Wizara ya Afya yamruka Manumba, wahoji alikoipata ripoti ya Mwakyembe!

Kwa wasiofahamu nawajuza na wanaofahamu nawakumbusha;

Robert Manumba anatoka sehemu moja na Andrew Chenge: Ndio maana kwenye sakata la rada alivujisha siri kwa chenge baada ya maafisa wa SFO kupanga kuja kumhoji chenge juu ya paundi 600,000 alizompatia Dr. Idrisa Rashid toka kwenye akaunti yake. Alimshauri chenge ajibu kuwa amemkopesha rafiki yake ili aendeleze mradi wa fenicha.Chenge aliwajibu hivyo SFO.

Kwenye sakata la Mwakyembe hatutegemei chochote cha maana toka kwa Manumba. Ushauri wangu kwa Mwakyembe atuambie kwanza aliyotuficha kwani ndiyo yanayomtesa yeye mwenyewe na sisi watz kwa ujumla. Pili atuambie ni nini kilichoharibu ngozi yake ili watz tuamue kabla mambo hayajazidi kuharibika.

Robert Manumba anafadhiliwa na mafisadi.
 
SCREW 'EM! Serikali moja, chama kimoja, utawala mmoja lakini wanafanya kazi utadhani nchi ya wagagagigikoko na wale wa mgonenagonago!

Rais hajui anachosema Wazrii Mkuu, Waziri Mkuu hajui anachosema Rais, Spika hajui Rais alisema nini, Waziri hajui Waziri mwenzie amesema nini! Sijui wakiingiaga kwenye hivyo vikao vyao wanafanyaje kwa kweli!

MM
We acha tu kazi ipo hapo,hakuna msimamo mmoja ndani ya serikali moja,yaani hapo ni kama kuna serikali ya nseto

Polisi wana serikali yao na wasemaji wao
bunge lina serikali yake na wasemaji wake
Baraza la mawaziri lina serikali yake na wasemaje wake
Raisi ana uongozi wake na kurugenzi yake ya habari

tume baki wananchi tunaserikali yetu na wasekaji wetu

kila mtu anaibuka na kusema lake,ndani ya serikali kauri zaidi ya mia zinatofautiana,

Mh Sita nae kasema tena yeye ni waziri hawezi sema uongo

swali langu kwa DCI atamshitaki vipi Mh Sitta kama ile ripoti aliyosema kaipata wizara ya afya nayo ni ripoti tata na imekanushwa na wizara husika?
 
Kwa wasiofahamu nawafahamisha na wanaofahamu nawakumbusha;

Robert Manumba anatoka jimbo moja na Andrew Chenge;
Ndio maana kwenye sakata la rada wale jamaa wa SFO walipopanga kumhoji chenge kuhusu paundi 600,000 alizotoa kwenye akaunti yake iliyoko kisiwa cha Jersey na kumpa Dr Idrisa Rashid, Manumba alivujisha siri kwa Chenge na wakapanga chenge ajibu kuwa alimkopesha rafiki yake kwa ajili ya mtaji wa fenicha. Wazungu walidhani Manumba ana integrity! kumbe ana kichwa cha nazi.

Kwa suala la Mwakyembe polisi hawawezi kusema ukweli hata ukiwa mdogo kiasi cha punje ya haradali!
Mwakyembe atuambie yeye mwenyewe anachoumwa. Isitoshe kile alichotuficha kinaendelea kututesa yeye mwenyewe na watanzania kwa ujumla mpaka leo. Fyatuka Dr. watz tuamue kabla mambo hayajazidi kuharibika. Mwenzio EL alishalipuka kwenye kikao wewe lipuka hadharani.
Manumba kwao Lamadi kule Magu. Jamaa wamejipanga vizuri tu. DPP kijana wa Chenge, DCI ndugu ya Chenge, naibu AG naye ...Mwakyembe aumalize utata huu. Asimwachie Sitta wala Mungu.
 
kwa sasa jeshi la polisi si chombo cha kuamini wasemacho-wala wachunguzacho-maana wao ndio wanaoharibu mambo coz ufisadi umeshawaharibu-kila kitu wao wanafanya kwa uinterest ya watu flani-naamini rais pia anafaham hivi-ila naye anaacha system ijiendeshe yenyewe.wasipobadilika lazima itafikia hatua tuanze kuuana wenyewe kwa wenyewe
 
Tufikirie JWTz wachukue nchi wakuu.
Hakuna haja. Wametoka akina Mboma huko mafisadi wakubwa tu sasa. Tunataka Rais atakayesimamia KATIBA na SHERIA za NCHI basi. Hebu fikiria hata lile suala la vinasa sauti kwenye kitanda cha Dr Slaa kule Dodoma angali Mbunge halikuwahi kwisha wala kutoka hapo kwa Manumba.
 
"Alisema kwa kuwa Dk. Mwakyembe anatibiwa kwa gharama za serikali, ni lazima madaktari wanaomtibu wafikishe taarifa hizo serikalini."



Hivi ukitibiwa kwa gharama za mtu fulani siri zako za ugonjwa lazima apewe mfadhili wa matibabu?



Manumber apo alikuwa anamdanganya nani, sisi wananchi, yeye mwenyewe, m.k.e wake au watoto wadogo?



Hivi mtu akiumwa akalalamika kanyweshwa sumu halafu kuna watu wanapindisha pindisha ukweli wa mambo, picha gani mtu wa akili timamu anaipata?



Apo ndo utajua viongozi wetu wasivyofata utaratibu wala sheria. Mkurugenzi wa upelelezi anamuwekea maneno mdomoni Waziri wa Afya! Alijua Waziri angemuogopa akae kimya kwa vile ye ni mkurugenzi wa upele.lezi.


  • Alafu jamaa ni msomi wa sheria. Duh, entilligency doesnt only come by way of classes but birth!
 
Nimeipitia hiyo habari mwanzo mpaka mwisho mara tatu, sijaona pahala Wizara ya afya ilipomruka Manumba.

Wacheni udaku.

Wewe huwezi kuona kwa sababu labda umetumwa au uwezo wako ni mdogo. Kama hujaona tukusaidieje sisi? Wewe tumikia tu tumbo lako mkuu
 
Dr. Mwakyembe tueleze yote ili wananchi tuchukue maamuzi magumu. Ila tunachojua mpaka sasa mafisadi wanahusika.
 
Nimeipitia hiyo habari mwanzo mpaka mwisho mara tatu, sijaona pahala Wizara ya afya ilipomruka Manumba.

Wacheni udaku.

Zomba
soma hapa
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imemruka Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, na
kumtaka aeleze alikoipata taarifa aliyoitoa hivi karibuni kuwa ugonjwa wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, haihusiani na kulishwa sumu
.

soma hapa pia

Alichosema DCI

Akizungumza na waandishi mwishoni wa wiki iliyopita, Manumba alisema, “ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India. Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu."


Waziri amruka Manumba ripoti ugonjwa Mwakyembe Send to a friend
Monday, 20 February 2012 07:08
0digg
dk--mponda.jpg
Dk Hadji Mponda​
ASEMA HAJAONA RIPOTI ALIYOWAPA WAANDISHI, AELEZA RIPOTI YA UGONJWA ANAYO DK MWAKYEMBE MWENYEWE, DK SLAA NAYE ASEMA ,"SINA IMANI NA MANUMBA"
Waandishi Wetu
WINGU zito limetanda kuhusu afya ya Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk Harrison Mwakyembe baada ya Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hadji Mponda, kusema kuwa ripoti ya ugonjwa wa Mwakyembe, anayo mwenyewe na kwamba wizara haina ripoti iliyotolewa na Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai, Robert Manumba, kwa waandishi wa habari.

Lakini wakati Dk Mponda akitoa kauli hiyo, baadhi ya watu wa kada tofauti wakiwamo viongozi wa dini na wasomi, wamekosoa ripoti hiyo ya polisi.

Mmoja wa watu hao, Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Willibrod Slaa alisema,"hata mimi simwamini Manumba."

Malumbano hayo yanakuja wakati Dk Mwakyembe ambaye ni pia ni Mbunge wa Kyela, akitarajiwa nchini jana kwenda India kwa matibabu katika Hospitali ya Apollo.

Mahojiano na Waziri Mponda

Gazeti: Salaam Mheshimiwa waziri. Nimekupigia kutaka ufafanuzi kuhusu ripoti iliyotolewa na DCI Manumba kuhusu ugonjwa wa Dk Mwakyembe. Ninyi wizara mnaitambuaje?

Waziri: Kiutaratibu ripoti ya daktari ni ya mgonjwa. Sisi hatujaandika ripoti, muulizeni DCI Manumba awape ufafanuzi kama kuna kitu mnataka kuuliza zaidi kwa alichokizungumza na ninyi waandishi.

Gazeti: DCI Manumba alitoa taarifa kwa waandishi lakini aki-refer (rejea) ripoti kutoka wizarani (afya), baada ya kuwasiliana nanyi, kwa nini wewe usiizungumzie?

Waziri: Narudia tena, muulizeni yeye DCI au Dk Mwakyembe mwenyewe, wao wanaweza kuwapa ufafanuzi.

Gazeti: Tayari Dk Mwakyembe mwenyewe amekwishatoa tamko kwamba ripoti iliyosomwa na polisi, haina uhusiano na ripoti aliyokuwa nayo yeye kuhusu uchunguzi wa maradhi yake. Je, ripoti hii ya polisi ambayo wamedai wameipata kwenu (wizara) mmeitoa wapi?

Waziri: Ni hivi, baada ya daktari kumchunguza mgonjwa, hutoa ripoti na kumpa mgonjwa. Kwa hiyo, ripoti ya Hospitali ya Apollo anayo Dk Mwakyembe mwenyewe. Tena yeye kaeleza vizuri kabisa kwamba hata uchunguzi bado unaendelea. sasa hapo mnataka niseme nini tena?

Gazeti: Sasa kama ripoti anayo Dk Mwakyembe mwenyewe na tayari amesema ripoti ya polisi waliyosema imetoka kwenu siyo sahihi, je wizara iliwahi kupata ripoti ya Hospitali ya Apollo.

Waziri: Sisi tulichokifanya ni kumpa rufaa Dk Mwakyembe kwenda India. Ripoti hadi sasa anayo mwenyewe ingawa huwa tunapata taarifa baada ya yeye mgonjwa kuzileta kwetu. Hizo ndizo kanuni za taaluma ya udaktari, kwa hiyo ripoti anayo mwenyewe.

Gazeti: Sasa kama ripoti anayo Dk Mwakyembe mwenyewe, hii iliyosomwa na DCI imetoka wapi?

Waziri: Kumbuka DCI ana njia zake nyingi za kupata taarifa. Kwa hiyo ndiyo maana nasisitiza, muulizeni mwenyewe awape ufafanuzi kwa aliyozungumza na waandishi. Sisi wizara mnatuonea tu.

Gazeti: Lakini, hata kama ugonjwa ni siri, huoni mheshimiwa waziri kwamba kuna haja ya kuondoa utata kuhusu suala hili ikizingatiwa kuwa Dk Mwakyembe ni kiongozi anayegusa hisia za watu tofauti?

Waziri: Wanaoweza kuzungumzia maradhi yake, ni familia yake au yeye mwenyewe kwani ndiye mwenye ripoti. Mtafuteni au iulizeni familia yake iwapatie majibu. Lakini wizara haiwezi kufanya hivyo. Narudia tena, kuhusu hilo la DCI muulizeni mwenyewe awape ufafanuzi, mimi sijaona ripoti ya DCI aliyozungumza na waandishi wa habari.

Alichosema DCI

Akizungumza na waandishi mwishoni wa wiki iliyopita, Manumba alisema, “ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India. Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu."

Jana, alipoelezwa kwamba Dk Mwakyembe ameikana ripoti yao, Manumba alisema "sasa suala hilo litashughukiliwa kisheria."

Alisisitiza kuwa suala hilo litashughulikiwa kwa kufuata misingi ya kisheria na kwamba, Jeshi la Polisi haliko tayari kuendeleza malumbano kupitia vyombo vya habari.

"Hatua zaidi zinachukuliwa dhidi ya jambo hilo, kwa sasa litashughukiliwa kwa kufuata misingi ya kisheria kama nilivyokwishaeleza awali,"alisema Manumba.


 
Fool manumba!!!!, a lie never lives to be old, and the best way to escape from a problem is to solve it.
 
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imemruka Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, na kumtaka aeleze alikoipata taarifa aliyoitoa hivi karibuni kuwa ugonjwa wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, haihusiani na kulishwa sumu.

Wizara hiyo imetoa kauli hiyo siku moja baada ya Dk. Mwakyembe kusema kuwa Jeshi la Polisi limetoa taarifa feki kuhusiana na ugonjwa unaomsumbua tangu Oktoba mwaka jana kuwa hautokani na kulishwa sumu.

Dk. Mwakyembe katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi, alieleza kuwa alichokieleza DCI Manumba hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya hospitali inayomtibu ya Apollo nchini India na kuongeza kuwa sumu inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, alisema suala hilo limezungumzwa na Manumba, hivyo ni bora atafutwe na kueleza ametoa wapi taarifa hiyo na kueleza kuwa wizara hiyo kwa sasa haina la kusema.

Mponda alisema wizara kama wizara haihusiki katika suala hilo na kuongeza kuwa si haki kuzungumzia ugonjwa wa mtu hadharani. “Naomba usininukuu vinginevyo hao ndiyo waliosema ni vema mkawafuata na kuwauliza nadhani mtapata majibu sahihi,” alisema Waziri Mponda.

Kwa upande wake, Manumba alisema taarifa aliyoitoa mwishoni mwa wiki kuhusiana na ugonjwa wa Dk. Mwakyembe ameipata kutoka kwa madaktari waliokuwa wakimtibu. Hata hivyo hakueleza madaktari hao ni wa hapa nchini au wa nchini India.

Alisema kwa kuwa Dk. Mwakyembe anatibiwa kwa gharama za serikali, ni lazima madaktari wanaomtibu wafikishe taarifa hizo serikalini.

Aidha alisema huu si wakati wa kubishana kwenye vyombo vya habari, kwa kuwa suala hilo linahusiana na ushahidi zaidi, hivyo ni vema ukasubiriwa wakati utakapofika. “Faili tayari limekwishafunguliwa na limefikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka, hivyo ni bora mkasubiri upelelezi utakapokamilika na haipendezi kuendelea kuliongelea,” alisema Manumba.

Juzi akihojiwa na Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) Taifa kuhusiana na suala hilo, DCI Manumba alisema alichokizungumza kimetokana na madaktari, hivyo kama kuna uongo basi waliosema uongo watakuwa ni hao madaktari.

Akizungumzia suala hilo juzi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Dk. Mwakyembe alisema taarifa halisi ya hospitali ya Apollo inatamka kuwa kuna kitu kwenye uboho (bone marrow) kinachochochea hali aliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaika kukijua, kukidhibiti na kukiondoa.

Alisema kuwa anapata taabu kuamini kama DCI Kanumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yake au walisoma taarifa feki.

Dk. Mwakyembe alikaririwa akisema anachokiona sasa hasa kutokana na kauli hiyo ya jeshi hilo kuanza kuingilia kati na kutoa taarifa kuhusu ugonjwa unaomsumbua wakati bado hajamaliza matibabu ni mpango wa wazi wa mafisadi kuingilia kwenye suala hilo. Ameeleza kukerwa na tamko hilo la polisi hasa katika hali aliyonayo ya ugonjwa na kushangazwa na ufinyu wa uelewa wa jeshi hilo kusisitiza kuwa hajalishwa sumu wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru.

Amesema amelishangaa jeshi hilo kujiingiza kulizungumzia suala ambalo takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati kulichunguza na kulituhumu kwa kulifanyia mzaha jambo hilo kwenye vyombo vya habari. Dk. Mwakyembe alianza kuugua Oktoba mwaka jana na baadaye kupelekwa nchini India na kulazwa kwa matibabu kwa takriban miezi miwili. Alirejea nchini Desemba 11 mwaka jana.

Ugonjwa wake umekuwa ukihusishwa na kulishwa sumu na mara kadhaa Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amenukuliwa akisema ugonjwa huo umetokana na kulishwa sumu na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi lina ushahidi.


CHANZO: Tanzania Daima

mimi c pilice,wala mpelelezi lakini kwa upeo wangu mdogo huyu kanumba oooh manumba ni kilaza haswa.ametoa statment kuwa mwakyembe hakulishwa sumu,means upelelezi umeshaisha na ametoa conclusion,sasa anaposema upelezi unaendelea na jalada limeshafunguliwa,ni upelelezi gani tena huo? Mbona kauli zake zinapishana?
 
zomba
usipo elewa na hapo juu basi tena,shule za kata zipo kwa ajili yako,kusoma uzeeni si kosa waweza rudi tena kupata elimu ya ngumbalo
 
Zomba
soma hapa
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imemruka Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, na
kumtaka aeleze alikoipata taarifa aliyoitoa hivi karibuni kuwa ugonjwa wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, haihusiani na kulishwa sumu
.

soma hapa pia

Alichosema DCI

Akizungumza na waandishi mwishoni wa wiki iliyopita, Manumba alisema, “ukweli kuhusu kauli hiyo inayodai kuwekewa sumu, tumeupata baada ya kuwasiliana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, ambayo nayo imewasiliana na hospitali aliyokuwa amelazwa Dk Mwakyembe nchini India. Taarifa zinaonyesha kuwa hakuna sumu."





Usiwe mvivu wa kusoma, hayo ni maneno ya kanjanja aliyeandika, ni wapi anapo quote waziri au msemaji wa wizara. Upo hapo ulipo?
 
Nchi hii imefikia mahala ambapo Mwl. Nyerere alishapatabiri, sasa ndo yametimia. Mwalimu alisema, pasipo viongozi wenye NIDHAMU na UWAJIBIKAJI Taifa litateketea. Sasa ndo tumefikishana hapa. Adui zetu wakati ule wa Mwalimu walikuwa UJINGA, MARADHI na UMASKINI lakini leo hao si maadui wakubwa tena kwani walau watu wana uelewa wa kutosha kujilinda, sasa maadui zetu wakubwa ni WENYE MAMLAKA.

Kweli Yametimia ila TUTASHINDAAAAAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom