Mwita Maranya
JF-Expert Member
- Jul 1, 2008
- 10,564
- 7,970
Matokeo kama hayajachakachuliwa majimboni yakifika NEC hakuna tena uchakachuaji kwa sababu rekodi zitakuwa wazi kwa kila mtu...on that line you are pursuing a dead end my friend...............Uchakachuaji ni kwenye vituo vya kupiga kura tu baada ya hapo hakuna uchakachuaji maana rekodi za makaratasi zitakuwa tayari zimekwisha sambaa kila mahali........................
Ndugu yangu tusije tukajidanganya kwamba kura zikishahesabiwa vituoni na mawakala wakapata kopi ndiomwisho wa mchezo. Kumbuka kwamba matokeo ya urais hayapingwi mahakamani kwahiyo tume ikichakachua na ikatangaza mshindi kinyume na matakwa ya wapiga kura hayo makaratasi ya vituoni hayatakuwa na maana yoyote. Hakuna namna hapa ni lazima vyama vijipange kucheza ngoma na NEC jino kwa jino, wakiwaachia nafasi kidogo tu wameumia. Hata Kenya mwaka 2007 mawakala walikuwa na makaratasi yao na baada ya ODM kufanya majumuisho wakakuta Raila ameshinda lakini kivuiti hakuona aibu kufanya uchakachuaji. Lazima kujua kila kitu kinachofanyika kuhusiana na kura zetu, lazima tuzilinde kura zetu kadri tunavyoweza kuanzia vituoni hadi nec.