WAZIRI WA ELIMU- unayajua yanayofanyika CBE- DODOMA?

Nanyi CBE Dom baadhi yenu wameendekeza sana ngono na ulevi.Someni, starehe baadaye
Kuna mtafaruku mkubwa ndani ya Chuo cha elimu ya biashara kampasi ya Dodoma.Mwaka 2009 kuna baadhi ya wanafunz waliokuwa mwaka wa pili (Advanced diploma) ktk matokeo yao ya semister ya nne walipata dicso(discontinuity) lakin wakiwa ktk harakati za kukata rufaa na kufuata taratibu zote wakapata ushawishi toka kwa mkuu wa idara ya masomo ya jioni kua rufaa hizo wasingeweza kushinda, hivyo kuwasaidia tu ni kwamba angewaruhusu kuwaingiza ktk programu ya masomo ya jioni. Hivyo wanafunz hao wapatao kumi wakakubaliana nae na kweli wakaingizwa ktk program ya masomo ya jioni (NIGHT COLLEGE) wakaanza kusoma toka december 2009 wakafanya tena mitihani ya mwaka wa 2 upya (semister ya III&IV) wakaingia mwaka wa 3 mwez June 2010 wakafanya mitihani ya semister ya V vizuri bila matatizo, wakaendelea kusoma semister ya VI ilipofika wakati wa mitihani mwezi wa 5 mwaka huu, hapo ndipo zilipoanza sarakasi, wengine wakaambiwa kuwa hawakuwa wanafunzi HALALI wakati huo wengne kati yao wakiruhusiwa kufanya mitihani. Wakajaribu kumfata yule mkuu wa idara ya masomo ya jioni (ndiye aliye wafanyia usajiri) akasema file lipo kwa Accademic officer, wakienda huko wanaambiwa file lenu halionekani, mpaka leo hawajapata suluhsho wanahangaika tu mtaani.Sasa nikajiuliza tangu mwaka 2009 wanalipa ada, wanapewa namba za kufanyia mitihani, matokeo yanatoka, iweje leo si wanafunz halali?, kwa nini wengine waliokuwa na the same issue waruhusiwe kufanya mitihan?. Serikali iwasaidie vijana hawa kupata haki yao.
 
mkuu mimi si muhusika, nimepewa full details na vijana hao nilipo kuwa ktk shughul zangu binafsi hapo chuoni isitoshe hawa jamaa niliwaacha chuoni hapo mwaka 2008.
Ungewashauri watafute vyuo kuliko kuendelea kupoteza muda wao. Wamefanya makosa naamini prospectus inaelekeza kila kitu; ni namna gani mtu anaweza kukoma kuwa mwanafunzi.
 
Ungewashauri watafute vyuo kuliko kuendelea kupoteza muda wao. Wamefanya makosa naamini prospectus inaelekeza kila kitu; ni namna gani mtu anaweza kukoma kuwa mwanafunzi.
me mwenyewe nashangaa..m2 ukiisha disco,solution ni kutafuta chuo kingne na kuanza upya,sasa wao wamepoteza mda wao huko bure 2.
 
Ushauri kwa wahusika. Hilo swala ni la ajabu na ukielezea kwa mtu yoyote anayejua sheria za kitaaluma atashangaa sana. kwa kawaida mtu akiwa amedisco hawezi kuendelea na masomo kwa namna yoyote ile. Ukiwa kama mwanafunzi ni vema ukasoma sheria za kitaaluma katika kaozi yako unayoifanya na chuo husika. Ushauri wangu kwenu kama mnapenda kusoma ni kutafuta kozi nyingine kwenye chuo hicho au kingine. Hii inategemea na sifa ulizo nazo katika kupata usajili katika kozi husika.

Kama mtaamua kwenda mbele, kwa hapa namaanisha mahakamani, wote mtapatikana na hatia. mlioendelea kusoma bila kuwa na sifa sitahiki ni kosa (sijui wanasheria wanaliitaje), huyo mkuu wa idara aliyewaruhusu kuijiunga na hiyo program ya jioni naye ana makosa (amefanya vitu ambavyo havipo kweye taaluma yoyote duniani. huwa sheria ni ngumu na inategemea hoja na mtu husika. kama mtaamua kwenda mahakamani mjipange kujibu hoza za kwenu kwamba kwanini mlikuwa mnafanya ufisadi wa elimu.

Nadhani kwa haayo machache mmepata picha na mtachukua hatua.
 
Huyo mkuu wa idara ndiye aliyewaponza, ni bora wangekata rufaa mapema wakajua hatma yao tokea mwanzo! Ila kiukweli management za vyuo vyetu hivi haziko makin kabisa! Mimi naamin katika hili IFM inaongoza! Yaan principal ndo hakuna kitu kabisa....!
 
College of ............... wala sishangai, madent wengi hawana sifa na viongozi wao wa vyuo pia,mi simo huko
 
Mtu unapopata chuo kitu cha kwanza kutafuta ni prospectus na almanac ambazo ni dira zako katika maisha yako yote chuoni,kama huna huwezi kuwa na base ya kuraise arguement mbona wengine tulipewa chuoni S....? wengi wetu wanajua wakishapata admission kinachofuata ni kitabu tu kumbe wanakosea, pole yao
 
Back
Top Bottom