Wema Sepetu ataka kugombea ubunge

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
[h=2]Saturday, June 18, 2011[/h][h=3]WEMA SEPETU ATAKA KUGOMBEA UBUNGE[/h]
Posted by Abby Hass on 11:44 PM


Wema akiwa na Cate

HE! Mhusika rasmi katika ‘industry’ ya filamu za Kibongo, Wema Abraham Sepetu (pichani) ametoa kauli iliyojaa mshtuko kuwa, anajipanga kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2015.

Akizungumzia na ‘The Five Star Paper’, Risasi Jumamosi ndani ya Hoteli ya The Atriums iliyopo Sinza-Afrikasana, Dar es Salaam juzikati, Wema ambaye ni Miss Tanzania 2006/07 alisema kuwa, katika mipango na ndoto zake za miaka minne ijayo, ni pamoja na kugombea nafasi ya ubunge.

Wema alifunguka kwamba, nyuma ya mpango huo kuna baba yake ambaye aliwahi kutumikia siasa kwa ngazi ya kidiplomasia ikiwa ni pamoja na kuwa balozi ambaye amekuwa akimshauri mara kwa mara kujikita kwenye kilinge cha siasa.

“Mwazo nilikuwa silifikirii sana jambo hilo, lakini baba amekuwa ‘akini-inspire’ mno.
“Nimeshaanza maandalizi kuelekea 2015, naomba Watanzania wanipe sapoti,” alisema Wema.
Alipoulizwa chama na jimbo atakalogombea, Wema alisema:

“Kuhusu chama nitaangalia kitakachokuwa na nguvu hadi kufikia 2014. Jimbo nitakalogombea bado nalitafiti hivyo nitaliweka hadharani ‘leita’.”

Wema ambaye kwa sasa ‘anatoka’ kimapenzi na msanii wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond’ amekuwa akikumbwa na skendo za hapa na pale lakini sasa ameahidi kubadilika ili kujijenga kisiasa​
 
Atagombea chama kitakachokuwa na nguvu, 'kuhusu chama nitaangalia chama chenye nguvu..' mhh! ALL THE BEST WEMA.
 
ivi anaujua ubunge uyu au anausikia
ila kwa bongo sitashangaa.....
all the best mamito
 
Labda ubunge wa umalaya ndiyo utapata ukawawakilishe bunge lao lakinia siyo hili la watu makini.
 
Jamani what is a big deal with Ubunge?

We have Komba, Rostam, Mr II, why not Wema?

Please, please, please, do not make it a big deal. I agree with you that we have bright wabunge, Tindu Lissu, Mnyiak, Zitto kwabwe, but still we have others who are .....useless materials....

Please, give her a break, mwacheni!
 
Yaliyopita si ndwele, na si ajabu kuwa ilikuwa utoto tu. Kwa miaka minne ijayo onesha kwamba umekua na utapata hiyo sapoti unayoitafuta. Kila la heri.
 
au kabugia viagra nini? bilashaka amejitangaza rasmi kwa wanamagamba ili waanze kumhudumia apite bila kupingwa au viti maalum vya jk. CDM hapamfai kabisaaaaaaaaaa...
 
Ivi na Rostam nae ni msanii? naona umemuweka kwenye kundi la Mr II na Komba!
 
Back
Top Bottom