Waziri wa Kilimo tupe msimamo wa serikali juu ya lumbesa katika zao la vitunguu

Camp 05

JF-Expert Member
Apr 27, 2013
2,129
1,544
Ndugu mheshimiwa Waziri wa Kilomo Hussein Bashe,Kumekua na utata mkubwa juu ya ushonaji wa gunia za Lumbesa hasa kwa mazao ya vitunguu.
Wakati wa mavuno.Mheshimiwa ulitoa tamko Mkoani Mbeya msimu wa nanenane ukiwa na mheshimiwa number one,juu ya katazo la ushonaji wa magunia makubwa (Lumbesa) kwa mazao ya kilimo.Lakini cha ajabu mheshimiwa wakati wa kuuza Lumbesa imerudi kwa Kasi katika masoko ya mazao.
Tunaomba ofisi yako isimamie tamko lako la kupiga marufuku Matumizi ya gunia kubwa wakati wa mavuno na mauzo.
Pia tunaomba soko liwe na usawa bei ya vitunguu iko chini wakati gharama za uzalishaji ziko juu na hasa kwa mazao yanayomalizika ya msimu wa mwaka 2021-2022.
 
Back
Top Bottom