Wizara ya Afya yamruka Manumba, wahoji alikoipata ripoti ya Mwakyembe!

Tatizo kubwa hapa ni Mwakyembe mwenyewe. Aseme kinachomsibu basi. Akiendelea kuficha kama alivyoficha baadhi ya mambo kwenye taarifa ya Richmond basi. Nawaona wanakwenda kwa Mchungaji Gwajima kwa zamu. Jana mshirika wake wa karibu, Nape, alikuwa huko. Tusubiri miujiza ya Mchungaji huyu?
 
Mkuu Richard samahani usiseme hatuna jeshi la Polisi Tanzania, sema ndani ya jeshi la Polisi kuna wababaishaji na wanatumiwa!!!! Kama kungekuwa hakuna jeshi la polisi, wewe usingelilala nyumbani mwako, panapostahili kusifia sifia, polisi wapo na wanafanya kazi zao vizuri tuu!!!!!

Nakubaliana na wewe Mtumishi Wetu! Lakini fikiria uonevu unaofanywa na Jeshi hili. Hapa tunazungumza jinsi wanavyojikanyaga kuhusiana na WAZIRI! Je ingekuwa ni mwnanchi wa kawaida, si wanadharau tu! Ona ni kesi ngapi ziko mahakamani, tena za shutuma kali dhidi ya watu fulani fulani. Huyu Manumba na mwenzie DPP na yule Hosea walifanya usanii mkubwa kwenye kesi ya Richmond, EPA na hatuna uhakika sana kama wale walioko mahakamani na gharama kubwa za kesi zile kwamba ni wahusika. Kwa namna hii unashawishika kuamini hawa mapolisi wetu wanatumiwa na wababishaji- ndio maana nimekubaliana na hoja yako.

Sitaki niamini kuwa jeshi la Polisi ndio linanifanya nilale kwa amani! Ukipata shida ukapiga simu- watakuja kwa wakati wao, watauliza maswali ya kijinga! Usingizi wangu ninahakikishiwa na ulinzi shirikishi katika maeneo yangu na hawa makampuni ya binafsi! Polisi wanaua hovyo hovyo siku hizi, bora lifute- ni kama hatuna Jeshi la Polisi Tanzania!

Mungu Ibariki Tanzania
Pole sana ndugu yangu ni kweli hawa jamaa ni wababaishaji hasa linapokuja swala la ufisadi, inaonekana kwenye ufisadi wanajali mshiko si vinginevyo!!!! Ninacho amini the whole government system is kaput iko ICU inahitaji mabadiliko makubwa saana, nadhani a new system with a new constitution utakuwa uponyaji wa TANZANIA!!!! Vinginevyo na kutwanga maji kwenye kinu!!!!!

 
Juzi juzi nikampigia mshikaji simu yuko nairobi, nikamwambia asee embu angalia series nzuri uninunulie. Akanijibu hivi, "acha uzembe wewe unataka kununua series nzuri wakati bongo kuna series kali kuliko zote,

1.Bunge (season III-Posho),
2. Migomo (season II-Blandina vs Madaktari),
3. Dr.Mwakyembe (season II- Majibu Gongana)

sasa imeanza kuamini.
 
Dada siku ulikuwa ushaimaliza vizuri tu kwa kweli, ila sijui shetani gani kakusukuma ujambe mawazo yako usiku huu wa manane. Kwanini usilale tu dada yangu??Chadema katokea wap kwenye hii habari??Mbona chadema inawaumiza sana???kwanini upate shida si ujiunge na chadema tu nawe uwe huru kifikra??

Kwako wewe taarifa ya Tamko la waziri wa afya, taarifa ya Manumba na ya Dk. Mwakyembe iliyoelezewa humu na Tanzania Daima ni ya Chadema??Je ulitaka magazeti yasiandike habari hizi ili yaandike habari zipi???Dada hebu lala kabla wengine hawajaanza kukushambulia kwa upuupu uliouweka hapa. Yaani umeweka maneno machache tu ila umaharibu, hivi ukijaza paragraph si itakuwa balaa humu?

Kwani tatizo lako hapa ni nini? Kwamba Tanzania Daima ni gazeti la propaganda la Chadema? Mbona this is obvious: Tanzania Daima ni chombo cha propaganda cha CHADEMA kama lilivyo gazeti la Uhuru kwa CCM. Period!
 
Nimeipitia hiyo habari mwanzo mpaka mwisho mara tatu, sijaona pahala Wizara ya afya ilipomruka Manumba.

Wacheni udaku.

WINGU zito limetanda kuhusu afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda, kusema kuwa ripoti ya ugonjwa wa Mwakyembe, anayo mwenyewe na kwamba wizara haina ripoti iliyotolewa na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, kwa waandishi wa habari.

Lakini wakati Dk Mponda akitoa kauli hiyo, baadhi ya watu wa kada tofauti wakiwamo viongozi wa dini na wasomi, wamekosoa ripoti hiyo ya polisi.

Mmoja wa watu hao, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa alisema,"hata mimi simwamini Manumba."

Malumbano hayo yanakuja wakati Dk Mwakyembe ambaye ni pia ni Mbunge wa Kyela, akitarajiwa nchini jana kwenda India kwa matibabu katika Hospitali ya Apollo.

Mahojiano na Waziri Mponda

Gazeti: Salaam Mheshimiwa waziri. Nimekupigia kutaka ufafanuzi kuhusu ripoti iliyotolewa na DCI Manumba kuhusu ugonjwa wa Dk Mwakyembe. Ninyi wizara mnaitambuaje?

Waziri: Kiutaratibu ripoti ya daktari ni ya mgonjwa. Sisi hatujaandika ripoti, muulizeni DCI Manumba awape ufafanuzi kama kuna kitu mnataka kuuliza zaidi kwa alichokizungumza na ninyi waandishi.

Gazeti: DCI Manumba alitoa taarifa kwa waandishi lakini aki-refer (rejea) ripoti kutoka wizarani (afya), baada ya kuwasiliana nanyi, kwa nini wewe usiizungumzie?

Waziri: Narudia tena, muulizeni yeye DCI au Dk Mwakyembe mwenyewe, wao wanaweza kuwapa ufafanuzi.

Gazeti: Tayari Dk Mwakyembe mwenyewe amekwishatoa tamko kwamba ripoti iliyosomwa na polisi, haina uhusiano na ripoti aliyokuwa nayo yeye kuhusu uchunguzi wa maradhi yake. Je, ripoti hii ya polisi ambayo wamedai wameipata kwenu (wizara) mmeitoa wapi?

Waziri: Ni hivi, baada ya daktari kumchunguza mgonjwa, hutoa ripoti na kumpa mgonjwa. Kwa hiyo, ripoti ya Hospitali ya Apollo anayo Dk Mwakyembe mwenyewe. Tena yeye kaeleza vizuri kabisa kwamba hata uchunguzi bado unaendelea. sasa hapo mnataka niseme nini tena?

Gazeti: Sasa kama ripoti anayo Dk Mwakyembe mwenyewe na tayari amesema ripoti ya polisi waliyosema imetoka kwenu siyo sahihi, je wizara iliwahi kupata ripoti ya Hospitali ya Apollo.

Waziri: Sisi tulichokifanya ni kumpa rufaa Dk Mwakyembe kwenda India. Ripoti hadi sasa anayo mwenyewe ingawa huwa tunapata taarifa baada ya yeye mgonjwa kuzileta kwetu. Hizo ndizo kanuni za taaluma ya udaktari, kwa hiyo ripoti anayo mwenyewe.

Gazeti: Sasa kama ripoti anayo Dk Mwakyembe mwenyewe, hii iliyosomwa na DCI imetoka wapi?

Waziri: Kumbuka DCI ana njia zake nyingi za kupata taarifa. Kwa hiyo ndiyo maana nasisitiza, muulizeni mwenyewe awape ufafanuzi kwa aliyozungumza na waandishi. Sisi wizara mnatuonea tu.

Gazeti: Lakini, hata kama ugonjwa ni siri, huoni mheshimiwa waziri kwamba kuna haja ya kuondoa utata kuhusu suala hili ikizingatiwa kuwa Dk Mwakyembe ni kiongozi anayegusa hisia za watu tofauti?

Waziri: Wanaoweza kuzungumzia maradhi yake, ni familia yake au yeye mwenyewe kwani ndiye mwenye ripoti. Mtafuteni au iulizeni familia yake iwapatie majibu. Lakini wizara haiwezi kufanya hivyo. Narudia tena, kuhusu hilo la DCI muulizeni mwenyewe awape ufafanuzi, mimi sijaona ripoti ya DCI aliyozungumza na waandishi wa habari.

Alichosema DCI

Akizungumza na waandishi mwishoni wa wiki iliyopita, Manumba alisema, “ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India. Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu."

Jana, alipoelezwa kwamba Dk Mwakyembe ameikana ripoti yao, Manumba alisema "sasa suala hilo litashughukiliwa kisheria."

Alisisitiza kuwa suala hilo litashughulikiwa kwa kufuata misingi ya kisheria na kwamba, Jeshi la Polisi haliko tayari kuendeleza malumbano kupitia vyombo vya habari.

"Hatua zaidi zinachukuliwa dhidi ya jambo hilo, kwa sasa litashughukiliwa kwa kufuata misingi ya kisheria kama nilivyokwishaeleza awali,"alisema Manumba.
 
Kama kawaida yao viongozi wa nchi,kila mtua hajui anachosema.Ndugu zangu picha linaendelea kae vizuri kwenye vitiwale walionje waiteni.[

Inatubidi kuwa makini kama viogozi wetu wanapishana kauli niwazi hakuna kuelewana. hofu yangu wasituleete KIMBALI maana kama kweli wamepeana sumu na ikathibitika,tena m2 akafa kwasababu hiyo choki ijengeka miongoni mwa wanajamii kwamba kundi furani(mafisadi) ndio pekee wenye haki ya kutawala.

kwahali hii ya kupishana kauli haileti picha nzuri kwataifa kama hili, natoa tahahali kuwa makini na jambo hili na sio kutumia ushabiki kwani ni hatari sana kwa usiwi wa taifa.
 
Usiwe mvivu wa kusoma, hayo ni maneno ya kanjanja aliyeandika, ni wapi anapo quote waziri au msemaji wa wizara. Upo hapo ulipo?

What exactly is your interest? Unataka kumwokoa Manumba ili umlaumu kanjanja? Kaa kimya tu bro!
 
READ BETWEEN THE LINES MKUU ZOMBA! Hujaona??????????? Waziri anaposema hajui report kaipata wapi....na Manumba anasema ameipata wizara ya afya unasema huoni wapi wizara imemkana?
Nimeipitia hiyo habari mwanzo mpaka mwisho mara tatu, sijaona pahala Wizara ya afya ilipomruka Manumba.

Wacheni udaku.
 
Kwani tatizo lako hapa ni nini? Kwamba Tanzania Daima ni gazeti la propaganda la Chadema? Mbona this is obvious: Tanzania Daima ni chombo cha propaganda cha CHADEMA kama lilivyo gazeti la Uhuru kwa CCM. Period!
Wewe unataka habari au kujua chombo cha habari ni cha nani??magamba mmefungwa kifikra, badala ya kusoma habari, mnatafuta mmiliki wa chombo, inawahusu nn someni habari muhabarishwe???Haya na Mwananchi limeandika hivi hivi nacho ni chombo cha propaganda cha chadema?

Pia naona umesahau kuwa Tanzania Daima ilichofanya ni kucombine taarifa 3 huru na kuzichambua. Hakuna kilichotungwa na Tanzania Daima, mana kama Taarifa ya Mwakyembe ipo hadharani, ya Manumba ipo hadharani, ya waziri ipo. Hapo upropaganda unatokea wap??Nasukumwa kuamini kuwa matumizi ya neno propaganda na maana yake hujaijua vizuri. Chadema kinauzika tu hakina haja ya kutumia njia mnazozifikiria nyinyi.
 
Tanzania Daima kagazeti ka propaganda ka chadema.

someni muone maneno ya waziri mengine ya huyo mwandishi wenu.

Kwa hiyo Mwakembe nae ni mtu wa propaganda? Manake alikanusha kwa riport ya Manumba sio ya ukweli. Weka interest za chama pembeni, then changia hoja!
 
Dr. Mwakyembe alikuwa Mzima wa Afya akifanya shughuli zake za kila siku bila matatizo yoyote, Aliwahi kupata kutishiwa kuuawa na akatoa taarifa POLICE, na Police aikuchukua hatua yoyote, Ghafla hali yake imebadilika kwa kuwa na ugonjwa usiojulikana akalazimika kupelekwa India kwa matibabu baada ya matibabu yake kushindikana hapa Tz katika hospitali zetu, Leo Hii Manumba amekuja na Taarifa ya uchunguzi toka kwa madakitari wanaomtibu mwakyembe kuwa akupewa sumu, Basi na atueleze Madakitari wake wamesema anaumwa nini?? Kama hakulishwa sumu.

Kwa Mtizamo wangu naona sasa umefika wakati wa kubadilisha mfumo wa jeshi la Polisi, Jeshi hili liwe huru kutoka mikononi mwa wanasiasa. Uteuzi wa mkuu na watendaji wote wakuu wa jeshi toka kwa wanasiasa hauleti tija kwa Tanzania na Watanzania, Jeshi limekuwa Onevu kwa Raia na mali zao, Rushwa imekithiri ndani ya jeshi, Ukabila ubinafsi vyote tunaviona. Iundwe bodi huru ya kusimamia jeshi hili. Nafasi ya IGP Iombwe na watendaji wenye sifa ndani ya jeshi. IGP Ateuwe Ma-RPC na wakuu wa Idara Bodi ipitishe, Bodi iundwe na Ma-ex IGP Waadilifu kama Mahundi na member wengine wakiwemo raia. Tumechoka na Polisi wasiobadilika.
 
READ BETWEEN THE LINES MKUU ZOMBA! Hujaona??????????? Waziri anaposema hajui report kaipata wapi....na Manumba anasema ameipata wizara ya afya unasema huoni wapi wizara imemkana?
Okay mi nshamwelewa, huyu jamaa nini kinamtatiza, yeye anataka aone sehemu imeandikwa "Hivyo Wizara inamkana/inamruka Manumba". So kwa kuwa hajaona neno hilo yeye haamin kuwa manumba amekanwa na wizara. Watu wa hivi wapo kwenye jamii, tusiendelee kumshangaa huyu jamaa.
 
Tulitegemea yote haya kutokea. Na bado mengi yatajulikana.

Kuna msemo kwa Kiluguru unaosema "NO SECRET UNDER THE SUN"


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Dr. Mwakyembe alikuwa Mzima wa Afya akifanya shughuli zake za kila siku bila matatizo yoyote, Aliwahi kupata kutishiwa kuuawa na akatoa taarifa POLICE, na Police aikuchukua hatua yoyote, Ghafla hali yake imebadilika kwa kuwa na ugonjwa usiojulikana akalazimika kupelekwa India kwa matibabu baada ya matibabu yake kushindikana hapa Tz katika hospitali zetu, Leo Hii Manumba amekuja na Taarifa ya uchunguzi toka kwa madakitari wanaomtibu mwakyembe kuwa akupewa sumu, Basi na atueleze Madakitari wake wamesema anaumwa nini?? Kama hakulishwa sumu.

Kwa Mtizamo wangu naona sasa umefika wakati wa kubadilisha mfumo wa jeshi la Polisi, Jeshi hili liwe huru kutoka mikononi mwa wanasiasa. Uteuzi wa mkuu na watendaji wote wakuu wa jeshi toka kwa wanasiasa hauleti tija kwa Tanzania na Watanzania, Jeshi limekuwa Onevu kwa Raia na mali zao, Rushwa imekithiri ndani ya jeshi, Ukabila ubinafsi vyote tunaviona. Iundwe bodi huru ya kusimamia jeshi hili. Nafasi ya IGP Iombwe na watendaji wenye sifa ndani ya jeshi. IGP Ateuwe Ma-RPC na wakuu wa Idara Bodi ipitishe, Bodi iundwe na Ma-ex IGP Waadilifu kama Mahundi na member wengine wakiwemo raia. Tumechoka na Polisi wasiobadilika.
Polisi wamemzuia Mwakyembe kusema UKWELI juu ya afya yake? Mbona WM Pinda alimwambia awaeleze WATANZANIA kinachomsibu! Akaenda kwa Gwajima akabaki kuumauma maneno. Taarifa yake hii ya juzi nayo haina kitu. Kwa nini aliweke TAIFA katika utata wa namna hii? Ananufaikaje na mkanganyiko huu? Wapo WATANZANIA wengi tu wagonjwa kuliko hata yeye. Hivi kweli Mwakyembe ni wa kusemewa na Sitta? Ili iweje?
 
kilichobaki na inavyoonekana hapa ni kummaliza mwakyembe anatakai awe makini ..na mwakyembe anatakiwa a resign kwa usalama wake
 
READ BETWEEN THE LINES MKUU ZOMBA! Hujaona??????????? Waziri anaposema hajui report kaipata wapi....na Manumba anasema ameipata wizara ya afya unasema huoni wapi wizara imemkana?

Why should I read between the lines? haya hapa maneno ya waziri:

"Naomba usininukuu vinginevyo hao ndiyo waliosema ni vema mkawafuata na kuwauliza nadhani mtapata majibu sahihi,"

Yaliyobaki ni maneno ya kanjanja, sasa huyo kanjanja wa Tanzania Daima kwanini nimuamini? anaweza kusema chochote mradi ajaze chuki na fitina kama kawaida. Hujui Tanzania Daima ni gazeti la nani?
 
Kiranja mkuu wa mawaziri wote na watendaji wote serikalini ikiwemo na Robert Manumba amekwishasema:

"TUKIWAKAMATA MAFISADI NCHI ITAYUMBA".
..........sasa hawa wadogo wafanye nini? lazima wakanyagane (upande hofu ya mafisadi upande mwingine hofu ya umma..hakutakosekana mikanganyiko)....but am still interested with this movie though soon itakuja mpya nyingine tena..tusubiri
 
Back
Top Bottom