Mtanzania unachosema ni kweli ila pia kuna ukweli kwenye argument hiyo nyingine kuwa ubovu wa barabara sio tu unachangia kwenye ajali Tanzania bali pia unakwamisha shughuli nyingi sana za kuinua uchumi kitu ambacho kinapelekea watu kuwa masikini na wengine kufa kwa njaa au kufa kwa kukosa usafiri mzuri na wa haraka wa kuwapeleka hospitalini.
Mwafrika wa Kie,
Ubovu wa barabara ni kweli unachangia ajali. Hoja yangu ilikuwa inahusu udogo wa barabara na wala sio ubovu.
Shimo lililoachwa bila kufikiwa barabarani linaweza kusababisha ajali hata kwa dereva mzuri. .
Barabara ya kwenda Mbeya inaongoza kwenye ajali wakati ni katika barabara nzuri sana kwa TZ. Pia barabara ya kwenda Moshi nayo nzuri lakini pia ina ajari nyingi sana.
Barabara pekee ambayo naona labda kuna haja ya kuipanua ni hii ya kutoka Dar mpaka Morogoro, maana hapo katikati kuna magari mengi. Ukienda Moshi kuna wakati unaendesha hata nusu saa hujapishana na gari, sasa hapo kuongeza upana wa barabara si ni kupoteza pesa tu. Afadhali hizo pesa zijengee barabara huko Lindi au Rukwa.