Ushauri kwa Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile na Kikosi Kazi cha Injili

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2023
4,695
6,396
Ninajua kuwa upo gerezani kwa sasa, lakini naamini hutaliruhusu gereza kuingia moyoni mwako. Ni kwa sababu hiyo basi, nimechukua hatua hii nikiamini kuwa hata kama hutakuwa na simu gerezani, wapendwa wako wataweza kukufukishia huu ujumbe kwa wakati sahihi.

Awali ya yote, ninakupa pole kwa unayoyapitia. Naamini si mapenzi ya Mungu, lakini pia si mwisho wako. Badala yake, huenda ikageuka kuwa ushuhuda utakaobariki wengi katika kizazi hiki na vizazi vijavyo.

Mch. Mbarikiwa, naamini na wewe unaliamini Andiko la 1Wakorintho 13:9, kuwa "tunafahamu kwa sehemu", hivyo hutakuwa umefunga mlango wa kusikia ushauri toka kwa wengine bila kujali itikadi zao za kiimani, maadam ushauri wenyewe haupingani na Maandiko Matakatifu. Naamini, hata wewe, pamoja na hatua kubwa uliyopiga kihuduma, ungali una utayari wa kujifunza kwa wengine ikitokea fursa ya aina hiyo, bila kujali kama ni wakubwa au wadogo kwako kiumri, kielimu, kiuchumi, kihuduma na katika uzoefu wa maisha. Ni kama Paulo anavyosema, "tufarijiane mimi na ninyi, kila mtu kwa imani ya mwenzake..." Warumi 1:12.

Ndiyo maana Musa, pamoja na kuwa alikuwa ni mtumishi aliyekuwa na ukaribu sana na Mungu, bado alikubali kuupokea ushauri wa Yethro; baada ya kugundua kuwa ni ushauri mzuri; Kutoka 18:1-27.
Ni imani yangu kuwa wewe nawe utapata wasaa wa kuutafakari huu ushauri na hatimaye kufanya maamuzi stahiki kwa maslahi ya Mwili wa Kristo Tanzania na duniani kote.

Kabla ya kushauri, nina machache ya kusema kama ifuatavyo:

1. Inawezekana ikawa si mapenzi ya Mungu wewe uwepo gerezani.

Labda tu kama Mungu alikutaka uende huko kwa lengo maalum. Na hata kama si mapenzi ya Mungu wewe kuwepo huko, bado unaweza ukatumia hiyo fursa kwa manufaa ya Ufalme wa Mungu. Kwa hiyo, endelea kuhubiri Injili hata huko gerezani.

Na hata kama si mapenzi ya Mungu, haimaanishi kuwa umetenda dhambi. Isitoshe, wewe hutakuwa mtu wa kwanza kufanya kitu kizuri japo hukuagizwa na Mungu kufanya hivyo. Angalia mifano ya hawa wafuatao.

(A). Mtume Paulo
Yeye aliitwa na Mungu akawahubirie Mataifa. Alipolazimisha kwenda Yerusalemu, pamoja na kuwa alionywa na Roho Mtakatifu kuwa atakutana na vifungo, bado alienda. Kilichotokea? Alipelekwa Rumi kama mfungwa, nchi ya watu wa Mataifa. Unaweza kusema alipelekwa alikokuwa akihitajika kwa ajili ya kuhubiri Injili. Lilikuwa ni jukumu lake kuwahuburia wasiotahiriwa kama ambavyo Petro alipewa Injili ya waliotahiriwa; Wagalatia 2: 6-7

(B). Yohana Mbatizaji
Mungu alimwita kuwa kama mtangulizi wa Yesu, au, kumtambulisha Yesu kwa Wayahudi. Lakini aliingia matatani pale alipomkemea Herode.

Ilikuwa ni sahihi kumkemea Herode, lakini pengine alikosea "timing" na "approach". Japo alifanya jambo jema, lakini sina uhakika kama Mungu alimwagiza kufanya hivyo. Wakati mwingine, kuna mambo ambayo kabla ya kuyafanya, unapaswa kupata uongozi wa Roho Mtakatifu. Ndiyo maana Paulo hakulikemea haraka pepo lililokuwa kwa kijakazi aliyekuwa akiwashuhudia, mpaka wasaa sahihi ulipowadia; Matendo 16:6-18

(C). Kenneth Hagin
Huyu alikuwa ni mhubiri aliyeanza huduma kama Mchungaji, lakini miaka kumi na mbili baadaye, aliingia kwenye huduma ya Ualimu. Baada ya miaka kumi na mbili ya huduma ya uchungaji, aliamua kufunga na kuomba kumwuliza Mungu sababu inayomfanya asijisikie "comfortable" kwenye huduma ya uchungaji.

Ni katika maombi hayo Mungu alimjibu kuwa hakumwita kuwa Mchungaji bali Mwalimu. Mungu alimwambia wazi kuwa katika kipindi cha miaka kumi na mbili ya Uchungaji wake, pamoja na kuwa watu walikuwa wakiokoka na kuponywa, si kwa sababu anafanya alichomwagiza, bali kwa kuwa analiheshimu Jina la Yesu. Kwa hiyo, kwa Mungu, ni pale alipoanza huduma ya Ualimu ndiyo alihesabiwa kuwa kaanza huduma. Ile miaka kumi na mbili haikuhesabiwa.

(D). Mwl. Christopher Mwakasege
Naamini unamfahamu Mwl. Mwakasege. Alishawahi kushuhudia kuwa wakati aliposikia wito wa huduma, aliamua kutafuta Chuo cha Theolojia kwa lengo la kuwa Mchungaji. Yeye alikuwa akiamini kuwa ili mtu awe mhubiri, sharti aende kwanza Chuo cha Uchungaji. Lakini kabla hajalifanikisha hilo, Mungu alimwambia kuwa hajamwita kuwa Mchungaji. Na kama ulishawahi kumsikiliza, utakubali kuwa kihuduma, Mwakasege ni Mwalimu.

(E). Ayubu
Wasomaji wa Biblia wanafahamu kadhia aliyoipata mtumishi wa Mungu Ayubu. Wengine wanafikiri kuwa hayo yaliyompata yalikuwa hayazuiliki, lakini si kweli.

Ayubu 3:25 inaonesha kuwa Ayubu ndiye aliyefungua mlango wa majaribu yaliyompata. Ayubu alikuwa anahofia kuwa mabaya yanaweza yakampata. Na kiroho, hofu humfungulia Shetani mlango kama ambavyo imani huualika uwepo wa Mungu; 2Timotheo 1:7, Marko 9:23.

Kama akina Meshaki, Shadraka, na Abednego wangekuwa na hofu kama Ayubu, wangetekea kwenye tanuru la moto.

Kama Ayubu angekuwa na imani kama ya Danieli, Shetani asingeweza kumyumbisha. Alishindwa kumwanganiza Danieli kwenye
tundu la Simba si kwa sababu Danieli alikuwa "special", bali Danieli alifahamu Neno la Mungu na akasimama nalo; Danieli 3: 13-30, 6:1-24.

Na kama kuna mtu anafikiri kuwa Danieli alinusurika kutafunwa na Simba kwa sababu ya "uspecial" wake kwa Mungu, napenda kumfahamisha kuwa kila aliyemwamini Yesu ni "special" kwa Mungu, tena ni mkuu kuliko Danieli. Ndiyo, ni mkuu kuliko Danieli, Mfalme Sulemani, Mfalme Daudi, na hata Yohana Mbatizaji. Kwani Neno linasemaje?

"Amin, nawaambieni, Hajaondokea mtu katika uzao wa wanawake aliye mkuu kuliko Yohana Mbatizaji; walakini aliye mdogo katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko yeye" Mathayo 11:11.

Na kama aliyemwamini Yesu ni mkuu kuliko Yohana Mbatizaji, inamaanisha anaweza kupata matokeo makubwa zaidi kuwazidi akina Yohana Mbatizaji, Danieli, Daudi, n.k.

Neno la Mungu ni ulinzi, kinga, na silaha.

Mch. Mwakipesile, kwa kutoa hiyo mifano, simaanishi kuwa umekosea, la hasha! Lakini pia kama ulikosea, wewe si wa kwanza kukosoea. Isitoshe, wakati mwingine, ni sahihi kuwa tunajifunza kupitia makosa.

2. Nguvu ya ulimi
Nakumbuka kipindi cha Corona, wewe ni miongoni mwa watumishi wachache mlioonekana kutokutishwa na mlipuko wa Corona. Hivi unafikiri ingekuwaje kama na wewe ungepatwa na hofu na kuanza kusema, "tutamalizwa na corona?" Huenda usingelikuwa hai sasa.

Kwa nini nasema hivyo? Ni kwa sababu, kulingana na Marko 11:23, "UTAPATA UKISEMACHO". Hiyo ni kanuni ya kiroho inayotawala maisha ya watu. Mtu hupata kile anachokikiri.

Imeandikwa, "Tumbo la mtu litajazwa matunda ya kinywa chake; Atashiba mazao ya midomo yake" Mithali 18:20

"... umetegwa kwa maneno ya kinywa chako, Umekamatwa kwa maneno ya kinywa chako" Mithali 6:2

Naongezea na shuhuda 2 nilizizozisoma kwenye kitabu kiitwacho THE EXPLOITS OF FAITH.

I. Mtu aliyekuwa amehukumiwa kunyongwa hadi kufa aliweza kutoka salama gerezani baada ya kufahamu jinsi ya kutumia kinywa chake kiusahihi.
Alipokuwa gerezani, alimwamini Yesu na akaanza kuvisoma Vitabu vya IMANI. Alipofahamu kuwa MTU AKIWA NDANI YA KRISTO AMEKUWA KIUMBE KIPYA, alijua kuwa haimpasi kuyaishi matokeo ya maisha yake ya zamani; 2Wakorintho 5:17.
Aliamini kuwa kwa vile alishasamehewa na Mungu, na adhabu ya kifo haikuwa halali kwake. Aliamua kutokufa.

Kuanzia wakati huo, alianza kukiri kuwa Mungu kamweka huru toka gerezani. Aliwaambia hata na wafungwa pamoja na maaskari Magereza kuwa ataenda kuwa mhubiri. Wengine hawakumwamini, lakini yeye aliendelea kukiri hivyo. Mwaka wa kwanza ulipita bila kunyongwa, na hatimaye mwaka wa pili aliachiliwa huru.

Hakuwa amefanya jitihada zozote za Kisheria ili kuzuia asinyongwe. Inasemekana, alipaswa kunyongwa muda mfupi baada ya kuhukumiwa kifo. Lakini kwa ukiri wake, alisahaulika kunyongwa. Miaka miwili baadaye, Jaji Mkuu ambaye ndiye aliyekuwa amemsomea hukumu ya kunyongwa, alilitembelea gereza lao na akamkuta humo, na akashangaa kuwa hajanyongwa mpaka wakati huo. Huyo huyo Jaji, aliyemsomea hukumu ya kunyongwa, ndiye aliyemtoa tena gerezani, akifikiri anatekeleza matakwa ya Kisheria, kumbe alikuwa akiendeshwa na ulimwengu wa roho kupitia kinywa cha huyo mtu.

Ukiri wake ulimpatia matokeo aliyoyatamani. Alipotoka gerezani, alilianzisha Kanisa aliloliita RESURRECTION CHAPEL.

2. Ushuhuda mwingine ni wa mtu aliyesalimika kufa kimuujiza baada ya kunywa tindikali (acid). Alienda maabara ya kazini kwao akiwa na kiu na kunywa tindikali (acid) akifikiri ni maji. Mwenzake aliyekuwemo humo maabara alipoona kilichokuwa kikitendeka, alimpazia sauti kuwa anakunywa acid, lakini ilikuwa ni "too late", alikuwa ameshakunywa. Huyo mtu alifahamu kuwa alikuwa akikabiliana na mauti uso kwa uso, lakini alijua cha kufanya. Alijua kanuni ya IMANI, kuwa hana budi kusema sawasawa na Neno la Mungu ili Mungu alithibitishe. Imeandikwa, "NILITHIBITISHAYE NENO LA MTUMISHI WANGU" Isaya 44:26.

Kwa hiyo, baada ya kuambiwa hivyo na mwenzake, na yeye akiwa ameshafahamu kuwa amekunywa acid, alijibu kwa sauti, "Si tindikali, ni maji".

Ili kumthibitishia kuwa ni tindikali, mwenzake alichukua kimiminika kilichosalia kwenye glasi ambapo alipoipima, ilionesha kuwa ni maji. Lakini alipoipima iliyokuwa kwenye chupa, ambayo iliyokuwemo kwenye glasi ndipo ilipotoka, matokeo yalionesha kuwa ni tindikali. Alipoyaona hayo, alimtazama mwenzake na kumwambia, "wewe si mtu wa kawaida".

Mch. Mwakipesile, wewe si mtu wa kawaida, na unalijua hilo, maadam unamwamini Yesu.

Una mamlaka ya kuamua juu ya hatma yako. Ukisimama katika NENO la Mungu, Mungu atajitukuza. Neno la Mungu limesimama imara Mbinguni hata milele; Zaburi 119:89. Ukiliruhusu lisimame imara moyoni mwako, mazingira yako yatakupigia saluti. Litazame Neno la Mungu Peke Yake. Ukifanya hivyo, halitaruhuhusu uzame; Mathayo 14:25-33, Warumi 4:16-22

Imani katika NENO la Mungu itakuweka juu.

Mamlaka ambayo Mungu amempa mtu aliyemwamini ni makubwa mno. Ndiyo maana Paulo aligoma kufa kabla ya kumaliza kazi ya Mungu; Wafilipi 1:20-26.

Bila shaka ulishasikia habari za Yohana, kuwa waliotaka kumwangamiza hawakufanikiwa. Upanga haukuweza kumwua. Walipomchemsha kwenye mafuta hakufa. Hiyo ni kwa sababu aliamini kuwa "... huku ndiko kushinda kuushindako ulimwengu, hiyo imani yetu" 1Yohana 5: 4.

Na hivyo basi, ninakushauri haya:

JAMBO LA KWANZA: SAMEHE
Msamehe kila mtu aliyekukosea, na pia utubu kwa Mungu ikiwa kuna mtu ulimkosea. Hilo ni hitaji la kwanza kwa mtu yeyote anayetaka kupata matokeo kwa njia ya imani.

"Nanyi, kila msimamapo kusali, sameheni, mkiwa na neno juu ya mtu; ili na Baba yenu aliye mbinguni awasamehe na ninyi makosa yenu"
Marko 11:25

"...Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi, ili mpate kuwa wana wa baba yenu aliye mbinguni..."
Mathayo 5:44-45

"Adui yako akiwa ana njaa, mpe chakula, Tena akiwa ana kiu, mpe maji ya kunywa... na BWANA atakupa thawabu"
Mithali 25: 21-22.

"Kila amchukiaye ndugu yake ni mwuaji..."
1 Yohana 3:15

Naamini huna uhitaji wa kufafanuliwa hayo Maandiko, kwamba kati ya kikwazo kikubwa kinachoweza kuzuia majibu ya maombi ya mtu ni kuruhusu kutawaliwa na chuki. Nafasi ingeruhusu, ningetoa shuhuda/ mifano mingi halisi inayoonesha uhusiano uliopo katia ya Upendo na majibu ya maombi ya imani.

Usiruhusu wazo la hasira au chuki dhidi ya watu unaoamini wamekutendea isivyo sahihi kukaa moyoni mwako.

Kama kuna mtu unayeamini kakuokosea, msamehe na umwombee. Ndivyo Biblia inavyoagiza.

Waombee mema! Wabariki! Ombea amani katika familia zao, kazi zao, n.k.

Kuna siri katika kuwaombea wengine mema, hata kama wao wenyewe hawakupendi wala hawajui kuwa unawaombea.

Unakumbuka kilichotokea kwa Ayubu? Wakati angali yupo majaribuni, Mungu aliagiza awaombee marafiki zake waliokuwa wamemkejeli, na alipofanya hivyo, uteka wake uliisha.
"Kisha BWANA akaugeuza uteka wa Ayubu, hapo alipowaombea rafiki zake; BWANA naye akampa Ayubu mara mbili kuliko hayo aliyokuwa nayo kwanza"
Ayubu 42:10.

JAMBO LA PILI: JIZAMISHE KWENYE AHADI ZA MUNGU
Naamini huwa unasoma Biblia, lakini sina uhakika kama ulishawahi kuisoma Biblia nzima. Nakushauri uwekeze kwenye usomaji wa Biblia, kwa kuisoma kuanzia kitabu cha Mwanzo hadi Ufunuo. Fanya hivyo, hata kama ulishawahi kuisoma yote zaidi ya mara moja.

Wakati unaisoma, nukuu AHADI zote za Mungu utakazoziona kwenye Biblia, Ahadi ambazo unaamini ni kwa ajili yako. Hata kama hutahitaji kuandika hizo Ahadi, kuna faida tele katika kuisoma Biblia nzima.

Wakristo wengi bado hawajafanikiwa kufanya hivyo. Matokeo yake, wanashindwa kuhusianisha Maandiko ya Agano la Kale na ya Agano Jipya. Hawajui kuwa namna Mungu alivyuhusiana na watu Wake katika kipindi cha Torati ni tofauti na anavyohusiana na watoto Wake sasa katika Agano Jipya. Ni muhimu kwa kila Mkristo, kuisoma Biblia nzima, na kama hana nafasi ya kufanya hivyo, basi awekeze muda wake mwingi kusoma alau Agano Jipya, hasa Nyaraka. Nyaraka za kwenye Biblia, unaweza kuziita ni barua waliyoandikiwa Wakristo.

Kunaweza kukawa kugumu kwa Mkristo kuielewa Biblia katika mtazamo wa Agano Jipya endapo hatasoma Nyaraka za Biblia.

JAMBO LA TATU: KIRI USHINDI KILA SIKU
Lipi hasa unalotaka Mungu alifanye kwako? Kinywa chako kinaweza ama kumpa Mungu uhuru wa kukusaidia au kumwekea mpaka. Kama unataka akuonekanie mahali ulipo, huna budi kukubaliana Naye: "Je! Watu wawili waweza kutembea pamoja, isipokuwa wamepatana?"
Amosi 3:3

Na namna ya kupatana na Mungu ni kukiri kile anachosema juu yako kwa njia ya Neno Lake. Kama amesema "Kila silaha itakayofanyika juu yako haitafanikiwa" (Isaya 54:17), huna budi na wewe kukiri hivyo kwa ujasiri kila siku.

Naomba nikuambie hili, ila kwa nia njema. Tafadhali usinikasirikie! Na ninatangulia kuomba radhi, endapo hili kitakukera kwa namna yo yote ile!

Ninafikiri, hata wewe kuweko gerezani kwa sasa, kunaweza kukawa kulichangiwa na kinywa chako. Wana wa Israeli walishafanya jambo kama hilo. Walijifananisha na mifupa mikavu, na maisha yao yakafanania hivyo. Ilibidi Mungu amwelekeze Nabii Ezekieli awatabirie uhai kwa lengo la kuyabatilisha maneno waliyojinenea
Ezekieli 37:1-12.

Nilishakusikia mara kadhaa ukijitabiria kufungwa na hata kifo, jambo ambalo si salama, kwa mujibu wa kanuni ya kiroho. Ulimwengu wa roho ndiyo unaotawala ulimwengu wa asili. Na ulimwengu wa roho unatawaliwa na maneno. Maneno yaliyopo kwenye ulimwengu wako wa roho ndiyo huamua nini kitokee kwenye ulimwengu wako wa asili.

Mama mmoja alikuwa na kawaida ya kusema mara kwa mara, hasa anapopishana na gari, "hili gari lilitaka kunigonga!" Aliendelea kukiri maneno yanayofanania hayo mpaka hatimaye akapoteza maisha kwa kugongwa na gari.

Sehemu nyingine, kulitokea msiba wa watu wawili - mume na mke wake. Walikufa siku moja kwa ajali ya gari.

Msibani, kila mtu aliongea la kwake, katika hali ya mshangao! Kuna waliostaajabu kuwa ni kwa nini Mungu aliruhusu watu wema kiasi hicho kufa kwa ajali siku moja. Lakini kwa wale waelewa wa kanuni ya kiroho, waliacha kushangaa baada ya kuelezwa na ndugu wa marehemu kuwa walikufa kama walivyotamani. Alishawahi kuwasikia wakisema kuwa wanataka wafe pamoja. Kwa ajali hiyo ya gari, walipata walichojitabiria. Sasa hiyo haimaanishi kuwa ni Mungu Ndiye aliyewajibu "maombi" yao.

Maneno humfungulia mlango Mungu au Shetani. Maneno yao yaliifungulia roho ya mauti maishani mwao, wakafa kwa ajali.

Hata Rais wa awamu ya tano, alikuwa na kawaida ya kuongea maneno ambayo kwa wanaoifahamu hii kanuni, waliamini ya kuwa ni maneno ya hatari. Maneno ni roho; Yohana 6:63. Pengine, angekiri kuwa asingekufa kabla ya kumaliza kipindi chake cha uongozi, huenda angekuwa hai mpaka sasa.

Nilimsikia mjane wa Dr. Magufuli, Mama Janeth, akisema kuwa kipindi akiwa binti, nafikiri , kipindi hicho alikuwa mwanafunzi wa Sekondari, alisalimiana na Mwl. Nyerere, na alipomwuliza anataka kuja kuwa nani, alimwambia, "mke wa Rais". Kwa kanuni hiyo, Janeth Magufuli alipata alichokisema.

Hata mke wa Abraham Lincoln, inasemekana alimwambia baba yake kuwa ni lazima aje kuwa "first lady" wa Marekani. Japo aliolewa na mtu ambaye hakuonekana kuwa na mrengo wa Kisasa, huenda kinywa chake, kilimsukuma mumewe kuingia kwenye Siasa ili tu kutimiza "unabii" aliojitabiria. Alipata alichojitamkia. Abraham Lincoln alikuja kuwa Rais wa Marekani hivyo "unabii" wa mkewe aliojitabiria kuwa atakuja kuwa mke wa Rais ukawa umetimia.

Kuna wanawake wameua waume zao kwa vinywaji vyao bila wao kujua. Kuna wazazi wamewaharibu watoto wao kwa vinywa vyao bila kukusudia. Na kuna watumishi wa Mungu waliowaua watu, wakati mwingine, bila kukusudia, kwa kutumua vinywa vyao.

• Petro aliwaua Anania na Safira kwa kinywa chake
Matendo 5:1-10

• Eliya aliwaua wanajeshi 102 kwa kinywa chake
2Wafalme 1:1-15

• Elisha aliwaadhibu kwa kinywa chake vijana 42 waliomdhihaki
2 Wafalme 2:23-24

• Kwa kinywa chake, Paulo alimpofusha kwa muda mchawi aliyeitwa Bar- Yesu
Matendo 13:6-12.

Hiyo ni mifano ya kwenye Biblia. Muda hauruhusu kutoa mifano ya watu ninaowafahamu, waliopata matokea mazuri au mabaya kutokana na maneno ya vinywa vyao au vya watu wao wa karibu.

Mtumishi wa BWANA Mch. Mbarikiwa, simama katika NENO la Mungu kwa kulikiri kila siku na hakika, kifungo chako kitageuka kuwa ushuhuda.

Lakini katika yote uyafanyayo, hakikisha kuwa unatawaliwa na upendo, kwa kuwa imani hutenda kazi katika Upendo. Na kamwe, huwezi kushindwa endapo utakubali kutawaliwa na upendo

~ "Maana katika Kristo Yesu kutahiriwa hakufai neno, wala kutokutahiriwa, bali imani itendayo kazi kwa upendo"
Wagalatia 5:6

~ "Upendo haupingui neno wakati wo wote..."
1Wakorintho 13:8

~ "Nasi tumelifahamu pendo alilo nalo Mungu kwetu sisi, na kuliamini. Mungu ni upendo, naye akaaye katika pendo, hukaa ndani yake..."
1Yohana 4:16.

~ "Basi, sasa inadumu imani, tumaini, upendo, haya matatu; na katika hayo lililo kuu ni upendo" 1Wakorintho 13:13

Hakika, kuchagua kutawaliwa na upendo, kuamua kuenenda katika upendo kwa kuwapenda hata wanaokuchukia, kuwabariki wanaokulaani, kuwaombea mema wanaokutamania mabaya, ni kutembea katika ushindi na usalama.

Mtu anayeenenda katika upendo yupo salama wakati wote kwa kuwa kuenenda katika upendo ni kuenenda ndani ya Mungu. Ili mtu amdhuru mtu anayeenenda katika upendo, itamlazimu kwanza kumdhuru Mungu, ndipo aweze kumfikia mtu anayeenenda katika upendo, jambo ambalo halitawezekani asilani!

Mchungaji Mbarikiwa, wewe ni mshindi, maana imeandikwa, MUNGU AKIWAPO UPANDE WAKO, NI NANI ATAKAYEKUWA JUU YAKO? Warumi 8:31.

Hitaji pekee ulilo nalo, ni Mungu kuwa upande wako. Na Mungu na Neno Lake ni Mamoja. Neno lake likiweka makao kwako ni Yeye kaweka makao Yake kwako. Wewe ni mshindi!!!

Shalom!!!
 
Unayemzungumzia ni nani na yupo gerezani kivipi
au una assume wote tunaelewa kuhusu ulichoandika
Ni kiongozi wa "Kanisa" liitwalo Kikosi Kazi cha Injili. Amehukumiwa miaka mitatu gerezani kwa kosa la kuendesha Kanisa bila usajili.

Lakini kuna mengi yanayosemwa kuhusiana na kifungo chake.
 
Amina, umenena vyema
 
alifanyaje mkuu
Amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu kwa kosa la kuongoza Kanisa lisilo na usajili.

Lakini mengi yamekuwa yakisemwa juu ya hiyo hukumu aliyohukumiwa.

~ Kuna wanaosema amepelekwa gerezani kwa lengo la kumnyamazisha baada ya kuwa mkosoaji mkubwa wa Serikali

~ Kuna wanaosema ameponzwa na tabia yake ya kuwakosoa wahubiri wa madhehebu mengine

~ n.k.

Ikumbukwe pia kwamba ameshawahi kulalamika kuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa ndiye aliyemwua mtoto wake kwa lengo la kumnyamazisha.

Lakini kwamba hayo yasemwayo ni kweli au si kweli, au malalamiko yake yana ukweli au la, kwa kweli mimi sina jibu mkuu.
 
du atakuwa chadema huyu
 
Back
Top Bottom