What if?

Mkuu, watu walimchagua Kikwete kwa sababu alikuwa ni mgombea wa CCM na hivyo hivyo ingekuwa kwa mgombea yeyote wa CCM. Suala la Kikwete kushinda kwa kishindo hilo ni jingine na halimaanishi kwamba angeshindwa kama hangekuwa na mvuto!!!

That's why mkuu nika sema the CCM machinery builds personalities. They build personalities among the party. Angalia kama UK. UK haijalishi nani ni mgombea bali chama kipi kipo juu pindi ya uchaguzi. Angalia hata Mkapa. Mkapa hakuwa na personality yoyote ikabidi Mwl Nyerere ambae ndiyo the most charismatic leader ampige tough. I could be wrong but that's the way I see it at the moment but I am objective about myself.
 
Wakuu zangu najaribu kutazama possibilities hapa kwa akili ya kufikirika!..
Mathlan Dr.Slaa akipata mgombea mwenza na mgomea Urais wa Zanzibar kuwa Salim A. Salim (ambaye aoondoke CCM) itakuwa vipi?

Nimefikiria hili kwa sababu siwezi kuficha - I still have faith in this guy kwamba ni mwana Mapinduzi na anaweza kuondoka CCM kujiunga na ukombozi huu kwa sababu he has nothing to loose!

mmh na Mungu aweke mkono waje
 
Hatuwezi kuepuka ukweli kwamba tanzania tunachagua vichwa. CCJ haikutisha mtu yeyote kama chama isipokuwa zile tetesi za kuingia vichwa kutoka CCM. Nakumbuka vizuri nikiwa Bongo kishindo cha habari hizi kilivyoweza kutembea haraka hadi baadhi ya viongozi hao kuwekwa kitimoto na kuulizwa kama kuna ukweli ktk tetezi hizi. Ilisadikika kwamba Salim, Butiku, Warioba na watu wote wa mfuko wa mwalimu wataingia huko, wale wapiganaji pia wataingia huko na alipojitoa Mpendazoe ndipo uhai mpya wa CCJ ukaanza kusambaa zaidi.. hii ni kabla Mwanakijiji kuja hapa na kuzungumzia kwa undani itikadi na sera za chama hiki.

Na sii kweli labda watu walizipenda sera za CCJ zaidi ya Chadema,CCNM au NCCR isipokuwa vichwa pinzani ndivyo viliwapa wa tu tumaini..kwa maana kwamba Tanzania ili kushindana na CCM inatakiwa uonyeshe uwezo wa pambano lenyewe kama alivyosema Rev.Kishoka katika mada fulani kwamba uchaguzi wa Tanzania ni sawa na mashindano ya ndondi ambayo ni lazima Bondia wako awe na uzito sawa na ranked as a contander.

Huu ni mtihani mkubwa sana nakama alivyosema Mwanafalsafa1, huu ni mtihani kwetu sote hata kama sisi tunatofautiana ktk mtazamo wetu na wananchi wengine. Tukubali usemi usemao - Wengi WAPE na hakika Dr.Slaa ana kila sifa zaidi ya JK isipokuwa hizi mila zetu za kuchagua viongozi kwa rangi zao na kuhofia upande wa pili watasema nini ndio inatulazimu kutazama pembeni.

Bila shaka Hamad anaweza kabisa wakilisha nafasi hiyo with no doubt anaweza mpiku Bilal na hoja sio bara haswa kwani hata huyo Bilal sii maarufu Bara wala Shein na wote waliotangulia kina Jumbe na mwinyi hakuwa maarufu.. Hoja ya msingi ni kwamba unapopigana na Gozilla CCM inatakiwa uwe na Arsenals za uhakika, na Dr.Slaa peke yake bado anahitaji nguvu zaidi iwe kuna ukakika wa ushindi mkubwa ambao hata CCM wakiiba kura kama kawaida yao itabidi washindwe kusafisha ushahidi ktk mikono yao.
 
.............................mimi ningefurahi zaidi kuona Dr. Slaa anaunganisha nguvu na Maalim Seif. Ndugu yetu Prof. Lipumba akae pembeni. Kura zote za CUF kwa mgombea wa Urais wa Jamhuri ziunganishwe na kura za CHADEMA nadhani moto wake utakuwa sio mdogo..............


hayo juu ndio maneno............
 
Wakuu zangu najaribu kutazama possibilities hapa kwa akili ya kufikirika!..
Mathlan Dr.Slaa akipata mgombea mwenza na mgomea Urais wa Zanzibar kuwa Salim A. Salim (ambaye aoondoke CCM) itakuwa vipi?

Nimefikiria hili kwa sababu siwezi kuficha - I still have faith in this guy kwamba ni mwana Mapinduzi na anaweza kuondoka CCM kujiunga na ukombozi huu kwa sababu he has nothing to loose!

Hili wazo hata mimi limenijia aisee.. Japo lina vizuizi vikubwa vitatu:

a. SAS itambidi awe tayari kulipa gharama ya kusupport upinzani dhidi ya "chama chake". Tatizo hli litavunjwa endapo baadhi ya wakongwe wengine kama Warioba, Butiku, Sozigwa na wengine wataamua kumuunga mkono.

b. Mchezo mchafu wa 2005 utarudiwa dhidi yake; hili litaweza kushughulikiwa endapo na yeye hatokubali kuwa victim tena.

c. Nafasi yake kimataifa itadhurika vipi. SAS ni sura ya Tanzania kwa muda mrefu katika medani za kimataifa; kwa kusupport upinzani itakuwa ni kama Al Baradei aliyekuwa IAEA na wa Misri. Inahitaji ushujaa sana kwenda kinyume na serikali ambayo unaweza kuicredit kuwa ndiyo imekufikisha ulipo.

Akiweza kuovercome hayo matatu.. na matokeo yake Dr.Slaa/Salim tiketi itashinda vizuri tu.. ila kwa hakika itaipa CUF Zanzibar.
 
Wakuu zangu najaribu kutazama possibilities hapa kwa akili ya kufikirika!..
Mathlan Dr.Slaa akipata mgombea mwenza na mgomea Urais wa Zanzibar kuwa Salim A. Salim (ambaye aoondoke CCM) itakuwa vipi?

Nimefikiria hili kwa sababu siwezi kuficha - I still have faith in this guy kwamba ni mwana Mapinduzi na anaweza kuondoka CCM kujiunga na ukombozi huu kwa sababu he has nothing to loose!

Nahofu endapo Salim ataamua kuihama CCM si ajabu baada ya siku kadhaa kabla hata ya uchaguzi ukasikia amevamiwa na majambazi na ameuwa (Mungu apishilie mbali).
"Ndoa" ya CCM kuivunja hasa kwa mtu muhimu kama Salim inabidi ujipange sana.
 
Hili wazo hata mimi limenijia aisee.. Japo lina vizuizi vikubwa vitatu:

a. SAS itambidi awe tayari kulipa gharama ya kusupport upinzani dhidi ya "chama chake". Tatizo hli litavunjwa endapo baadhi ya wakongwe wengine kama Warioba, Butiku, Sozigwa na wengine wataamua kumuunga mkono.

b. Mchezo mchafu wa 2005 utarudiwa dhidi yake; hili litaweza kushughulikiwa endapo na yeye hatokubali kuwa victim tena.

c. Nafasi yake kimataifa itadhurika vipi. SAS ni sura ya Tanzania kwa muda mrefu katika medani za kimataifa; kwa kusupport upinzani itakuwa ni kama Al Baradei aliyekuwa IAEA na wa Misri. Inahitaji ushujaa sana kwenda kinyume na serikali ambayo unaweza kuicredit kuwa ndiyo imekufikisha ulipo.

Akiweza kuovercome hayo matatu.. na matokeo yake Dr.Slaa/Salim tiketi itashinda vizuri tu.. ila kwa hakika itaipa CUF Zanzibar.

MM, hapo kwenye blue ni ukweli mtupu, na si kwa SAS tu bali hiki ni kikwazo wa wengi tu wakiwemo kina Warioba na wengineo. Huwezi kukikimbia chama na serikali yake iliyo kulea miaka yote na mafanikio uliyonayo, utakachoshauriwa ni kukisosoa chama na serikali yake na si vinginevyo.

Hata mi naunga mkono mada, lakini ki uhalisia ni vigumu mno jambo hili kutokea. Kwa kuongezea juu ya hili pia ningependa sana Prof Lipumba ange step down kugombea urais na badala yake akagombee ubunge kwao Lolanguru basi Nafasi ya DR slaa ingekuwa kubwa mno.

Pia wao CHADEMA wakubali kuisupport CUF zanzibar uwezekano wa CUF Zanzibar kuwa na serikali ya mseto hata kushinda uchaguzi ingekuwa kubwa zaidi.

Najua haya yote yameshajadiliwa humu na yana vikwazo vingi tu vya kisiasa, lakini hawa viongozi wakumbuke sisi wananchi wa kawaida tusio wanachana wa chama chochote tungefurahi mno kama yangetokea.

CUF unga mkono CHADEMA - BARA
CHADEMA unga mkono CUF - Zanzabar
 
Wote mnashangaza! Kwa nini mnafikiria SAS atoke CCM ajiunge na Dk Slaa ili apate umakamu? Chadema itafaidi sana jama itafanya utafiti mzuri na kuibua Mzanzibari ambaye ana vision na anayependa sera za Chadema. SAS atakuwa CCM mamluki ndani ya Chadema - kumbuka "you cant teach an old dog new tricks" Nawashauri wana Chadema wasiwe na papara kuatafuta mtu CCM wa kununua. Bora kabisa atoke upinzani in which case Hamad is better.
 
Mimi nadhani kila kitu kinawezekana, japokuwa kama wengi wanavyosema, si rahisi sana kwa Dr. Salim kutoka CCM. Dr. Salim si mtu anaeonekana kama anaweza kufanya maamuzi magumu kama hayo. Ni mtu ambae anaridhika na kuridhia matokeo hata kama yana maumivu kwake.

Kama ingewezekana hisia hizi zikamfikia, nae akaona anaweza kuzifanyia kazi, nadhani ingekuwa jambo jema sana kwake na kwa Taifa kuchukua hatua ya kuungana na Dr. Slaa kama mgombea mwenza. Ila kwa hali ilivyo, nahisi ni vigumu hiyo kutokea kwa sababu zifuatazo;

1. Inawezekana sana kuwa Dr. Salim bado anaimani kuwa mambo yanayotokea kwenye CCM sasa ni ya mpito tu. Kitu ambacho si kweli. Huko tuendako mambo yatakuwa mabaya zaidi, na wenye nia njema na nchi watajilaumu kwa kutochukua hatua za mabadiliko mapema zaidi.

2. Dr. Salim bado anajisikia na kuamini kuwa ni sehemu ya uongozi wa CCM. Hii inaweza kuwa kweli, lakini itabaki hivyo kwa muda mfupi sana.

3. Dr. Salim anaweza kutokuwa na uhakika na sera, nia, imani na madhumuni ya vyama vya upinzani kiasi cha kutoweza kuchukua hatua za haraka kuhama na kujiunga na CHADEMA ili kuweza kushirikiana na Dr. Slaa kupata ushindi wa kishindo. Hii inaweza kuwa sababu kubwa zaidi ya yeye kuona ni afadhali zimwi likujualo ambalo halikuli likakwisha.

Kwa mtazamo wangu, Dr. Slaa ni mgombea mwenye nguvu sana kutoka upinzani. Anatosha kuweza kusababisha upungufu mkubwa wa kura za CCM kwenye uchaguzi mkuu ujao. Ila akipata watu kama Dr. SAS, atakuwa na uhakika mkubwa sana wa kushinda uchaguzi mkuu ujao. Sina uhakika kama CHADEMA wanataka kufanya hivyo (kwasababu nao ni sehemu ya mafanikio ya hili) na wala sina uhakika kama Dr. Salim anaweza kuchukua hatua kama hiyo kwa muda huu (maana yeye ni sehemu kubwa zaidi ya mafanikio hayo).
 
Mzee Mwanakijiji,
Nakubaliana na hoja zenu sana tu lakini sii kweli kwamba viongozi wote wa kiafrika Wapinzani waliochukua uongozi wa nchi hizo leo hii wametoka chama tawala kilichowalea wote?..Iweje iwe rahisi kwa wale wa nchi nyingine tena hatari zaidi ya Tanzania wameweza kuunda Upinzani wa ghafla na wakapata sifa za ushindi tushindwe sisi kwa kuhofia joto la CCM.

Je, huoni kama CCM wamefanikiwa kutembeza FEAR miongoni mwetu kiasi kwamba tunatawaliwa kwa Woga badala sisi na hao kina Salim kukaa na kufikiri kwamba inawezekana. Why I'm doing this? nataka kuwapa challenge Chadema wafanye approach hii kwa sababu wakati ni sasa hatuhitaji kusubiri..

Nilipokuwa Bongo nilifanikiwa kuonana na mshikaji ndiugu yake Paul Sozigwa huwezi kuamini jinsi serikali yetu ilivyomtelekeza mpiganaji huyu sasa itakuwa maajabu ya Mussa mtu kama huyu kubakia royal kwa chama kilichobakia jina baada ya mwalimu kututoka. Ni mgonjwa sana hana uwezo na CCM chama kilichomlea wamemtelekeza. Wapo watu wengi sana toka viongozi wa wizara, idara na taasisi za serikali kama Usalama leo hii wana maisha magumu huwezi kuamini. Hawa wote hawana la kupoteza kwani maisha yao kisiasa tayari yameisha fikia ukingoni.
 
Dr Salim anaweza kufanya hivyo but he wont kwa kuwa umri umeimbia sasa na si yule tena wa kuanza kuimbizana na kujikinga na siasa chafu za ccm sasa.

Anahitajika mtu kijana zaidi na watu wakiungana kupiga kampeni yoyote anauzika tu........
 
Wakuu zangu najaribu kutazama possibilities hapa kwa akili ya kufikirika!..
Mathlan Dr.Slaa akipata mgombea mwenza na mgomea Urais wa Zanzibar kuwa Salim A. Salim (ambaye aoondoke CCM) itakuwa vipi?

Nimefikiria hili kwa sababu siwezi kuficha - I still have faith in this guy kwamba ni mwana Mapinduzi na anaweza kuondoka CCM kujiunga na ukombozi huu kwa sababu he has nothing to loose!

Guys,am repeating again,hii mijadala kama hii lengo lake ni kupoteza fikra za Wa Tanzania kwa tumain jipya la ukombozi wa Tanzania,Dr Slaa,sioni kwanini tuanze kufikiri vitu ambavyo kimsingi ni vigumu kutokea ilhal tunavyo ambavyo tunaweza kuvipangia mikakati na kunafaika navyo,namaanisha Dr Slaa,kwanini tuanze kumuota Dr Salim,its fact,ni mtu makin,lakin fikra za mkandara si kama ndoto za alinacha,so why should we spent time discuss about dreams while facts zipo????
Ntarudi tena baadae
 
..Salim na Warioba ni waoga.

..hata kwenye lile kongamano ambapo Butiku na Mateo Quares waliamua kubwatuka wao[salim na warioba] waliamua kuwapooza-poza.

..mnaotaka Dr.Salim aungane na Chadema, mnaukakika kwamba ataweza kuikosoa CCM na sera zake kwa moyo na ujasiri uleule alionao Dr.Slaa?

NB:

..tena na hivi mnavyosema-sema hapa msije mkashangaa Dr.Salim anatokezea kwenye mkutano wa kampeni na JK na kutambulishwa.
 
Mada hii inanikumbusha adithi ya fisi mwenye njaa aliyekuwa anamfuata mkulima alfajiri akizani mikono ya mkulima itadondoka ili apate mlo. Tofauti na JF, fisi kwa sababu ni "fisi" hakuwa na akili na utashi wa kumwomba mkulima mkono. JF tuna akili na utashi pamoja na mapenzi kwa taifa letu....lakini kama alivyofanya fisi, tunashindwa kumwomba Salim A Salim aondoke CCM, badala yake tunashinda kupiga ramli.
 
Kiranga,
Mkuu unaposema toe to toe una maana gani? ebu nipe jina la mtu yeyote Tanzania ambaye mimi siwezi kwenda toe to toe na wewe!..mkuu hakuna binadamu asiyekuwa na mapungufu lakini pamoja na yote haya Salim - stand on his own.. Hakuna mwakilishi wetu hata mmoja aliyeweza kupata Umaarufu duniani zaidi yake akiwa waziri wa mambo ya nje, UN na hata OUA toka tumepata Uhuru. Pima kwa nafasi moja moja au zote kwa ujumla wake hata Nyerere mwenyewe alihofia uwezo wa Salim.
Ukisema chuki binafsi hizo zinakubalika popote!

Hili ndilo tatizo letu wabongo, tunapima mafanikio ya mtu kwa nafasi alizoshika bila kusema alifanya nini cha maana katika nafasi hizo.

SAS amefanya nini hasa cha kumtofautisha na hawa viongozi wetu run of the mill ? Angekuwa mjanja angeshindwa karata na huyu buffoon Kikwete ?

Hizi mentality ndizo zinazodumaza upinzani, watu wanaona kama hawawezi kupata mafanikio bila kuchukua makombo ya CCM.
 
Chuki binafsi nazo huwa na matatizo yake! It seems Dr. Salim stepped on your toe at one point or another. Lakini tukichukulia historia yake kama kiongozi wa kitaifa na kimataifa aliyoianza tangu ana umri wa miaka 22, nani anayeweza kumshinda Salim kwa uwezo na uzoefu wa kuongoza?

Chuki pekee ninayoiona hapa ni kukimbilia kusema chuki bila hata kujadili masuala. Mimi simjui Salim on a personal level kumchukia like that, na aliondoka Tanzania kwenda OAU kitambo, na alivyorudi hajawa active sasa chuki yangu itoke wapi? Mimi si mwanasiasa. Hivi ni haki mtu mkitofautiana kisiasa kitu cha kwanza kusemwa kiwe chuki? Wote wanaomsema Kikwete hapa wana chuki binafsi naye?

Majibu yako yanazunguka pale pale tunapoangukia Watanzania wengi, eti unanitajia miaka yake ya uongozi, unaweza kuwa kiongozi milele lakini kama huna results huna results tu, na SAS hana results za kuonyesha.

Kama unabisha nionyeshe results zake ziko wapi. SAS ni sehemu ya matatizo ya nchi yetu na kamwe hawezi kuwa sehemu ya solution.

Mkitaka wapinzani waonekane jokers mchukueni huyo SAS.
 
SAS amefanya nini hasa cha kumtofautisha na hawa viongozi wetu run of the mill ? Angekuwa mjanja angeshindwa karata na huyu buffoon Kikwete ?

Hili swali hata mimi nimeshindwa kupata jibu...tusipojibu swali hili tunakuwa upande wa pili wa sarafu tuliyoitumia kumuhukumu Kiranga: mapenzi binafsi.
 
Kiranga,
Kiranga ukizungumzia position za madaraka hapa nchini nitakubaliana na wewe kwani hazina vigezo vyovyote isipokuwa unyenyekevu..lakini kimataifa huwezi kupanda wala kupewa nafasi za juu moja hadi nyingine pasipo kufanya cha maana. Wewe fuatilia uongozi wake na mchakato wa hoja zilizokuwepo wakati akiwa ktk nyadhifa hizo utaona ni kwa kiasi gani alifanikiwa..Kufanikiwa ndicho cha maana na huwezi kumlinganisha na kiongozi yeyote Bongo walioipita - that one nakuhakikishia.

Haya ya kusema kushika position sio kitu isipokuwa kile cha maana alichokifanya nadhani cha msingi ni Kujiuliza ni position gani aloshika na akaharibu kwa sababu cha maana kwangu kinaweza kuwa sii muhimu kwako.
 
Kama Watanzania bado wanafikiri ukombozi utatoka kwa akina Salim, Warioba, Butiku et al bado safari ni ndefu sana. Hii ni mizoga ambayo imeshindwa mapambano kwenye Chama Cha Majambazi itawezaje kuwa mahiri kwenye karne ya internet? Tweetering, facebook etc.

Chama Cha Majambazi kina kila dalili ya kushindwa kama Watanzania watasimama kidete na kusema Tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumedhalilishwa kiasi cha kutosha asiye na mwana aeleke jiwe na kumwambia kila ndugu na jamaa usiwape kura Chama Cha Majambazi kinachoongozwa na Jakaya Kikwete. Hawa ni wasaliti na endapo ingekuwa China wangenyongwa wote.
 
Mkandara please badili hii mada na tu discuss ukombozi wa nchi yetu kupitia "Th Black Messiah" Dr Slaa,kuanza kupiga Ramli za SAS kuja Chadema...sijui nini mi naona haina mashiko sana kujadili Ndoto na wishes ambazo kimsingi ni vigumu sana kuwa true,lets us face kile ambacho tunaweza kukifikia...Nadhan mkandara,mwanakijiji,Steve D,Joka kuu,Gender Sensitivity,Game theory (Ingawa simsikii nowdays) NA WENGINE WOTE WENYE UWEZO MKUBWA WA KUJENGA HOJA,ITS HIGH TIME NOW,UNLESS MUWE MNATUMIWA....
 
Back
Top Bottom