Wimbo wa Nay wa Mitego umewagusa Wakenya, wajiuliza ni jiwe kwa serikali yao au kwa Tanzania!

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
Wakuu,

Nay wa Mitego amedondosha jiwe jingine, ngoma inaitwa "Wapi Huko", kwenye wimbo huu anagusima mambo mengi ikiwemo hali ngumu ya maisha, akisema kwenye nchi hiyo bei ya pombe ni rahisi kuliko chakula, uchumi unachechemea, muda wa kazi umeme haupatikani, soka imeingiliwa na siasa, wananchi hawasikilizwi, wasanii wote ni chawa wa serikali sipokuwa mmoja tu naye anapigwa vita na serikali, nchi ambayo hutoboi bila kuwa mbishi, nchi ambayo wezi wanajulikana lakini hawawezi kukamatwa, nchi yenye wasomi wengi lakini ajira hakuna nk bila kutaja nchi hiyo ni nchi ipi hasa!

Wakenya wanasema Nay anawaongelea wao, huku Wabongo wanasema hili dongo lakwetu wala haliwahusu wao, sema kwakua Tanzania na Kenya ni kama watoto wa mama mmoja ndio maana hata wao wameguswa.

1706680426854.png

Sasa Nay kajifunza kurusha makombora kisayansi, BASATA wanabaki kukodoa macho tu huku sindano inawaingia.😂😂😂

Wimbo huu hapa chini👇👇👇

Wakuu,

Nay wa Mitego amedondosha jiwe jingine, ngoma inaitwa "Wapi Huko", kwenye wimbo huu anagusima mambo mengi ikiwemo hali ngumu ya maisha, akisema kwenye nchi hiyo bei ya pombe ni rahisi kuliko chakula, uchumi unachechemea, muda wa kazi umeme haupatikani, soka imeingiliwa na siasa, wananchi hawasikilizwi, wasanii wote ni chawa wa serikali sipokuwa mmoja tu naye anapigwa vita na serikali, nchi ambayo hutoboi bila kuwa mbishi, nchi ambayo wezi wanajulikana lakini hawawezi kukamatwa, nchi yenye wasomi wengi lakini ajira hakuna nk bila kutaja nchi hiyo ni nchi ipi hasa!

Wakenya wanasema Nay anawaongelea wao, huku Wabongo wanasema hili dongo lakwetu wala haliwahusu wao, sema kwakua Tanzania na Kenya ni kama watoto wa mama mmoja ndio maana hata wao wameguswa.

Sasa Nay kajifunza kurusha makombora kisayansi, BASATA wanabaki kukodoa macho tu huku sindano inawaingia.

Wimbo huu hapa chini

True Boy
 
Viherehere vyao wakenya...huo wimbo kaiimba Tanzania ila katumia code ili basata wasimzingue
 
Back
Top Bottom