Wizara ya Ujenzi yamuaga Rais Kikwete rasmi, yamzawadia trekta

Njanga Tz

JF-Expert Member
Mar 19, 2015
843
653
Hapa mnazi mmoja jijini Dar es salaam kumeshapendeza tayari kabisa kwa Wizara ya Ujenzi inayoongozwa na Mh Magufuli kumpa kwa heri ya kuonana Mh Jakaya.

Msondo ngoma bendi ya Ukaya ft inatumbuiza hapa.Update mtapata

Update . Mh Magufuli kisha wasili katika viwanja hv na sasa anasubiliwa mh Jakaya. Sitaweza kutuma pcha kamera yangu imeharibika kama kuna mtu yupo karibu anaweza kutupia pcha.

Sasa raisi anaingia katika viwanja hi i vya mnazi mmoja.
Wakala mbalimbali zinatoa taarifa zao za miaka kumi tanroad tba temesa.

Tanroads wanaelezea mafunikio waliyopata kwa kujenga km5000 na zaidi na kuafanya usanifu wa km4000 hadi sasa.

TBA wanaeleza jinsi walivyojenga nyumba kwa watumishi wa umma
Temesa wanaelezea kuhusu mafanikio ya vivuko
Bodi ya mifuko ya barabara inatoa mafanikio yake
 
wangemualika huyu jamaa ingekuwa safi sana
 
Last edited by a moderator:
Kuna maonyesho ya bendi au ni ufunguzi wa bendi hadi msondo watumbuize.
 
Safii sana Magufuri nchi yako sasa chapa kazi ili heshima irudi, achana na wahuni wa makupe
 
Tunamwomba Mhe. Kikwete aje kutuaga Mikoani tumuulize maswali yafuatayo:- (1) Ulituahidi kupata maji safi na salama hapa Bunda na ikaja kupigiwa msumari na Mhe. Waziri Mkuu kuwa tutapata maji baada ya miezi miwili lakini leo hii ni miezi minane hakuna kinachoendelea. Hii ni danganya toto. (2) Ulituahidi kuleta meli kubwa Ziwa Victoria ili kupunguza adha ya usafiri. Mpaka leo hatujaona hiyo meli. (3) Sasa ni miaka miwili miradi yote ya maendeleo imesimama na Mikoa na Halmashauri haziltewi fedha, Je kama tunalipa kodi na hatuoni maendeleo je kuna tatizo gani?.
 
Jamani zile ahadi za kikwete za 2010 zimetimizwa kweli. Kuna ahadi ilikuwa inasema Tanga itajeuzwa mji wa viwanda..
 
Safii sana Magufuri nchi yako sasa chapa kazi ili heshima irudi, achana na wahuni wa makupe
Mkuu, umeusoma vizuri uzi kweli? tumeambiwa Msondo wapo wanapiga show hapo viwanja vya mnazi 1 na Magufuli ameisha fika, sasa mambo ya kuchapa kazi na kula music wa Msondo wapi na wapi bwn.
 
Aondoke tu fisadi,tunamsubiria october tuionyeshe dunia uchafu wake na familia yake,tutamkumbuka kwa madeni ya nchi,uchumi kushuka kwa 2.1,migomo ya madereva,doctors,Escrow,ahadi hewa za maisha bora kwa kila mtanzania
 
Kuhusu kuondoka kwaaliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja na kujiunga naChadema alisema, "Mgeja alitegemewa kuondoka muda mrefu kutokana na uswaibawake na Edward Lowassa lakini alichelewa kwa sababu alikuwa anasubiri mtotowake aliyegombea viti maalum aliyekosa kura, hivyo alitumia nafasi yakekushawishi viongozi wa chama wampitishe na alipoona ameshindwa aliamua kutimizaazma yake ya siku nyingi ya kukihama chama,"
Akimzungumzia aliyekuwa Mwenyekiti waVijana UVCCM na Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita,alisema aligombea ubunge Jimbo la Kilombero lakini alishindwa hivyo kwa hasiraakaamua kuondoka na kujiunga na Chadema.
 
  • Thanks
Reactions: cpt
Kuhusu kuondoka kwaaliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga, Khamis Mgeja na kujiunga naChadema alisema, “Mgeja alitegemewa kuondoka muda mrefu kutokana na uswaibawake na Edward Lowassa lakini alichelewa kwa sababu alikuwa anasubiri mtotowake aliyegombea viti maalum aliyekosa kura, hivyo alitumia nafasi yakekushawishi viongozi wa chama wampitishe na alipoona ameshindwa aliamua kutimizaazma yake ya siku nyingi ya kukihama chama,”
Akimzungumzia aliyekuwa Mwenyekiti waVijana UVCCM na Mwenyekiti mstaafu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, John Guninita,alisema aligombea ubunge Jimbo la Kilombero lakini alishindwa hivyo kwa hasiraakaamua kuondoka na kujiunga na Chadema.

Ni kweli kila anayekatwa anahama
 
Kikwete na Magufuli Leo pale Mnazi mmoja wamejumuika ambapo wahandisi na Wakandarasi wamemuaga Raisi Kikwete.

M2.jpg

M4.jpg

M3.jpg

M1.jpg
 
Hivi hizi hafla za kuagaaga zinagharamiwa na kodi zetu au?
Na kama ni hivyo kwanini isifanyike hafla moja itakayojumuisha makundi yote ili kuokoa ufujaji wa fedha za walipa kodi.
 
Huku mwanza tuko bize na maandalizi ya raisi wetu lowassa. Kesho atatia team hapa rock city.
Yaan shamrashamra zilishaanza ndo natoka ofice za cdm pale kona ya bwiru yaan hadi raha. Kesho mapeeema ntawai airport kuona raisi wetu akiwasili palee.
 
Jamaniiii tuweke wazi tu....Magufuli Urais wala hana hata SURA NAYO...!!! Yaani hata ukimwona tu, huvutiwi nae kuwa kiongozi...!!! yaani ni kama yuko nyuma ya JK kama mlinzi wake vile..alafu akiongea kidogo MASIFAAA MAELFU KWA JK...anajiharibia sana maskini... SILAZIMISHI MOYO WANGU....LOVE IS FREEEEEE.......
Aaaaarrrgghh...!!! Nimesema ya moyoni...!!! hawa ndio wanao mkatia mkwanja mrefuuuuu...!!!

Atakwambia barabara kilometer 115...usikute iliyojengwa kwa lami ni kilometer 75 tu...nyingine yote anapiga panga...!!! Daaahh...!! Nani anakagua urefu wa barabara mmesikia..!?
 
Back
Top Bottom