Wimbo mpya wa Roma Mkatoliki wapigwa marufuku kuchezwa katika vituo Radio na Televion.

hayaland

JF-Expert Member
May 4, 2012
712
399
Kwa taarifa zilizotufikia hivi punde zinaeleza kuwa wimbo mpya wa nguli wa Hipphop ROMA MKATOLIKI wa Vivaaaa roma umepigwa marufuku kuchezwa katika vyombo vyote vya habari nchini.
 
tunao tayari kwenye gadgets zetu,ahahaha!tutaupiga mikutanoni na magetoni!tena hii ban itabackfire kwa katazo hilo!mbaya zaidi katazo litaufanya wimbo utwaje zaidi midomoni na hivyo kuitajika kusikilizwa hili kujua yaliyomo kwa wale ambao hawaja usikia!hii itaufanya wimbo kuwa on demand!asante kwa kuupaisha,ahahaha
 
..anyway sioni tofauti yoyote,wengi tayari wanao, so, sitashangaa nikiuskia kwenye daladala,stendi,sokoni, na kwingineko..
 
Mbona upo kila sehemu mpaka kijijini?
Na huu ndio wimbo uliosikilizwa na watz wengi toka tupate uhuru
 
Waliomtuma wanasemaje??

Mistali ya nyimbo nne za Roma katika miaka minne tofauti:-
1.Mwakyembe aliwafundisha monduli siasa (Tanzania).

2.Nakomba pesa zote nasepa kama Lowasa (Mechi za ugenini).

3.Bwandugu bwaga manyanga ayaokote Magufuli (Mathematics)

4.Kombe linakwenda Monduli ( viva Roma).

Ni vigumu kuwa ukawa bila kuwa mnafiki.
Ni bora wangejiita umoja wa katiba ya Wanafiki (UKAWA).
 
Ninao waje wau delete kwenye simu yangu na nishauweka kwenye pc nime choma kopi kwenye cd. #viva Roma vivaa
 
aliwahi kusema usipocezwa redio utapigwa na bajaji za Mwenge..
 
hapa nilipo naskiza. ndo ringtone yangu. ntaupiga mpk roma atoke jasho.
 
Mmmh huyu jamaa boya nimeipakua sasa hvi msanii anatukana kisanii sio kibwege kivile stupid
 
Back
Top Bottom