Waziri Selemani Jafo: Shule za umma zimeboreshwa sana, shule nyingi za binafsi zitashindwa kujiendesha na kufa

eddy

JF-Expert Member
Dec 26, 2007
15,262
10,287
Jana kwenye kipindi cha ITV nilimsikia waziri Selemani Jafo akisema shule za umma zimeboreshwa sana hivyo anategemea shule nyingi za binafsi zitashindwa kujiendesha na kufa.

Kwakweli mawazo haya yamenistua hasa kutolewa na kiongozi kijana kama Selemani Jafo. Nilitegemea kaja na mawazo mbadala kuhakikisha shule binafsi zinaboreka na kujiendesha sawa na shule za umma kwani lengo lao ni moja kuelimisha nguvu kazi ya Tanzania.

Nilitegemea kaja na wazo la kuzipatia shule binafsi ruzuku angalau nao wazikarabati shule zao ziendane na shule za umma.

Naimani shule binafsi zikipewa ruzuku ya elfu hamsini kwa kila mtoto wataweza kusomesha watoto bure sawa na shule za serikali.
 
Sasa zikipewa ruzuku si zitakuwa za umma? Ila pia kusema zinaboreshwa ili kuuwa za binafsi ni kuchemka maana malengo ni mamoja.

Natamani lengo liwe ni kuinua kiwango cha elimu Tanzania kiendane na mataifa mengine ulimwenguni na siyo lengo liwe ni kuuwa shule binafsi, kosa kubwa.

Wanatakiwa pia wajifunze kwa sekta binafsi wanawezaje, na wao waboreshe za umma.

Ila pia, natamaani mtaala wa kufundisha kiswahili primary ubadilishwe uwe kwa kiingereza.

Uwezo wa mtoto kushika vitu na kujifunza unaanza akiwa mdogo. Tunawakosesha watoto wetu uwezo wao wa kuja kushindana kimataifa kwa sababu ambazo hazina msingi.

Tupende tusipende kama tunataka watu wetu waweze kuwa na competition nzuri tuwaandae wakiwa wadogo.

Haingii akilin kiongozi huyo huyo anayengangana kiswahili kiwe shule za msingi lakini mwanaye anampeleka English medium. Its not fair at all kwa mtanzania mnyonge asiyeweza kumlipia mwanaye hizo English medium.
 
Kila waziri anapaswa aje na matokeo yanayoonyesha kitu binafsi kilichokufa chini wizara yake ili cha umma kichukue nafasi. Hiyo ndiyo mikakati waliyopewa. Mwakyembe anaendelea kufanikiwa kuyaua magazeti kabla ya kugeukia vyimbo vingine binafsi.

Myswada unaandaliwa ambapo vipindi vya vyombo binafsi (Tv and Radio) kuwa asilimia 45 viwe vinachukua vile vya TBC.

Ni suala la muda tu kabla ya kugeukia sekta ya usafiro wa anga, makampuni binafsi ya ulinzi, makamouni ya ujenzi n.k
 
Kuongea bila kutafakari !

Kwa hivyo tuseme hata biashara wanataka kuua biashara za watu binafsi ili serikali iingize za kwao ?

Huyo waziri amesahau makubaliano ya kupunguza gharama za uendeshaji wa serikali katika huduma za kijamii,kwa kuhusisha sekta binafsi ?

Je amefanya tathmini ya takwimu ya wanafunzi wanaofaulu na kuja kutumika kwa maendeleo,kutokea hizo shule binafsi ukilinganisha na idadi ya wanaotoka shule za serikali ?!.
 
Jana kwenye kipindi cha itv nilimsikia waziri jafo akisema shule za umma zimeboreshwa sana hivyo anategemea shule nyingi za binafsi zitashindwa kujiendesha na kufa.


Kwa hili huyo waziri amefilisika mawazo
 
Kama zimeboreka awapeleke watoto wake huko. Shule za umma haina miundombinu kama majengo pia vitendea kazi kama waalimu kuna shule utakuta ina mwl mmoja wa sayansi. Hapo ni kuwahadaa walalahoi waione serikali inapiga kazi.
 
yaani serikali izipe ruzuku shule binafsi? Nawe umenishtua kama jafo alivyokushtua.

Waiter niongeze Safari nyingine!
 
Fanya utafiti wako mdogo tu, wa kujua shule wanazosoma watoto wa mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi wizarani na wakuu wa taasisi za serikali (zikiwamo za elimu), utakuta wengi wanasoma shule binafsi.

AKLI ZA KUAMBIWA CHANGANYA ZA KWAKO
 
Ameongea hayo jana wakati anaongelea Bunsen Burner na Youtube za zamani kuendelea kutumika kwenye mashule?
 
Mkuu maelezo yako kama vile yanakubaliana na Waziri kuwa shule za umma ni bora kuliko zile za binafsi; ni kweli?

Mimi sikubaliani na hiyo hoja; shule binafsi ni bora kuliko zile za umma kwa majengo, muda wa walimu kukaa darasani na idadi ndogo ya wanafunzi kwa mwalimu mmoja
 
Akili za kitz ndio maana miaka 55 ya uhuru mtu anaandika PhD kulia alafu akiwekewa tonge la ugali kushoto anaikana! Yaani waziri mzima kwenye nchi ya watu milioni 50 unaamini kuwa ubora wako utaonekana baada ya aliyekuwa mbele ako kupotea!

No wonder tunapoteza wanadiplomasia wazuri kama Ben Saanane na kutamani kufuta vyama ili wasio na viwango nao waonekane!
 
Back
Top Bottom