What can be done to prevent our economy from collapsing?

Kikwete aache visasi na chuki za kiasiasa,ukweli ni kwamba Mkullo na Ndulu wameshindwa ku-deliver and they should be ejected.Dr. Kigoda apewe wizara ya fedha na pia kikwete angeweza kumsogeza ata Prof. Mbilinyi hawa wangemsaidia sana kuliko kung'ang'ania watu waliofeli ku-deliver.

Kisheria Ndullu hawezi kufukuzwa na Raisi ninavyokumbuka na hata akimwomba ajiuzulu kistaarabu hii inaweza kusababisha matatizo makubwa zaidi maana watu watazidi kupoteza confidence na BOT mbayo itasababisha shillingi kuporomoka zaidi.
 
hata mimi nahisi hili. Uchumi wetu unahitaji kusahihishwa au kujisahihisha kwani ulivyo sasa ni unsustainable. Swali litakuwa ni maumivu kiasi gani yatatokea ili tutoke hapa.
...Kuna mambo mengi sana yanayochangia uwepo wa hali hii, ambayo ni mbaya na itakayotupeleka pabaya zaidi ya hapa, huu ni mwanzo tu.

...Pamoja na kuwa na baadhi ya sera ambazo ni nzuri na hazisimamiwi au kutekelezwa, kwa kuwa watu wakubwa wanataka kutolipia gharama au wanapenda bure, tumeshindwa kuweka sera nyingine za maksudi ambazo zingeleta nafuu kubwa kwa uchumi wetu. Mathalani, kupunguza utegemezi na ununuzi wa bidhaa kadhaa toka nje ambazo kuna uwezo uliopo au unaoweza kujengwa wa kuzizalisha nchini. Ziko nyingi, unaweza kuzitambua.

...Kuna kansa kubwa ya kutowajibika, kutumia akili, na kufanya kazi yenye tija na inayoleta maendeleo kwa taifa na kunufaisha wananchi. Watu hawafikirii kuendeleza miundombinu; bahati nzuri tunaijua. Hawafikirii kuendeleza raslimali watu; ambayo kwa dunia ya leo ndio tegemeo kuu la nchi yeyote. Huwezi kuwa na uchumi mzuri kama watu wako hawana lishe, elimu hitajika ya kujikwamua kimaendeleo, afya yao ni mgogoro na hawajatulia kuweza kuzalisha mali. Kila siku wanahangaika kutafuta chakula, kwa kufanya hili, kuliacha na kufanya lile na kutopata faida yeyote.

...Nchi yeyote yenye kuhitaji kujikwamua kwenye umaskini, lazima iwe na viapaumbele vikuu vichache kwa wakati na mtazamo unaolenga kulikwamua taifa unaotekelezeka na wenye kusimamiwa, na sio maneno matupu yasiyo na mantinki kiutekelezaji. Mathalani, umeamua kupunguza umaskini, je?, ni mambo gani yanayowaletea umaskini watu wako? Ni elimu? Ukosefu wa ardhi? Kutokuwepo viwanda? Ugumu wa kupata mikopo; na sio mitaji, kwa maana tunayo mingi, kilichobaki ni kujua namna ya kuifanya iweze kutumika. Au, ni ukosefu wa chakula? Je, miundombinu ndio kikwazo? Maana, tumeona jinsi ukosefu wa umeme na barabara mbovu jijini Dar zinavyokwamisha shughuli za uzalishaji, biashara na maendeleo.

...Sasa, hivi vitu vyote vinahitaji uongozi makini, usio na ubinafsi au ulafi na unaopenda utaifa wake kwa vitendo. Kama kiongozi, unahitaji kufahamu matatizo ya watu wako, kujua au na kutafiti nini cha kufanya, kwa wakati gani, kwa kuwatumia kina nani na kwa gharama gani. Kazi kubwa ya kiongozi ni kusimamia na kufuatilia matokeo ya mwisho. Wajibu wake mkuu ni kuona mambo yanaenda sawa, kama ilivyotegemewa.

...Tatizo kuu la uchumu huu ni matumizi makubwa, yanayohusisha fedha za kigeni. Uzalishaji mdogo wa ndani na uagizaji mkubwa wa mali toka nje. Hivyo, hata kufanyike nini, shillingi itashuka thamani kila siku. Majuzi, sera ya fedha imetumika kupunguza makali ya kushuka thamani shillingi. Hata hivyo, hii haitafua dafu, kwani mhalifu ni sera ya matumizi na mapato. Matumizi makubwa kuliko mapato. Hatari zaidi ni hela chafu kusafishiwa kwenye uchumi huu ulio hoi; kunakuwa na ongezeko la matumizi ambayo hayatokani na mapato ya uzalishaji katika uchumi huu.

...Watu wamelala, wanahitaji kuamka na kutekeleza majukumu yao; tatizo ni kama wataamka mapema vya kutosha.
 
wanasema raisi alisomea uchumi je? Kwanin uchumi unashuka?

Mipango mizuri isiyotekelezeka.

Kashfa za ufisadi ni mingi kuliko mipango ya kuikombo tsh.

We subili mwishoni mwa mwaka rais huyo huyo atakapo kwambia uchumi wetu umekua kwa 18% ndipo utakapo shangaa
 
Kikwete aache visasi na chuki za kiasiasa,ukweli ni kwamba Mkullo na Ndulu wameshindwa ku-deliver and they should be ejected.Dr. Kigoda apewe wizara ya fedha na pia kikwete angeweza kumsogeza ata Prof. Mbilinyi hawa wangemsaidia sana kuliko kung'ang'ania watu waliofeli ku-deliver.
...Umewahi kujiuliza kama kutokubweka kwa mbwa ni ukoko wake au uzembe wa mwenye mbwa kumshindisha njaa na kumnyima mazoezi na mahamasisho? Hii inahusiana na Prof. Ndullu.
 
We subili mwishoni mwa mwaka rais huyo huyo atakapo kwambia uchumi wetu umekua kwa 18% ndipo utakapo shangaa
...Tatizo si kukua kwa uchumi, bali ukuaji huo umetokea katika sekta ipi au zipi? Kama ukuaji upo katika sekta ya madini na utalii, unafikiri mwananchi wa kawaida hasa anyeishi mbali na maeneo ya migodi na utalii, ataona manufaa yeyote?
 
Mimi walipo issue new currency notes in January while maintaining the old ones nilijuwa tayari mambo yeshaenda mrama ........na zaidi ya kununua hiyo nyumba kwa $24m na hisi Dowans wamelipwa kimyakimya

Na mbaya zaidi ilikuwa tu baada ya matumizi makubwa ya pesa kwenye uchaguzi. HApo ndo ujue BOT na CCM wao wote hovyo kabisa. Imekula kwetu. Mpaka tushilke adabu.
 
Huwezi kuendesha gari bila kujua unakwenda wapi, kufanya hivyo unaweza kujikuta unazunguka siku nzima mpaka mafuta yanaisha!. Mkapa alipoingia aliandaa Vision (2025) na akaandaa mkakati wa kufikia kufikia vision (MKUKUTA). Na kitu kikubwa alichozingatia Mkapa wakati wa utawala wake ni Fiscal descipline'. Baada ya miaka mitano Ikulu Kikwete amekuja na mpango wa maendeleo 2011 -2016. Lakini haieleweki kama mipango ya serikali inaongozwa na MKUKUTA au huu mpango mpya wa maendeleo! Na kama tuko kwenye mpango mpya MKUKUTA umekufa? Au MKUKUTA ulikuwa na kasoro gani hadi tukawa na mipango miwili? Kwa nini wasiboreshe MKUKUTA na mipango yote ya serikali ikawa under a single development-framework?


Sasa hivi ni vigumu sana kujua Tanzania inataka kuwa nchi ya namna gani! Ni nchi ya kilimo au ya viwanda?. Common sense tu inatosha kukuongoza kuwa kama unataka kuwa nchi ya i.e kilimo au viwanda unaandaa mipango itakayo beba 'population' ili waweze kutimiza hiyo mipango. Kwa mfano kwenye shule zotu tunaandaa watoto wa kitanzania wawe kitu gani?

Lingine, uchumi wa Tanzania umerudi kuwa 'black market'.Too much money circulating outside 'formal system'. Tunategemea misaada kulipa mishahara, kununua vitafunwa. Hakuna hela ya kuwekeza kwenye development programme i.e kujenga barabara. Wawekezaji wanakwepa kulipa kodi, wananchi nao hawako kwenye system ya kulipa kodi. Nchi inaendeshwa na Uncle Sam.
 
Na mbaya zaidi ilikuwa tu baada ya matumizi makubwa ya pesa kwenye uchaguzi. HApo ndo ujue BOT na CCM wao wote hovyo kabisa. Imekula kwetu. Mpaka tushilke adabu.
Tuta endelea kuimba nyimbo za Komba"......wembe ni ule ule ushindi, ..........sisiem nambari wani, ........wapinzani tuwachane chane tuwatupe, ........Kiwete wetu anameremeta oye oye oye. Tanzania inawenyewe na wenyewe ni CCM." Kudadadeki walah!
 
Sio siri uchumi wa nchi unaelekea pabaya sana kuliko nyakati zote ulipopitia na sioni jitihada za dhati za kuokoa thamani ya uchumi wetu usizidi kushuka. Last week nilisikia central bank wamechukua hatua lakini hali ndo inazidi kuwa mbaya na kwa taarifa za ndani nimedokezea kuwa hata leo central bank itakuwana na wadau wa mabenk yote kuangalia namna ya kufanya kuokoa jahazi ila sijui kama hili nalo litapita soon tutajikuta tupo kama zimbambwe
 
Unajua sometime unabaki unacheka, naibu waziri anajinadi tumezuia uuzwaji wa sukari nje ili bei ishuke wakati bei haishuki. Mimi naona bora tungewaachia wafanya biashara wauze ili walau tupate hivyo vijipesa. Nchi gani mnanunua tu nyie hukana mnacho uza nje hizo foreign currency mtazipata wapi ili muweze kuagiza hivyo msivyo zalisha. Nyerere aliweka viwanda sisi tumeviuza. Urafiki sasa wanauza Magari ya Foton, Zana za kilimo ubungo wanauza mabomba ya maji............................... Seriously sijui wasomi wa nchi hii tunafundishwa kuja kufanya nini when we are entitled with madaraka.
 
Hivi huu tunaouita uchumi wetu bado upo kweli au ulisha collapse siku nyingi? Labda swali lingebalika na kuwa how can we resuscitate our collapsed economy? Viashiria kuwa uchumi umekufa na unahitaji kufufuliwa ni:-

(i) Uzalishaji viwandani kupungua kwa sababu ya ukosefu wa umeme;
(ii) Mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa na gharama za maisha;
(iii) Kupungua kwa makusanyo ya kodi za serikali;
(iv) Serikali sisiyoweza kulipa gharama za uendeshaji wake na kutegemea misaada/mikopo;
(v) Mgao endelevu wa umeme unaoathiri siyo tu shughuli za viwandani bali hata biashara ndogodogo;

Wachumi wanisaidie ni viashiria gani vingine zaidi ya hivyo hapo juu vinavyotuambia kuwa uchumi wetu umekufa.

Wameua reli ya kati na kudhoofisha TAZARA kwa makusudi ili maroli yao machakavu yatawale barabara. Huwezi kusafirisha bulk freight kwa barabara, the result is catastrophic!! Nachi zote za magharibi hazijawahi ku-ignore reli... Bandari ndo hivyo tena ina msongamano kuzidi wa barabarani. The port is never efficient, efficiency huwa ni ya msimu, mpaka mkulu atembelee....

Chronic desease of electricity, peasant farming; serikali haitaki kabisa kufungua productions in agriculture, revolutions ya kilimo hawaitaki kabsa; jusr because hina maslahi ya harakaharaka katika kukwapua fedha, tunahanghaika na kuchimba uranium.... ambayo nina uhakika hatuko tayari....

Rushwa, now this is the fundamental policy of the ruling party and its government. It is amazing kila kukicha ninavyoona uvundo unavyofumuliwa na POAC!!! Its pathetic.... TRA, oooooh my gosh thats another prob... imejaa watendaji wezi, wazembe na wala rushwa wakubwa... TRA imekosa ubunifu katika kuongeza wigo wa kukusanya kodi.....

Governance.... From the prezidaa to the last cadle in the gov, kila mtu anajifanyia mambo kivyake; serikali imekosa kabisa coordination, kila mtu anaangalia atamfurahishaje aliyemteua kushika public office. Top and senior management levels in the government and its agencies is full of friends, relatives, people with same religion beliefs. Agencies responsible in vetting government seniors is totally asleep, them too are very busy to kill people's voices!! Leadership vacuum is now being taken by the first family, the wife and kids are now at the centre of the steering wheel, driving everything.... The prezidaa is busy with travelling and shopping....

Bandugu bana bodi these few I have in mind!!! The truth is I agree, we are in the centre of collapse..... we are dancing its music.....
 
Mnataka kuniambia kwamba viongozi wetu hawaigani kwa mazuri huku wakipuuza maovu katika kusukuma gurudumu la maendeleo? Nini maana ya kurithishana uongozi.
 
hakuna sera madhubuti za kuokoa uchumi wa nchi hii...wataalamu karibu wote wamemezwa na siasa na hata wakiwa wanaongea wanaongea kisiasa......kwa hali hii hatuwezi kupiga hatua yoyote kabisa hata ushauri wanaopewa ten mzuri wanaupiga kwa sababu za kijinga na kibafsi...kwa hali hii lazima uchumi uyumbe tena sna....kidogo kilichopo kinatumika vibaya tena bila uangalizi...angalia ziara za huyu mbayuwayu huyu anasafiri na msafara wa watu 50 kwenda australia na tena anawahi kweli akisikingizia eti kuna kikao cha ufunguzi tar 25 na kikao kamili kinaanza tar28..uongo mtu wako huko wanaponda kodi zetu kwa kwenda kwenye makasino.....

wawekezaji hawalip kodi hiyo misamaha ya kodo sijui wanaita tax holiday ya miaka 5 huu ni ujinga na ni lzima nchi iyumbe tena kwa kasi zaid....ukionekana unawaambia ukweli wanamuagiza zudrev ghev aje kutoa mafunzo ya namna ya kukuua...

nimesikia kuna maandamano yanafanyika dar jumamosi juu ya kupinga dowans na ufisadi....ningeshauri maandamno yafanyike nchi nzima lakini nasikia leo jioni au kesho asubuhi watakuja na tangazo la kusema habari za kiintelijensia zimesema kundi la alshabaabu linaweza kulipua dar mda wowote na hivyo kuyasambaratisha maandamano......maana wanasema toka ubungo hadi huko jangwani ni parefu mno so wanahisia machafuko ili kuwatisha watu watatoa vitisho vya alshabaab....

nami nasema mwaka huu utaisha lakini mwaka kesho kutazuka vita ya wenyewe kwa wenyewe tena juu ya ardhi maana naona kila kona nchi hii ardhi imekuwa na maatizo na watu wanauana sana na serikali haikiri udhaifu wake....wenzetu sierra lione wameliona hilo na sasa wanaweka mikakati ya kudhibiti ugawaji wa ardhi kwa wageni (Sierra Leone sets up unit to monitor foreign land deals after locals protest http://t.co/ZlByF4b7)...

hakuna tunachosafirisha nje hata kama kipo sio kwa msimu wote wa mwaka...tunanunua karibu kila kitu toka nje..we fikiria hata tooth pick hizi zinatoka nje..hakuna jiihada ya kuboresha local industries ziweze kushindana zaidi na kujengewa mazingira mazuri ...viongozi wapuuzi wamejaa wapo wapo tu kazi kusimangana na kulishana sumu..mkuu wa nchi hajui anaongoza nchi gani na yawatu gani hana mipango he cant think beyond the next meal sasa hapo uchumi usishuke kwa nini?!!! lazima ushuke tne kwa kasi ya ajabu..

wote tumeina uchaguzi wa juzi hapo igunga hivi kama kweli jitihada zilizowekwa hapo kuhakiksha ushini zinegekuwa zinawekwa kwenye maendelo leo si tungekuwa mbali kabisa katika kutatua matatizo yetu...miaka mitano hili sharo baro lipo pale ikuru hakuna kipya kazi kubwa ninayoina pale anayofanya ni kupokea hati za utambulisho za mabalozi wapya wanaokuja hapa nchini hakuna jingine analofanya mpuuzi huyu baada ya hapo anaruka kwenda nje...ndo maana nasema hatuna raisi ni haki uchumi ushuke maana kuanzia raisi wasaidizi wake, washauri wake, walipoewa dhamana ya kuongoza vitengo nyeti kama BOT n wiza ra ya fedha wote wana vichw vya nazi
 
Mwanakijiji,

Unakumbuka tulikuwa na debate 2009 kuhusu hali ya kiuchumi ya Tanzania na muelekeo wake. Nikasema uchumi wa Tanzania kwa miaka ijayo kama ukikua sana ni asilimia 4.5%. Uchumi wa nchi unamatatizo na kikubwa ni watu wanaendekeza siasa zaidi ujuzi wa watu. Kuna mambo niliyataja mwaka juzi yanasababisha uchumi wetu kuyumba:-
a. Umeme:
Tatizo la nishati la umeme limechangia kwa kiwango kikubwa kuua uchumi wa Tanzania. Hilo ni kwasababu nishati hii imepotea na hivyo kusababisha uzalishaji wa vitu nchini na huduma nyenginezo kupanda bei maradufu. Na kuchangia ukuaji wa mfumuko wa bei na kuyumba kwa uchumi.

b. Miundo mbinu mibovu:-
Barabara, foleni, mipango miji mibovu vyote vimechangia kuongezeka kwa gharama za maisha na kuyumba kwa uchumi. Mkulima anaona bora auze mchele na sukari nje ya nchi kuliko kuleta Dar kwasababu barabara mbovu. Kama umeangalia statistics za September inflation ya vyakula iko juu kuliko inflation ya vitu vyengine. Sababu kuu ya hayo ni kwamba inflation ya chakula ndio inajumuisha basket of michele, sukari nk. Mchele wa rukwa na mbeya sasa hivi unazidi mchele kutoka pakistan kwa bei. Matokeo yake ni kuongeza importation kuliko kutumia michele ya hapa nchini. Vile vile mipango miji mibovu inachangia ukuaji wa gharama za maisha. Vitu kama foleni za barabara zinamuongezea gharama za maisha mlalahoi kwani vitu kama usafiri wake wa kila siku vinakua maradufu.

c. Ufisadi.
Ufisadi unarudisha nyuma uchumi wa nchi yetu. Hivi sasa ufisadi unatafuna zaidi ya 20% ya GDP na tatizo linakuwa kila mwaka. Hilo linachangia kuzorota kwa shughuli za uzalishaji, an increase in purchasing power of households (maana matajiri ambao ni wafanyakazi wa serikalini na taasisi nyenginezo wana pesa za kuchezea), kuongezeka kwa gharama za maisha.

d. Dollarisation.
Hii nimeshaielezea katika thread hii hapa
https://www.jamiiforums.com/habari-...bot-3-key-policies-to-rescue-shillings-3.html

e. Kuanguka kwa shillingi na athari zake kwenye gharama za maisha. Nimeshaielezea hapa.
https://www.jamiiforums.com/habari-...bot-3-key-policies-to-rescue-shillings-3.html

f. Ukopaji wa serikali usiokuwa na mpangilio.
Serikali yetu inakopa kwa kasi ya ajabu na hakuna mtu ameliangalia kwa uangalifu. Thread moja nilianzisha ya kuorodhesha madeni ya serikali inasemekana deni la serikali ni karibia Trilioni 15 je kuna mtu analijua hilo??? Trilioni 15 inamaanisha kila mtanzania analipa si chini $214 sawa na Tshs 385,200. Bado hujaiangalia level of interest charged for the debt. Na deni linakuwa kwa kasi kwani kama tukifanikiwa kuuza Eurobonds za $500 Billioni our national debt litakuwa karibu Tshs Trilioni 800. Kuna hatari tukawa kama Greece kama hatujawa waangalifu. Zaidi kuna thread nilianzisha kuhusu deni la taifa hii hapa taarifa utaziona zaidi:-

https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...-na-ndani-na-uwezo-wa-nchi-yetu-kuyalipa.html

Ni vema ukopaji huu ukadhibitiwa na bunge kuzuia nchi kufilisika kwani kasi hii ni hatari kwa mustakabali wa nchi hii.

g. Ukubwa serikali na bunge:
Serikali yetu inajibebesha mizigo isiyokuwa na maana na ukubwa serikali unaliumiza taifa. Tusipokuwa waangalifu tunaelekea kuwa kama ugiriki ambapo uchumi wa nchi unategemea wafanyakazi wa serikali. Serikali inahaja kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali yake kusave pesa. Manunuzi ya Magari ya ghali, gharama zisizo na umuhimu na safari za viongozi zisizo na ulazima vinahitaji kusimamiwa. Vyenginevyo ni mzigo kwa taifa.

h. Vyanzo finyu vya kodi. Tuweni wakweli watanzania hasa waliopo katika sekta kujiajiri wengi hawapendi kulipa kodi. Kumekuwa na mianya mingi ya kukwepa kodi na kutokulipa kodi. Mfano biashara za upangishaji nyumba zimekuwa zikiachwa watu hawalipi kodi. Wafanyabishara wa kati na wakubwa wengi hawalipi kodi (including Vodacom). Kuna haja kuongeza vyanzo vya kodi.

i. Tofauti kati ya matajiri na maskini na kupotea tabaka la kati nalo limechangia.

Hayo mwanakijiji ndio matatizo ya nchi yetu. Nilikuwapo!!!
 
MMKJ,
I believe the problem is moral and not economic. Our leaders are not God fearing and anybody holding to that kind of utilitarianism will do anything which he thinks will bring about happiness. He is not concerned about accountability, and wait a minute, if he doesn't fear God whose rule will he else obey?
If he thinks it will bring happiness then he will do it whether it be pilling up money, stealling from treasury or sailing with convoy abroad.
The only thing can serve our country is repairing our foundations. We aknowledge God in our national song because founders knew it was necesary for moral reference. If we fear God we will fear stealing, killing (whether for power mongery or political strife).... And as result our economy will bloom.
Economy collapse is a logical result of bad morals as result of lack of God fearing leaders. So if we want to repair doors and walls (economic issues, et al) and leave foundations crumbling (moral issues) then we have lost the battle and the war!
 
Kikwete has screw up our country, wish i could have AK-47 and shoot all who are responsible for this me$$$$$$$. I am so F**** angry with this foolish People. am not happy they way the lead this country.
 
Je ndio wakati wa CCM na serikali yake kujikuta wanalazimishwa kulipa gharama ya sera na utendaji wao? Je ndio wakati ambapo Tanzania hatimaye itajikuta inalazimishwa kulipa gharama ya kuruhusu mfumo wa utawala wa kifisadi? Je, nani ataitwa kuikoa Tanzania endapo uchumi utaanza kuwa vurugu hasa bidhaa za kila siku (vitunguu, nyanya, mikate n.k) zitakapoonekana kuwa ni za juu kuliko uwezo wa watu wetu wengi?

Jibu la hivyo viulizo (????) ni NDIYO!!!
Kitu chochote kilichojengwa bila kuzingatia misingi ya ujengaji ni lazima kisambaratike!
Cha kusikitisha/kufurahisha ni kuwa lazima haya yatokee mbele ya macho yetu ili ile dhana ya kutaka "tuanze upya" itimie na ieleweke!
Tunayashuhudia ulaya na Marekani... tutayashuhudia na kwetu tu!
Hakika hatuwezi kuokoka sababu tupo ndani ya mfumo usiowasikiliza waokoaji...!
Njoo hapa kaka, tusimame juu hapa ya mlima kidogo ilituweze kuyashuhudia haya "maangamizi"
We unaona kitu tunaweza fanya yasitokee hayo?
 
mie maomba kuuliza hivi tanzania tunazalisha nini hasa cha ku export? (pamba, mkonge, korosho, karafuu, almasi, dhahabu,chuma?????) kama kiwanda ch bia ndio walipaji wa kodi wakubwa then we are really ****d up
 
Back
Top Bottom