Elections 2010 Wizi wa Kura unafanyika hivi...

Habari zinaenea ya kuwa CCM na mawakala wao pamoja na Tume ya Uchaguzi wa Mpango mbaya wa kuharibu KURA yako kwa wewe mwenyewe kwa mkono wako kuiharibu. Iko hivi, nimeipata hii kwa Mmoja wao aliyefikiri mimi niko pamoja nao kumbe mimi sio CCM (JK Family). Habari yenyewe ndio hii.
Jambo lenyewe lahusu elimu ya karatasi za kura hususan UKUNJAJI wa karatasi hizo. Ukichukua karatasi ya kupiga kura majina ya wagombea yameandikwa na picha mkono wa kulia na sehemu ya alama kushoto, sasa kalamu za TUME zina wino mwingi sana hivyo karatasi ikikunjwa vibaya wino huo wa alama ya ndio utaangukia pengine hivyo karatasi hiyo ikawa na alama mbili kwenye wagombea wawili tofauti, hivyo kufanya kura yako kuwa IMEHARIBIKA.
Sasa elimu hii ya ukunjaji vizuri wa karatasi imeanza kutolewa kwa wana-CCM nchi nzima ili kufanya wapinzani kuharibu KURA zao nyingi, hii ni baada ya CCM kuona kuiba kura kwa KURA FEKI itashindikana, hivyo kufanya kura za UPINZANI kuharibika.
Elimu hii iko hivi.
Kunja karatasi yako ya KURA ifuatavyo kuepuka ALAMA kutokea kwa wagombea wawili tofauti, kunja karatasi ya KURA aina za A4 yaani karatasi zilizo ndefu na si pana yaani kutoka juu kwenda chini ni kurefu kuliko kutoka kulia kwenda kushoto.
SASA KUNJA KARATASI YAKO KUTOKA KULIA KWENDA KUSHOTO SIYO KUTOKA JUU KWENDA CHINI.
PIA KUMBUKA KUSUBIRI WINO KUKAUKA KIDOGO KABLA YA KUKUNJA.
Elimu hii wapewe mawakala wote wa upinzani kwani CCM wameanza kimya kimya ili kuwaacha WAPINZANI kwenye
mataa. Pia tuma ujumbe huu kwa kila mpinzani unayemfahamu. JK harudi mjengoni hata kidogo.
TUPIGE KURA BILA KUHARIBU KURA, NA TUZILINDE HASWA.

2010 Hatudanganyiki. JK Family chini, chini zaidi. SLAA JUU, JUU ZAIDI.
 
Zimebaki Siku 3. Tukazane ushindi ni wetu kabisa bila woga tunaingia Ikulu. Wamama watafanya Aiyululululuuuu aiyu....
 
Lakini si zitaharibika pia zile kura kwa JK na CCM? CCM nao watakuwa wahanga wa unachoisema, au?
 
Issue niliambiwa na binti fulani nikiwa Moshi, inawezekana ni kweli kabisa. naanza kuelimisha wapiga kura
 
Habari zinaenea ya kuwa CCM na mawakala wao pamoja na Tume ya Uchaguzi wa Mpango mbaya wa kuharibu KURA yako kwa wewe mwenyewe kwa mkono wako kuiharibu. Iko hivi, nimeipata hii kwa Mmoja wao aliyefikiri mimi niko pamoja nao kumbe mimi sio CCM (JK Family). Habari yenyewe ndio hii.
Jambo lenyewe lahusu elimu ya karatasi za kura hususan UKUNJAJI wa karatasi hizo. Ukichukua karatasi ya kupiga kura majina ya wagombea yameandikwa na picha mkono wa kulia na sehemu ya alama kushoto, sasa kalamu za TUME zina wino mwingi sana hivyo karatasi ikikunjwa vibaya wino huo wa alama ya ndio utaangukia pengine hivyo karatasi hiyo ikawa na alama mbili kwenye wagombea wawili tofauti, hivyo kufanya kura yako kuwa IMEHARIBIKA.
Sasa elimu hii ya ukunjaji vizuri wa karatasi imeanza kutolewa kwa wana-CCM nchi nzima ili kufanya wapinzani kuharibu KURA zao nyingi, hii ni baada ya CCM kuona kuiba kura kwa KURA FEKI itashindikana, hivyo kufanya kura za UPINZANI kuharibika.
Elimu hii iko hivi.
Kunja karatasi yako ya KURA ifuatavyo kuepuka ALAMA kutokea kwa wagombea wawili tofauti, kunja karatasi ya KURA aina za A4 yaani karatasi zilizo ndefu na si pana yaani kutoka juu kwenda chini ni kurefu kuliko kutoka kulia kwenda kushoto.
SASA KUNJA KARATASI YAKO KUTOKA KULIA KWENDA KUSHOTO SIYO KUTOKA JUU KWENDA CHINI.
PIA KUMBUKA KUSUBIRI WINO KUKAUKA KIDOGO KABLA YA KUKUNJA.
Elimu hii wapewe mawakala wote wa upinzani kwani CCM wameanza kimya kimya ili kuwaacha WAPINZANI kwenye
mataa. Pia tuma ujumbe huu kwa kila mpinzani unayemfahamu. JK harudi mjengoni hata kidogo.
TUPIGE KURA BILA KUHARIBU KURA, NA TUZILINDE HASWA.

2010 Hatudanganyiki. JK Family chini, chini zaidi. SLAA JUU, JUU ZAIDI.

Comedy show
 
Kila baya halitasimama
Mungu ailinde tanzania.
Sisi ndio tutakaochagua kiongozi. Mungu aongoze akili zetu

Dr. Slaa for presidency
 
Naam,

kuna maneno mengi yamesemwa hapa kuhusu wizi wa kura. Kwa ujumla sikuziamini

Nimepata habari, sioni sababu ya aliyeniambia kusema uongo, na mnajua kuwa siyo rahisi kumtaja. Hivyo mna hiari ya kuamini na kuzifanyia kazi, au kupuuza na kujiandaa kulia.

Karatasi za kura ya urais ziko aina mbili. Kuna zile ambazo ukipiga kwa mgombea yeyote alama inabaki pale pale. Aina ya pili ni zile ambazo ukimpigia mgombea yeyote asiye JK, alama hiyo inafutika baada ya dakika chache kisha inajitokeza kwenye kiboksi cha JK.

Kura za ubunge hazikufanyiwa sayansi hii, ndiyo maana wabunge wa CCM safari hii wanapigana kufa na kupona.

Mtoa habari anataka wale wanaobisha wajiulize, ni kwa nini uamuzi wa kuchapa karatasi za kura nje ya nchi ulifanyika gafla wakati serikali ilishatangaza zitachapwa tz na mitambo ulishanunuliwa? Pia anadai, ilikuwaje katika chaguzi zilizopita vituo fulani vya kupiga kura hata kura moja haikwenda kwa mpinzani including hata mgombea wa upinzani aliyepiga kura yake katika kituo husika

Binafsi nitatamani kupuuza haya, lakini?
 
Mawakala wa vyama ya siasa wanaosimamia uchaguzi,wametegewa “kiasi kikubwa”cha fedha ili kusaliti wagombea wao.Taarifa za ndani ambazo zimethibitishwa na mwenyekiti wa CHADEMA,Freeman Mbowe zinasema fedha hizo zitatolewa mara baada ya zoezi la kupiga kura.
Mbowe amesema tayari chama chake kimegundua mpango huo,na kwamba wamejiandaa kukabiliana na kila hatua katika kipindi hiki cha “lala salama”.
Taarifa zinasema mawakala hao wamepangwa kununuliwa ili kufanikisha mpango wa CCM kumuingiza mgombea wake,Jakaya Kikwete madarakani.
Imeelezwa kuwa viongozi wa vyama tayari wamejiandaa kufikisha taarifa za njama hizi kwa vyombo vya habari na jumuiya ya kimataifa wakati wowote kuanzia leo.
Mpango wa kuiba kura kupitia mawakala unatarajiwa kufanyika kupitia kile kilichoitwa, “kuokoa majimbo yasiteketee”.Unadaiwa kusukwa na baadhi ya viongozi wa juu wa CCM (Mwanahalisi,27 Octoba 2010.u.k 2)

My take
Duh!muda wa lala salama inabidi tuwe macho sana, maana kuna mbinu chafu zilizoandaliwa kupora ushindi.Naona jamaa wameanza kutapatapa,"mwisho wao umefika".
 
Hizi habari za wizi wa kura ziko wazi na zinajulikana.
Inahitajika nguvu ya ziada kukabiliana na mbinu hizi chafu za CCM ili kuiondoa madarakani. Fikiria kauli yao ya USHINDI NI LAZIMA TENA KWA ASILIMIA 80 NA HAPO HAPO WANATUMIA JESHI LIKIWAAMBIA WAPIGA KURA KUWA LAZIMA KUKUBALI MATOKEO YA KURA YATAKAPOTANGAZWA!! Hii inadhihirisha kabisa kuwa uchaguzi tunaofanya ni kiini macho tu!!

Kweli tuna safari ndefu kufikia demokrasia ya kweli.
 
Wanajamii, jana jioni nilikuwa nikisikiliza idhaa ya Kiswahili ya BBC na kumsikia mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi-NEC akisema kwamba teknolojia ya kisasa itatumika kuhesabu kura za rais, yaani kura zikishahesabiwa vituoni, kutakuwa na mtu wa tume akiwa na laptop na connectivity katika database iliyopo NEC makao makuuili kutuma matokeo mara baada ya kuhesabiwa katika kituo cha kupigia kurakwa ajili ya compilation ya matokeo yote na kutangaza matokeo ya nchi nzima.Sasa wasiwasi wangu unakujakatika mambo yafuatayo:

  • Connectivity inayotumiwa na tume ya uchaguzi ni ya operator gani?
  • Je, connectivity hiyo ipo managed na nani/kampuni ipi?
  • Connectivity route ni ipi?-ni vizuri kujua hili kwa sababu inawezekana kabisa kukawa na wajanja wa CCM somewhere na tetesi zipo kwamba tayari jamaa wapo kwa ajili ya kuchakachua daftari la wapiga kura wakawa na access ya database ya matokeo hivyo kuyafanyia alteration kabla hayajatangazwa na tume.
  • Tujifunze kwamba katika message zilizotumwa za kumchafua Mh. W.P.Slaa (PHD) zilipita katika mtandao ambao upo managed na SIX TELECOM ambayo wabia wake wanafahamika kwamba ni Rostam Aziz na Peter Noni na wengineo. Je, kama connectivity ya database ya tume ya uchaguzi ipo managed na SIX TELECOM, what next????
  • Na kama connectivity ipo katika network ya Vodacom, wat next? Si tunawajua akina Maharage?Watu wanaoshiriki moja kwa moja katika kumchafua Dr. W.P.Slaa(PHD) wapo VodaCom ambayo mbia mkubwa ni Rostam Aziz?
  • Je, vyama vya upinzani vilishirikishwa katika design na kutengeneza database hiyo?
  • Tayari vyama vya upinzani vimeshalalamika kwamba havikushirikishwa katika kupokea karatasi za kupigia kura isipokuwa waliitwa wakati tayari karatasi zimefikishwa katika bohari ya Serikali, je, wanajua ni karatasi ngapi zilipokelewa?
  • Ile idadi ya wapiga kura milioni 19 ina uhusiano gani na hili la kura na kuhesabiwa kwa kura katika makao makuu ya tume ya uchaguzi?

Mwenye macho haambiwi tazama na biblia inasema kwamba “Kwa mtini,jifunzeni mfano”
Tumeshaona tume ya uchaguzi ilivyoharibu uchaguzi kwa Jirani zetu Kenya, pia tukumbuke jinsi George W. Bush alivyoshinda katika uchaguzi nchini Marekani!!! Kura ziliibiwa katika njia zinazoitwa za kisayansi.

Wito wangu kwa Vyama Makini- na hapa simaanishi CCM, NoNoNo, namaanisha vyama vinavyopigania uhuru wa kweli katika kumkomboa mtanzania view makini katika hili vya vilifuatilie kwa umakini sana.

Ni hayo tu.
 
Hali ni tete katika hili!

Limekuja dakika za mwisho na Tume haitaki wapinzani wapate majibu ya maswali yako!
 
CHADEMA na vyama vingine inabidi vidai uhakikisho kwa NEC, kabla ya uchaguzi, kuhusu haya:

(1) NEC itahakikishaje idadi ya kura zilizohesabiwa ndiyo idadi inayotumwa kwao? Maana wanaweza kuhesabau kura 911 na mtumaji akatuma kura 119.

(2) NEC itahakikishaje idadi inayotumwa ndiyo inayofika?
 
Kwa sababu tunakwenda kisayansi basi mawakala wa vyama wapewe copy ya kile kitakachotumwa NEC kwa maana ya kupewa flash disks zenye matokeo na pia kuwe na printer ili waweze kupata hardcopy kama back up ya hizo flash disks. Kingine ni kwamba database itumie encryption yaani https na sio http. Naomba vyama vya upinzani wahakikishe mtandao ni https. Pia ikiwezekana vyama vya upinzani pamoja na CCM viunganishwe na mtandao huo kwenye laptops zao. Pia database hiyo iwe webbased na users wake wajulikane kuanzia administrators mpaka watuma matokeo ili wa chama kingine aweze kuwaona.

La sivyo hali ni mbaya sana!!
 
Matokeo kama hayajachakachuliwa majimboni yakifika NEC hakuna tena uchakachuaji kwa sababu rekodi zitakuwa wazi kwa kila mtu...on that line you are pursuing a dead end my friend...............Uchakachuaji ni kwenye vituo vya kupiga kura tu baada ya hapo hakuna uchakachuaji maana rekodi za makaratasi zitakuwa tayari zimekwisha sambaa kila mahali........................
 
Kuanzia leo,, sionekani tena JF, hadi Tarehe 1 Nov... Maana naona mnataka kuniua na presha.
 
Wana JF,

Twapiga Kura kwa Analog system arafu Kura zetu zinabadilishwa na kuhesabiwa kwa Digital System hapo kuna kupona? Kwahiyo walikataaa kupiga kura kwa mfumo wa digital kwa ku click na ku select wagombea uwatakao na wapiga kura wakimaliza tu system yenyewe inawapa majibu jioni bila ubishi.

Sasa hii ya kuya toa majibu kutoka analog kwenda Digital system kunajambo kubwa sana la kiufundi litatumika.
 
Back
Top Bottom