Sijajua sababu inayofanya Vijana wengi hapa JF kunichukia ni ipi!

UMUGHAKA

JF-Expert Member
Sep 1, 2021
2,157
10,718
Nsikuchoshe na Usinchoshe,tusichoshane!

Mimi UMUGHAKA nimekuwa nikichukiwa sana na Vijana hapa JF tangu nilipokuwa Mwanachama Bora wa jukwaa la Michezo mwaka 2022.

Yaani kuanzia hapo ni kama nilitonesha vidonda vya miongoni mwa vijana wengi wenye roho mbaya hapa JF!.

Ni kwanini Vijana mnakuwa na roho mbaya kama wachawi niliokutana nao kule tabora kwenye simulizi yangu ya Tulichomfanya yule mchawi hatakuja kusahau kamwe

Sijawahi kutembea na demu wa mtu hapa JF lakini nachukiwa bila sababu!

Sijawahi kumpiga mtu hapa JF lakini nachukiwa bila sababu!

Au ndo mnataka niamini ile kauli ya kwamba "hakuna vijana wapumbavu kama vijana kutoka Tanzania"?

Kuna mmoja anasema eti sina chochote na utafuta umaarufu tu! "POPULARITY:

Mimi UMUGHAKA ni Tunu kwa Taifa hili la Tanzania kama mlikuwa hamfahamu!

Nimekuwa nikiwaondolea watu wengi misongo ya mawazo hapa jukwaani hasa kwenye jukwaa la Entertainment kutokana na simulizi za maisha yangu niliyopitia,simulizi hizi zimekuwa na mafunzo na kuwatia moyo vijana wenye akili timamu,lakini wenye wivu zimekuwa ni mwiba mkali mno!.

Mimi UMUGHAKA wala sitafuti umaarufu hata kidogo,yawezekana umaarufu ndo unanifuata mimi bila kuulazimisha!.

Labda tu niwaambie vijana wenye wivu ya kwamba haturingani hata kidogo na nimewazidi mbali mno!.Mimi sijafika chuoni lakini kwa pale nipofika naamini mimi ni bora kuliko vijana wote mnaonichukia humu ndani!

PROFILE YANGU KWA UFUPI

Nimezaliwa Wilayani katika hospitali ya wilaya ya Tarime

NIMEKULIA TARIME na KUSOMEA TARIME ( Shule ya Msingi nimesoma Rebu na Sekondary nikafauli kwenda Tarime Secondary )

MAENDELEO YANGU SHULE YA MSINGI REBU

Nikiwa shule ya msingi nimefanikiwa kushika namba 1 hadi 2

Darsa la kwanza muhula wa kwanza nilikuwa mwanafunzi wa 2,muhula wa pili nikawa mwanafunzi wa 1

Darasa la pili muhula wa kwanza nikawa mwanafunzi wa 1,muhula wa pili nikawa mwanafunzi wa 1

Darasa la tatu muhula wa kwanza nikawa mwanafunzi wa 1,muhula wa pili nikawa mwanafunzi wa 1

Darasa la nne muhula wa kwannza nikawa mwanafunzi wa 2,muhula wa pili nikawa mwanafunzi wa 1

Darasa la tano muhula wa kwannza nikawa mwanafunzi wa 1,muhula wa pili nikawa mwanafunzi wa 2

Darasa la sita muhula wa kwannza nikawa mwanafunzi wa 2 na muhula wa pili nikawa mwanafunzi wa 2 (Hapa nilinyanyaswa na dogo mmoja hivi sasa ni Marehemu!)

Darasa la 7 mtihani wa Mock nilikuwa mwanafunzi wa Kwanza kwenye somo la Hesabu wilaya nzima ya Tarime

MAENDELEO YANGU SHULE YA SEKONDARI TARIME

Kidato cha Kwanza muhula wa kwanza
mtu wa 1
Kidato cha Kwanza muhula wa pili nilikuwa mtu wa 1

Kidato cha Pili kwenye mtihani wa Mock ulioshirikisha shule zote za Wilaya ya Tarime mjini na Vijijini nilikuwa mtu wa 2 kwa Wilaya nzima,nilizidiwa na mpuuuzi mmoja kutoka Rorya (Kabla Rorya haijawa wilaya ilikuwa sehemu ya wilaya ya Tarime Vijijini)

Kidato cha pili kwenye mtihani wa Taifa wa kuingia kidato cha tatu nilifauli kwa ufaulu wa wastani wa daraja A

KIdato cha Tatu muhula wa kwanza nilikuwa mwanafunzi wa 2 kati ya wanafunzi 52

Kidato cha Tatu muhula wa pili nilikuwa mwanafunzi wa 1 kati ya wanafunzi 52

Darasa nililokuwa nikisoma lilikuwa na wanafunzi 52.

Wakati nasoma nilikuwa mbabe kwenye masomo yafuatayo;-

1.Chemistry
2.Physics
3.Mathematics
5.Biology
6.Geography

Haya ndiyo masomo niliyokuwaga nayaonea,nilikuwaga napiga A,Nilikuwa nikifeli kwenye hayo masomo napata B na pia nilikuwa nikifeli nilikuwa nalia wiki nzima 🤣

Kutoka kidato cha nne kulekea kidato cha tano,nilifaulu kwa ufaulu wa Divisheni 2 ya 18 (Niliumia na kusikitika sana kwasababu ni kama nilifanyiwa uhuni,mimi nilikuwa wa kupiga divisheni 1 🤣)

Nilichaguliwa kuelekea Tanga kusoma combination ya PCB

Niwe mkweli form 6 nilifeli,siyo kwamba sikuwa na akili la hasha!,nilijiingiza kwenye mahusiano na binti mmoja wa kitanga aitwaye Shamima,hapo ndo chanzo cha mimi kufeli kwasababu niliacha kusoma nikaendekeza Kusukuma Miti shamba!

Baada ya hapo nilifanya mambo mengi mno ikiwemo kupata fursa ya kutembelea nchi zifuatazo Africa ikiwemo Ethiopia, Rwanda, Kenya, Uganda, Southafrica, Morocco, Madagascar, Seychelles, Nigeria, Congo RDC, Zambia, Malawi, Mozambique, Burundi, Central Africa Republican.

Nimewahi kutunukiwa cheti cha msajili line za simu Bora wa Mwaka kutoka Mtandao wa Tigo (Fleelancer of The Year) na nilizawadiwa kiasi cha Tsh 4 M.

Nimewahi kutunukiwa cheti cha Mwanafunzi Bora (Smart & Intelligent) kutoka katika shule ya Sekondary ya Tarime.

Nimewahi kutunukiwa cheti cha Mwanafunzi bora wa kutunza Mazingira kutoka Shirika la SAVE THE ENVIRONMENT OF TARIME (SETA)

Nimewahi kutunukiwa cheti cha Mwanafunzi bora wa kupambana na Rushwa enzi hizo ikiitwa (PCB -TAKURU) kabla haijaitwa PCCB -TAKUKURU

Nimewahi kuwa Mwanachama Bora wa Jukwaa la Entertainment hapa JF mwaka 2022 na kutunukiwa kiasi cha fedha pamoja na bidhaa nyingine zenye nembo ya JF.

Haya kwangu ni mafanikio makubwa mno,sasa sijajua vijana wa hapa JF kwanini mnichukie mpambanaji mwenzenu badala ya kunitia moyo!

Ndugu zangu yawezekana umaarufu (Popularity) ukawa unanitaka mimi ila siyo kwamba mimi nautaka umaarufu,kama ndivyo basi mimi ni maarufu tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu!

Mimi ni mtu muungwana sana na mnyenyekevu mno sema ni kwamba watu au vijana wa hapa JF wanapenda sana majigambo!

Mimi nimekutana na watu maarufu (Wasanii na wanasiasa) lakini sijawahi kuposti wala kujisifu!,na pia wananipa heshima sana kwasababu uenda wanaona mimi si mtu wa kawaida!.


Kuna mambo mengi ya kusimulia Vijana wenzangu ili mjifunze lakini huwa naogopa mashambulizi mnayonishusiaga nabakiaga tu kuishi nayo moyoni!.


Vijana acheni chuki,Jifunzeni hata kwa mazuri tu kutoka kwangu na mabaya muyaache!
 
Ukiileta kwa wahuni
Tunaila na hatuitoi gundu
Kwa utamu gani kwani
Tukitaka kuila tunaila hata kwa Sabuni
Aeeshu ushu ushuu
Wezombi ee wezombi
Nasimba lamasimba dangote
Ushu zi
🤪

Shamima mtoto wa Tanga akakuingiza Chaka la wahuni 🤪
 
Nimesoma story zako ni nzuri sana.
Kuhusu kuchukiwa, Sidhani kama ni kweli nadhani ni jinsi akili yako ulivyo iweka.

Siwezi mchukia mtu nisie mfahamu nje ya hapa. Na hata ingekuwa hivyo sina sababu ya kumchukia mtu.

Ila mpaka kuanza kujihisi ni kweli unaçhukiwa basi kuna namna unajihisi ww ni bora sana kuliko wengine (Kichwa). Huo umaarufu unaojiona unao kiukweli yaweza kuwa huna.
 
Nimesoma story zako ni nzuri sana.
Kuhusu kuchukiwa, Sidhani kama ni kweli nadhani ni jinsi akili yako ulivyo iweka.

Siwezi mchukia mtu nisie mfahamu nje ya hapa. Na hata ingekuwa hivyo sina sababu ya kumchukia mtu.

Ila mpaka kuanza kujihisi ni kweli unaçhukiwa basi kuna namna unajihisi ww ni bora sana kuliko wengine (Kichwa). Huo umaarufu unaojiona unao kiukweli yaweza kuwa huna.

Mkuu wewe pitia nyuzi zangu uone vijana wanavyonichukiq waziwazi!

Mimi si maarufu na labda au uenda umaarufu unanitaka mimi ijapokuwa mimi siutaki mkuu!
 
Back
Top Bottom