigo wa
gram 100 kujaza inafika mpaka mwezi wakati tulizoea siku 5 au au 7 tayari Ila Hali ili change ghafla sasa ikawa unakuta muda wa ushuru mpaka unafika ujaenda sokoni ushuru unakutana wa mwez uliopita mpaka unaokuja sokoni ujaenda hapo ushuru iliku jumla sehemu zote tunazolipa inakaa laki 7+
Hapo bado ujagusa gharama za usafiri mpaka Dar kwenda na kurudi na mpaka kufika tena Mozambique.

Mzunguko mdogo wa dhahabu na ndio biashara kubwa tuliokua tunategemea kwa kipindi hicho ukiacha duka moja ambalo alikua nalo na baadae alifunga sababu kubwa madogo waliokua anawaweka pale dukani wakianza kujua mbususu basi inakua hatari yani Wana honga kupitiliza ivyo alifunga.
Ikabidi tutafakari njia nzuri ya kupata dhahabu kwa haraka baada ya kukaa na mshikaji na kujadiliana tukapata njia ambayo ilibidi tuanze process ili kukamilisha.......

Wakuu bado Kesho nayo siku ntarejea chaooo.
IMG_20230215_233937.jpg
 
Ikabidi tutafakari njia nzuri ya kupata dhahabu kwa haraka baada ya kukaa na mshikaji na kujadiliana tukapata njia ambayo ilibidi tuanze process ili kukamilisha.......

Tuendelee 03
Iyo njia ni ipi wazo likaja inabidi kua na kiwanda, hiki kiwanda ni mahususi kwaajili ya kufanyia process ya kupata dhahabu yani kua na karasha ambapo watu wataleta mawe wanapotoa huko migodini alafu Sisi tutakua tunazamini Yale mawe na yatasagwa pale ivyo mtu akileta mawe yakiwa pale tunazamini kwa kumpa labda pesa ya kula mfano elfu 10 au ef 5 kulingana na hitaji lake

Alafu iyo pesa itakuja kulipwa pindi yale mawe yakishasagwa na kukamatisha dhahabu ivyo lazima atauzia pale na hapo ndio Ile pesa ambayo aliazima itakatwa na itakayo Baki atachukua mwenyewe,
mpango ukawa ivyo hapa uyu jamaa yangu alifanya process akatengeneza karasha au mtungi toka tz kwajili ya kusagia mawe na akagiza Gia boks toka Dar mpya ya injection ule mtungi lazima uzunguke kama vile Tu gari linapo tembea.

Aliagiza vitu vyote ambavyo vitakamilisha kiwanda na karasha kuanzia mtungi,Gia box, propela n.k na akavisafirisha mpaka msumbiji pale machimboni kiujumla iligharimu milioni 8+ mpaka kukamilika pamoja na kufunga mtungi na kila kitu pia kutengeneza Banda kwajili ya sehemu ya kazi.

Yesss kazi ikaanza Tu baada ya kiwanda kufunguliwa na wachimbaji wakaanza kuleta mawe kwa wingi hapo ki ukweli lile wazo lilifanya kazi kwani dhahabu zikaanza kupatikana kwa wingi na ule uhaba ukatukimbia wa kukosa dhahabu hapo tukawa tunasaga mawe ambapo pia mchimbaji analipa mfuko mmoja 15 nusu mfuko elfu 10, pia tulipata wadau wengi pale kwa sababu mchimbaji alipoleta Tu mzigo tulimpa pesa ya kula na iyo pesa atalipa baadae ivyo kiwanda kikawa na wateja wengi

Basi kazi ikafanyika na faida ikawa inapatikana ya kusaga mawe ya wachimbaji pia dhahabu tukawa tunapata kwa wingi kwenye ili swala la udhamini ilifika muda Mambo ya kabadirika yalibadrika vipi Yale mawe yaliokua yakiletwa yakawa ayana dhahabu kwa wingi na Mimi ndio nilikua nikisimamia kiwanda na pesa za kuzamini Mimi ndie niliekua nikitoa Ila mi sikushtuka kwa muda huo niliamini Tu Kwamba labda Leo Amna kesho itakua Sawa ivyo mtu unampa elf 50 ambayo ni Sawa na dhahabu point 5, alafu akija kumaliza process zote tukienda pima dhahabu kapata point 2 Sawa na elfu 20 aijakidhi kiwango anachodaiwa unakuta pesa inaishia kwenye mashine pekee.
Linabaki deni hapo sasa kuna wengine labda uliwapa laki na 50 wakanunue labda baruti na vibati vya kulipulia migodi wakishatoa mawe kuleta kiwandani baada ya process zote unakuta wamepata point 7 elfu 70 deni tayar na hapo wataomba uwaongeze pesa nyingine alafu kesho watakuja kulipa baada ya kuleta mawe kiwandani kesho inakua tofauti ni deni juu ya deni kwa siku unakuta milioni ipo nje,
ukawa mwendo ndio huo ilifika muda nikawa nadai pesa nyingi nikiwa na matumaini kesho wanalipa wengine ndio Kwanza wanakimbia kiwanda wanahama kabisa sababu ya madeni Mambo yakawa mparanganyiko vibaya Sana zile pesa ambazo nilikua nadai zikafika mpaka milioni 6 huko jamaa yangu anielewi hata kidogo na Mimi pia nilishajiona nimefanya mistake tayari.

Pale kiwandani pakawa Napo ovyo mashine ikifanya kazi kidogo imeharibika pesa zote zinaishia kwa fundi atujakaa Sawa ushuru huo pesa ndefu lazima ulipe wakati Una ugulia ushuru wa wa karasha laki na 50, ununuzi wa madini laki 3, kituoni laki 2, amjakaa Sawa (Mozambique revenue) mapato wa msumbiji hawa wanataka pesa nao laki na 50.
Inabidi muanze kurudisha pesa kwa kupiga kazi mashine ina haribika fundi anakuja kulamba pesa kuna muda tukaita mganga aje aweke vizuri Mambo pale kiwandani lakini wapi sijui nae alitupiga changa la macho, mashine aikomi kuharibika tena inaharibika muda ambao mawe yapo mengi ya kusaga watu wanahamisha mawe wanapeleka viwanda vingine.

Hali ilizidi kua mbaya zaidi ya mbaya ukicheki pia nadai pesa nyingi mpaka ikafika hatua tukaanza kuyumba mtaji umetetereka lakini chanzo kikuu ni zile pesa za madeni ambazo nilikua nadai hili swala kwa wakati mwingine tena likanipa mawazo chungu nzima.

Kuna muda wakati jamaa yangu anang'aka kuhusu Yale madeni nayo dai na Mimi napambana vilivyo kuwadai wachimbaji lakini ikawa ni kama kutwanga maji kwenye kinu wapo waliokua wanalipa lakini ni pesa kiduchu ambayo bado aikuweza fidia mapengo yaliyokua yanatukabiri, niliwaza Sana wakati mwingine hata nikiwa peke angu natembea niliongea peke angu kuna kuna jamaa alinishtua vipi niliona mpaka aibu jamaa aliona Niko bize kurusha rusha mikono aise ilikua tabu Sana pindi napokumbuka nyakati hizi.

Jamaa yangu yeye nae alikua akinishushia lawama kila leo na sometimes alikua akikaa na watu huko na kuwaambia Mambo yaliyokua yanaendelea kuhusu pesa nilizokua nadai walikua wakimwambia Mimi watu siwadai isipokua izo pesa napiga mwenyewe yani na make alafu nadanganya nadai madeni Aya maneno alikua akiniambia pindi akitoka kupiga mtungi akishalewa ndio ananipa Aya maneno mwanzo mwisho.
Ilibidi nikubali Tu Ayo maneno lakini ukweli ulibaki kwa Mimi na mungu wangu wala sikuwai make pesa kwa kumpiga changa mshikaji nikawa mpole Sana kwa Mambo yaliyokua yananisakama na hata mawazo ya jamaa Kwamba atakuja kunilipa uko mbeleni niliona kabisa haiwezekani habadani.

Maisha yalisonga nikiwa mtu wa mawazo sikua na furaha hata kidogo kingine niliwaza Sana ntakapo ludi tz sitakua na pa kuanzia sababu niliona kabisa jamaa hawezi nipa pesa alafu pia nimekaa muda mrefu narudi vipi nyumbani ntaonekanaje nilienda fanya nini muda wote huo narudi sina kitu hii ilinipa mawazo chungu nzima alafu nikawa mtu wa hasira hasa ninapo muona mtu nnae mdai yeye anadunda Tu alafu mi kaniweka kwenye mazingira magumu naonekana hopeless katika kazi.

Kuna siku mshikaji akaenda pub moja kupiga gambe pale Pana mademu wazuri ambao ni wahudumu mi kipindi hicho mudi yote ilikata na siku nikienda huko kabisa sasa uko kwenye pombe katika kunywa kunywa mitungi kupanda kichwani ukazuka ugomvi mshikaji na polisi wa kule msumbiji chanzo ni demu kugombania lile purukushani likawa kubwa Sana baadae mshikaji wangu alichukua chupa na kumtandika nacho afande yule kichwani jamaa akazima hizi habari nilikuja kusimuliwa baada ya Mimi kuja kuitwa nikamtoe jamaa analeta vurugu kule pub.

Nilipoenda nikamchukua mshikaji mpaka geto yupo chakali alafu bado anataka kwenda kwenye pombe mi nikamzuia akalala usiku Sana mishale mingi mi nilisikia mlango unagongwa kuuliza alikua sungu sungu kaambatana na polisi wamemfata jamaa kwani anahitajika kituoni kutokana na lile songombingo nikamuamsha mshikaji na kumwambia anahitajika nje kufungua mlango kutoka Tu mshikaji ana Pingu
jamaa walikuja full wapo na bunduki

wamejipanga hasa kama wanamfata jambazi flani,
fasta bila kuchelewa na safari ikaanza kuelekea kituoni mi nikafunga nakuelekea huko jamaa wakamuweka lockup alikuja Mzee mmoja na vijana flani ambao waliungana na Mimi na kuanza kufanya utaratibu wa kuongea na wale Askari ili tujue tunafanyaje tuwez kumtoa mshikaji.

Walikaza ule usiku aikuwezekana tukaondoka,,. Asubuhi mapema tukajiimu tena kituoni kufanya mipango katika maongezi Yao wakasema mpaka wakae kikao ndio watoe mahamuzi kwani sio muda mrefu watakaa kujadiri kwaiyo Tusubiri mpaka wakae wamalize hapa ilikua ni swala la pombe na wote walilewa lakini mwsisho wa siku ikaonekana mshikaji ndie mwenye makosa sababu kubwa wapo katika nchi Yao akuna kingine hapo.

Muda ulifika baada ya kumaliza wao kikao Chao walikuja na jipya sababu yule Askari alikua na Ka cheo basi wakaamua kutupiga faini miloni 8 ili jamaa aachiwe tulipe faini ndio atoke hapo sasa pesa tunatoa wapi lazima tuingie kwenye mtaji wa dhahabu tutoe pesa tukalipe kitu ambacho kilikua kina zidi kudidimiza mtaji na kufanya uzidi kushuka zaidi na zaidi,, jamaa nikaongea nae akaniambia nikachukue pesa niwaletee kama kuna Dhahabu basi niuze kwa madigara wengine ili tufikie kiwango cha pesa tukalipe ili atoke tofauti na hapo itatulazimu tuondoke hapo na tusifanye kazi yoyote alafu wanataifisha kila kilicho chetu kinakua chao tunaondoka kama tulivyo.

Pesa tukalipa na jamaa akaachiwa tukarudi mzigoni Ila sasa Mambo yapo mbaya yameyumba Sana mshikaji alivyotoka akukaa Sana akaondoka. Akarudi tz Kwanza kule nikabaki Mimi,, nikabaki nasimamia (karasha) mashine ya kusaga mawe Ila sasa ushuru ukawa changamoto unafatana Sana mashine ndio Ivo aitulii kuharibika kila muda.
Tukawa na madeni mengi tunadaiwa tukikopa pesa labda kuweka Mambo fresh ndio Kwanza tunaongeza madeni inakua ngumu Sana kulipa hili likawa janga kubwa.

Wakuu ntarudi ...............
IMG_20230217_223539.jpg
 
Back
Top Bottom