Wenye busara "NAOMBENI USHAURI WENU"

Unaweza kumuoa yes,lakini kuna ugumu naupata katka kukupa ushauri.

1. Ana watoto wawili, je ni wa baba mmoja au baba tofaut. Kama baba yao ni mmoja, je anandoa nae? Kwa sababu usije ukawa unataka kuoa mke wa mtu..hata kama amempiga sawa lakini ni mke wake bado kwani mwanaume kumpiga mke sio kumtaliki.

2. Uko tayar kuchukua jumkumu la kumlea yeye na watoto alio nao bila kubagua endapo utapata mtoto baadae. Usije ukamtafutia mdada wa watu maumivu zaidi endapo utaona ngumu baadae kwa kumkimbia.

Sio vibaya wewe kumuoa kama unavigezo vyote vya uhalali wa wewe kumuoa huyo binti lakini angalia pia usalama wako kwa mume aliekua nae.

Tambua sababu ya wewe kumuoa, kama umemtamani kumbuka tamaa ni ya kitambo tu, kama ni mambo kitandani then what next..akili kumkichwa bos
 
sikushauri kabisa... kila mahusiano yana changamoto zake. Lakini haya yanazidi coz, hao aliozaa nao mahusiano huwa hayaishi kabisaa, tena unaweza kushangaa ukaja kuwa na bifu nao dhidi ya mkeo. Duh! Tafuta mwingine bana.
 
Usioe huyo

Hao watoto wawili utalea lakini si wako,kama utalazimika kumuoa fanya mpango umiliki japo mtoto mmoja,yaani uende akamuasili kisheria.Kama ikishindikana kumilki mtoto hata mmoja then achana na hiyo mambo,wanawake wapo wengi acha kuzubaa,fanya maamuzi magumu usije kuaribu future yako!
 
NO MKUU. sikushauri coz;
1. mambo ya kusema umempenda sana hayapo bwana, kwa wanaume suala la kupenda ni ishu ya mazingira tu. ukija mbeya utapenda, ukija mtwara utapenda, ukija mwanza utapenda nk.
2. kwa nini uoe mtu ambaye ameshazaa? well, sio ishu but nimeshuhudia wengi wakurudi kucheza dramma na mzazi wa zamani au kutoa visingizio eti naenda kwa mzazi wa zamaani kuwapeleka watoto. in short utakuwa na mambo meeengi bila 7bu.
3. wanawake ni wengi, tafuta kigoli bwana.
4. ni maoni yangu na mtazamo wangu, sijaoa but sitakuja penda aliyezaa kwa kigezo eti nimempenda why?? hakunaga..... ntatafuta kitoto kibichi naoa.
5. yaani wewe unaoa leo, tayari familia ina watu wanne na itabidi utafute housegirl mnakuwa watano.... hapo bado haujapata mtoto wako.... think big!!

Nimeupata ushauri wako mkuu ngoja nifuatilie wengine huko chini nimechelewa
kuja hapa kwani nimeformat Computer.
 
Nashukuru kwa michango yenu, nashindwa kumjibu mmoja mmoja kutokana na
mtandao kuwa Slow. Kwa ufupi nimejifunza haya

1. Kuoa mwanamke aliyezaa kunaweza kusababisha gharama kubwa ya kimaisha
kutokana na ukubwa wa familia.

2. Wengine wanahisi kwamba huenda kukawa na muendeleo wa mahusiano na
mwanamme aliyeachana nae

3.Wapo ambao wanatabiri kutokea mateso ambayo hawajafafanua.

Nashukuru kwa ushauri wenu na nitarudi tena mtandao utakapokaa sawa.
 
Kaka Gazeti, Ushauri ni mwingi na ni mzuri lakini kaa chini kwanza utafakari (Ushauri huu changanya na akili zako) halafu uchukue hatua. Mwisho wa siku wewe ndie utayechukua maamuzi yote.
Nakutakia kila la kheri!
 
Hizo hoja zote ulizopata hazina msingi wowote!

1 unaweza kuoa mwanamke anaetegemewa na wadogo zake na ww ndugu zako wakawa wanakutegemea. Babangu amesomesha shemeji zake wote na watoto wa ndugu zake wote, as a result wote ni wanae na akikohoa tu wanaitika kwa pamoja! Kukwepa mwanamke kwa ajili ya watoto ni ubinafsi na uchoyo tu,tena wa kinyonge!

2. kuendeleza mahusiano na ex ni tabia tu ya mtu na visingizio visivyoisha! Kuna wangapi wanatembea na bf zao ama gf wa zamani, na hawakua na watoto? Jifunze kuamini, na zaidi mwanamke huyo keshatendwa. Ukimuonesha upendo atakua kama mtoto wa somalia akipewa maziwa anavyoshukuru!hata ww umeshawahi kuwa na mahusiano na ukiamua kurudisha mtoto sio kisingizio!

3. mateso yapo tu! Bible inasema 'duniani mnayo dhiki,lakini jipeni moyo. Nimeushinda ulimwengu'. Kuna wadada wameolewa na bf wa kwanza na wanateswa tu na waume wasio waaminifu! Siiti mateso lakini challenge za maisha zipo na zitakuwepo hata kama hakuna watoto!
Ushauri Wangu:

Jichunguze nafsini mwako. Kabla hujazama sana huyo bibie atafute talaka kwa mumewe na awe huru. Miezi 6 ni michache kwa wanandoa kuachana. Pili,kubalianeni idadi ya watoto mtakaoongeza (ya Mungu mengi,huenda usijaliwe watoto baba nani anajua?).

Mkubaliane mtakavyowalea hao wawili waliopo ikiwa na pamoja na open communication kati ya baba yao na mama (wewe utahusika moja kwa moja).

Kila la kheri,mapenzi hayana formula baba

Nashukuru kwa michango yenu, nashindwa kumjibu mmoja mmoja kutokana na
mtandao kuwa Slow. Kwa ufupi nimejifunza haya

1. Kuoa mwanamke aliyezaa kunaweza kusababisha gharama kubwa ya kimaisha
kutokana na ukubwa wa familia.

2. Wengine wanahisi kwamba huenda kukawa na muendeleo wa mahusiano na
mwanamme aliyeachana nae

3.Wapo ambao wanatabiri kutokea mateso ambayo hawajafafanua.

Nashukuru kwa ushauri wenu na nitarudi tena mtandao utakapokaa sawa.
 
mkuu , hapo suala la kuoa halina ubaya sana ila kuna mambo ambayo ni ya msingi kwanza kuyaweka wazi..
  1. tofauti ya umri wako na wake
  2. je wewe una watoto wangapi??
  3. je yeye alikuwa na ndoa ya aina gani (kanisani, bomani etc)
  4. je ulishawahi kuwa kwenye ndoa?
  5. mmewe anaishi / mko nae mkoa mmoja?
naomba majibu ya haya maswali mkuu
 
Gazeti!

Ni wanaume wacahe sana tunaweza kufanya maamuzia kama ya kwako!

Oa...wapende hao wanenu ..............utaniambia siku moja!
Wengine wetu hapa tumelelwa na mababa wa kambo! Tumefaidi maisha ya baba bila hata wasiwasi..................kingine nachokushari ni kuwa huyu dada takuheshimu na kukuenzi nakuonea hata wivu kwa mapenzi atakayokuonyesha!................achana na huu upupu kuwa ohoo ni matatizo sijui nini gharama................nani kakuambia kuwa mke asiyezaa hana ghrama?

Kaeni chini elewana na huyu dada oaneni kisha hameni hata nchi mkiweza mkajifaidie hukoooooooo
 
Hizo hoja zote ulizopata hazina msingi wowote!

1 unaweza kuoa mwanamke anaetegemewa na wadogo zake na ww ndugu zako wakawa wanakutegemea. Babangu amesomesha shemeji zake wote na watoto wa ndugu zake wote, as a result wote ni wanae na akikohoa tu wanaitika kwa pamoja! Kukwepa mwanamke kwa ajili ya watoto ni ubinafsi na uchoyo tu,tena wa kinyonge!

2. kuendeleza mahusiano na ex ni tabia tu ya mtu na visingizio visivyoisha! Kuna wangapi wanatembea na bf zao ama gf wa zamani, na hawakua na watoto? Jifunze kuamini, na zaidi mwanamke huyo keshatendwa. Ukimuonesha upendo atakua kama mtoto wa somalia akipewa maziwa anavyoshukuru!hata ww umeshawahi kuwa na mahusiano na ukiamua kurudisha mtoto sio kisingizio!

3. mateso yapo tu! Bible inasema 'duniani mnayo dhiki,lakini jipeni moyo. Nimeushinda ulimwengu'. Kuna wadada wameolewa na bf wa kwanza na wanateswa tu na waume wasio waaminifu! Siiti mateso lakini challenge za maisha zipo na zitakuwepo hata kama hakuna watoto!
Ushauri Wangu:

Jichunguze nafsini mwako. Kabla hujazama sana huyo bibie atafute talaka kwa mumewe na awe huru. Miezi 6 ni michache kwa wanandoa kuachana. Pili,kubalianeni idadi ya watoto mtakaoongeza (ya Mungu mengi,huenda usijaliwe watoto baba nani anajua?).

Mkubaliane mtakavyowalea hao wawili waliopo ikiwa na pamoja na open communication kati ya baba yao na mama (wewe utahusika moja kwa moja).

Kila la kheri,mapenzi hayana formula baba

king'asti....great lady.
ushauri mwema sana BUT kwamimi sitaufanyia kazi.
 
mkuu , hapo suala la kuoa halina ubaya sana ila kuna mambo ambayo ni ya msingi kwanza kuyaweka wazi..
  1. tofauti ya umri wako na wake
  2. je wewe una watoto wangapi??
  3. je yeye alikuwa na ndoa ya aina gani (kanisani, bomani etc)
  4. je ulishawahi kuwa kwenye ndoa?
  5. mmewe anaishi / mko nae mkoa mmoja?
naomba majibu ya haya maswali mkuu
ebwana BPM, hili la umri limekaaje? nataka maelezo zaidi kimtazamo ktk hili. tofauti iwe kubwa, wastani au ndogo sana?
 
mkuu , hapo suala la kuoa halina ubaya sana ila kuna mambo ambayo ni ya msingi kwanza kuyaweka wazi..
  1. tofauti ya umri wako na wake
  2. je wewe una watoto wangapi??
  3. je yeye alikuwa na ndoa ya aina gani (kanisani, bomani etc)
  4. je ulishawahi kuwa kwenye ndoa?
  5. mmewe anaishi / mko nae mkoa mmoja?
naomba majibu ya haya maswali mkuu

  1. Tofauti miaka 4 nimemzidi.
  2. Sina
  3. Ya kimila
  4. Hapana
  5. Wote tuko Dar Yeye Kinondoni mimi Ilala
 
Ni bora mwanamke akiwa na watoto kuliko mwanaume!Mi nafikiri kama umeamua kua nae tazama mazingira ya mawasiliano ya baba wa hao watoto na mama yao,hilo ndo la muhimu,kama hakuna tatizo hapo go on!
 
Ni bora mwanamke akiwa na watoto kuliko mwanaume!Mi nafikiri kama umeamua kua nae tazama mazingira ya mawasiliano ya baba wa hao watoto na mama yao,hilo ndo la muhimu,kama hakuna tatizo hapo go on!
Inawezekana! Maana naona wanawake wengi wanatesa watoto wa waume zao
lakini sijaona mwanaume akitesa watoto wa mwanamke!
 
Back
Top Bottom