Rais Samia, Unda kikosi kazi cha taifa kuhusu elimu tuitakayo Wizara ya Elimu iwe mbali na kikosi kazi hicho

Chipoku

JF-Expert Member
May 19, 2011
254
181
Kongole Mh.Samia Kwa Uwekezaji mkubwa katika Elimu Yetu
Ila Usiruhusu Wizara Ya Elimu Kufanya Hili

Kassim Mpingi Rufiji- Pwani

Ni ukweli usiofichika Kwamba Mh. Rais Samia Amefanya Uwekezaji Mkubwa Kwenye Elimu Yetu Kuanzie Ile Ya Awali Mpaka Elimu Ya Juu.

Wakati Mwalimu Nyerere Anaamua Kupitia Upya Sera Yetu Ya Elimu Ya 1967 (ESR 1967 ) aliunda Kamisheni Ya Rais Katika Elimu Mwaka 1981.

Jopo Hili Lilitafiti na Kuja Na Mapendekezo Muhimu Kwa Mustakabali Wa Taifa Letu. Mfano wa Mapendekezo hayo Ambayo Serikali Iliyafanyia Kazi Ni pamoja na :
-Kuundwa Kwa Tume Ya Utumishi Wa Walimu (TSC),
-Kuundwa Kwa Idara Ya Elimu Udsm
-Kuundwa Kwa Chuo Kikuu Huria,
-Kuundwa Kwa Sera Ya Nchi Ya Sayansi Na Technolojia n.k.

-Mzee Mwinyi Alipoona Elimu Yetu Inayumba Akaunda Kikosi Kazi Cha Taifa Kwenye Elimu Na Akawapa Hadidu Za Rejea (TOR) Tatu:

-Kuangalia Kwa Kina Matatizo Yote Ya Elimu Tuliyoyarithi Kuja Na Ufumbuzi,

-Kuandaa Sera Mpya Ya Elimu,

-Kuja Na Mikakati Ya Utekelezaji.

Mapendekezo Ya Timu Hio Ndio ilileta Sera Yetu Ya Elimu Na Mafunzo Ya 1995,
Sera Ya Elimu Ya Ufundi 1996,
Sera Ya Elimu Ya Juu 1999,
Sera Ya Tehama 2006, na
-Kutenganishwa SUA Na Muhimbili Toka UDSM, ambalo hili ni zao la kuanzishwa kwa "University Act 2005"

Mzee Mwinyi na Mzee Nyerere Walipotaka Mabadiliko katika Elimu Yetu Walifanya Hivyo Kupitia Timu Za Wataalamu Walioziunda na Kujikita Kwenye Tafiti Kabla Kuamua Na Kufanya Lolote Kwenye Elimu Yetu, Hawakuwachia Wizara Ya Elimu Waunde Kikundi Cha Watu Wachache Wakusanye Maoni Wakajifungie Mahala Kuyachakata.

Mabadiliko Mengi Ya Elimu Yetu Kati ya miaka ya 1970 Mpaka miaka ya 1980.

Kuanzia Azimio La Musoma 1974 Lililota UPE,
Sheria Yetu Ya Elimu Ile Ya 1969 na Baadaye mwaka 1978 Zilijikita Kwenye Tafiti Na Kuwahusisha Wataalamu Bobezi Na Sio Wizara Ya Elimu Pekee yao.

Moja Ya Tafiti Hizo Ni Ile Ya 1965 "Vocation Education Fallacy ".
Mzee Mkapa Alitumia Sana Sera Ya Elimu na Mafunzo 1995 iliyotokana Na Vikosi Kazi na Tafiti Kutekeleza Mipango Yake Maarufu Kwa Mafanikio Makubwa,
Ule Wa Maendeleo Ya Msingi Na Sekondari Na Utekelezaji Wa Malengo Wa Milenia 2000 (Hapa Tulipata Zawadi MDGs)
Lakini Mpaka Anaondoka Duniani Alisisitiza Umuhimu Wa Mjadala Wa Kitaifa kuhusu Elimu Yetu.

Mzee Kikwete Kafanya Mengi Katika Elimu Yetu.
Unaweza Tazama Kwenye Andiko Maarufu " Ten Years Of Jakaya Kikwete Presidency In Tz Promise , Achievement And Challenge In Education: ya Kitila Mkumbo

Moja Ya Mafanikio Hayo Ni Ujenzi Wa Shule Za Kata.

Pia Ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Dodoma (UDOM)

Tatizo Kubwa Lilianza 2014 Kwenye Sera Yetu Ya Elimu Na Mafunzo 2014.

Ambapo Kwa Mara Ya Kwanza Nchi Iliandaa Sera Ya Elimu Bila Ushahidi Wa Tafiti.

Nchi Imeandaa Sera Ya Elimu Bila Mabadiliko Ya Sheria Yetu Ya Elimu Na 25,1978.

Mh. Rais Sera Yetu Ya Elimu 2014 Inagongana Na Sheria Yetu Ya Elimu 1978 Mf. Wakati Sheria Ya Elimu Inatamka Miaka Saba Umri Wa Kuanza Shule Sera Inatamka Miaka Sita.
Wataalamu Wale Walitunga Sera Na Kulitia Hasara Taifa Bado Wako Wizara Hiyo Unayoipa Jukumu La Kuangalia Tena Sera Na Mitaala Yetu.

(Hakimu Hawezi Kuwa Shahidi)
-Mh. Rais Hayati Magufuli Aliagiza Somo La Historia Lianze Kufundishwa Kuanzia Darasa La Kwanza, Wizara Kupitia TET Wakajifungia Bila Kufanya Tafiti Wakandaa Vitabu Vilivyotumia Mabilioni Ya Watanzania Kabla Ya Mchakato Kusitishwa Na Sasa Maelfu Ya Nakala Ya Vitabu Vile Viko Mahala Fulani Vikisubiri Kuharibiwa.
Nani Atalipa Gharama Hii Mh. Rais?

(Ukichunguza TET Mh. Rais hata Kitabu Cha Kidato Cha Tatu Kiswahili Kinachoweza Kutungwa Na Mwl Bobezi Mwenye Shahada Ya Kwanza Wao Wanaalika Maprofesa Na Kujifungia Hoteli Moja Kwa Miezi Kadhaa Wakitumia Mabilioni Ya fedha)
Mh. Rais Tunamshukuru Sana Kwa Miongozo Yako Ya Kutaka Mabadiliko Kwenye Mfumo Wa Elimu Lakini Ukitaka Mabadiliko Ya Kweli Na Jina Lako Likumbukwe Na Watanzania Wa Leo Na Kesho Unda Timu Ya Wataalamu Wape Muda Na Hadidu Rejea Wafanye Tafiti Ya Kutosha Kisha Waje Na Majibu Ya Dawa Ya Elimu Yetu.

Haya Mambo Ya Wizara Ya Elimu Na TET Kuita Watu Na Kuwapa Dakika Tano Ya Kutoa Maoni Hayatupeleki Mahala.
Ni Mambo Haya Ndio Yalileta Sera Ya Elimu Ya 2014 Iliyozinduliwa 2015 Wakati Nchi Ipo Kwenye Fikra Nzito Ya Uchaguzi Na Hakuna Wa Kukumbuka Sera Hiyo Imesahau Marekebisho Ya Sheria.

Ushauri Wangu Kwako Mh. Rais.
Kama Ulivyofanya Kwenye UVIKO-19 na Kwenye Kikosi Kazi Cha Masuala Ya Demokrasia Unda Kikosi Kazi Cha Taifa Kuhusu Elimu Tuitakayo Wizara Ya Elimu Iwe Mbali Na Kikosi Kazi Hicho Wape Hadidu za Rejea na Muda.
Wewe Hautokuwa Wa Kwanza Kufanya Hivyo, Alifanya Mzee Nyerere (Makweta Commission 1981), Mzee Mwinyi (National Task Force 1990).
Tena Mzee Mwinyi Aliwapa Muda 1990-1992.
Kwa Kuwa Mama Yetu Ni Msikivu Bila Shaka Utazingatia Haya.
Mwisho Usisahau Kumtuma CAG Kukagua Yale Mabilioni Ya Vitabu Vya Historia Vinavyosubiri Kuharibiwa Na Tusiruhusu Tena Maamuzi Yasiyo Na Tafiti Katika Elimu Yetu.

Asante Mama.
Kassimu Mpingi.
Rufiji-Pwani.
 
Lakini mchakato wa maboresho ya Elimu umeanza toka mwaka huu na utakoma mwezi desemba ndio watahitimisha,so hawajajifungia kama unavyosema bali wanaitisha makongamano ya wadau maeneo mbalimbali..
Wao pia wanafahamu fika hili uliloandika kwa hiyo qatafanyia Kazi na kuja na kitu muhimu..
Najua wataipeleka elimu kuwa skills based competancy lakini changamoto kubwa bado itakuwa ni aina ya lugha ya kufundishia kufikosha ujuzi na maarifa kwa watu.
 
Back
Top Bottom