Wengi tungeswekwa magerezani awamu ya tano wakati Serikali inataka IP adress za accounts zinazoikosoa, tunashukuru JamiiForums mlitusimamia

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Kuna kipindi hapo awamu ya tano palikuwa na hali ya hatari kwa mtandao wa jamii forums kushinikizwa kutoa kutoa namba za utambulishi za internet IP ADRESS za wanachama wanaokosoa serikali.


Ili uzielelewe kirahisi ip adress ni kwamba tunavyopiga simu ama kutuma meseji namba zetu huwa zinarekodiwa kwenye simu za watu tuliowapigia pamoja na kwenye rekodi za mitandao ya simu, hizi namba mfano wake ni 0769xxxxx. Basi na kwenye internet hakuna utofauti sana ila huku namba za utambulisho zinaitwa ip adress mfano wake huwa ni 192.268.xxx.xxx, hizi namba hazijirudii kama ilivyo kwa namba za simu kila mtu ana yake (ukizima simu na kuwasha ip inabadilika lakini itakuwa ya kwako tu), ukitaka kuijua ip adress yako tembelea >> hapa <<

ukitembelea tovuti yoyote mfano jamiiforums. com, mitandao ya simu itaona kwamba ip adress inayotumika kwenye simu yako imetembelea jamii forums lakini hawawezi kujua account unayotumia, hapa watajua tu umetembelea tovuti zipi na wanaweza kublock ip adress zote za mitandao yote simu nchini zisiweze kuingia tovuti flani na ndio maana watu hapa huwa wanatumia vpn ambazo zinawaruhusu kutumia internet kwa kutumia ip adress za nchi nyingine na inakuwa ngumu mitandao ya simu kuju hata tovuti unazotembelea maana ip adress unayotumia sio yao tena.

Kwa upande wa tovuti tunazotembelea kama jamiiforums, wao ndio wenye wanaweza kujua account flani inatumia ip adress flani lakini hawana uwezo wa kujua namba ya simu ya anaeitumia hio ip adress. kwa lugha nyepesi hapa ni kwamba ili mtu mwenye account humu jf akamatwe kupitia namba yake ya simu inabidi jamiiforums na mitandao ya simu waungane, Yani wanaosimamia jamiiforums waziambie idara zinazosimamia mitandao ya simu kwamba account flani inatumia ip adress flani au iliwahi kutumia adress flani, hizo ip adress zinaanza kufuatiliwa zilikuwa zinatumika kwenye simu ipi, hapo watajua namba ya simu na mmiliki mwenye wake.

Sasa kilichotokea enzi hizo ni kwamba tayari kule walikuwa na access ya kujua namba za simu zinazotembelea jf na wanauwezo wa kumjua mtu endapo jf wakitoa ushirikiano, na ndio hapo sasa jamiiforums wakawa wanafatwa kutoa ip adress zinazotumika na accounts kadhaa ili kuweza kuwatambua ni kina nani wanaikosoa serikali.


Palizuka patashika na tafrani humu ndani isiyo ya kawaida, ilifikia kipindi jamii forums ilitaka kufungwa kabisa kwasababu ya kuwaambia serikali kwamba server za jamiiforums zipo huko ulaya na sheria za server za huko zinatia ngumu kwenye kuvujisha ip adress kwenye masuala ya uhuru wa maoni. Serikali nayo ilichachamaa na kesi zikawa nyingi na figisu kibao tu na baadhi ya viongozi wa jf waliwekwa kizuizini walikatazwa hata kusafiri nje ya jiji.

Tunashukuru hili lilipita salama hasa kwa usaidizi wa sheria za server za nje kuwa na sheria kali zinazolaani kuvujisha ip adress kiholela, balozi za nchi za ulaya na marekani nazo ziliweza kukemea uvunjifu wa privacy za watu mitandaoni, nao uongozi wa jamiiforums hawakutuangusha.

Baada ya balaa hili, ilipelekea kuongezewa baadhi ya vipengere katika sheria za nchi zinazohusu privacy za watu mitandaoni na pia kwa sasa jamiiforums hawarekodi ip adress zetu kwa usalama wetu endapo zikiweza kuvuja kwa watu wanaoweza kuhatarisha usalama wetu watumiaji.

Leo hii watu wengi sana humu waliokuwa wakikosoa serikali awamu ile wangekua wameshapitia msoto mkali sana gerezani, hasa ikizingatiwa maafande walishapewa ruhusa na rais wa awamu hio kuwashushia vipigo vizito wafungwa na namnukuu "Wafungwa wafanyishwe kazi usiku na mchana", "wapigwe mateke"
 
Back
Top Bottom