Wito: Gomeni kwenda kuangalia mechi ya Brazil na Taifa Stars!

Hili la Brazil kuja limekamilika. Limeisha. Tuangalie tu jinsi ya kuyazuia matumizi kama haya kwa visingizio vya kukuza utalii. Angalau BUNGE letu liwe linaulizwa. Natumaini pia kikao kijacho cha bajeti wabunge wetu watahoji hili. Serikali/TFF wataulizwa mapesa haya ya kuwaleta Brazil yametoka wapi, yametumikaje, yamerudi kiasi gani, tumenufaika vipi kama TAIFA.

Yogi Berra anakwambia "It ain't over 'til it's over"

Kutumia mfano wa mpira, kabla kipyenga cha mwisho hakijapulizwa mpira haujaisha.
 
wacha nionekane chizi sitii mguu uwanjani hata kidogo sidhani kama nitaweza kutuliza hisia za moyo wangu. Kuna agent ambaye angewalete brazili hao hao na fee yake ilikuwa ni $ 600,000 wakampa huyo wa $1.8. Hiyo budget ilitengwa kwa timu tatu wenyewe wameitumia kwa timu moja tu!

Hata kama wangeitumia vizuri hili wazo mimi siliafiki kabisa. hela za walipa kodi ni takatifu!

Naona sasa muda wa kuchukua action ni huu, hatuwezi tukawa tunatembeza bakuli huku tukifuja na kutapanya mali zetu. Tafadhali Mwandikie Andrew Mitchell, mbunge wa Sutton Coldfield na ni Secretary of State wa DFID ambaye muda si mrefu atakuwa na kazi ya kuapprove mamilion ya msaada kwa Tanzania ambayo yatakwenda kutumiwa kwenye upuuzi kama huu.

andrewmitchellmp@parliament.uk

Tafadhali unachotuma tushee hapa ili tusirudie rudie kitu kimoja

TIME FOR ACTION!
 
Hivi TFF walipokuwa wanaweka viingilio walikuwa na mawazo gani? Nchi ya Zimbabwe ambayo kiuchumi iko hoi bin taabani kuliko yetu kiingilio kikubwa ni $60 na cha chini $10 ambapo wao wamekuwa wa wazi kwa kusema sehemu fulani ya gharama itabebwa na serekali. Sasa huku kwetu ambako gharama zote ni za serikali kwa nini watukamue? Maana hizo billion 7 zilizotengwa hii ndio mara ya kwanza kutumika na wala hazitaisha au ndio ufisadi mwingine?
 
naomba niwe tofauti hapa. demokrasia inaniruhusu. tumeambiwa kwamba mechi hiyo itaonyeshwa live na kushuhudiwa na zaidi ya nchi 160!, zikiwamo za Ulaya na Amerika, jamani huo si ndio utalii wenyewe kwamba Tz itajulikana kupitia mechi hio na watalii watakuja kuangalia kuna nini Tanzania mpaka mabingwa mara 5 wa world cup waje.
 
Wakuu

Nimepata ujumbe toka TFF kuwa nawapotosha watanzania na sina nia njema na Taifa langu.

Nomba kuwaambia kabisa toka kwenye moyo wangu mkunjufu

1.MMesema serikali haijatoa Pesa,ila imewaguarantee nyie kupata Mkopo kwa ajili ya kuwaleta Brazil.Uzugaji,Naomba kuwaambia Serikali imetumia sheria gani kuwadhamini nyie ndani ya muda mfupi wakati imeshindwa kudhamini kampuni kama TTCL ambazo zimekuwa zikiomba udhamini kwa muda mrefu

2.Hoja ya kuwa kiasi kingine cha pesa kitatolewa na wadhamini waliojitokeza,Mbona hamuweki wazi ni wadhamini gani wametoa pesa na ni kiasi gani ambacho kimeshakusanywa mpaka sasa.

3.Ningependa kupata mchanganuo wa mapato yote ya mechi itakayokuja na ni kiasi gani serikali imewekeza hapo

4.Hivi ni kwanini serikali haitaki kuwa wazi kwa mambo kama haya?Waziri asimame na aseme wamewapa shilling kadhaa (several billions) toka kwenye mfuko flani..

Mwisho kabisa,Mzee Mwanakijiji mwishoni mwa mwaka 2008 aliwasihi muache kutuzuga,tumechoka kuzugika.

Who signed the deal?nani alikuwa anawaunganisha hawa TFF...

TFF pengine wanatarajia kupata fedha yote kutoka kwenye gate collections na sponsourship deals ila hawana uhakika na si wafanyabiashara. Pengine hili ndo linalosumbua. TFF wangepata advice ya business people utakuta hata hizi politics za kuwa pesa ya walipa kodi inaliwa zisingekuwepo. Kutokana na kukosekana kwa hiyo advice ndo maana baadhi ya watu wanapata bullets za kuwa attack. Hii purely ingeendeshwa kibiashara, hata kama serikali ingetoa udhamini, isingekuwa na problem na niendelee kusema si problem kabisa.

Kwa sababu commercially hii pesa inaweza ikapatikana through udhamini na gate collections pale uwanja wa Taifa. Kwa hiyo TFF walihitaji kuwa na business model inayoonesha kuwa watatumia kiasi kadhaa, watapata revenues kiasi kadhaa; Na biashara inalipa. TFF hawaendeshwi na fedha ya walipa kodi. TFF ni independent organization. Serikali ingedhamini kupitia Tanzania Tourist Board, kama ambavyo advertizers wengine wangedhamini. Halafu weka na viingilio vya mlangoni pamoja na TV rights (itakuwa broadcast Duniani kote) sioni tatizo hapa.

Tatizo tunafikiria negatively kila wakati kuwa hatuwezi na ni maskini. This is downright absurd and I don't buy it!! Go TFF, Go!!
 
David Mwakalebela alikuwa beki mbili wa wanatupwisa PAMBA FC ya Mwanza baadaye alihamia Yanga FC aliichezea Taifa stars kwa muda mrefu. Nakumbuka mechi moja uwanja wa taifa aliteswa sana na Lunyamila kipindi hicho akiwa bado RTC Shinyanga!!!!!!!

Nsajigwa na Haroub Canavarro msiwaumize wa Brazil maana nyie mtachezea sifa badala ya viwango!

Umenikumbusha ile mechi ya Ivory Coast - Kuna kijana mmoja anaitwa Abdlahim (kitu kama hicho), alichezea sifa mpaka anatoka uwanjani anasema "hawa ni kama sisi tu ... hawana lolote" ... Alianzisha tafrani fulani na Dindane!

Nikirudi kwenye mada: Binafsi nagoma! Huwezi kuchukua MSIMBAZI TATU zangu hivi hivi Jumatatu Jioni - Haiwezekani! Afadhali nichukue 5,000 nipitie Standard - Ubungo nipate tatu za baridi halafu niwahi foleni ya Kimara
 
TFF pengine wanatarajia kupata fedha yote kutoka kwenye gate collections na sponsourship deals ila hawana uhakika na si wafanyabiashara. Pengine hili ndo linalosumbua. TFF wangepata advice ya business people utakuta hata hizi politics za kuwa pesa ya walipa kodi inaliwa zisingekuwepo. Kutokana na kukosekana kwa hiyo advice ndo maana baadhi ya watu wanapata bullets za kuwa attack. Hii purely ingeendeshwa kibiashara, hata kama serikali ingetoa udhamini, isingekuwa na problem na niendelee kusema si problem kabisa.

KipimaPembe,

Mbona unaongelea mambo ya kusadikika? Uwezi kufanya "mradi" kama huu kwa kufanya "projections" za "gate collections". Ki-mantiki ni kwamba TFF wana pesa tayari mkononi ndio maana wameweka viingilio vya ajabu ajabu (30K - 200K)! ili kujaribu kutuonyesha kwamba "pesa ilirudi" na hii mechi ya "mazoezi ya Brazil" was worthy it - Ni wizi mtupu unaendelea hapo - trust me

Kwa sababu commercially hii pesa inaweza ikapatikana through udhamini na gate collections pale uwanja wa Taifa. Kwa hiyo TFF walihitaji kuwa na business model inayoonesha kuwa watatumia kiasi kadhaa, watapata revenues kiasi kadhaa; Na biashara inalipa.

Isipopatikana TFF through sponsorships deals (kama zipo) na gate collections ni nini hasa tutegeme? Serikali ita-write-off hiyo pesa na ku-declare TFF kama bad-debtors? au? Hii mechi tumeifahamu via media hata wiki mbili hazijapita, kwa nini imekuwa "fast-tracked"?

Acheni hizo bwana! TUMECHOKA na FISHY BUSINESS/DEALINGS - VERY TIRED INDEED
 
T
Tatizo tunafikiria negatively kila wakati kuwa hatuwezi na ni maskini.

This is downright absurd and I don't buy it!! Go TFF, Go!!
mkuu

tumefikia hapa?umeamua kujitusi kabisa?Ndiyo watanzani ni masikini ila umechangiwa na viongozi walion masikini wa mawazo endelevu .

Mungu anajua mwisho wake,umasikini wa watanzania si wa milele .

Screw KM!kama unaona tupo negative basi tueleze unachokijua.

Let me ask you one question.Kulikuwa na haja ya Kuwaleta Brazil kipindi hiki?

Eti Brazil wanakuja kuwafariji masikini?does it make sense siyo?inaonekana unajua sana nini kinachoondelea na unakereka sisi kuwagomea hao TFF..

Nyani Ngabu has this to say

As a principled man I would not under any circumstance support this stupidity and I never break my principles no matter what. It is wrong for the govt. to cough up that kinda money for a one day event that has no real benefits whatsoever while there are real and legit problems where that kind of money could be earmarked and it is equally wrong for any sensible person to support it, whether directly or indirectly.

If you are a sensible, upstanding citizen and know that what the govt. is about to do or has done is wrong, then you ought to be outraged by this. I will not spend my hard earned money to go and watch that match. By going to see it shows to me that you are not outraged and you support them (the govt.) fully. You are enabling them in misusing our meager resources.

So Kiranga, as the Q-Dwag told you yesterday, most of these folks here don't understand where you are coming from. You obviously think on different wavelengths.

It is not complicated logarithm. It's as simple as ABC. You are just as wrong when you support someone or something that is wrong.

And we sit here and wonder how come we are poor? How come we don't develop? How come our hospitals are overcrowded? Why our school kids sit and "learn" under baobab trees? FMES said it best: our leaders are a reflection of ourselves - the people.
 
Wakuu

Nimepata ujumbe toka TFF kuwa nawapotosha watanzania na sina nia njema na Taifa langu.

Nomba kuwaambia kabisa toka kwenye moyo wangu mkunjufu

1.MMesema serikali haijatoa Pesa,ila imewaguarantee nyie kupata Mkopo kwa ajili ya kuwaleta Brazil.Uzugaji,Naomba kuwaambia Serikali imetumia sheria gani kuwadhamini nyie ndani ya muda mfupi wakati imeshindwa kudhamini kampuni kama TTCL ambazo zimekuwa zikiomba udhamini kwa muda mrefu

2.Hoja ya kuwa kiasi kingine cha pesa kitatolewa na wadhamini waliojitokeza,Mbona hamuweki wazi ni wadhamini gani wametoa pesa na ni kiasi gani ambacho kimeshakusanywa mpaka sasa.

3.Ningependa kupata mchanganuo wa mapato yote ya mechi itakayokuja na ni kiasi gani serikali imewekeza hapo

4.Hivi ni kwanini serikali haitaki kuwa wazi kwa mambo kama haya?Waziri asimame na aseme wamewapa shilling kadhaa (several billions) toka kwenye mfuko flani..

Mwisho kabisa,Mzee Mwanakijiji mwishoni mwa mwaka 2008 aliwasihi muache kutuzuga,tumechoka kuzugika.

Who signed the deal?nani alikuwa anawaunganisha hawa TFF...

naomba uwaongezee TFF swali:
katika nchi 160 ambazo mechi hii itaonyeshwa ''LIVE'' wameingiza kiasi gani kwa kuuza TV RIGHTS??
 
Mazee unaweza kutoa breakdown ya mahesabu yako? Tutarudishaje hizi gharama?

Unataka kutuambia Brazil itatumia $ 6m kwa siku chache itakayokaa hapo bongo?

Is this the best use of this money in therms of ads? Unajua ukitaka kuchukua prime time ads za CNN zinazowafikia Wamarekani nchi nzima ni kiasi gani kwa 30 seconds? na kwa kutumia hela hizi ungeweza kupata ads hizi ngapi? Prime time, nationwide, kwa watalii haswa si watazamaji mpira tu? Unajua kitu kinaitwa "Return on Investment" ? Unajua ad spanning? Unajua kitu kinaitwa target market ?

Siyo tunakuja kuimbishana ngonjera za "follow the leader" tu hapa, mradi wakubwa wamesema tuwa support tu.

Haya ni matumizi mabaya ya pesa za umma na ni lazima tuseme.

Zaidi ya yote hayo, unataka kutangaza utalii kwa mamilioni ya dola wakati hata infrastructure za ku support utalii huo huna.

I concur! Kama hoja ni kukuza utalii, they could have achieved a big bang for our bucks by training tour guides rather than investing in a day event [siamini kwamba kuna watu wa kutosha "in our target market" watakaoitazama hii mechi. Who are we in the world of soccer anyway?]. Ma-tour guide wanatuangusha mno. Mimi ukuniuliza nitaje jambo moja ambalo ni muhimu katika kukuza utalii nchini Tanzania, jibu langu ni kuhakikisha tour guides wote wamepata mafunzo stahili na wamesajiliwa. Pia wanahakikiwa kila mwaka. Pamoja na mambo mengine, sababu kubwa ya Kenya or SA "kufanya vizuri" katika biashara ya utalii ni kuwa wana waongoza watalii wazuri wanaoweza kumfanya mgeni kuapa kurudi tena na tena na tena.
 
Brazil wanakuja kuwafariji watanzania kwa machungu gani?

Labda ya kudanganywa kuwa kilimo kwanza nasi tukakubali.
Ndiyo ikawa ni sababu hata Manji kuwalipia kiingilio wanachama wa Yanga. Japo haingii akili kwa mapenzi gani aliyonayo kwa watanzania hata kuwagharamia. Bure ghali...tutaona mwisho gharama watakayo endelea kuilipa kwa kulipiwa siku hiyo na ufadhili wanaoupata siku zote.
 
CCM wanatafuta hela za uchaguzi kinguvu, we huoni hata hela zenyewe zinasemwa kwa wingu la utata.

Wasitake kutufanya watu wajinga.

Kwanza hizi extravagances za kimichezo huwa hazirudishi hela, katika recent history ya Olympics Olympic pekee iliyorudisha hela ni ya Barcelona, nyingine zote zimeflop, kina NN wanalipa kodi mpaka leo kusupport Olympic ya miaka kibao iliyopita.

Hata hao wa South wanafanya kwa sababu ya pride kujionyesha tu, lakini hawatarudisha gharama.

JK anakausha hazina.
 
Jamani hebu tuwe serious kidogo kwani kuna watu humu ndani .. yaani nigekuwa karibu nao ningetembeza bakora ili iwaamshe. Wanaotetea huu ujinga naomba niwaulize maswali mawili matatu.

  • Hii mechi itaweza kuitangaza Tanzania kuliko hifadhi ya wanyama Serengeti ambayo ni ndoto ya watalii na inayojulikana dunia nzima ikiwa haina mfano popote pale.
  • Hii mechi itaweza kuitangaza Tanzania kuliko Mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio cha watalii dunia nzima na huwapa majivuno ya pekee wote walioweza kuja na kuupanda.
  • Hii mechi itaweza kuitangaza Tanzania kuliko lulu ya Tanzanite ambayo haipatikani popote pale isipokuwa hapa nchini na biashara yake hutangazwa katika vituo vingi tu vya TV duniani.
  • Hii mechi itaweza kuitangaza Tanzania kuliko Ngorongoro, Mikumi, mapango ya Amboni, makumbusho ya Bagamoyo na oh, yaani ni listi ndefu tu.
Hivi tumewekeza kiasi gani kuvitangaza hivi vivutio ambavyo hatuwalipi matajiri ili waje kuvitembelea kwani wanajileta wenyewe na pesa zao. Sasa leo hii tunapowalipa hawa jamaa mabilioni ya hela ili wakafanye mazoezi kwa kisingizio cha kuitangaza Tanzania, dunia itueleweje ? Kwa nini mpaka leo kuna tangazo la utalii linaendeshwa na jirani zetu linalosema if you want to see Kilimanjaro, come to Kenya - kweli wajinga ndio waliwao !

Mwingereza kwa jina Thomas Tusser aliwahi kusema yafuatayo mwaka 1573
A foole & his money,
be soone at debate:
which after with sorow,
repents him to late.
If they pay a penie or two pence more for the reddinesse of them..
let them looke to that,
a foole and his money is soone parted.

Tofauti ya harusi na hii mechi ni kwamba harusi by default hazihusishi matumizi ya public funds.

Hii mechi imehusisha irresponsible use of public funds.

Big difference.
Unajua Kiranga kuna watu hapa hawajui tunachojadili au wanajua lakini wanajifanya hamnazo, watu kama hawa wanaofananisha matumizi ya michango ya arusi na matumizi ya public fund wananisikitisha sana hawana tofauti na wanaouza kitambulisho cha kura kwa kupewa kofia na kanga.

Mimi si kama nashindwa kutoa kiingilio cha elfu 30 au hata laki 2, nitatoa hiyo hela kama nikijua nachangia huduma ya jamii kujenga darasa, zahanati nk,

kama wengi wanavyosema ni starehe basi "bora ninywee hiyo hela na marafiki zangu watanikumbuka kuliko kumchangia mpumbavu (serikali) ambaye hanijali aliyeamua kufanya biashara ya kijinga huku akijua wazi kuwa biashara hiyo ni ya kipumbavu".

Serikali ingekuwa na busara hizo dola mil.6 zinatosha kabisa kuanzisha shamba kubwa la mpunga Mbalali na kuajiri zaidi ya vijana 300, hapo serikali ingekuwa imetengeneza ajira ya kudumu kuliko kuziteketeza kwa DAKIKA 90, nasikia kichefu chefu.
 
TFF pengine wanatarajia kupata fedha yote kutoka kwenye gate collections na sponsourship deals ila hawana uhakika na si wafanyabiashara. Pengine hili ndo linalosumbua. TFF wangepata advice ya business people utakuta hata hizi politics za kuwa pesa ya walipa kodi inaliwa zisingekuwepo. Kutokana na kukosekana kwa hiyo advice ndo maana baadhi ya watu wanapata bullets za kuwa attack. Hii purely ingeendeshwa kibiashara, hata kama serikali ingetoa udhamini, isingekuwa na problem na niendelee kusema si problem kabisa.

Kwa sababu commercially hii pesa inaweza ikapatikana through udhamini na gate collections pale uwanja wa Taifa. Kwa hiyo TFF walihitaji kuwa na business model inayoonesha kuwa watatumia kiasi kadhaa, watapata revenues kiasi kadhaa; Na biashara inalipa. TFF hawaendeshwi na fedha ya walipa kodi. TFF ni independent organization. Serikali ingedhamini kupitia Tanzania Tourist Board, kama ambavyo advertizers wengine wangedhamini. Halafu weka na viingilio vya mlangoni pamoja na TV rights (itakuwa broadcast Duniani kote) sioni tatizo hapa.

Tatizo tunafikiria negatively kila wakati kuwa hatuwezi na ni maskini. This is downright absurd and I don't buy it!! Go TFF, Go!!
Umetumia kiswahili cha 'ngeli' sana, TFF ingekuwa na wataalamu wa biashara, ingedhaminiwa na serikali, inge...., tunajua TFF haina hizo pesa na haijasema imedhaminiwa na nani mbona inapata kigugumizi? biashara kama hii inayotumia mtaji wa dola mil.6 kwa dakika 90 huwezi kutegemea eti zitarudi kwa gate collection, hapo lazima kuna mtu atalia kama si serikali basi wadhamini, hizo kelele mnazozisikia eti tiketi za laki mbili zimeisha ni pesa ndogo sana ukilinganisha na mtaji uliotumika.
 
Jamani hebu tuwe serious kidogo kwani kuna watu humu ndani .. yaani nigekuwa karibu nao ningetembeza bakora ili iwaamshe. Wanaotetea huu ujinga naomba niwaulize maswali mawili matatu.

  • Hii mechi itaweza kuitangaza Tanzania kuliko hifadhi ya wanyama Serengeti ambayo ni ndoto ya watalii na inayojulikana dunia nzima ikiwa haina mfano popote pale.
  • Hii mechi itaweza kuitangaza Tanzania kuliko Mlima Kilimanjaro ambao ni kivutio cha watalii dunia nzima na huwapa majivuno ya pekee wote walioweza kuja na kuupanda.
  • Hii mechi itaweza kuitangaza Tanzania kuliko lulu ya Tanzanite ambayo haipatikani popote pale isipokuwa hapa nchini na biashara yake hutangazwa katika vituo vingi tu vya TV duniani.
  • Hii mechi itaweza kuitangaza Tanzania kuliko Ngorongoro, Mikumi, mapango ya Amboni, makumbusho ya Bagamoyo na oh, yaani ni listi ndefu tu.
Hivi tumewekeza kiasi gani kuvitangaza hivi vivutio ambavyo hatuwalipi matajiri ili waje kuvitembelea kwani wanajileta wenyewe na pesa zao. Sasa leo hii tunapowalipa hawa jamaa mabilioni ya hela ili wakafanye mazoezi kwa kisingizio cha kuitangaza Tanzania, dunia itueleweje ? Kwa nini mpaka leo kuna tangazo la utalii linaendeshwa na jirani zetu linalosema if you want to see Kilimanjaro, come to Kenya - kweli wajinga ndio waliwao !

Mwingereza kwa jina Thomas Tusser aliwahi kusema yafuatayo mwaka 1573
A foole & his money,
be soone at debate:
which after with sorow,
repents him to late.
If they pay a penie or two pence more for the reddinesse of them..
let them looke to that,
a foole and his money is soone parted.

Mazee huyo fool anaye-part na hela zake kirahisi katika Kiswahili wanasema "Shetani wake hapendi pesa"

Yaani tunatumia pesa ovyo utafikiri tuna allergy nazo, utafikiri tuna shetani ambaye hapendi pesa, tukiwa na pesa tu anapanda kwa hiyo inabidi tukipata kidogo tu tuzitumie, tena tununue vitu kwa gharama kubwa kuliko kawaida ili mradi tu tubaki kuwa masikini.

Shetani wetu hapendi pesa!

Mauzauza ya wakubwa kuganga njaa zao, uchaguzi karibu, saa mbaya, kalagabaho.
 
Back
Top Bottom