Gwappo Mwakatobe

JF-Expert Member
Nov 22, 2019
1,494
1,874
Katiba iliyopo ni ya mfumo wa chama kimoja ambacho ni CCM na ilitungwa na CCM mwaka 1977.

Tanzania hatuna mfumo wa vyama vingi, bali tuna mfumo wa chama kimoja (CCM), ambamo kuna vyama vingi ndani yake. Kwa ufupi tuna vyama vingi ndani ya mfumo wa chama kimoja - CCM.

Kamwe CCM hakiwezi kuleta katiba mpya yenye mfumo wa vyama vingi maana itakuwa ni kujimaliza chenyewe.

Katiba mpya ni mpaka CCM kitoke madarakani kama Kenya walivyokiondoa kwanza KANU ndiposa ikaja katiba mpya. Kwanza tuondoe kikwazo ambacho ni CCM, ndiposa tutapata katiba mpya inayokidhi mfumo wa vyama vingi.

La sivyo tutaendelea na maigizo (seasons) ya katiba mpya bila kupata katiba mpya.

Tulikuwa na season ya "kamati" ya katiba mpya, ikaja "tume" ya mabadiliko ya katiba, mara kikaja "kikosi" kazi, na sasa umekuja Mkakati wa Taifa wa Elimu ya Katiba kwa Umma (MTEKU) hadi 2026.

Pasina kukiondoa CCM madarakani, seasons zitaendelea bila ya kupata katiba mpya. Tunapigwa danadana za freestyle football mpaka tunaona kizunguzungu.
 
Ugumu sasa upo kwenye njia sahihi ya kuitumia kuiondoa hiyo ccm madarakani! Maana wameweka mamluki wao kila idara, kila sehemu nchini!! Mpaka kwenye vyama vya siasa vyenyewe wamejaa mamluki wa ccm, vyama vya wafanyakazi kote huko wamejaa wao! Ukienda kwenye vyombo vyetu vya dola, wamejaa!

Binafsi natamani sana kuona hiki chama kinatoka madarakani. Maana kwa sasa kimegeuka kuwa kikundi cha watu wachache wanaofaidi zaidi keki ya Taifa, huku mamilioni ya wananchi wakiishi maisha ya dhiki! Ila sasa tunakiondaje hiki kikundi cha wapigaji, ili nchi iyafikie maendeleo ya kweli?
 
"... huku mamilioni ya wananchi wakiishi maisha ya dhiki!" Uko sahihi kabisa!

Napendekeza tujikite zaidi huko kwa wananchi wanaoishi maisha ya dhiki na kuwaelimisha, kuwahamasisha na kuungana nao kukataa ulaghai, dhuluma na fedheha wanayotupa watawala waovu tulionao. Uwingi wao ni nguvu yetu!
 
Back
Top Bottom