Jana kwenye kipindi cha ITV nilimsikia waziri Selemani Jafo akisema shule za umma zimeboreshwa sana hivyo anategemea shule nyingi za binafsi zitashindwa kujiendesha na kufa.
Kwakweli mawazo haya yamenistua hasa kutolewa na kiongozi kijana kama Selemani Jafo. Nilitegemea kaja na mawazo mbadala kuhakikisha shule binafsi zinaboreka na kujiendesha sawa na shule za umma kwani lengo lao ni moja kuelimisha nguvu kazi ya Tanzania.
Nilitegemea kaja na wazo la kuzipatia shule binafsi ruzuku angalau nao wazikarabati shule zao ziendane na shule za umma.
Naimani shule binafsi zikipewa ruzuku ya elfu hamsini kwa kila mtoto wataweza kusomesha watoto bure sawa na shule za serikali.
Hata mm kauli hii imenishangaza mno kutolewa na kiongozi wa cheo cha juu kama yy.Nini maana ya PPP?kama anajua kuwa serikali inawezafanya yote hayo basi ijenge na viwanda na ifanye biashara.serikali moja ya kazi zake ni kukusanya mapato na kujenga mazingira wezeshi ili kupanua wigo wa kodi na kama serikali hii hii inaombea sekta binafsi zife kwa kweli mm nashindwa kuelewa alikuwa anamainisha nn! kwa kijana kama yy ambaye najua kwa kiasi fulani anafahamu uchumi unaendeshwaje kuja na mbadala wa kuua sekta binafsi its awkward.namwondolea kuwa na sifa ya uwazir moja kwa moja.