...Unaifahamu nchi yako vizuri? nani kakwambia wameshindwa kupeleka?
...Unavijua vikwazo vilivyopo kwenye biashara ya chakula nchini? Ukiondoa ada mbalimbali, kuna ubovu wa miundo mbinu pia.
...Labda nikujulishe kidogo. Biashara hufanyika pale inapoleta au kutengeneza faida zaidi. Kama unafahamu vizuri. Wafanyabiashara hawa walipangiwa mpaka bei ya kuuza hayo mahindi. Nikuulize, unafikiri hiyo bei inavutia wao kupeleka mahindi sehemu ambayo hawatapata faida?
...Kwa taarifa yako, kuna hali ya soko kuingiliwa kisiasa kwa kiasi kikubwa na hii ndio inayoondoa maslahi ya kufanya biashara hiyo katika baadhi ya maeneo nchini.
...Narudia tena, tatizo sio uwekezaji wa nje kukosekana na biashara hii hatuhitaji mwekezaji toka nje. Tatizo ni kuingiliwa kwa soko.
Kama umenisoma vizuri post yangu ya mwanzo niliorodhesha matatizo ya nchi hii kama ifuatavyo
Mwanakijiji,
Unakumbuka tulikuwa na debate 2009 kuhusu hali ya kiuchumi ya Tanzania na muelekeo wake. Nikasema uchumi wa Tanzania kwa miaka ijayo kama ukikua sana ni asilimia 4.5%. Uchumi wa nchi unamatatizo na kikubwa ni watu wanaendekeza siasa zaidi ujuzi wa watu. Kuna mambo niliyataja mwaka juzi yanasababisha uchumi wetu kuyumba:-
a. Umeme:
Tatizo la nishati la umeme limechangia kwa kiwango kikubwa kuua uchumi wa Tanzania. Hilo ni kwasababu nishati hii imepotea na hivyo kusababisha uzalishaji wa vitu nchini na huduma nyenginezo kupanda bei maradufu. Na kuchangia ukuaji wa mfumuko wa bei na kuyumba kwa uchumi.
b. Miundo mbinu mibovu:-
Barabara, foleni, mipango miji mibovu vyote vimechangia kuongezeka kwa gharama za maisha na kuyumba kwa uchumi. Mkulima anaona bora auze mchele na sukari nje ya nchi kuliko kuleta Dar kwasababu barabara mbovu. Kama umeangalia statistics za September inflation ya vyakula iko juu kuliko inflation ya vitu vyengine. Sababu kuu ya hayo ni kwamba inflation ya chakula ndio inajumuisha basket of michele, sukari nk. Mchele wa rukwa na mbeya sasa hivi unazidi mchele kutoka pakistan kwa bei. Matokeo yake ni kuongeza importation kuliko kutumia michele ya hapa nchini. Vile vile mipango miji mibovu inachangia ukuaji wa gharama za maisha. Vitu kama foleni za barabara zinamuongezea gharama za maisha mlalahoi kwani vitu kama usafiri wake wa kila siku vinakua maradufu.
c. Ufisadi.
Ufisadi unarudisha nyuma uchumi wa nchi yetu. Hivi sasa ufisadi unatafuna zaidi ya 20% ya GDP na tatizo linakuwa kila mwaka. Hilo linachangia kuzorota kwa shughuli za uzalishaji, an increase in purchasing power of households (maana matajiri ambao ni wafanyakazi wa serikalini na taasisi nyenginezo wana pesa za kuchezea), kuongezeka kwa gharama za maisha.
d. Dollarisation.
Hii nimeshaielezea katika thread hii hapa
https://www.jamiiforums.com/habari-...bot-3-key-policies-to-rescue-shillings-3.html
e. Kuanguka kwa shillingi na athari zake kwenye gharama za maisha. Nimeshaielezea hapa.
https://www.jamiiforums.com/habari-...bot-3-key-policies-to-rescue-shillings-3.html
f. Ukopaji wa serikali usiokuwa na mpangilio.
Serikali yetu inakopa kwa kasi ya ajabu na hakuna mtu ameliangalia kwa uangalifu. Thread moja nilianzisha ya kuorodhesha madeni ya serikali inasemekana deni la serikali ni karibia Trilioni 15 je kuna mtu analijua hilo??? Trilioni 15 inamaanisha kila mtanzania analipa si chini $214 sawa na Tshs 385,200. Bado hujaiangalia level of interest charged for the debt. Na deni linakuwa kwa kasi kwani kama tukifanikiwa kuuza Eurobonds za $500 Billioni our national debt litakuwa karibu Tshs Trilioni 800. Kuna hatari tukawa kama Greece kama hatujawa waangalifu. Zaidi kuna thread nilianzisha kuhusu deni la taifa hii hapa taarifa utaziona zaidi:-
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-na-ndani-na-uwezo-wa-nchi-yetu-kuyalipa.html
Ni vema ukopaji huu ukadhibitiwa na bunge kuzuia nchi kufilisika kwani kasi hii ni hatari kwa mustakabali wa nchi hii.
g. Ukubwa serikali na bunge:
Serikali yetu inajibebesha mizigo isiyokuwa na maana na ukubwa serikali unaliumiza taifa. Tusipokuwa waangalifu tunaelekea kuwa kama ugiriki ambapo uchumi wa nchi unategemea wafanyakazi wa serikali. Serikali inahaja kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali yake kusave pesa. Manunuzi ya Magari ya ghali, gharama zisizo na umuhimu na safari za viongozi zisizo na ulazima vinahitaji kusimamiwa. Vyenginevyo ni mzigo kwa taifa.
h. Vyanzo finyu vya kodi. Tuweni wakweli watanzania hasa waliopo katika sekta kujiajiri wengi hawapendi kulipa kodi. Kumekuwa na mianya mingi ya kukwepa kodi na kutokulipa kodi. Mfano biashara za upangishaji nyumba zimekuwa zikiachwa watu hawalipi kodi. Wafanyabishara wa kati na wakubwa wengi hawalipi kodi (including Vodacom). Kuna haja kuongeza vyanzo vya kodi.
i. Tofauti kati ya matajiri na maskini na kupotea tabaka la kati nalo limechangia.
Hayo mwanakijiji ndio matatizo ya nchi yetu. Nilikuwapo!!!
Hata hivyo suala la kuruhusu wawekezaji kutoka nje kuja kuwekeza katika ardhi yetu ni la umuhimu kwa mazingira tuliyonayo sasa. Wafanyabiashara wamepangiwa kuuza bei kwa vile bei wanazouza haziendani na uwezo wa mtanzania kununua. price ceiling ina faida kama hizo ila sio jambo zuri ni vema waboreshe usambazaji wa vyakula nchini.
Wawekezaji wa nje wanauwezo wa kusaidia kutatua hilo na pia kuongeza pato la nchi hii. Fikra kama hizi za kwako zishapitwa na wakati ndugu serikali haiwezi kuwa kila kitu inafanya itashindwa kama ilivyoshindwa kipindi cha nyerere kwasababu government expenditure itakuwa kubwa. Wawekezaji wanasaidia kupunguza tatizo la vijana wasio na ajira nchini, wanaongeza kodi na kusaidia bei za vyakula kushuka.