Mbunge Kamonga Apokea Kilio cha Lumbesa Madilu Jimbo la Ludewa

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,903
945

MBUNGE KAMONGA APOKEA KILIO CHA LUMBESA MADILU JIMBO LA LUDEWA

Wananchi wa kata ya Madilu iliyopo Wilayani Ludewa Mkoani Njombe wamelalamikia vipimo vya viazi wanavyohitaji wanunuzi ambapo wamekuwa wakihitaji ujazo wa Lumbesa kitu ambacho kinawapa hasara wakulima hao.

Wakitoa malalamiko hayo mbele ya Mbunge wa jimbo la Ludewa Joseph Kamonga mara baada ya kufika katani hapo na kufanya mikutano katika vijiji mbalimbali vya kata hiyo ikiwa ni ziara ya kupita kijiji kwa kijiji katika jimbo hilo iliyolenga kusikiliza changamoto mbalimbali za wananchi.

Fabian Msigwa ni miongoni mwa wananchi hao amesema japo kilimo cha mwaka huu wamekifanya kwa urahisi kutokana na kupata mbolea za ruzuku kutoka serikalini lakini wanapokuja kuuza mazao hayo wanakumbana na changamoto hiyo inayopelekea waone uraisi walio upata wa mbolea ya ruzuku ni sawa na bure.

"Tunamshukuru sana Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupa ruzuku ya mbolea ambayo imetufanya tulime kwa urahisi sana, ila Mbunge wetu tunaomba ufikishe salamu hizi za lumbesa zinatuumiza wakulima na kutufanya tuone kama ruzuku ya mbolea inajifidia kwenye vipimo vya lumbesa ya viazi". Amesema Msigwa.

Aidha kwa upande wake Mbunge Joseph Kamonga amesema agenda hiyo ya lumbesa wataipeleka bungeni kwa kushirikiana na wabunge wenzie wa majimbo ya mkoa wa Njombe lakini pia wataungana na wabunge wa mkoa wa Mbeya ambapo watamuomba waziri wa kilimo Hussein Bashe kuweka mfumo usio umiza wakulima ikiwezekana viazi hivyo kupimwa kwa kilo.

"Wakati wa bunge la akina Makweta na Mathias wale walikuwa na utarabu wa kuungana na kusukuma agenda kwa pamoja hivyo hii hoja ya lumbesa mtanisikia bungeni nikiisemea kwani haiwezekani wakulima mshindwe kunufaika na mazao yenu waje wanufaike watu wengine" Amesema Kamonga.
 

Attachments

  • WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.08 AM (1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.08 AM (1).jpeg
    70.4 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.09 AM.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.09 AM.jpeg
    62.4 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.06 AM (1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.06 AM (1).jpeg
    72.5 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.06 AM (2).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.06 AM (2).jpeg
    98.8 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.06 AM.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.06 AM.jpeg
    72.2 KB · Views: 2
  • WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.07 AM (1).jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.07 AM (1).jpeg
    66.8 KB · Views: 3
  • WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.07 AM.jpeg
    WhatsApp Image 2023-07-08 at 4.59.07 AM.jpeg
    63.6 KB · Views: 3
Sielewi ni kwa nini Serikali imeshindwa kupiga marufuku Lumbesa. Inawanyonya sana Wakulima. Hata Wilayani Makete Lumbesa imekuwa kitu cha kawaida kabisa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom