Nukuu 10 za Jenerali Mabeyo

FbUser

JF-Expert Member
Oct 22, 2014
430
623
1. Magufuli aliomba akafie nyumbani kwake, maana alisema hawezi kupona.

2. Alishangaa nilipomwambia sina mamlaka ya kuruhusu hilo.

3. Aliomba aitiwe Paroko wake, Pd Makubi na Kard. Pengo ambao walifika na kumpa upako wa wagonjwa!

4. Alikata roho mbele yetu wakuu wote watatu wa vyombo vya usalama.

5. Makamu wa rais, Waziri Mkuu na Katibu Mkuu kiongozi hawakuwepo Dar. Tukaamua kuwaita Waziri Mkuu na Katibu Mkuu kiongozi ambao walifika na kuwapa taarifa ya msiba.

6. Ilibidi tutumie njia nyingine kumjulisha makamu wa rais ambaye ndiye alitakiwa kutangaza taarifa ya msiba.

7. Kulikuwa na mjadala kipi kianze kati ya mazishi na kumwapisha makamu wa rais kuwa rais.

8. Wengi walishauri yafanyike mazishi kwanza, lakini nilishauri uapisho uanze kwanza, kwa sababu marais wa nchi nyingine walitakiwa wapokelewe na rais wa nchi.

9. Lilikuja suala la gwaride la uapisho ambapo walishauri kusiwe na gwaride. NILIWAKATALIWA kwa sababu aliyekuwa anaapishwa ni amiri jeshi mkuu,na lazima bendera ya amiri jeshi mkuu ipandishwe kwa gwaride. Kinyume na hilo, jeshi LISINGEMTAMBUA kama amiri jeshi mkuu.

10. Kulikuwa na baadhi ya mawazo, kwamba inakuwaje juu ya makamu wa rais kushika nafasi ya urais. Nadhani walisahau kuwa katiba ya nchi inasema nini, ikiwa rais aliye madarakani anafariki au akishindwa kuongoza. Nami nilisema ni vema utaratibu huo ukafuatwa na ni jambo jema.
 
Hii namba kumi ndiyo inayochafua hadhi na heshima ya akina Kabudi, Bashiru na Ndugai.
 
Kitendo cha CDF Mabeyo kuzungumzia hili jambo ninaona anastahili pongezi sana, kwa namna fulani amekuja kuondoa baadhi ya sintofahamu zilizokuwepo juu ya msiba wa Hayati Magufuli, ameonesha ujasiri kwa kiwango cha kuridhisha.

Ameona hakuna sababu ya kufichana kuhusu hizi taarifa zinazotuhusu watanzania, Magufuli [RIP] alikuwa kiongozi wetu, hivyo nibhaki yetu kupata taarifa zinazohusu nini kilitokea wakati wa msiba wa ugonjwa wake mpaka mauti yalipomkuta.

Natumai hili litakuwa fundisho kwa viongozi wa sasa waliopo serikalini, tabia za kufichana taarifa za ugonjwa au vifo vya viongozi wetu sio sawa, ni uoga usio na maana, inaenda kinyume na haki yetu ya kupata taarifa sahihi kwa wakati, hasa zinazowahusu viongozi wetu ambao kimsingi ni watumishi wetu.
 
1. "Rais aliomba akafie nyumbani kwake, maana alisema hawezi kupona.
2. Alishangaa nilipomwambia sina mamlaka ya kuruhusu hilo.
3. Aliomba aitiwe Paroko wake, Pd Makubi na Kard. Pengo ambao walifika na kumpa upako wa wagonjwa!
4. Alikata roho mbele yetu wakuu wote watatu wa vyombo vya usalama.
5. Makamu wa rais, Waziri Mkuu na Katibu Mkuu kiongozi hawakuwepo Dar. Tukaamua kuwaita Waziri Mkuu na Katibu Mkuu kiongozi ambao walifika na kuwapa taarifa ya msiba.
6. Ilibidi tutumie njia nyingine kumjulisha makamu wa rais ambaye ndiye alitakiwa kutangaza taarifa ya msiba.
7. Kulikuwa na mjadala kipi kianze kati ya mazishi na kumwapisha makamu wa rais kuwa rais.
8. Wengi walishauri yafanyike mazishi kwanza, lakini nilishauri uapisho uanze kwanza, kwa sababu marais wa nchi nyingine walitakiwa wapokelewe na rais wa nchi.
9. Lilikuja suala la gwaride la uapisho ambapo walishauri kusiwe na gwaride. NILIWAKATALIWA kwa sababu aliyekuwa anaapishwa ni amiri jeshi mkuu,na lazima bendera ya amiri jeshi mkuu ipandishwe kwa gwaride. Kinyume na hilo, jeshi LISINGEMTAMBUA kama amiri jeshi mkuu.
10. Kulikuwa na baadhi ya mawazo, kwamba inakuwaje juu ya makamu wa rais kushika nafasi ya urais. Nadhani walisahau kuwa katiba ya nchi inasema nini, ikiwa rais aliye madarakani anafariki au akishindwa kuongoza. Nami nilisema ni vema utaratibu huo ukafuatwa na ni jambo jema.
Hiyo namba 10 ni yako.
 
Watu wakizoezwa kukiuka katiba huwa nihatari sana...wanataka kufanya mambo tofautii na katiba nivile kamanda alisimama wima!! Najiuliza mkaa hapa angelikuwepo ingelikuwajeee? Anyways hayamambo ni mazito najela si pazuri
Hata kama angekuwepo ni lazima katiba ingefuatwa !
 
Back
Top Bottom