Huu ni upuuzi kwa sababu zifuatazo:
Amandla.....
- Angewataja hao watatu kama kweli kachukizwa. Anaogopa nini?
- Mkataba wowote unaoingia una kifungu cha migogoro na chombo kitakachohusika kuitatua pale itakapotokea. Kwa mikataba na mashirika ya nje chombo hicho mara nyingi ni ICC ambacho kinaaminika kuwa neutral. Kudai kuwa mahakama zetu zimerukwa ni kuthibitisha ukweli wa uoga wa mashirika ya nje kutumia vyombo vya usuluhishaji vya nchini kwetu. Inaelekea kuwa imani ya Sitta na wengine ni kuwa tungependelewa. Tabia yetu ya kutumia sababu za kisiasa kuvunja mikataba ya kibiashara matokeo yake ndiyo haya. Hapa hatujaonewa bali tunavuna tulichopanda.
- Kutolipa faini hii matokeo yake ni mabaya mno maana credibility yetu itaondoka kabisa. Hatutaweza tena kumpata mwekezaji wa maana kuwekeza nchini maana watajua kuwa sisi ni dhulumati.
nakushangaa, hujamwelewa sitta, ina maana hao majaji walipelekewa ushahidi feki toka humo nchini kwa kuwa mafisadi walisuka na watendaji humo serikalini, ujue kuwa jaji au hakimu hawezi kufanya maamuzi bila kupewa ushahidi na kuwa kama ushahidi ni feki basi na uamunzi ni feki