- Thread starter
- #61
Hakika wewe ndio umekuwa personal toka unaandika hojayako ya kwanza na unaendelea kusema mimi naokoteza na kudanganya nikiwafanya nyie watoto wadogo na kadhalika. Haya ni mawazo yako wewe mimi sikuja hapa kumdanganya mtu isipokuwa kuandika nachokifahamu mimi, sasa iwe wewe unaelewa tofauti ni vizuri ukituletea unachokifahamu kisha watu watapata kupima na hata kuelewa japo kidogo ukweli ni upi.Mkuu, wote hapa JF ni wakongwe wa kukata issue. Sitegemei kwamba utakwenda "personal" katika mjadala huu kama inavyoonekana kwenye mistari kadhaa ya posting yako.
Posting yako ndefu bado haituambii kwa vipi TAZARA ni miongoni mwa mafanikio ya SAS ambayo tunaweza kujivunia.
At one point kwenye posting yako unajaribu kutushawishi kwamba Nyerere alikuwa mjamaa kwa kushawishiwa na akina Babu na SAS, sijui haya umeyatoa wapi maana historia ya ujamaa wa JKN haisomeki hivyo. Nisingependa nitumbukie kwenye mada nyingine juu ya ujamaa wa Nyerere, ila ningependa sana nijuwe SAS anapataje credit ya uanzishaji wa TAZARA.
Ukweli ni kwamba huwezi kuelezea uzuri wa hata kiongozi mmoja ukitumia mifano yako kwa sababu unashindwa kuelewa wajibu wa mtu pasipo kushika madaraka fulani. Sidhani kama unajua hata key players ktk mradi wowote nchini iwe hata kujengwa kwa uwanja wa Taifa zaidi ya kumtaja Mkapa. Kwa hiyo sina muda wa mabishano, unaweza fikiria unavyoweza kufikiria lakini huna unalochangia isipokuwa kutafuta makosa ktk maandishi yangu. Kuhusiana na ukongwe wa kukata issue mkuu wangu hufanyi hivyo hata kidogo kwa sababu hadi sasa hivi hujatueleza wahusika hasa ni kina nani waliotuwezesha mkataba wa Tazara na Salim hayupo ktk list hiyo.
Kuhusiana na swala la Nyerere na Ujamaa sintaweza kuzungumza mengi lakini hata ukichukulia tu mradi wa Tazara, baada ya Nyerere kurudi toka China bado alikuwa akitafuta donors wengine kwa sababu hakuwa na uhakika na China pia kaunda hakuafiki China kutokana na siasa za nchi za magharibi (UK na USA). Na nakumbuka hata Chu el Lai alipotembelea Tanzania, bado Nyerere hakuwa na jibu kwa sababu hizo hizo.
Kwa hiyo unaweza kuendelea na kile unachoamini wewe kwamba Salim hakuchangia chochote ktk ujio wa Tazara na maendeleo ya nchi yetu zaidi ya mitumba. Na sikumbuki lini umewahi kumsifia kiongozi hata mmoja!. Nachosisitiza mimi unapopinga kitu ni vizuri uwe na data sahihi kupinga zile unazokataa sio kupinga ili mradi unapinga kutafuta kujua usichokijua.
Oooh by the way karibu sana T.O. unajua tena Caribana jumamosi usijichimbie huko njoo mjini ili tuzungumze zaidi..