Wizara ya Afya yamruka Manumba, wahoji alikoipata ripoti ya Mwakyembe!

WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imemruka Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, na kumtaka aeleze alikoipata taarifa aliyoitoa hivi karibuni kuwa ugonjwa wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, haihusiani na kulishwa sumu.

Wizara hiyo imetoa kauli hiyo siku moja baada ya Dk. Mwakyembe kusema kuwa Jeshi la Polisi limetoa taarifa feki kuhusiana na ugonjwa unaomsumbua tangu Oktoba mwaka jana kuwa hautokani na kulishwa sumu.

Dk. Mwakyembe katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi, alieleza kuwa alichokieleza DCI Manumba hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya hospitali inayomtibu ya Apollo nchini India na kuongeza kuwa sumu inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, alisema suala hilo limezungumzwa na Manumba, hivyo ni bora atafutwe na kueleza ametoa wapi taarifa hiyo na kueleza kuwa wizara hiyo kwa sasa haina la kusema.

Mponda alisema wizara kama wizara haihusiki katika suala hilo na kuongeza kuwa si haki kuzungumzia ugonjwa wa mtu hadharani. “Naomba usininukuu vinginevyo hao ndiyo waliosema ni vema mkawafuata na kuwauliza nadhani mtapata majibu sahihi,” alisema Waziri Mponda.

Kwa upande wake, Manumba alisema taarifa aliyoitoa mwishoni mwa wiki kuhusiana na ugonjwa wa Dk. Mwakyembe ameipata kutoka kwa madaktari waliokuwa wakimtibu. Hata hivyo hakueleza madaktari hao ni wa hapa nchini au wa nchini India.

Alisema kwa kuwa Dk. Mwakyembe anatibiwa kwa gharama za serikali, ni lazima madaktari wanaomtibu wafikishe taarifa hizo serikalini.

Aidha alisema huu si wakati wa kubishana kwenye vyombo vya habari, kwa kuwa suala hilo linahusiana na ushahidi zaidi, hivyo ni vema ukasubiriwa wakati utakapofika. “Faili tayari limekwishafunguliwa na limefikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka, hivyo ni bora mkasubiri upelelezi utakapokamilika na haipendezi kuendelea kuliongelea,” alisema Manumba.

Juzi akihojiwa na Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) Taifa kuhusiana na suala hilo, DCI Manumba alisema alichokizungumza kimetokana na madaktari, hivyo kama kuna uongo basi waliosema uongo watakuwa ni hao madaktari.

Akizungumzia suala hilo juzi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Dk. Mwakyembe alisema taarifa halisi ya hospitali ya Apollo inatamka kuwa kuna kitu kwenye uboho (bone marrow) kinachochochea hali aliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaika kukijua, kukidhibiti na kukiondoa.

Alisema kuwa anapata taabu kuamini kama DCI Kanumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yake au walisoma taarifa feki.

Dk. Mwakyembe alikaririwa akisema anachokiona sasa hasa kutokana na kauli hiyo ya jeshi hilo kuanza kuingilia kati na kutoa taarifa kuhusu ugonjwa unaomsumbua wakati bado hajamaliza matibabu ni mpango wa wazi wa mafisadi kuingilia kwenye suala hilo. Ameeleza kukerwa na tamko hilo la polisi hasa katika hali aliyonayo ya ugonjwa na kushangazwa na ufinyu wa uelewa wa jeshi hilo kusisitiza kuwa hajalishwa sumu wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru.

Amesema amelishangaa jeshi hilo kujiingiza kulizungumzia suala ambalo takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati kulichunguza na kulituhumu kwa kulifanyia mzaha jambo hilo kwenye vyombo vya habari. Dk. Mwakyembe alianza kuugua Oktoba mwaka jana na baadaye kupelekwa nchini India na kulazwa kwa matibabu kwa takriban miezi miwili. Alirejea nchini Desemba 11 mwaka jana.

Ugonjwa wake umekuwa ukihusishwa na kulishwa sumu na mara kadhaa Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amenukuliwa akisema ugonjwa huo umetokana na kulishwa sumu na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi lina ushahidi.

CHANZO: Tanzania Daima
Hii hali ni kushangaza kweli DCI Manumba ambaye anamjua Mheshimiwa Mwakwembe tena si kijujuu tuu bila hata aibu anatoa taarifa kwenye vyombo vya habari bila hata ya kwenda kumjulia hali apate taarifa halisi????? Maanake kama wangeonana Mheshimiwa ambaye ni waziri na mbunge wa Kyela asingeongea maneno ya kumdiscredity na waandishi wa habari baadae waziri aje kukanusha!!!! Hivi nchi yetu inakwenda wapi ina maana hata ubinadamu umekwisha shauri ya ufisadi, au tusemeje????

Ingawa sijawahi kumwamini Waziri wa Afya kutokana na "kutojua kitu Wizarani kwake", kwa hili napata hisia kwamba atatokea mtu asiye makini na kuanika mawasiliano (si ripoti ya ugonjwa) yaliyofanyika kati ya Jeshi la Polisi na Wizara kuhusu suala hilo na matokeo ya mawasiliano hayo. Asipojiuzulu mtu safari hii watakuwa "wamerithi uongozi."
Kombo mimi nafuatilia sana postings zako. Hakika wewe ni muongo, kigeugeu sana
 
Lakini kwa nini uyo manumba atoe riport wakati mwakyembe mwenyewe yupo, tunakusubili jembe letu uje useme ukweli wa mambo, wasitake viherehere ulikuficha ukweli!!!
 
ndo kwanza movie imeanza ... watu wanakurupuka lakini wacha tuzidi kusubiri
 
Mnashangaa nini? mshasahau ndo style nya serikali ya jk-ccm viongozi wenye dhamana kurukana/kila mmoja kutoa tamko lake?
 
DCI aeleze vizuri alikoipata hiyo taarifa na apeleke ujinga wake kwa waliomtuma kusoma vitu vya kijinga kijinga. Na akome kutuambia eti swala liko kwenye upelelezi wakati mpaka hivi nnavyoandika hakuna cha upelelezi wala uchunguzi, na wapeleleze nini wakati ushahidi hawajapelelewa... Jitu zima na familia kazi kudanganya lol! Aibu...
 
Yaani hii 'mijamaa' (JK na kundi lake) mpaka naionea huruma! Wanatia aibu kwa kweli...sio Rais, sio WM, sio Spika...na sasa hata DCI kumbe hamna kitu. Juzi tu hapa tulikuwa tunamshangaa AG anavyotia aibu bungeni...leo DCI naye huyo anajifunua! Tumsubiri IGP nae afunue mdomo wake.
 
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imemruka Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, na kumtaka aeleze alikoipata taarifa aliyoitoa hivi karibuni kuwa ugonjwa wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, haihusiani na kulishwa sumu.

Wizara hiyo imetoa kauli hiyo siku moja baada ya Dk. Mwakyembe kusema kuwa Jeshi la Polisi limetoa taarifa feki kuhusiana na ugonjwa unaomsumbua tangu Oktoba mwaka jana kuwa hautokani na kulishwa sumu.

Dk. Mwakyembe katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi, alieleza kuwa alichokieleza DCI Manumba hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya hospitali inayomtibu ya Apollo nchini India na kuongeza kuwa sumu inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, alisema suala hilo limezungumzwa na Manumba, hivyo ni bora atafutwe na kueleza ametoa wapi taarifa hiyo na kueleza kuwa wizara hiyo kwa sasa haina la kusema.

Mponda alisema wizara kama wizara haihusiki katika suala hilo na kuongeza kuwa si haki kuzungumzia ugonjwa wa mtu hadharani. “Naomba usininukuu vinginevyo hao ndiyo waliosema ni vema mkawafuata na kuwauliza nadhani mtapata majibu sahihi,” alisema Waziri Mponda.

Kwa upande wake, Manumba alisema taarifa aliyoitoa mwishoni mwa wiki kuhusiana na ugonjwa wa Dk. Mwakyembe ameipata kutoka kwa madaktari waliokuwa wakimtibu. Hata hivyo hakueleza madaktari hao ni wa hapa nchini au wa nchini India.

Alisema kwa kuwa Dk. Mwakyembe anatibiwa kwa gharama za serikali, ni lazima madaktari wanaomtibu wafikishe taarifa hizo serikalini.

Aidha alisema huu si wakati wa kubishana kwenye vyombo vya habari, kwa kuwa suala hilo linahusiana na ushahidi zaidi, hivyo ni vema ukasubiriwa wakati utakapofika. “Faili tayari limekwishafunguliwa na limefikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka, hivyo ni bora mkasubiri upelelezi utakapokamilika na haipendezi kuendelea kuliongelea,” alisema Manumba.

Juzi akihojiwa na Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) Taifa kuhusiana na suala hilo, DCI Manumba alisema alichokizungumza kimetokana na madaktari, hivyo kama kuna uongo basi waliosema uongo watakuwa ni hao madaktari.

Akizungumzia suala hilo juzi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Dk. Mwakyembe alisema taarifa halisi ya hospitali ya Apollo inatamka kuwa kuna kitu kwenye uboho (bone marrow) kinachochochea hali aliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaika kukijua, kukidhibiti na kukiondoa.

Alisema kuwa anapata taabu kuamini kama DCI Kanumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yake au walisoma taarifa feki.

Dk. Mwakyembe alikaririwa akisema anachokiona sasa hasa kutokana na kauli hiyo ya jeshi hilo kuanza kuingilia kati na kutoa taarifa kuhusu ugonjwa unaomsumbua wakati bado hajamaliza matibabu ni mpango wa wazi wa mafisadi kuingilia kwenye suala hilo. Ameeleza kukerwa na tamko hilo la polisi hasa katika hali aliyonayo ya ugonjwa na kushangazwa na ufinyu wa uelewa wa jeshi hilo kusisitiza kuwa hajalishwa sumu wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru.

Amesema amelishangaa jeshi hilo kujiingiza kulizungumzia suala ambalo takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati kulichunguza na kulituhumu kwa kulifanyia mzaha jambo hilo kwenye vyombo vya habari. Dk. Mwakyembe alianza kuugua Oktoba mwaka jana na baadaye kupelekwa nchini India na kulazwa kwa matibabu kwa takriban miezi miwili. Alirejea nchini Desemba 11 mwaka jana.

Ugonjwa wake umekuwa ukihusishwa na kulishwa sumu na mara kadhaa Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amenukuliwa akisema ugonjwa huo umetokana na kulishwa sumu na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi lina ushahidi.

CHANZO: Tanzania Daima
Hivi ni kwa nini DCI Manumba akurupuke kutoa taarifa feki kama hii bila kuhakikisha wakati si kazi yake???? Nadhani taarifa ya ugonjwa tena wa waziri ingelitolewa na wizara ya afya inayoshughulikia matibabu yake India!!!!Toka lini DCI Manumba akawa dakitari??????Lazima tutakuwa na shaka kuwa huo msukumo wa kukimbilia kutoa taarifa ya ugonjwa wa Mheshimiwa waziri una maana gani????????

Hata hivyo polisi huajiriwa kwa viwango gani vya ufaulu? Kimsingi ukiwa na division four ya point 28 unaruhusiwa kuingia jeshi la polisi. Kusema kweli, division four 28 ni hakuna kitu kabisa. Huyu ndiye anayechunguza nini kimempata Mwakyembe kwangu ipo wazi kabisa, mtu wa namna hii hawezi kuchunguza chochote. Sana sana atafanya kazi kwa mazoea tu. Polisi yetu haina watu wenye weledi, yaani IQ ni ndogo sana. Hii inaathiri sana kazi na tafiti wanazofanya. Mara nyingi taarifa zao siziamini na kiujumla siwaamini.
Tunaongea kuhusu matamko wanayotoa na taarifa zao, lakini kimsingi tunapaswa kujua historia zao na ni kwa namna gani wamefika hapo walipo. Polisi ni kimbilio la wakosefu, yaani baada ya mtu kukosa kwenda form five au chuo ndiyo anakwenda polisi. Ipo wazi tunakundi la division four 28 wengi sana. Hawa hawawezi kutufanyia kazi zenye ubora. Kwa hiyo tunapaswa kufumua mpango mzima wa namna ya kujiunga na polisi na hasa inapofika kwenye vetengo nyeti hunahitaji, Christmas tree.
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Safari yetu bado ndefu na hatujui tutafika lini. Tumuombee uponyaji wa haraka ndugu yetu Dr. Mwakyembe
 
Yaani hii 'mijamaa' (JK na kundi lake) mpaka naionea huruma! Wanatia aibu kwa kweli...sio Rais, sio WM, sio Spika...na sasa hata DCI kumbe hamna kitu. Juzi tu hapa tulikuwa tunamshangaa AG anavyotia aibu bungeni...leo DCI naye huyo anajifunua! Tumsubiri IGP nae afunue mdomo wake.
Nooo IGP namuheshimu nadhani ana busara kidogo na hakurupuki,at least nina imani naye!!!!!!

  • Thanks
Reactions: SMU
Kichwa cha habari na habari yenyewe ni vitu viwili tofauti. Hili gazeti limekuwa la udaku.

Maneno ya Waziri ni haya hapa: "Naomba usininukuu vinginevyo hao ndiyo waliosema ni vema mkawafuata na kuwauliza nadhani mtapata majibu sahihi,"

Sasa hapo na kichwa cha habari ni mbingu na ardhi.
 
kuna thread hapa iliandikwa,mtoto wa kigogo kanunua faili,so inawezekana Manumba kapewa second Version.Patamu hapo
Yawezekana ni kweli lile faili la kununua toka wizarani na kuna mtu alisema riport ya Mwakyembe inatafutwa kwa udi na uvumba!!! Vijana baada ya kuona mshiko unamtafuta mtu na wao wanapiga miayo wakamkabidhi kitu mtu anataka, wenyewe hao Kempisk!!!! Sasa DCI Manumba ni kafara wa kutoa ripoti feki!!!!

Manumba is just puppet!..... BLOOD STATE. utawala huu wa kikatili na wamauaji ya kupanga utapita, he will kill our body but not our soul, why he killing bright christian only?
 
SCREW 'EM! Serikali moja, chama kimoja, utawala mmoja lakini wanafanya kazi utadhani nchi ya wagagagigikoko na wale wa mgonenagonago!

Rais hajui anachosema Wazrii Mkuu, Waziri Mkuu hajui anachosema Rais, Spika hajui Rais alisema nini, Waziri hajui Waziri mwenzie amesema nini! Sijui wakiingiaga kwenye hivyo vikao vyao wanafanyaje kwa kweli!

Kuna mwaka hawa wakuu wa vitengo walipelekwa na JK semina kuhusu maswala ya 'mawasiliano' nadhani ndo matunda yake haya.
 
WIZARA ya Afya na Ustawi wa Jamii, imemruka Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba, na kumtaka aeleze alikoipata taarifa aliyoitoa hivi karibuni kuwa ugonjwa wa Naibu Waziri wa Ujenzi, Dk. Harrison Mwakyembe, haihusiani na kulishwa sumu.

Wizara hiyo imetoa kauli hiyo siku moja baada ya Dk. Mwakyembe kusema kuwa Jeshi la Polisi limetoa taarifa feki kuhusiana na ugonjwa unaomsumbua tangu Oktoba mwaka jana kuwa hautokani na kulishwa sumu.

Dk. Mwakyembe katika taarifa yake kwa vyombo vya habari juzi, alieleza kuwa alichokieleza DCI Manumba hakifanani kabisa na picha iliyo kwenye taarifa halisi ya hospitali inayomtibu ya Apollo nchini India na kuongeza kuwa sumu inaweza kudhuru hata kwa kugusishwa.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Haji Mponda, alisema suala hilo limezungumzwa na Manumba, hivyo ni bora atafutwe na kueleza ametoa wapi taarifa hiyo na kueleza kuwa wizara hiyo kwa sasa haina la kusema.

Mponda alisema wizara kama wizara haihusiki katika suala hilo na kuongeza kuwa si haki kuzungumzia ugonjwa wa mtu hadharani. "Naomba usininukuu vinginevyo hao ndiyo waliosema ni vema mkawafuata na kuwauliza nadhani mtapata majibu sahihi," alisema Waziri Mponda.

Kwa upande wake, Manumba alisema taarifa aliyoitoa mwishoni mwa wiki kuhusiana na ugonjwa wa Dk. Mwakyembe ameipata kutoka kwa madaktari waliokuwa wakimtibu. Hata hivyo hakueleza madaktari hao ni wa hapa nchini au wa nchini India.

Alisema kwa kuwa Dk. Mwakyembe anatibiwa kwa gharama za serikali, ni lazima madaktari wanaomtibu wafikishe taarifa hizo serikalini.

Aidha alisema huu si wakati wa kubishana kwenye vyombo vya habari, kwa kuwa suala hilo linahusiana na ushahidi zaidi, hivyo ni vema ukasubiriwa wakati utakapofika. "Faili tayari limekwishafunguliwa na limefikishwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka, hivyo ni bora mkasubiri upelelezi utakapokamilika na haipendezi kuendelea kuliongelea," alisema Manumba.

Juzi akihojiwa na Shirika la Utangazaji Nchini (TBC) Taifa kuhusiana na suala hilo, DCI Manumba alisema alichokizungumza kimetokana na madaktari, hivyo kama kuna uongo basi waliosema uongo watakuwa ni hao madaktari.

Akizungumzia suala hilo juzi katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, Dk. Mwakyembe alisema taarifa halisi ya hospitali ya Apollo inatamka kuwa kuna kitu kwenye uboho (bone marrow) kinachochochea hali aliyonayo, kitu ambacho mabingwa wanahangaika kukijua, kukidhibiti na kukiondoa.

Alisema kuwa anapata taabu kuamini kama DCI Kanumba na wenzake waliisoma taarifa halisi ya matibabu yake au walisoma taarifa feki.

Dk. Mwakyembe alikaririwa akisema anachokiona sasa hasa kutokana na kauli hiyo ya jeshi hilo kuanza kuingilia kati na kutoa taarifa kuhusu ugonjwa unaomsumbua wakati bado hajamaliza matibabu ni mpango wa wazi wa mafisadi kuingilia kwenye suala hilo. Ameeleza kukerwa na tamko hilo la polisi hasa katika hali aliyonayo ya ugonjwa na kushangazwa na ufinyu wa uelewa wa jeshi hilo kusisitiza kuwa hajalishwa sumu wakati sumu si lazima unyweshwe ili ikudhuru.

Amesema amelishangaa jeshi hilo kujiingiza kulizungumzia suala ambalo takriban mwaka mzima halijawahi kuwa na dhamira ya dhati kulichunguza na kulituhumu kwa kulifanyia mzaha jambo hilo kwenye vyombo vya habari. Dk. Mwakyembe alianza kuugua Oktoba mwaka jana na baadaye kupelekwa nchini India na kulazwa kwa matibabu kwa takriban miezi miwili. Alirejea nchini Desemba 11 mwaka jana.

Ugonjwa wake umekuwa ukihusishwa na kulishwa sumu na mara kadhaa Waziri wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amenukuliwa akisema ugonjwa huo umetokana na kulishwa sumu na kusisitiza kuwa Jeshi la Polisi lina ushahidi.

CHANZO: Tanzania Daima

Nchi imefurugika!
 
kuna thread hapa iliandikwa,mtoto wa kigogo kanunua faili,so inawezekana Manumba kapewa second Version.Patamu hapo

.....Sure Mkuu, nami niliwaza hivyo kuwa baada ya mtoto huyo wa kigogo kuhitaji hiyo ripoti ya ugonjwa, wajanja wa wizara ya afya wakafyatua ripoti feki wakakamata mshiko wao. Na kwa vile kulikuwa na lengo la kuichapisha ripoti hiyo magazetini-hususani gazeti la Mtanzania (kama ilivyodai Thread hiyo) na wao Mtanzania kuhofia masuala ya kisheria na kimaadili juu ya kuichapisha, huenda plan B ikawa ni kuwapatia Polisi ili waitoe kama matokeo ya uchunguzi! Na kwa vile polisi wetu ni polisi jina, pasipo hata kuingia deep juu ya reliability ya taarifa hiyo (bila kuchanganya na zao), wakajiona tayari wamesha-win, wakakurupa (kama alivyosema Mwakyembe) kuhitimisha kuwa HAKUNA SUMU!
Na bado, lazima ataibuka Mkubwa mwingine kuongezea utata juu ya hili.
 
Back
Top Bottom