Who is to Blame? Mholanzi amchapa Vibao Mwalimu Mkuu

Sumba-Wanga

JF-Expert Member
Feb 2, 2011
5,349
1,224
Nani alaumiwe? Mholanzi aliyemchapa vibao Mwalimu Mkuu baada ya kukuta wanafunzi wako madarasani hawasomi wakati walimu wamekaa wanapanga ratiba? Huyo Mholanzi ni mfadhili wa shule.

Au ndio kale kaugonjwa ketu ka Watanzania?

Soma zaidi:

Home
 
Mholanzi amzaba vibao mwalimu mkuu
Na Thobias Mwanakatwe
11th March 2012
Raia mmoja wa Uholanzi, Marise Koch, anatuhumiwa kumfanyia kitendo cha udhalilishaji Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Marera iliyopo kata ya Rhotia wilayani Karatu mkoani Arusha kwa kumpiga vibao mbele ya wanafunzi na walimu wenzake.
Taarifa ambazo NIPASHE Jumapili imezipata na kuthibitishwa na viongozi wa Idara ya Elimu wilaya ya Karatu na Jeshi la Polisi, ni kwamba kutokana na udhalilishaji uliofanywa, raia huyo ameshafunguliwa jalada lenye namba KRT/RB/835/2012 katika kituo cha polisi Karatu kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Marera, Emmanuel Ginwe, akizungumza na gazeti hili kwa simu kutoka Karatu, alisema alipigwa vibao viwili na raia huyo wa Uholanzi ambaye ni mwanamke baada ya kuwakuta walimu wa shule hiyo wakipanga ratiba ya shule.
Ginwe alisema tukio hilo lililotokea Februari 14, mwaka huu majira 4:30 asubuhi ambapo raia huyo ambaye anaifadhili shule hiyo kwa kukarabati majengo ya shule, ofisi nyumba ya walimu na kompyuta ndogo za wanafunzi kufanyia michezo (games) na kujifunzia kuandika alifika shule hapo kutembelea kama kawaida.
Alisema Mholanzi huyo baada ya kufika shuleni hapo, alikuta walimu wakipanga ratiba ya shule na kuanza kuhoji kwanini walimu hawajaingia madarasani kufundisha wanafunzi madarasani ambapo alijibiwa kuwa wamepewa maelekezo ya kuandaa ratiba ya shule na baada ya kumaliza kazi hiyo wataingia madarasani kuendelea kufundisha.
Hata hivyo, majibu ya walimu hao hayakumridhisha ambapo Mholanzi huyo aliamua kwenda ofisini kwa Mwalimu Mkuu na kuanza kumfokea kwamba yeye (Mholanzi) anafadhili vitu vingi lakini kumbe walimu hawafundishi madarasani na kuanza kukusanya kompyuta zake ndogo (Exo-Laptop) kwa lengo la kuzichukua.
Mwalimu Mkuu wa shule hiyo hata hivyo alimsihi asichukue kompyuta hizo lakini alikataa na alipoona anazuiwa alimpiga vibao mwalimu huyo huku akiendelea kuzikusanya komputa akiwa na mwenzake ambapo kwa mara ya pili alimnasa vibao tena Mwalimu Mkuu huyo.
Kitendo cha Mwalimu Mkuu kupigwa vibao kiliwashitua walimu na wanafunzi wa shule hiyo ambapo walianza kuhoji kulikoni na walipoelezwa walisikitishwa na udhalilishaji uliofanywa na raia huyo wa Uholanzi kwa kutumia kigezo cha ufadhili kufanya udhalilishaji.
Ginwe alisema baada ya Mholanzi huyo kumfanyia udhalilishaji huo na kuchukua kompyuta zake 70 kati ya 93 zilizokuwepo na kuondoka zake, alikwenda kutoa taarifa kwa viongozi wa kijiji, kata na wilayani ambapo alishauriwa kufungua jalada la kesi katika kituo cha polisi.
“Nimedhalilishwa sana mbele ya walimu, wanafunzi na mke wangu ambaye ni mwalimu, tena mbele ya bendera ya Taifa iliyopo katika shule hii, namshukru Mungu wakati Mholanzi huyu ananipiga vibao japo ni mwanamke sikuweza kujibu mapigo,” alisema Ginwe.
Katibu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) wilaya ya Karatu, Peter Simwanza, akizungumza na gazeti hili kuhusiana na tukio hilo, alisema kitendo alichofanyiwa Mwalimu Mkuu huyo ni cha kiudhalilishaji na kimedhalilisha taaluma ya ualimu na taifa kwa ujumla kwa sababu kimefanyika ndani ya ofisi ya mwalimu ambayo ni ya serikali.
Alisema CWT inataka kuona raia huyo wa Uholanzi anachukuliwa hatua kali za kisheria na vyombo vinavyohusika na kwamba chama hicho kitahakikisha kinamtafuta mwanasheria atakayemsimamia kesi ya Mwalimu Mkuu huyo ili haki iweze kutendeka.
Simwanza alisema baadhi ya wafadhili wanaosaidia katika shule mbalimbali za msingi na sekondari wilayani Karatu wamekuwa kero kubwa ambapo wamefikia hatua ya kuingilia utendaji wa maofisa wa elimu kiasi kwamba wanataka kuingiza mambo wanaoyataka wao ndiyo yafanyike kwenye mitaala ya elimu.
Hata hivyo taarifa ambazo gazeti hili imezipata ni kwamba raia huyo wa Uholanzi anajiandaa kuondoka nchini kwenda kwao baada ya kufanya udhalilishaji huo.
CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
tena achukuliwe hatua kali,huo ni udhalilishwaji mkubwa sana,ufadhili wake usiwe kigezo cha kudhalilisha watanzania,siku hizi hata mwanafunzi hachapwi fimbo hovyo.
 
Ningependa post hii ibaki hapa hapa kwani siasa za Tanzania ni chanzo cha tatizo hili.
Alihamisi iliyopita nilipita katika shule fulani pale Dodoma, shule hii ipo maeneo ya maili mbili kule CDA, ni moja ya shule za kata. Sina uhakikwa wa jina la shule ile ila ipo karibu sana na shule ya Azimio. Anyway, nilichokuta pale shuleni mida ya saa sita ni kwamba walimu wote walikuwa wamekaa nje na wanafunzi wanapiga kelele kweli kweli madarasani. Kimsingi nilikereka na nilisema ingekuwa shule yangu ningewanasa vibao walimu waliokuwa wamekaa nje. Siasa zetu ni za kipumbavu sana. Hatuna tabia ya kuwajibika kabisa.
Kimsingi mimi namuunga mkono huyo mfadhili. Tena kama inawezekana angewatandikwa walimu wote. Fikiri tarehe 14 mwezi wa pili wanapanga ratiba! Inaingia akilini kweli? Shule za serikali zilifunguliwa tarehe 16 mwezi wa kwanza halafu walimu wakakwambia kwamba tarehe 14 mwezi wa pili wanapanga ratiba. Huu ni upumbavu! Kwa mtindo huu, nchi hii haitaendelea hata siku moja. Nimewahi kuwa mwalimu wakati wa likizo ya mkapa, kimsingi sikuwa na mda wa kusogoa na wanafunzi wangu walifaulu, tena masomo ya sanyansi. Inakuwaje walimu washindwe kuwafundisha kwa miaka minne?
Jamani tuungane kupinga udhalimu huu wanaofanyiwa watoto wetu. Tukiendelea kusema tunadhalilishwa, tutakufa na umasikini. Ni upumbavu kwenda shuleni na kusogoa! Ni upumbavu kwenda ofisini na kupiga hadithi bila kufanya kazi. Ni wizi kulipwa bila kufanya kazi. Tunaua taifa.
Acheni ushambiki huyu mwalimu alipaswa kutandikwa vibao.
 
Kwa kweli watanzania tumezidi sana uzembe.
Sio swala la kumlaumu tu Mholanzi, lakini tujiangalie na sisi tunaonekanaje?
Japanese volunteers wamekuja Tanzania kufundisha, only to be disappointed kwamba walimu hawana morale kabisa wa kufundisha, most of the time wanafunzi wanacheza darasani.

Let us look at it outside the box: ni kweli Mholanzi amekosea, lakini na sisi wenyewe tunalionaje swala hilo?
bado tunataka kutetea ujinga?
 
tena achukuliwe hatua kali,huo ni udhalilishwaji mkubwa sana,ufadhili wake usiwe kigezo cha kudhalilisha watanzania,siku hizi hata mwanafunzi hachapwi fimbo hovyo.

Nadhani hata hawa walimu wanaopanga ratiba mwezi wa 3 wachukuliwe adhabu.
 
Lazima kufikiri sana kuhusu mfumo wa elimu. Walimu wanachangia sana. Uzembe ni wa kutisha mashuleni. Si shule za serikali tu bali hata shule za binafsi. Hakuna desturi ya uwajibikaji kabisa.
 
Ukitaka kujua walimu wanatakiwa kuchapwa vibao angalia kipindi cha skonga Eatv . Watoto hawafundishwi kitu yaani ni vilaza wa kufa mtu.
 
Back
Top Bottom