Nawezaje kupata huduma kwa Wizara ya Mambo ya Ndani kupitia mtandao au namba ya simu?

black abdu

Senior Member
Dec 2, 2022
152
208
Leo nimeingia kwenye tovuti ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi, (hii ni wizara serious sana), lengo langu ni kupata huduma za usajili wa taasisi yetu.

Imekuwa vizuri sana serekali walivyotuwekea mfumo wa huduma mitandaoni, inarahisisha Mambo kwa kiasi kikubwa.

Cha kwanza nimepaswa kusajili akaunti nitakayotumia, nimeweka taarifa zote zinazotakiwa pamoja na picha...ila kuna kipengele cha kutengeneza Control number, hii button yake haifanyi kazi, una click hapo lakini hakuna kinachokuja, lakini usajili unagoma, inaleta jibu kuwa control number haijalipiwa. Sasa hii control number naipataje ikiwa hii sehemu yake haifanyi kazi?

Narudi kutafuta mawasiliano ya simu, ili nipige nipate msaada zaidi. Kwenye tovuti ya wizara kuna namba +255262323189, ambayo kila nikipiga inasema namba si sahihi ingawa nimejaribu kuipiga bila kuanza na +255.

Kutoka kwenye tovuti nikaingia kwenye mitandao ya kijamii, kuanzia Instagram, huko hakuna mawasiliano yoyote yaliyowekwa, naingia twitter, nakuta page ya Malalamiko ya Wizara, nahisi nitapata msaada baada ya kuona namba ya simu 0677767778, lakini jibu ninalopata kwenye namba hiyo ni kuwa namba imezuiliwa!

Kwa hiyo nimeganda hapa sijui nifanyeje. Au ndio nifunge safari kuwafata ofisini kwao? Sijajua bado ila kusema ukweli this is so frustrating. Wizara zetu zina wataalamu wa hali ya juu kwa vitengo vyote, sasa tunashindwa wapi kuwa na huduma rafiki kwenye wizara muhimu kama hii, kwa vitu vidogo kama hivi?
 
Back
Top Bottom