Wenye busara "NAOMBENI USHAURI WENU"

GAZETI

JF-Expert Member
Feb 24, 2011
5,277
6,673
Kama kuna wakati nimeomba ushauri nikiwa serious basi leo ni zaidi. Siku nyingi nimekuwa
nikitafuta mwenza wa kuishi naye katika maisha lakini imekuwa ni kazi ngumu kutokana na
sababu mbalimbali ambazo siwezi kuzieleza zote.

Kitu ambacho kinanifanya niombe ushauri kwa sasa ni kuwa kuna Dada ambaye nimempenda
kutokana na tabia yake. Kinachonitatiza ni kuwa tayari ana watoto wawili. Nataka kujua kutokana
na uzoefu wenu kwani mimi sina mtoto hata mmoja.

Je kuna matatizo yoyote naweza kukabiliana nayo kwa kumuoa mwanamke ambaye tayari ana
watoto 2.

Naomba wenye ushauri wanisaidie!
 
kama mmependana hakuna tatizo.

Je upo tayari kulea mtoto wa mwenzio? Kwa upendo wote, kuwafunza maadili mema?

Huyo dada umri unaruhusu akuzalie watoto(kama mtaoana mkabarikiwa)

baba wa hao watoto wana uhusiano gani na huyo dada? Usije penda hapo ukakuta wenza wa mwanzo full drama, au wanamegana kwa siri.

Kumbuka ukipenda boga penda na ua lake.
 
1. Nina tabia ya kupenda watoto hivyo kulea watoto wa mwenzangu si
tatizo
2. Umri wake unaruhusu kuzaa mtoto mwingine
3.Uhusiano wa baba watoto wake ni mbaya sana kwani alikuwa anamtesa
walipokuwa pamoja na hili mimi ni shuhuda kwani siku ya kwanza kumfahamu huyu
dada alipigwa na mumewe hadi kupoteza fahamu baada ya kumfumania na mwanamke mwingine kwa
kushirikiana na dada wa mwanamke tukampeleka hospitali. Alifikiri amemuua hivyo alitoroka
na kwenda kusikojulikana kwa miezi sita. Amerudi hivi karibuni baada ya kusikia yule
mwanamke yuko hai. Mtoto wa kiume yuko kwa ndugu wa mwanaume.
 
NO MKUU. sikushauri coz;
1. mambo ya kusema umempenda sana hayapo bwana, kwa wanaume suala la kupenda ni ishu ya mazingira tu. ukija mbeya utapenda, ukija mtwara utapenda, ukija mwanza utapenda nk.
2. kwa nini uoe mtu ambaye ameshazaa? well, sio ishu but nimeshuhudia wengi wakurudi kucheza dramma na mzazi wa zamani au kutoa visingizio eti naenda kwa mzazi wa zamaani kuwapeleka watoto. in short utakuwa na mambo meeengi bila 7bu.
3. wanawake ni wengi, tafuta kigoli bwana.
4. ni maoni yangu na mtazamo wangu, sijaoa but sitakuja penda aliyezaa kwa kigezo eti nimempenda why?? hakunaga..... ntatafuta kitoto kibichi naoa.
5. yaani wewe unaoa leo, tayari familia ina watu wanne na itabidi utafute housegirl mnakuwa watano.... hapo bado haujapata mtoto wako.... think big!!
 
Pia mimi kwa busara zangu sikushauri kuoa huyo mwanamke kwa sababu zifuatazo:-

Huta enjoy maisha kwani tayari mwenza wako ana watoto hivyo hatakuwa huru kujiachia na wewe huku watoto wako pembeni.

pia kwa sisi tulioowa tunajua mama kabla ya kuwa na mtoto ni mtamu kivipi. baada ya kuzaa upendo kiasi fulani huamia kwa watoto baba akibaki nyuma so take care ndugu

Jambo jingine kumbuka "First love never die" watakumbushia tu hao tafuta wa kwako usichukulie adhaifu wa mumewe wa kwanza kuwa ndiyo ubora wako. labda na huyo dada ni mvivu kwenye mavitus na ndiyo maana mumewe wa awali alitoka nje we msaisie tu arudi kwa mumewe. ni hayo tu kaka.

Pia angalia usalama wako unaoa mke wa mtu unadhani sawa tu
 
aise ni ugonjwa wa moyo kuoa mwanamke mwenye watoto na mdingi wa watoto yu bukheri wa afya,mbandue tu usimuoe. Nalog off
 
Kama kuna wakati nimeomba ushauri nikiwa serious basi leo ni zaidi. Siku nyingi nimekuwa
nikitafuta mwenza wa kuishi naye katika maisha lakini imekuwa ni kazi ngumu kutokana na
sababu mbalimbali ambazo siwezi kuzieleza zote.

Kitu ambacho kinanifanya niombe ushauri kwa sasa ni kuwa kuna Dada ambaye nimempenda
kutokana na tabia yake. Kinachonitatiza ni kuwa tayari ana watoto wawili. Nataka kujua kutokana
na uzoefu wenu kwani mimi sina mtoto hata mmoja.

Je kuna matatizo yoyote naweza kukabiliana nayo kwa kumuoa mwanamke ambaye tayari ana
watoto 2.

Naomba wenye ushauri wanisaidie!

Ningekuwa nina namna ya kuwasiliana na wewe nifanya hivyo ili nikupe ushaidi na uzoefu juu ya jambo unalotaka kufanya. Lakini kwa kifupi kwa uzoefu wangu, mateso utakayopata hapa ni mara nne ya raha utazopata. Sikushauri uoe hapo. Lakini uamuzi ni wako na kama itatokea umemuoa huyo mdada, tunaomba utujulishe ili tuendelee na research zetu watu. Na ukumbuke jambo moja. Ikitokea siku moja mmeachana, ujue na wewe utakuwa mtu mbaya sana na ulikuwa unamtesa sana. Hilo nakuhakikishia

Asent.
 
USIOE huyo dada

wewe unataka kumuoa kwa kuwa tu unamuonea huruma na ulishiriki wewe na dada ake kumpeleka hospitali sio? usiwe mtu wa ajabu namna hiyo.fikiria nje ya box mpwa wangu.....mimi ninakuambia kabisa mpwa kuwa utaona maisha machungu zaid ya mara nne ....nimewahi kusuruhisha ugomvi wa mtu na mkewe...nae alikuwa anapigwa sana.kutoka na kile kipigo ndugu wa binti na sisi majirani tukasema waachane na yule binti arudi kwao.....kumbe bwana ndoa huwa haivunjwi na watu ila huwa inavunjwa na wanandoa wenyewe.....yule dada alikaa kwao huko kama miez 44 lakini siku moja asubuhi akarudi kwa mumewe na akasema huyu ndo mume wangu wa SHIDA NA RAHA...kipigo kikaendela.....kama umempenda huyo dada kias cha kutaka kumuoa hyo ni juu yako chini yetu ...ila mimi kama mimi nakushauri usioe maana hyo bado ni mke wa mtu....
 
Binafsi sikushauri kuoa mwanamke mwenye watoto wawili!Nachelea unaweza ukapata mateso mithili ya jehanam ya dunia.Mahusiano ya namna hiyo huwa yana changamoto zake ambazo wengi huwa zinawatesa inabaki majuto ni mjukuu.ACHA!
 
kama mmependana hakuna tatizo.

Je upo tayari kulea mtoto wa mwenzio? Kwa upendo wote, kuwafunza maadili mema?

Huyo dada umri unaruhusu akuzalie watoto(kama mtaoana mkabarikiwa)

baba wa hao watoto wana uhusiano gani na huyo dada? Usije penda hapo ukakuta wenza wa mwanzo full drama, au wanamegana kwa siri.

Kumbuka ukipenda boga penda na ua lake.

pia ajipange kutoa huduma sawa kwa watoto atakaozaa na wa huyo mama. Kuwa baba wa watoto zaidi ya wawili kwa wakati mmoja si jambo dogo kama hatokuwa njema kiuchumi.
 
nyie acheni kumpotezea bahati dada wawatu
si mmesikia mwenyewe kasema mdada wawatu anapigwa huko snaa jamani ssa yy mwataka aolewe na nani au mwataka yy akae bila mpz kisa nn
zen kwako ww kaka huwez jua kwann mungu kakukutanisha na huyo dada.............just follow ur heart kama wampenda kweli muoe
sasa kama ushamuonjesha penzi na kuonesha kama uko serious kuoa yy then gafla umuache mbona wamtakia machungu mwana wa mwenzio aione dunia chungu bure loh!
TAKE UR TIME ...........THINK TWICE B4 U SAY NO TO HER
 
Kama umependa muoe,unaweza kupata hara na huyo mwenye watoto na ameshaona dunia kuliko umpate mwengine aku sugue roho ujute kuao,kaanae chini muelewane mpesheria zako kama atazikubali hakuna tatizo,kwanza atakua dawa manake maisha ya ndoa amesha yaona anajua tabu zake na raha zake,kuhusu watoto huwezi jua hao watoto ndio wanaweza kukuheshimu wewe kuliko watoto wako mwenyewe mtangulize Mungu kwenye kila jambo lako na utafanikiwa....
 
Mmmh kwa hzo comment hapo juu!!!duh naona kwa kiac gan mwanaume anavyopata upinzan anapoamua kuoa m,ke mwenye mtoto na jnc wanawake wenye watoto wanavyopata shda yakuolewa,
jaman hata nao wanahak yakuolewa na kupendwa na kupenda.mtoto ckibandiko kuwa mda wote atakuwa amemgandaa na mara nyngi wanaokuwaga nawatoto huwa hawaolew nao(hawaend kukaa na watoto kwa mme)huwa wanakuja kutembea 2.
na huu usemi wa first love does not die,cjui unakuwaje manake kuna wengne hapa ha2uply.
m2 km kaumizwa na kaamua kuachana na huyo aliyekuwa nae hata km walizaa watoto zaid ya hao kwa maumivu m2 aliyonayo huwa hamkumbuki na hamtak kabsa.
km unajiamin unampenda na anakupenda kweli kaka tia 2 miguu yote.
 
kama uko tayari kujenga uadui na huyo mume wake wa zamani, endelea. Lakini uwe tayari kwalolote litakalotokea. Nasema hivyo nikiwa na maana kuwa mara mtakapochokana ataona ni bora yule wa zamani. Na inavyoonekana ni majirani kwahiyo ni rahisi kuonana. Watarudiana taratibu kisha jamaa ataanza kukuwinda. All in all wewe mwenyewe ndiye unayetakiwa kufanya cost-benefit analysis ya kutosha kwa kuwa inawezekana kuna mambo mengi unayoyajua hujayaweka bayana hapa. Kila la kheri
 
Wewe unaonekana 100% domozege(inspector) umezoea vya kuchinja kiulaini,kuna vigori kibao street hawana watu acha uoga rusha nduano utapata achana na wazee kama unaogopa mtumie hata mtu akutongozee
 
Mkuu sikushauri hata kwa Dawa!mimi mwenyewe nimeshuhudia nyumba jirani dada kazaa na jamaa mtoto mmoja baadae wakaachana kwa makosa kama hayohayo!baada ya kama miezi kadhaa akapata bwana mwingine ambae akaolewa nae tena kwa ndoa ya kiislam,cha kushangaza baada ya miezi kadhaa mwanamke uhusiano na yule bwana wa zamani ukaanza!siku nyingine alikuwa akilala kulekule kwa mme wa kwanza akiulizwa anasema nimekuta mtoto wangu mgonjwa so siwezi kumwacha wakati anaumwa kumbe ilikuwa ni porojo!siku zinavyokwenda inakuwa vituko juu ya vituko yaani haviishi.Kwa kiyo mimi sikushauri bcoz hao watoto sizani kama utakuwa nao watachukuliwa na baba yao,na kama watachukuliwa drams hapo ndo inapoanza!
 
Sioni tatizo kama umempenda naye kakupenda na kama upo tayari kwa majukumu ya kifamilia. Pia jitahidi ujue maana ya ndoa kabla ya kuingia. Ndoa si kujirusha kama wengine walivyosema. Follow your heart and be responsible!
 
pia ajipange kutoa huduma sawa kwa watoto atakaozaa na wa huyo mama. Kuwa baba wa watoto zaidi ya wawili kwa wakati mmoja si jambo dogo kama hatokuwa njema kiuchumi.

ni kweli kutunza watoto wa mwenzio sio kazi ndogo. Ajitoe haswa. Ila ndoa ni maelewano, na uhusiano ni vile watakavyoujenga. Wakiamua na kujitoa wataweza.
 
Kama kuna wakati nimeomba ushauri nikiwa serious basi leo ni zaidi. Siku nyingi nimekuwa
nikitafuta mwenza wa kuishi naye katika maisha lakini imekuwa ni kazi ngumu kutokana na
sababu mbalimbali ambazo siwezi kuzieleza zote.

Kitu ambacho kinanifanya niombe ushauri kwa sasa ni kuwa kuna Dada ambaye nimempenda
kutokana na tabia yake. Kinachonitatiza ni kuwa tayari ana watoto wawili. Nataka kujua kutokana
na uzoefu wenu kwani mimi sina mtoto hata mmoja.

Je kuna matatizo yoyote naweza kukabiliana nayo kwa kumuoa mwanamke ambaye tayari ana
watoto 2.

Naomba wenye ushauri wanisaidie!

Kama mwenyewe umekubali hakuna tatizo ila ukumbuke, Jee, hao watoto atawatazama na kuwalea nani ki hali na mali? Wewe au Baba yao. Mkiliweka sawa hilo, sidhani kama kuna tatizo, mradi ukumbuke kuwa hao ingawa wewe sio "biological" baba yao, uwapende kama unavyo mpenda mama yao, waswahili hunena "ukipenda boga upende na maua yake".
 
Back
Top Bottom