Zakumi
JF-Expert Member
- Sep 24, 2008
- 5,063
- 2,471
Sawasawa, Zakumi
Labda tunapaswa kumlaumu baba wa taifa kwa system ya uongozi mbovu
tulio nao hivi leo. Lakini naomba nikuulize swali. Mimi ni baba mzazi. Nimezaa watoto, nikawalea, nikawapeleka shule, kuwalipia matumizi yao na kuwapa kila kitu walichokuwa wanahitaji. Baadaye mwanangu mmoja anageuka kuwa
jambazi. Hivi jamii itakuja kusema kuwa huyu mtoto ni jambazi na anayestahili kulaumiwa kweli ni baba yake? Tafakari. Mwalimu alifanya kila aliloweza. Alituunganisha Watanzania na kutuwekea misingi ya mshikamano. Alijenga chama imara CCM, lakini humo humo wakajiunga makanjanja akina Lowasa akina Mkapa akina etc. etc. ambao walishakiona chama kama njia ya kujipatia utajiri wa haraka. Kweli ni haki kumlaumu mzazi kwa tabia za wanae?
Kabla hatujaendelea ningependa niulize swali moja linalonisumbua. Kama Nyerere alifanya juhudi zote hizo kwanini Tanzania inakuwa kwenye ligi moja na nchi za kiAfrika zilizotawaliwa na madikiteta toka kupata uhuru ? Au kuwa ligi moja na nchi zilizokuwa kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe kwa miaka mingi?
Wewe kama mzazi unamfundisha mtoto wako basics. Akihamua kuziacha hilo shauri jingine lakini anazo basics. Na siku akihamua kujirudi basi atakumbuka juhudi zako.
Kwa leo Tanzania haina basics zozote zile. Yaani ni weupe. Basics zote alizoacha Nyerere ni archaic, pre-historic and outdated. Najua nachokoza watu hapa.