Wengi wa wanaotafuta wachumba JF ni waongo.

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,871
155,840
Nimekuwa nikifuatilia thread nyingi za wanao tafuta wachumba hapa JF. Nimegundua urafiki hushamiri siku ya kwanza kwa Pm za hapa na pale, watu hawabadilishani namba za simu kwa sababu za kijinga tu. Lakini sababu ya msingi ni kuwa hapa jamvini kuna mababa na midevu yao inajidai mijike, ndio hiyo mara nyingi inatangaza kutafuta waoaji. Nawakilisha kutoka Makongolosi Chunya.
 
utafiti wako umeufanyia wapi? tuone data,umeanza kuhukumu bila uhakika..
 
Nimekuwa nikifuatilia thread nyingi za wanao tafuta wachumba hapa JF. Nimegundua urafiki hushamiri siku ya kwanza kwa Pm za hapa na pale, watu hawabadilishani namba za simu kwa sababu za kijinga tu. Lakini sababu ya msingi ni kuwa hapa jamvini kuna mababa na midevu yao inajidai mijike, ndio hiyo mara nyingi inatangaza kutafuta waoaji. Nawakilisha kutoka Makongolosi Chunya.

wewe siyo yule mnaijeria wa Usofia in London?
 
Nimekuwa nikifuatilia thread nyingi za wanao tafuta wachumba hapa JF. Nimegundua urafiki hushamiri siku ya kwanza kwa Pm za hapa na pale, watu hawabadilishani namba za simu kwa sababu za kijinga tu. Lakini sababu ya msingi ni kuwa hapa jamvini kuna mababa na midevu yao inajidai mijike, ndio hiyo mara nyingi inatangaza kutafuta waoaji. Nawakilisha kutoka Makongolosi Chunya.

Mi nahisi ni WADADA NA WAKAKA wanaotafuta NGONO. Isitoshe ni watu waliopo humu humu wanatumia ID mpya. Yaani MMU imeshageuzwa biashara ya ngono.
 
Hisia sio nzuri, manake hata mimi nikitangaza nia kesho asubuhi, mtahisi natania, kumbe kweli.
 
ha ha ha ha ha Bujibuji bana...labda anakupima through PM anaona hufai kwahiyo hakuna haja ya kufika hatua ya kubadilishana namba za simu.....ni mtizamo tu.....watu waache usanii lakini,some people are seriously looking for life partners!!
 
Hisia sio nzuri, manake hata mimi nikitangaza nia kesho asubuhi, mtahisi natania, kumbe kweli.

Hisia za kuchezewa akili lazima ziwepo hasa kama mtu limeshawahi kukutokea au umeliona linamtokea mtu.
Mimi nina jamaa yangu aliniambia kwamba wengine wanaotafuta wachumba wa kiume ktk magazeti ni wanaume. Sikuamini nikaamua kuchukua namba moja wapo nikai-save GAZETI na nikamtumia kujitokeza kutaka uchumba kwake. Huwezi amini alikuwa anasema yeye anataka mwanaume mkweli na hatapenda kutumiwa hata vocha na mwanaume. Siku nikimwambia tukutane anakuwa anachenga nyngi sana lakin baadae (Baada ya siku 20 za mawasiliano) akaniambia yeye ni mwanaume na alikuwa ananitania tu
 
Noted CPU!!

Respect!!
 
Hawezi kukupa namba mpaka ahakikishe mmefikia hatua fulani, mimi nawaunga mkono sio wote wenye nia mbaya
 
Bujibuji humu MMU huwa kuna majadiliano makali yanayoamsha hisia na kuwafanya member makapela wajione wanamiss kitu fulani,uwazi wa michango huwatoa aibu nao kusema haja zao. na hufuatilia na hujibu na kuclarify hoja zao. wale waigizaji utagundua tu katika vipengele alivyotoa na pia kujifichaficha baadhi ya inf muhimu na hutasikia anajibu contribution zinazomwagika after his/her thread..wanapima mitazamo ya watu na kuwaenjoy.
pole mkuu kama yamekupata
 
Bujibuji itakuwa kaPM na kutuma vocha nyingi sana matokeo yake akaja kugundua kuwa ameingizwa mjini na wajanja wanzake.
Mkuu hii inavoonekana ni kweli, bujibuji atakuwa kalizwa na wajanja wenzake... lakini watu kutangaza nia sio tatizo, mwenye tatizo ni wewe unaeingia kichwa kichwa!!!!
 
tobaaaaa,ahsante kwa kunishtua,maana na mimi nilikuwa najipa muda siku nitakayokua tayari na mimi nitafute wangu humu humu,kwa hali hiyo,mmh nimeahirisha
 
Mbona kwangu mi ni tofauti tumeelewana na mpaka sasa tunawasiliana kwa simu na wala sio mwanaume,muwe na imani tu na mnachokifanya...
 
du hii kali:rain::rain::rain:kumbe huwa mnafanikiwa ngoja na mie nianze harakati na uzee huu nisije kufa mpweke.
 
Back
Top Bottom