Wimbo wa kina Mbarikiwa Mwakupesile "Tatizo Wanatuona Nyani" umezua songombingo aka patashika nguo kuchanika!

Burkinabe

JF-Expert Member
Feb 12, 2023
1,896
3,206
Wana jamvi,

Ni matumaini yangu wote hamjambo.

Lengo la hii thread ni kuhusiana na wimbo wa washiriki wa kanisa la Mbarikiwa Mwakipesile wa kanisa la Kikosi cha Injili huko Mbeya.

Kibao hiki kilicholeta shida kinaenda kwa jina "Tatizo wanatuona nyani" ambao ndani yake wamejaribu kuelezea namna raia wa hali ya chini wanavyotendewa vibaya mithili ya nyani na viongozi wao!

Huu wimbo naona umeviamsha vyombo vya ulinzi na usalama na kuanza kuwafuatilia wote waliohusika kwenye wimbo huo. Na tayari baadhi yao inasemekana tayari wako kunyea kwenye ndoo. Pia leo jioni wamefika kanisani kwa lengo la kuchukua vifaa vyote wanavyotumia kwenye huduma zao kwa lengo la kukomesha kabisa huduma ya Kikosi cha Injili.

Sina uhakika kama wimbo umeshafungiwa na BASATA au la, vinginevyo, ningeuweka hapa.

Ahsanteni.
 
Nimejiridhisha bado haujafungiwa
 

Attachments

  • Video_Song🐒,Mwafrika_wazungu_WANAKUONA_NYANI_TU😄_Hata_ujipendekezeje_kwao(144p).3gp
    4.4 MB · Views: 7
Wimbo mzuri sana. Unaelimisha. Dkt Samia anapenda uhuru wa habari. Wala siyo tatizo huu wimbo bali viongozi wezi wanamzunguka Dkt Samia.
Kweli kabisa.
Kwa ambao hawajausikiliza, nimeuweka hapo juu baada ya kujiridhisha haujafungiwa na BASATA.
 
Tatizo wanatuona nyani
 

Attachments

  • Video_Song🐒,Mwafrika_wazungu_WANAKUONA_NYANI_TU😄_Hata_ujipendekezeje_kwao(144p).3gp
    4.4 MB · Views: 4
Back
Top Bottom