What can be done to prevent our economy from collapsing?

Tufanye nini? Inawezekana tumefika mahali ambapo hatuwezi kuepuka tena?
Tuachiwe uhuru wa kujiamulia mambo yetu sisi wenyewe bila kigezo cha msharti kwasababu ya madeni, pia kama ikishindikana, tufanye mambo yetu wenyewe na kulipa madeni kwa masharti yetu sisi wenyewe huku tukijiletea maendeleo, hilo tutaweza?

Shida kuu ya uchumi wa nchi yoyote ile, ni kuhusiana na madeni waliyonao, kama ikionekana kuwa serikali inaweza isiyalipe madeni hayo kama ylivyo kwenye makubaliano(fear of default), basi hakuna kitakachowezekana zaidi ya uchumi kuanguka.
 
Tufanye nini? Inawezekana tumefika mahali ambapo hatuwezi kuepuka tena?

si kweli mwanakijiji, ila ni maamuzi na kujiamini ndio kunakotakiwa, viongozi wetu ama ni waoga ama wasioweza kuamua mambo mema ya kufanya ama kwa interest zao au kwa uzembe wao. tunaweza tusiwe na la kufanya katika yaliyopita ila bado tuna jambo la kufanya katika yajayo.
 
Kwa kweli nimependa sana maelezo ya watu wengi humu, yanaonesha siyo tu tunajali kinachotokea nchini bali pia tunakielewa tena labda kwa kina kikubwa sana. Lakini vile vile naweza kuona kabisa kuwa kwa kufuatilia tu baadhi ya mawazo humu sera mpya ya kiuchumi inaweza kuandikwa.
 
mambo yafuatayo yazingatiwe:-
1. Watanzania tufanye kazi tena kwa bidii tuzalishe in excess tuache manunguniko.
2.wawekezaji tunaowahitaji ni wa kufungua viwanda na kufufua vilivyopo hao wakipewa tax relief iko sawa.
3. Tukusanye kodi kwa wawekezaji hasa wanaouchukua rasilimali zetu, VAT exc na tax relief iondolewe kwa sababu hizo ni rasilimali tulzopewa na Mungu na ni kwa ajili ya watanzania hasa madini.
4. Energy is prime mover for development of any country, tunahitaji reliable power.

wanajf yapo mengi tuanze na hayo machache tutaona matunda ya uchumi

si kodi tu kutoka kwa wawekezaji ama migodini bali kodi kwa ujumla wake ikusanywe na kodi hiyo itumike kuboresha miundo mbinu ya nchi na kuboresha huduma za kijamii katika taifa. kama kodi inakusanywa vizuri na kuliwa na wachache hata moyo wa kizitoa kodi hizo hautakuwapo.lakinipia kama kodi zitakusanywa vizuri na kutumika katika viapumbele vibaya pia haitaleta maana. hivyo kodi ikusanywe kisahihi na itumike kisahihi hapo uchumi utakuwa na maendeleo yatakuja.
 
Kwa kweli nimependa sana maelezo ya watu wengi humu, yanaonesha siyo tu tunajali kinachotokea nchini bali pia tunakielewa tena labda kwa kina kikubwa sana. Lakini vile vile naweza kuona kabisa kuwa kwa kufuatilia tu baadhi ya mawazo humu sera mpya ya kiuchumi inaweza kuandikwa.

ni kweli usemayo lakini nachelea kusema kuwa kwanza sera nyingi zilizopo hazitekelezwi ipasavyo mfano kilimo kwanza nafikiri tungekuwa makini sana kutekeleza sera ziletazo maendeleo,na kuzisimamia ipasavyo, halafu sasa kubadili zile zisizofaa. nakubaliana ma wewe kabisa katika JF unaweza kupata mawazo mengi yafaayo kuleta maendeleo ila watunga sera sijui kama huona kama sehemu hizi ni sehemu wawezapo kupata mawazo haya mazuri matokeo yake huichukia mitandao ya kijamii na kuona kama ni sehemu ya uchochezi, kama wakiitumia vizuri mitandao hii mazuri yataweza kuja.
 
Mdondoaji, MTM, Dar Si Lamu, MMJ, na Jasusi

Mjadala ni mzuri saana, ila naomba kuwauliza kitu kimoja amabcho naona kwa walio wengi kimerlukwa kuzungumziwa. Kama ukitazama hali ya uchumi aliyoikuta Mkapa alipochukua nchi, lakini baada ya muda akaweza kuibadilisha kabisa. Mengi mmeyaongelea kuhusu hili, sasa kwa Kikwete, yameongelewa mengi saana hapa ikiwa ni pamoja na vacuum of ledership, ambayo mpaka wanafamilia wameamua kuchukua uongozi, na pia tumeona jinsi kwa sasa haijulikani nani mwenye kauri na hata kwa mara ya kwanza imetufungua macho kuwa waziri mkuu hana madaraka kabisa.

Kwa hali ya uchumi hivi aliyetufikisha hapa si makosa ya kumchagua Dr Kanza kuwa mshauri wa uchumi bila kuwa na uzoefu? na je man imani kweli na utendaji wa gavana wa BOT Pro. Ndulu?


 
Back
Top Bottom