Wenye watoto kutoruhusiwa kufunga ndoa kanisani wakiwa wamevaa Shela

Duh....kwa hiyo waliofiwa na waume zao hakuna kuolewa tena (madhabauni)?
Na vipi watawatambua wenye mimba changa? Na wanaume waliotia mimba inakuwaje?
Ni wapi wamesema kuwa waliofiwa na waume zao wasiolewe tena?

Ulipaswa uulize kwa wao kuna utaratibu gani hasa?
 
Ulipoanza tu kutembea na mama yako akili yote ikaisha, kamuombe msamaha baba yako. Karibu tena mkuu

Nafuu niliyetembea na mamangu kwa sababu ningekosea njia nkatembea na weye nadhani moto wa jehanna ungenihusu. Si nlikuambia weye huna dini ila unamvizia shekhe wetu?? Ufirauni wako unaanza kuufungua sasa. Naona nilipiga pua kabisa. Pole, vumilia tuuu
 
Naunga mkono hoja. Ndoa na iheshimiwe na watu wote, siyo mtu umeshazaa then unavaa shela..shela lina hadhi yake, dah ila najiuliza vp kwa wanaume wataofunga harusi ilhali wana watoto wa nje? Kwao itakuaje?hii sheria itawaumiza zaidi wanawake.
 
Kama hujaelewa unaweza pitia posts unazozielewa si lazima kuelewa kila post!
Kwanini si lazima mimi kuelewa ulichoandika hapa?

Uliandika ili nisielewe au uliandika kisichoeleweka?

Angalia usiingie katika lile kundi la mbumbumbu wabwabwajaji.
 
Jamani Babati matusi hayakupendezi kabisa, usitukane tena.
Mkuu ukiwaacha hawa wanadharau sana, toka nimeanza kuchangia hapa Oct, 2016 sijawahi kutukana mtu, hawa huwa wanadandia thread na kuanza kutukana kijinga. Mimi mwenyewe huwa sipendi kabisa hasa J2 kama ya leo, kama anaona nimeandika kitu ambacho hakimfurahishi ni vizuri kuachana nacho siyo lazima achangie.
 
Ninacho shukia nikule kusema huyu anafunga ndoa anastahili kufika kwenye madhabahu ,huyu anabariki ndoa hastahili kufika kwenye madhabahu ,huo wote ni uzushi tu .kama tunangalia nani katenda zambi na nani hajatenda zambi tutakuwa tunajidanganya uwezo huo hatuna.
Unajua nini maana ya kufunga ndoa na kubariki ndoa katika KKKT?

Tuanzie hapo.
 
Kanisa halikupotezi wewe ndio utapotea
Kwenda mbinguni sio lazima usali KKKT, naamini unalifahamu hilo. Kanisa ni njia tu lkn matendo yako ndiyo huamua uhusiano wako na Mungu.
Kanisa huhitaji waumini wengi, lkn kwa mpango huu wananiambia niondoke. Wanayoyatangaza hayahusiani na maandiko, bali mawazo ya kibinadamu.
 
KKKT wapuuz sana. Wanaacha kushughulikia ya maana wanakaa kuumiza wafuasi wao.

Huku Arusha bado wanachangisha mchango wa hoteli ya Korido Spring
Wala usitukane, kanisa lenu lina nia njema tu ambayo ni kuzuia uzinzi, Mwanaume na Mwanamke kushirikiana kimwili na kuishi pamoja kabla ya ndoa takatifu ni dhambi. Ndio maana kitendo kile kinaitwa tendo la ndoa, sasa mtu anafanya tendo la ndoa huku hata ndoa yenyewe haja funga.

Vipi mbao tayari wameandikisha kufunga ndoa mwezi huu na wana vitumbo na watoto? Waende kufungia Katoliki kabla nao hawajakaza?
Hili la kwako tayari nishalisemea, kuwa KKKT wato grace period huku wakiwahamisha waumini wote ambao hawajafunga ndoa lakini tayari wana watoto au ujauzito kutumia muda wa grace period kufunga ndoa

Kwa Roman Catholic sina uhakika ila nahisi nao hawana siku nyingi kuwa na sheria ya namna hiyo maana wale nao kwa vikanuni tu hawajambo
 
Nafuu niliyetembea na mamangu kwa sababu ningekosea njia nkatembea na weye nadhani moto wa jehanna ungenihusu. Si nlikuambia weye huna dini ila unamvizia shekhe wetu?? Ufirauni wako unaanza kuufungua sasa. Naona nilipiga pua kabisa. Pole, vumilia tuuu
Afadhali umekiri mbele za watu, hongera sana mkuu.
 
Nilitegemea huwezi kuelewa sababu unaishi kwa kukariri.
Naishi kwa kukariri nini?

Hebu thibitisha kuwa naishi hivyo

Wewe uliyetangaza kuwa muumin wa uislam, haya yanakuhusu nini?

Mbona hujibu maswali ninayokuuliza?
 
Mwenye mtoto anawekewa vikwazo aliiotoa mimba anafungia ndoa Madhabauni kazi kwelikweli
 
Maana yake Kanisa limeamua kuhukumu waumini wake. Ni mstari gani kwenye biblia unaotoa mamlaka kwa Kanisa kufanya hivyo? Na kama watu wote wanafanya 'mema' kuna sababu gani ya kuwa na Kanisa? Au wamesahau Yesu aliposema: "sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi" Marko 2: 15-17.

Halafu cha ajabu pamoja na unyanyapaa huo wa wazi bado Kanisa litapokea sadaka bila kujali nani kazaa lini na kwa utaratibu gani?
Umenena vyema, nadhani wanatakiwa kutafakari upya amri zao zisizo na mashiko
 
Kwanini si lazima mimi kuelewa ulichoandika hapa?

Uliandika ili nisielewe au uliandika kisichoeleweka?

Angalia usiingie katika lile kundi la mbumbumbu wabwabwajaji.

Kama kunikashifu inakuongezea chochote kwenye utashi wako basi barikiwa abundantly, aidha pia unaweza kuendelea kukashifu na kukejeli ili kuongeza hadhi yako! Karibu tena!
Narudia tena kusema kwamba si lazima kuelewa kila kitu na ndiyo sababu inayofanya hata wanafunzi wasifaulu kwa alama 100 kila somo!
 
Back
Top Bottom